Crypto na ahadi ambayo haijatimia

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,107
NB: Uzi ni mrefu, kinoma 👽

Uchumi wa dunia umekuwa ukidorora kwa miezi (Kama sio kwa miaka) kadhaa sasa, na mdororo huo umeathiri pia thamani ya cryptocurrencies kwa kiwango cha kutisha. Watu wamepoteza mabilioni ndani ya muda mfupi, kiasi ambacho wengine wamechukua maamuzi magumu ya kujiondoa duniani kwasababu walichotarajia, hakikutimia.

Hii imezua maswali juu ya ahadi iliyotolewa na wavumbuzi + chawa wa Crypto - kwamba sarafu za Crypto ni pesa ambazo ziko nje ya mifumo ya kawaida ya kibenki, kwahiyo ni salama na "stable" zaidi kwasababu hakuna mtu, wala kampuni, wala mamlaka ya serikali inayoweza kuzi-control. Lakini, uhalisia unaonesha crypto imeanza kwenda kwa kutumia mifumo ile ile ya kawaida ya kibenki ambayo waanzilishi na mashabiki kindakindaki wa crypto walikuwa wanaikwepa.

Nimeona si vibaya nikaweka uzi wangu juu ya kinachoendelea katika ulimwengu wa crypto. Asomaye na afahamu; Mimi pia ni mtumiaji wa crypto, huku niliko tunaendesha programu ambayo kwa 95% pesa zake zipo katika crypto na mpaka sasa tumeshafanya miamala ya zaidi ya TZS 25M. Lakini uamuzi wangu wa kuleta uzi huu ni kutokana na kwamba sijaona mtu alieiongelea crypto kama ambavyo nitafanya hapa. Karibu!​

KWANI, HALI YA CRYPTO IKOJE KWA SASA?
Mpaka Disemba 2022, crypto zilikuwa zimepoteza wastani wa asilimia 60 ya thamani zake. Hizi hapa chini ni crypto maarufu zaidi duniani, acha zitusaidie kupata uelewa wa pamoja wa hali ilivyo kwa sasa;​
  1. Terra: Imepoteza asilimia 100% ya thamani yake.
  2. Solana: Imepoteza asilimia 93% ya thamani yake.
  3. AMP: Imepoteza asilimia 93%
  4. Cardano: imepoteza asilimia 80%
  5. Ether: Imepoteza asilimia 67%
  6. Bitcoin: Imepoteza asilimia 63%
  7. Dogecoin: Imepoteza asilimia 55%
Kwa pamoja hizi crypto zote unazozisikia, katika ubora wake zilikuwa na thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Trilioni 3. Na sasa zina thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 1 kwa ujumla, maana yake kuna Trilioni 2 zimeyeya!​

DUH! LAKINI SI NDIO HALI YA UCHUMI ILIVYO? KAMA UCHUMI WA DUNIA UNAPOROMOKA KWANINI UNADHANI CRYPTO ZISINGEPOROMOKA?
Well, Crypto zilibuniwa ili zije kuwa mbadala wa masoko ya fedha ya kawaida. Waanzilishi wa Crypto walikuwa wanazipigia debe kama mbadala wa fedha za kawaida ambazo zinasimamiwa na benki kuu za nchi mbali mbali. Kwahiyo, matarajio ni kwamba fedha za kawaida zinapoporomoka kimbilio liwe ni crypto, ila ndo kama hivyo hali imekuwa tofauti.​

MH! SIJAELEWA BADO - FAFANUA ZAIDI.
Ok, twende kwenye Historia kidogo: Asili ya crypto ni kipindi kifupi kilichofuatia baada ya anguko la uchumi wa dunia la mwaka 2008. Katika anguko lile tulishuhudia kifo cha moja ya benki kubwa duniani iliyofahamika kama Lehman Brothers ambayo imekuwepo duniani kwa miaka 158! Ulikuwa ni msiba mkubwa.

Mabenki wakati huo yalifanya ujinga ambao watu hatutarajii wasomi wa benki waufanye kwa kutumia pesa zetu ambazo tunawapelekea watutunzie. Mabenki yaliwakopesha sana watu ambao hawastahili kukopeshwa, mabenki yalikuwa yamelegeza vigezo vya kukopa, ili raia wakope sana. Ilitokea hivyo kwasababu benki kuu zilikuwa zimepunguza riba; mfano - Marekani ilipunguza riba kutoka 6.5% mwaka 2000 mpaka 1% mwaka 2003%.

Ukiona Benki Kuu ya nchi yoyote inatangaza kupunguza riba ujue lengo ni kuifanya pesa iwe rahisi kupatikana kwa raia wa kawaida, hali ambayo ina-boost uchumi uliosinyaa. Kwahiyo watu wakakopa sana kwasababu riba ni ndogo, wengine wakachukua nyumba za mikopo, watu wakanunua magari kwa wingi n.k.

Ili kuchochea moto zaidi, Federal Reserve ya Marekani ikapunguza hitaji la kiwango cha chini cha mtaji ambacho benki zinatakiwa kuwa nacho (Kwa benki tano kubwa za Marekani). Lengo lilikuwa ni kuzihamasisha hizi benki zichukue "risk" zaidi ya kuwakopesha raia. Matokeo yake hizi benki zika-leverage mitaji yake kwa zaidi ya mara 30 hadi 40. Maana yake benki nazo zilikopa kwa zaidi ya mara 30 ya uwezo wake ili nazo zikopeshe!

