Nitazidi kuongea hata kama mkiniita tapeli

Humu ndani ukizungumza habari za Forex na Bitcoin, unaitwa tapeli. Iteni mpendavo lakini lazima niwachangamshe akili kidogo.

Bitcoin moja leo imefika USD 23,000 ( Kama Tzs 53 Million.

Na tarehe 16 March mwaka huu 2020, bei ya bitcoin moja ilikuwa inauzwa kwa Tzs 11 Million, maana yake ni kwamba kama uliwekeza milioni 11 mwezi march, sahiv ungekuwa na faida kama Tzs 42 Million.

Yaani ungeweza kabisa ku postpone kununua IST na ukarisk kwenye bitcoin, ungekuta sahiv unaongelea kununua Ford Ranger!!.

View attachment 1652679

Anyway, lengo la uzi wangu sio kuwatia watu machungu, najua kuna matomaso hapa wataniuliza, wewe umetengeneza faida ya sh ngapi mpaka sasa..?

Lengo langu kwenye huu uzi ni kuwakumbusha kwamba, FINANCIAL MARKETS IS REAL..

Somewhere, someone is making good monies out of it, so sio vizuri kutukana hustlers wa kwenye bitcoin na forex.

Kama kitu hutaki, potezea kimya kimya.. ila usiwavunje watu moyo.

Hivo yani.
Duh najuta kuzembea kuzichanga BTC manake tangu January nina 0.421 BTC tu kwenye wallet .....niliacha baada ya kutapeliwa mara mbili...ngoja niingie tena ulingoni kupitia Masternodes
 
Tuchukulie mfano kukawa na rush watu wengi wakawekeza huko. Unadhani nini kitatokea mkuu??
Watu wengi wa Tanzania? Au unaongelea duniani??

Kwenye financial markets watu wakiwa wengi kwenye soko ndo efficient inaongezeka in terms of liquidity.

Ndo itakuwa vizuri kwa soko endapo kama watu wengi wakiwa wawekezaji
 
Duh najuta kuzembea kuzichanga BTC manake tangu January nina 0.421 BTC tu kwenye wallet .....niliacha baada ya kutapeliwa mara mbili...ngoja niingie tena ulingoni kupitia Masternodes
Tumia credible exchange.. na usije kumuamini mtu ukampa pesa zako.. hii naisema wazi..
 
hizi mambo nazielewa ndiyo maana naelewa nini wazungumza. kuna kuwork hard na kuwork smart
Mara nyingi kwenye cryptos.. watu wanangalia zile coins ambazo zina support activity ambayo ipo potential kwa jamii..

Ndo mana utakuta watu wanakuambia Etherium ina potential kubwa kuliko hata Bitcoin
 
Watu wengi wa Tanzania? Au unaongelea duniani??

Kwenye financial markets watu wakiwa wengi kwenye soko ndo efficient inaongezeka in terms of liquidity.

Ndo itakuwa vizuri kwa soko endapo kama watu wengi wakiwa wawekezaji
Duniani nasema kama hivi unavyotangaza na au upepo wa ufahamu wa teknolojia na vitu kama hvyo ukabadilika

Dunia nzima ikawa macho ni huko watu wakazinunua kwa wingi bitcoin leo hii sawa liquidity itaongezeka

Unadhani thamani yake itakua hapo hapo kwenye mil53 za madafu? Itapanda? Itashuka kidogo?? Itashuka sana?
 
Duniani nasema kama hivi unavyotangaza na au upepo wa ufahamu wa teknolojia na vitu kama hvyo ukabadilika

Dunia nzima ikawa macho ni huko watu wakazinunua kwa wingi bitcoin leo hii sawa liquidity itaongezeka

Unadhani thamani yake itakua hapo hapo kwenye mil53 za madafu? Itapanda? Itashuka kidogo?? Itashuka sana?
Either way.. price ina move popote. Itategemea na demand na supply..
 
Financial market ni sekta kama sekta zingine

Kuna nyie mlioko huko,na kuna sisi tupo sekta zingine,wote hatuwezi kua Financial Markets sector kama nyie

Tatizo mnataka kutulazimisha wanadamu wote tuje Financial Markets sector....hatuwezi!

Na the real people waliopo kwenye Financial Markets sector hawataki kusikia utapeli wa Forex Trading na Bitcoin nonsense,shida nyie mnatufata sisi tusiojua Financial Markets sector mnatulizamishia tuingie kwavile hatujui lolote,mnasema mtatu offer training,another nonsense!

Kwanini nyie mlioko huko Financial Markets sector mbaki huko huko mjenge mapesa mengi mje kutukopesha sisi huku manufacturing kwa riba walao mtakua mmetusaidia zaidi...

Kuliko huu uchuuzi wa kulazimisha everybody aje huko ili mmtumie kama mtaji?

Nyie mlioko huko pigeni hela wachache hivyo hivyo,waacheni sekta zingine waendelee kupotea,cha ajabu hamlali mnawang'ang'aniza waje kwa lazima ujue you people are not up to anything good kabisa!
Unaongea bla bla nyingi..

Wapo nimesema mimi natoa training? Unanilisha vitu vingi ambavyo sijaviongea, hapo unakuwa hunitendei haki

Kwa kukusaidia tu elimu.. financial markets inatoa financing kwenye sekta zote unazozifahamu dunia hii.

Ufanisi wa financial markets maana yake ni ufanisi wa sekta nyingine zote. Mfano tu mdogo, biashara au kampuni, ikitaka kupata mikopo au mitaji zinajeukia kwenye financial markets kwa ku list equities au debt securities.

Viwanda vinategemea sana financial markets, raw materials zinazotumika viwandani ni commodities ambazo bei zake zipo decided kwenye financial markets..

Nakushangaa sana unaposhindwa kuona kama financial markets ndo key sector kwenye uchumi wa nchi yoyote including hizo unazoziita wewe ni 'real business' ..

Nakushangaa zaidi, unavotumia kutoelewa kwako financial markets kama standard ya maisha kwa watu wengine.. kwamba kwasababu kitu hukielewi vema basi ni matapeli..
 
Back
Top Bottom