Waneni husema hakuna hali ya kudumu; eventually Federal Reserve ya Marekani ikaanza kupandisha riba mwaka 2004 ambapo ilipanda mpaka asilimia 5.25 iliyodumu mpaka mwaka 2007. Mdogo mdogo mabenki yakajikuta yana orodha ndefu za wadaiwa sugu ambao hawana uwezo wa kurejesha mikopo kwasababu walikopa wakati riba iko chini sana, na sasa wanatakiwa kulipa wakati riba iko juu sana. Vivyo hivyo wale waliokopa nyumba, ikawa ni mtihani mzito kwenye kuzilipia, na kuziuza ikawa haiwezekani kwasababu zilikuwa zinaporomoka thamani yake siku hadi siku (Housing Bubble).

Hatimae Benki ya Uswisi ikawa ya Benki kubwa ya kwanza kutangaza hasara, ambapo ilitangaza kuwa imepata hasara ya Dola za Kimarekani Bilioni 3.4 kutokana na 'mikopo ya kimchongo'. Benki kuu mbalimbali duniani zikajaribu kuokoa jahazi kwa kumwaga pesa kwenye mabenki ili kuzuia mporomoko wa uchumi, lakini kama wasemavyo "La kuvunda halina ubani". Mabenki mengi tayari yalikuwa yamevuka mstari mwekundu; yakawa yanashindwa kukadiria kiasi cha hasara ambacho watapata kutokana mikopo mingi ya kimchongo waliyonayo kwenye hesabu zao.

Februari 2008 Serikali ya Uingereza ikalazimika kuitaifisha benki ya Northen Rock. Machi 2008 moja ya Benki kubwa ya uwekezaji duniani iitwayo Bear Stearns ambayo ilikuwa ni mhimili wa Wall Street kuanzia mwaka 1923 nayo ikatangaza kufilisika, ambapo ikanunuliwa na benki ya JP Morgan Chase kwa thumni za dola! Fahamu kwamba Wall Street ni kama center ya masuala ya uuzaji na ununuzi wa hisa duniani. Ikafuata IndyMac Bank nayo ikafariki, na ndiposa mwezi Septemba 2008, Lehman Brothers ika-rest in pieces.​

ENHE, KWAHIYO? HAYO YANAHUSIANA VIPI NA KUANZISHWA KWA CRYPTO?
Anguko la uchumi la mwaka 2008 liliwaumiza wananchi wengi wa kawaida (Rudia tena kusoma neno "Wananchi wengi wa kawaida"). Wengi walipoteza ajira zao, wengi walipoteza nyumba zao, na wengi walipoteza akiba zao. Hasira ziliwapanda wananchi hawa wa kawaida kwasababu, baada ya 2008 benki nyingi ziliweza kusimama tena kwa kuwa zilipata pesa(Bailout) kutoka serikalini (Ambazo ni kodi za wananchi). Kwa wengi ilionekana si sahihi kwa serikali kuwapa pesa za walipa kodi watu ambao walizichezea pesa za wavuja jasho. Ikaonekana kama Serikali na mabenki lao moja - kuwanyonya wananchi kwaajili ya kujineemesha wao.

Japo kwa ujumla kitendo cha serikali kuingilia kati kwa kutoa pesa kwa mabenki kilisaidia kuurudisha uchumi mahali pake, lakini kwenye akili za raia wengi ilionekana ni kama serikali ilikuwa inawazawadia watu wa benki badala ya kuwaadhibu kwa uzembe uliogharimu uchumi wa dunia.

Anguko la uchumi la 2008 lilionesha udhaifu wa mifumo ya kibenki na Serikali. Hapo ndipo watu wakaanza kufikiria kuanzia mfumo ambao utakuwa ni mbadala wa mfumo huu mbovu uliopo.​

OK, KWAHIYO HAPO NDIPO TUKASIKIA BITCOIN IMEVUMBULIWA SI NDIO?
Yap! Bitcoin kama Crypto ya kwanza kabisa, iliingia kama sarafu ambayo hakuna wa kuidhibiti. Ni pesa mtandao, sarafu ya kidijitali ambayo kila muamala wake unarekodiwa katika Kitabu cha kimtandao cha kumbukumbu kinachofahamika kama "Blockchain". Vijana wengi wakaipokea Bitcoin kwa mikono na miguu yote, wakaingia wazima wazima kwasababu walikuwa wamechoshwa na sarakasi zinazofanywa na mabenki na serikali.

Bitcoin ilionekana ni pesa inayomlinda mtu dhidi ya Serikali. Kivipi? Utaniuliza. Well, Serikali inaweza kuzisimamia na kuzidhibiti pesa zako zilizopo benki - mfano inaweza kuzuia usizitoe, inaweza kuongeza tozo, inaweza kuongeza riba, inaweza kupunguza riba, inaweza kuzibadilisha, na inaweza ikafanya maamuzi ambayo yanaathiri thamani yake. Lakini hakuna kitu serikali inaweza fanya kwenye Bitcoin, na sarafu mtandao zingine.

Kwahiyo, maono ya waanzilishi wa Crypto ni kuwa na jamii ambayo watu wanaweza kufanya miamala kwa kutumiana pesa, kununua na kuuziana vitu wao kwa wao pasipo kuingiliwa na/au kuitegemea mamlaka ya serikali yoyote ile au taasisi binafsi yoyote ile duniani.​

AISEE! SASA NDOTO HIYO ILITIMIA?
Mwanzoni mambo yalienda vizuri kabisa. Lakini usisahau kuwa, watu wa mwanzo kabisa kuikimbilia Bitcoin kwa wingi walikuwa ni wahalifu, hususani wauza madawa ya kulevya.

Kulikuwa na soko mtandaoni linaitwa Silk Road ambalo kwa asilimia kubwa lilikuwa linategemea crypto. Mtu alikuwa ananunua madawa ya kulevya kule Silk Road, halafu mzigo unamfikia mpaka mlangoni kwake na yeye analipia kwa Bitcoin. Ukawa ni mfumo ambao watu wanauamini na kuutumia kwa malipo ya biashara haramu.

Ilikuwa ni njia rahisi na ya haraka ya kutuma pesa umbali mrefu mfano kutoka nchi moja kwenda nyingine, bara moja kwenda jingine n.k, ikarahisisha namna ya ku-track miamala, na ikaweza ku-maintain thamani.

Lakini kuna watu hawakuipenda taswira hii ya Crypto na uhalifu, walitaka kuionesha dunia kuwa crypto inaweza kusafishwa na kuwa njia mbadala ya malipo na ikatumiwa na kila mmoja duniani pasipo kuhusisha uhalifu.​

NIMEKUPATA, SASA CRYPTO ILIWEZAJE KUPENYA NA KUKUBALIKA NA WATU WENGI NJE YA WAUZA UNGA?
Wajasirimali. Kwa kutumia mbinu za kimauzo ikiwemo mbinu ya kupandikiza kitu kinachoitwa FOMO (Fear Of Missing Out), wajasiriamali wengi waliibeba agenda ya Crypto kama fursa ya kiuwekezaji. Wakawashawishi watu kuwa Crypto itakuja kuziondoa pesa za kawaida. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja tena ya kuwa na Shilingi, au Dola, au Paundi, Au Euro n.k. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja ya kuwa na mabenki kwasababu watu watakuwa wanamalizana wao kwa wao bila kuwa na haja ya uwepo wa Serikali au "Mtu kati".

Mdogo mdogo watu wakaanza kuelewa somo, uhitaji wa Bitcoin ukaanza kuongezeka. Bitcoin ikaanza kupanda thamani kwasababu ya demand kubwa. Kampuni mbalimbali zikaibuka kwaajili ya kutumia fursa zitokanazo na Bitcoin. Na kwa kuona mafanikio ya Bitcoin, Crypto zingine zikaanza kuibuliwa pia. Zingine zilipata umaarufu kimasihara tu mfano Dogecoin🐶!​

NOMA SANA, NASIKIA WATU WANASEMA MLIPUKO WA KORONA ULIWEZESHA THAMANI YA CRYPTO KUPANDA, NI KWELI?
Ni kweli. Kila baada ya kipindi fulani Dunia huwa inashuhudia jambo linaibuka, linafikia kilele cha umaarufu, kisha linaporomoka ghafla na pengine linapotea kabisa. Kisha linaibuka jingine linaenda mzunguko uleule - wenyewe wanaita "Boom and bust cycles".

Hakuna watu wanaweza kumshukuru "aliyetengeneza" kirusi cha Korona kama watu wa Crypto. Maana Korona ilipelekea marufuku za watu kuzurura mitaani, kwenda makazini, kusafiri n.k. Hali hiyo ilipelekea watu kutumia muda mwingi wakiwa wamejifungia ndani. Lakini maisha ilikuwa ni lazima yaendelee; miamala ilikuwa ni lazima ifanyike. Na njia rahisi ilikuwa ni kulipa kwa njia ya mtandao. Hapo ndipo tukashuhudia crypto zikipanda thamani kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa kabla.

Watu wengi walijikuta wako majumbani, na hivyo muda mwingi walikuwa wanautumia mitandaoni. Hata manunuzi yakawa yanafanyika mtandaoni. Na kuna baadhi ya nchi raia walikuwa wanalipwa pesa kiasi kwaajili ya kujishikiza - maana yake watu wakaanza kupata pesa ambazo hawajazitolea jasho. Na kwakuwa watu walikuwa na pesa zisizo na jasho wakaanza kuzitumia hata kwa vitu "risky" kama vile kuwekeza kwenye crypto. Na tukaanza kushuhudia mtu anawekeza Dola 10 anapata Dola 100. Mtu anaweka TZS 500,000/= inapanda mpaka milioni kadhaa ndani ya muda mfupi. Tazama Bei ya Bitcoin ilivyoongezeka miezi mitatu tangu WHO walipotangaza kuwa COVID-19 ni Pandemic (Mwaka 2020).

Bitcoin.jpg

Hapa ndipo makampuni kibao yakaibuka. Na mengi yalikuwa yanahimiza watu kuwekeza kwenye crypto. Ilikuwa kila kona unakutana na matangazo ya Crypto. Watu maarufu duniani wakaanza kuwa ma-influencers wa Crypto. Kuna uwanja unaitwa Staples Center ambao unatumiwa na timu maarufu ya mpira wa kikapu ya LA Lakers nchini Marekani - ulibadilishwa jina na sasa unaitwa Crypto.com Arena.

Kuna tangazo moja linamhusisha muigizaji maarufu wa Marekani aitwaye Matt Damon; HILI HAPA kwenye hilo tangazo (La Crypto) anatoa ujumbe rahisi tu lakini ni mzito, kwamba "Fortune Favors The Brave." Matangazo ya hivi yalikuwa mengi sana.

Haya matangazo na hawa influencers walichokuwa wanajaribu kuwaambia watu ni kwamba; "Wekezeni kwenye crypto kabla hamjachelewa, mkiikosa hii nafasi leo mtakuja kuijutia kesho." Na karibu matangazo yote ya Crypto yanaegemea kwenye kitu kimoja - FOMO. Kwamba usiponunua crypto leo basi wewe ni mjinga, wewe hujielewi, wewe unapitwa na wakati, wewe ni mshamba, wewe ni muoga, na message zingine kama hizo.

Hii "hype" ya wakati wa pandemic ndio ilikuwa "Golden era" ya crypto. Watu wengi hawakutaka kupitwa kama ambavyo matangazo yanawashawishi. Hapa ndipo Crypto ikaingia "mainstream", ikawa habari kubwa duniani. Kila mtu akawa ni "mtaalamu" wa crypto, unapita kijiweni pale Njombe kwetu unakuta bodaboda wanaongelea biashara ya "Kucheza Bitcoin" 😝😆😆 na ikaambatana na biashara ya "Kucheza FOREX" na ikaambatana na biashara ya "Kuweka mikeka" 😎​

TUKO PAMOJA, NINI KIKAFUATA?
Well, nimeongelea mara kadhaa kuwa kampuni nyingi ziliibuka wakati huo wa pandemic. Ambacho sijasema ni kuwa hizi kampuni hazikuwa zinatengeneza crypto mpya, bali nyingi ziliingia kwaajili ya kuwawezesha watu kufanya miamala ya crypto.

Chukulia mfano wa Benki; benki hazitengenezi pesa, bali zinawawezesha watu kutunza na kufanya miamala ya pesa. Kwahiyo, kampuni nyingi zilizoibuka zilikuwa ni kama "Crypto Banks"; kwa maana kuwa hazikuwa zina-mine crypto mpya bali zilikuwa zinawezesha watu ku-store, ku-trade na ku-exchange cryptos zilizopo kama Bitcoin na wenzake.​

HEH!?! BENKI TENA? MIMI NILIJUA WATUMIAJI WA CRYPTO WANAZICHUKIA BENKI? INAKUWAJE KUNAKUWA NA "BENKI" ZA CRYPTO?🤔
Kwakweli hata mimi nashindwa kushangaa; ni ajabu na kweli. Lakini ninachojua hizi kampuni hazijiiti benki. Na wala hazisimamiwi kama benki. Lakini kiuhalisia zinafanya kazi kama benki 🤓 (Rudia tena kusoma). Unaweka crypto yako, unaiacha kwa muda fulani - inazalisha faida vile vile kama ambavyo ukiweka pesa benki kwenye "savings account" zinazalisha faida.​

Nitatoa mfano mmoja: Kuna kampuni inaitwa Celsius ambayo ilikuwa inajinadi kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 1.5

Screenshot 2023-01-08 140602.png

Hii kampuni ilianzishwa na mtu anaitwa Alex Mashinsky. Huyu mchizi ana historia ya utapeli-tapeli, anaongea sana na muongo muongo - ila ana nguvu ya ushawishi (Very charismatic). Kwahiyo, baada ya kupiga utapeli kwenye biashara zingine huko - akakutana na Crypto, akavutiwa na fursa zake, akaanzisha kampuni.​

ALIWEZAJE KUWASHAWISHI WATEJA?
Ni rahisi tu; alikomaa na pointi moja kwamba "Benki za kawaida zinawadanganya watu na kuwaibia pesa zao!". Hiyo ndio ilikuwa "Selling point" yake. Kwamba, "Sikieni nyie watu; Mfano una hela zako, unazipeleka benki, benki wao wakishazipokea wanazikopesha mikopo ambayo ina riba mpaka asilimia 25%, wakati huo wewe wanakupa chini ya asilimia 1% (Kwa akaunti ya kawaida). Hilo ni tatizo, kwasababu imefika mahali tunaona ni sawa na tunaendelea kuwapa pesa zetu na wao wanaendelea kutajirika wakati sisi maisha yetu yanabaki vile vile."

Baada ya kuwagonga watu na hiyo pitch, then anawaambia kuwa Celsius itafanya kinyume chake; Itachukua crypto zako, itawekeza na kuzalisha faida kubwa, kisha asilimia kubwa ya faida utachukua wewe!🥳 Kwahiyo, Celsius inakuwezesha wewe kutumia pesa zako kutengeneza pesa kirahisi kabisa!

Jamaa alikuwa anaweka videos YouTube kila wiki kama dozi. Akawa ana-tweet kinoma. Na kwasababu wakati huo watu wengi walikuwa majumbani, wameshiba, wananenepeana tu, ujumbe ukawa unawafikia barabara kabisa. Boom, wateja wakaanza kuzipeleka crypto zao Celsius. Jamaa alikuwa anahubiri injili ya Crypto kisawasawa na ikawa inawaingia watu; na watu wanaokoka kwenda kwenye Crypto kupitia Celsius kutoka benki za kawaida 🤪​

KWANI FAIDA ILIKUWA NI KIASI GANI UKIWEKEZA CELSIUS?
Kama ilivyokuwa kwa crypto banks nyingi, ilikuwa ni 18%. Hii haikuhitaji kufikiria mara mbili, hakuna benki itakupa riba ya asilimia 18% kwenye akaunti ya kawaida. Na kumbuka; hii haikuwa kama hisa au cryptocurrency zenyewe ambazo unanunua ukiwa na matumaini kuwa thamani yake itapanda (Japo moyoni una uhakika itashuka 🤣), hawa Celsius walichokuwa wanakifanya ni hivi;

Wewe unaweka crypto yako kwa kuanzia kama mtaji. Kisha baada ya hapo inakuwa ni mwendo wa kupokea 18%, huwazi suala la thamani kushuka wala nini. Inakuwa kama umepanda crypto hivi, baada ya hapo ni mwendo wa kuzivuna 🤑🤑🤑🤑

Na amini usiamini, wajinga duniani hawatokuja kuisha. Watu hawakuona kuwa huu ni utapeli, bali wengi waliamini hizi ni "Hela za bure" zinazotolewa na Celsius... asalaleee!!!🥱​

EBWANAEEEE! LAKINI, WAO CELSIUS FAIDA WALIKUWA WANAITENGENEZAJE?
Haijawahi kueleweka, lakini kitu kimojawapo ambacho Celsius walikuwa wanakifanya; ni kuchukua pesa (crypto) za wateja, kisha wanazikopesha kwa wawekezaji wakubwa na wafanyabiashara professional, na wale wawekezaji walikuwa wanakopa kwa riba, kwahiyo wakilipa na wao Celsius wanazisukuma kwenda kwa mteja.

Lakini, ukitumia "Common sense" hii mechanism inagoma - haiingii akilini. Namba huwa hazidanganyi, na kwenye mechanism hii namba zinagoma, haiwezekani kuwahudumia wateja wote hawa zaidi ya 1.5M kwa kutumia riba kutoka kwa wakopaji wachache ambao pengine hawafiki hata 100. Kimsingi, kuna mengi ambayo hatuyajui ambayo yalikuwa yanafanyika nyuma ya pazia. Tunachojua hawa Celsius kuna uhuni walikuwa wanafanya ilimradi siku ziende na watu waendelee kuweka crypto zao,... you know, "common sense is not common!"​

MH! KWANI HAKUKUWA NA WAKOSOAJI? HAKUKUWA NA WATU WA KUUANIKA HUU UTAPELI?
Walikuwepo; wanauchumi, wataalamu wa masuala ya kibenki na masoko ya mitaji n.k. Walijitahidi kwakweli kuwaelimisha watu kuwa hakuna pesa za rahisi namna hiyo katika mifumo ya kifedha. Wengi walikuwa wanawatahadharisha watu kuwa hii ni "Ponzi Sheme"

Kitu kingine kilichokuwa kinaleta hofu zaidi kwa wataalamu wa uchumi ni kwamba; Akiba ambazo watu huwa tunaweka benki huwa zinakatiwa bima, lakini kwa Celsius - akiba za watu hazikuwa na bima yoyote! Lakini kwa namna moja ama nyingine, ni vigumu sana kumshawishi mtu anaekaribia kutapeliwa kuwa atatapeliwa; huwa ni wabishi kinoma!

Usiniulize Serikali huwa hazioni au la, kwasababu hata mimi sijui!​

SASA, IKAWAJE? CELSIUS IKAISHIAJE?
Uchumi wa dunia ukaanza kuyumba yumba, Urusi ikaivamia Ukraine, mataifa bado yalikuwa yana "hangover" ya Korona, mifumo ya usambazaji wa bidhaa duniani ikaathirika kwa kiwango kikubwa sana. Benki kuu zikaanza kuongeza riba.

Kama nilivyoeleza hapo juu, hapa ni kinyume chake; Ukiona Benki Kuu yoyote duniani inaongeza riba, maanake wanalenga kupunguza spidi ya watu kufanya shopping zisizo na maana 😄 Wanajaribu kuwalazimisha watu waweke akiba pesa walizonazo badala ya kuzitumia ovyo.

Kwahiyo, zama za shopping za ovyo zikaishia hapo. Watu wakaanza kuuza hisa zao kwa kasi, kwasababu hisa zilikuwa haziaminiki kama ni uwekezaji salama, na ni kwasababu zilikuwa zinaporomoka bei - kwahiyo mtu anaona bora auze hisa kisha zile pesa apeleke benki kwenye savings account kwasababu atapata gawio kubwa na la uhakika. Vivyo hivyo crypto nazo zikaanza kuporomoka bei kwasababu watu wakawa hawaziamini kama ilivyokuwa kabla. Hivyo wakaanza kuzitoa (Ku-withdraw) kwa kasi.

Hata coin inayoitwa Terra USD ambayo ilibuniwa kwa namna ambayo thamani yake inaenda sambamba na thamani ya dola, kwenye ule mporomoko nayo haikuachwa salama. Ikawa ni mwanzo wa muvi la kutisha; project nyingi za crypto zikaanguka kwa pamoja ndani ya muda mfupi. Wazungu wanaita "Domino effect" - kikianguka kitu kimoja kinasababisha vingine vingi vianguke. Mabilioni ya dola yakageuka moshi ndani ya siku chache.

Kwahiyo, wateja wa Celsius wakawa wanataka kutoa pesa zao pamoja na riba ambazo wamejikusanyia kwa kipindi chote na ambazo walikuwa hawajazichukua. Kikatokea kitu ambacho mabenki huwa yanakiogopa , kinaitwa "Bank run".

Bank run ni pale ambapo wateja wengi wanataka kutoa pesa zao zote kutoka benki kwa mkupuo. Mara nyingi huwa inakuwa ni haiwezekani kwasababu pesa zilizopo benki huwa haziwezi kuwatosha watu wote wanaotaka kutoa kwa mara moja. So, kwa kawaida ikitokea "Bank Run" benki huwa zinalazimika kusitisha miamala.

Basi buana, Celsius ikasitisha miamala. Hiyo ilikuwa ni mwezi wa sita mwaka jana. Huku mtaani tunaamini kitu kimoja kuwa, kwenye ulimwengu wa crypto ukisikia wametangaza kuwa wamezuia kufanya miamala kwa muda basi ujue kama ni mgonjwa basi huyo ni wa leo au wa kesho: anzeni kuandaa taratibu za mazishi. Ni nadra sana kusikia kampuni ya crypto imesitisha miamala kisha ikaruhusu miamala kuendelea baada ya muda, sikumbuki kama imewahi kutokea.

So, tangazo la Celsius la kusitisha miamala likazidi kuutikisa ulimwengu wa crypto. Bei zikazidi kushuka kwa kasi ya 5G. Na hatimae wiki chache baadae parapanda likalia, Celsius ikatangaza kuwa imefilisika🤒. Watu wakabaki njia panda - hawajui kama crypto zao watapata au hawazipata tena. Na mpaka leo haijulikani ni nini kitatokea.​

PHEW! KWAHIYO SASA INAKUWAJE; KWANI INA MAANA WATU HAWAKUJUA KUWA CRYPTO NI KAMA KAMARI?
Watu wengi huwa wanawekeza kwenye crypto kwa ushawishi wa ma-influenza na matangazo, huwa hawatumii akili zao kufuatilia kwa undani uhalisia wa mambo ulivyo. Mwisho wa siku wakipoteza pesa zao, huwa wanajihisi kuwa wametapeliwa. Yale yale ya DECI, Mr. Kuku, Kalynda, Jatu.... am I talking to sambade!? 🤣

Kwamba watu wanawekeza kwa kuahidiwa usalama wa pesa zao, na uhakika wa faida (Gawio). Wengi wamepoteza akiba zao za maisha (Pensheni), wengine wamepoteza mitaji yao ambayo waliiwekeza wakitumaini itakua mikubwa ili wawekeze zaidi n.k. Na kuna wengi wanajinyonga kwasababu ya kupoteza pesa katika uwekezaji wa crypto, Rest in pieces.

Wengi huwa wanawalaumu watu maarufu kwa kutumika vibaya kuwashawishi watu kuingia kwenye biashara ambazo mwisho wa siku huwa zinawaumiza watu wa hali ya chini. Ni kwasababu huwa wanawaamini watu maarufu, wanafuata kila wanachosema pasipo kufuatilia kiundani. Kikwete aliwahi kusema, "Jamani za kupewa, changanya na zako... kama mbayuwayu!"​

ENHE, ULISEMA KUNA AHADI AMBAYO HAIJATIMIA - NI IPI HIYO?
Crypto ilidizainiwa kuwa mbadala wa mifumo ya kibenki; mifumo ambayo kuna "mtu" au "kikundi cha watu" au "mamlaka fulani" au "taasisi fulani" inasimamia na kufanya maamuzi juu ya pesa za watu wengine. Na kwasababu ni mtu mmoja au kikundi cha watu wachache ndio kimepewa mamlaka ya kusimamia pesa za watu wengi - uwezekano wa makosa kufanyika ni mkubwa. Nimeeleza kilichotokea kabla ya anguko la uchumi la 2008. Maamuzi mabovu ya watu wa benki yalipelekea watu kupoteza pesa zao. Lakini kama ulivyoona kwenye mfano wa Celsius, yanatokea yale yale ambayo watu wa crypto walikuwa wanayakwepa.

Kwahiyo; ahadi ambayo haijatimia ni ahadi ya crypto kuwa mbadala wa pesa za kawaida ambazo zinazimamiwa na serikali na kuratibiwa na mabenki na taasisi za fedha kwa sheria na kanuni mbalimbali.

Mtaani mijadala inaendelea kuhusu kama kweli crypto itaweza kuleta suluhisho la mapungufu yaliyopo katika mifumo ya kibenki. Kuna watu wanaona cryto ni utapeli tu, hivyo ni suala la muda kabla haijapotea kabisa. Kuna watu wanaona crypto ndio future, sema hivi sasa inapita katika tanuru la moto na ikitoka hapa itakuwa ni dhahabu.

Inawezekana wote wapo sahihi, na inawezekana wote wanaota ndoto za Abuu Nawasi (Abunuwasi). Muda ni hakimu mzuri zaidi, kwahiyo sisi tusiojua cha kufanya acha tuendelee kuishi.​

SO, CRYPTO IMEKUFA AU?😪
Ni mapema sana kulisema hilo. Ni kweli crypto imepoteza thamani kubwa, lakini bado kuna watu wanaendelea kuwekeza. Na sio kampuni zote za crypto zimekufa, kuna zingine bado zinaendelea kuwahudumia wateja mpaka sasa tunavoongea; Kwa mfano Binance.

Binance in Dar.jpg

Fahamu kwamba, kuna watu wapo katika ulimwengu wa crypto sio kwaajili ya faida au hasara; wao wana-enjoy kucheza na crypto; ni kama wanafanya utafiti kujua namna ilivyoundwa na namna inavyofanya kazi. Na wanatumia teknolojia ambayo ni msingi wa crypto, Blockchain (Cryptography na Hashing) kuleta mapinduzi mengine ya teknolojia.

Mnaikumbuka Dot Com Bubble? Kampuni nyingi za intaneti ziliibuka, na nyingi kati ya hizo zikafa... lakini zile chache zilizoweza kupenya kile kipindi intaneti inaingia duniani zimeweza kuwa ni kampuni kubwa sana duniani hivi sana; Unaongelea Amazon, eBay, Booking Holdings, Shutterfly, n.k.

Inaweza kutokea hivyo hata kwenye crypto, kwamba tumeshuhudia kampuni kubwa za Crypto zinafilisika; FTX, Blockfi, Three Arrows Capital (3AC), Voyager Digital, Celsius Network na nyingine zipo kwenye hali mbaya kama vile Silvergate Capital Corp, lakini chache bado zinaukaza mwendo kama vile hakijatokea kitu.

Ni nani ajuaye pengine tukivuka hapa Crypto itasimama tena. Yote kwa yote crypto haionekani kuwa ni kitu kinachoweza kupotea ghafla, bado tunayo sana; na baadhi yetu tuna shauku ya kujua ni nini kitafuata baada ya hapa. Ilipo crypto na sisi tupo.

Homework: Fuatilia kuhusu anguko la Quadriga CX na FTX, kuna mengi utajifunza kuhusu Crypto Banks.​

Naweka kipaza chini.

Mimi... ninashukuru.
 
NB: Uzi ni mrefu, kinoma

Uchumi wa dunia umekuwa ukidorora kwa miezi (Kama sio miaka) kadhaa sasa, na mdororo huo umeathiri thamani ya cryptocurrencies kwa kiwango cha kutisha. Watu wamepoteza mabilioni ndani ya muda mfupi, kiasi ambacho wengine wamechukua maamuzi magumu ya kujiondoa duniani kwasababu walichotarajia, hakikutimia.

Hii imezua maswali juu ya ahadi iliyotolewa na wavumbuzi + chawa wa Crypto - kwamba sarafu za Crypto ni pesa ambazo ziko nje ya mifumo ya kawaida ya kibenki, kwahiyo ni salama na "stable" zaidi kwasababu hakuna mtu, wala kampuni, wala mamlaka ya serikali inayoweza kuzi-control. Lakini, uhalisia unaonesha crypto imeanza kwenda kwa kutumia mifumo ile ile ya kawaida ya kibenki ambayo waanzilishi na mashabiki kindakindaki wa crypto walikuwa wanaikwepa.

Nimeona si vibaya nikaweka uzi wangu juu ya kinachoendelea katika ulimwengu wa crypto. Asomaye na afahamu; Mimi pia ni mtumiaji wa crypto, huku niliko tunaendesha programu ambayo kwa 95% pesa zake zipo katika crypto na mpaka sasa tumeshafanya miamala ya zaidi ya TZS 25M. Lakini uamuzi wangu wa kuleta uzi huu ni kutokana na kwamba sijaona mtu alieiongelea crypto kama ambavyo nitafanya hapa. Karibu!​

KWANI, HALI YA CRYPTO IKOJE KWA SASA?
Mpaka Disemba 2022, crypto zilikuwa zimepoteza wastani wa asilimia 60 ya thamani zake. Hizi hapa chini ni crypto maarufu zaidi zitusaidia kupata uelewa zaidi wa hali ilivyo kwa sasa;​
  1. Terra: Imepoteza 100% ya thamani yake.
  2. Solana: Imepoteza 93% ya thamani yake.
  3. AMP: Imepoteza 93%
  4. Cardano: imepoteza 80%
  5. Ether: Imepoteza 67%
  6. Bitcoin: Imepoteza 63%
  7. Dogecoin: Imepoteza 55%
Kwa pamoja hizi crypto zote unazozisikia, katika ubora wake zilikuwa na thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Trilioni 3. Na sasa zina thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 1, Trilioni 2 zimeyeya!​

DUH! LAKINI SI NDIO HALI YA UCHUMI ILIVYO? KAMA UCHUMI WA DUNIA UNAPOROMOKA KWANINI UNADHANI CRYPTO ZISINGEPOROMOKA?
Well, Crypto zilibuniwa ili zije kuwa mbadala wa masoko ya fedha ya kawaida. Kwa lugha rahisi, waanzilishi wa Crypto walikuwa wanazipigia debe kama mbadala wa fedha za kawaida ambazo zinasimamiwa na benki kuu za nchi mbali mbali. Kwahiyo, matarajio ni kwamba fedha za kawaida zinapoporomoka - kimbilio liwe ni crypto, ila ndo kama hivyo hali imekuwa tofauti.​

MH! SIJAELEWA BADO - FAFANUA ZAIDI.
Ok, twende kwenye Historia kidogo: Asili ya crypto ni kipindi kifupi kilichofuatia baada ya anguko la uchumi wa dunia la mwaka 2008. Katika anguko lile tulishuhudia kifo cha moja ya benki kubwa duniani iliyofahamika kama Lehman Brothers ambayo imekuwepo duniani kwa miaka 158! Ulikuwa ni msiba mkubwa.

Tuhamie kwenye uchumi; Mabenki wakati huo yalifanya ujinga ambao watu hatutarajii wasomi wa benki waufanye kwa kutumia pesa zetu ambazo tunawapelekea watutunzie. Mabenki yaliwakopesha sana watu ambao hawastahili kukopeshwa, mabenki yalikuwa yamelegeza vigezo vya kukopa, na ni kwasababu benki kuu zilikuwa zimepunguza riba; mfano - Marekani ilipunguza riba kutoka 6.5% mwaka 2000 mpaka 1% mwaka 2003%.

Kumbuka; lengo la benki kuu kupunguza riba ni kufanya pesa iwe rahisi kupatikana mitaani. Kwahiyo watu wakakopa sana kwasababu riba ni ndogo, wengine wakachukua nyumba za mikopo n.k.

Ili kuchochea moto zaidi, Marekani ikapunguza hitaji la kiwango cha chini cha mtaji ambacho benki zinatakiwa kuwa nacho kwa benki tano kubwa za Marekani. Lengo lilikuwa ni kuwafanya wachukue "risk" zaidi ya kuwakopesha raia. Matokeo yake hizi benki zika-leverage mitaji yake kwa zaidi ya mara 30 hadi 40. Maana yake benki nazo zilikopa kwa zaidi ya 30 ya uwezo wake ili nazo zikopeshe!

Waneni husema hakuna hali ya kudumu; eventually Federal Reserve ya Marekani ikaanza kupandisha riba mwaka 2004 ambapo ilipanda mpaka asilimia 5.25 iliyodumu mpaka mwaka 2007. Mdogo mdogo mabenki yakajikuta yana orodha ndefu za wadaiwa sugu ambao hawana uwezo wa kurejesha mikopo kwasababu walikopa wakati riba iko chini sana, na sasa wanatakiwa kulipa wakati riba iko juu sana. Vivyo hivyo wale waliokopa nyumba, ikawa ni mtihani mzito kwenye kuzilipia - na kuuza ikawa haiwezekani kwasababu zikawa zinaporomoka thamani yake siku hadi siku.

Ndiposa Benki ya Uswisi ikawa ya kwanza kutangaza hasara ya Dola za Kimarekani Bilioni 3.4 kutokana na 'mikopo ya kimchongo'. Benki kuu mbalimbali duniani zikajaribu kuokoa jahazi kwa kumwaga mihela kwenye mabenki ili ziingie mtaani, lakini kama wasemavyo "La kuvunda halina ubani". Mabenki yakawa yanashindwa kukadiria kiasi cha hasara ambacho watapata kutokana mikopo mingi ya kimchongo waliyonayo.

Februari 2008 Serikali ya Uingereza ikalazimika kuitaifisha benki ya Northen Rock. Machi 2008 moja ya Benki kubwa ya uwekezaji duniani iitwayo Bear Stearns ambayo ilikuwa ni mhimili wa Wall Street kuanzia mwaka 1923 nayo ikatangaza kufilisika, ambapo ikanunuliwa na benki ya JP Morgan Chase kwa thumni za dola! Ikafuata IndyMac Bank nayo ikafariki, na ndiposa hatimae mwezi Septemba 2008, baba lao mwenyewe - Lehman Brothers ikaaga dunia.​

ENHE, KWAHIYO? HAYO YANAHUSIANA VIPI NA KUANZISHWA KWA CRYPTO?
Anguko la uchumi la mwaka 2008 liliwaumiza wananchi wengi wa kawaida (Rudia tena kusoma neno "Wananchi wengi wa kawaida"). Wengi walipoteza ajira zao, wengi walipoteza nyumba zao, na wengi walipoteza akiba zao. Hasira ziliwapanda wananchi hawa wa kawaida kwasababu, baada ya 2008 benki nyingi ziliweza kusimama tena kwa kupata pesa kutoka serikalini (Kodi za wananchi). Kwahiyo kwa wengi ilionekana si sahihi kwa serikali kuwapa pesa za walipa kodi watu ambao walizichezea pesa za wavuja jasho.

Japo kwa ujumla kitendo cha serikali kuingilia kati kwa kutoa pesa kwa mabenki kilisaidia kuurudisha uchumi mahali pake, lakini kwenye akili za raia wengi ilionekana ni kama serikali ilikuwa inawazawadia watu wa benki badala ya kuwaadhibu.

Kwa lugha nyepesi, yaliyotokea yalionesha udhaifu wa mfumo wa kawaida kibenki. Hapo ndipo watu wakaanza kufikiria kuanzia mfumo ambao utakuwa ni mbadala wa mfumo huu mbovu uliopo.​

OK, KWAHIYO HAPO NDIPO TUKASIKIA BITCOIN IMEVUMBULIWA SI NDIO?
Yap! Bitcoin kama Crypto iliingia kama sarafu ambayo hakuna wa kuidhibiti. Ni pesa mtandao, sarafu ya kidijitali ambayo kila muamala wake unarekodiwa katika Kitabu cha kimtandao cha kumbukumbu kinachofahamika kama "Blockchain". Vijana wengi wakaipokea Bitcoin kwa mikono na miguu yote, wakaingia wazima wazima kwasababu walikuwa wamechoshwa na sarakasi zinazofanywa na mabenki na serikali.

Kwa lugha rahisi; Bitcoin ilionekana ni pesa inayomlinda mtu dhidi ya Serikali. Serikali inaweza kuzisimamia na kuzidhibiti pesa zako zilizopo benki - mfano inaweza kuzuia usizitoe, inaweza kuongeza tozo, inaweza kuongeza riba, inaweza kupunguza riba, inaweza kuzibadilisha, na inaweza ikafanya maamuzi ambayo yanaathiri thamani yake. Lakini hakuna kitu serikali inaweza fanya kwenye Bitcoin, na sarafu mtandao zingine.

Kwahiyo, maono ya waanzilishi wa Crypto ni kuwa na jamii ambayo watu wanaweza kufanya miamala kwa kutumiana pesa, kununua na kuuziana vitu pasipo kuingiliwa na kuitegemea mamlaka ya serikali yoyote ile au taasisi binafsi yoyote ile duniani.​

AISEE! SASA NDOTO HIYO ILITIMIA?
Mwanzoni mambo yalienda vizuri kabisa. Watu walidumbukiza kiasi kikubwa cha pesa kwenye crypto. Lakini usisahau kuwa, watu wa mwanzo kabisa kuikimbilia Bitcoin kwa wingi walikuwa ni wahalifu.

Kulikuwa na soko mtandaoni linaitwa Silk Road ambalo kwa asilimia kubwa lilikuwa linategemea crypto. Mtu alikuwa ananunua madawa ya kulevya kule Silk Road, halafu mzigo unamfikia mpaka mlangoni kwake na yeye analipia kwa Bitcoin. Ukawa ni mfumo ambao watu wanauamini na kuutumia kwa malipo ya biashara haramu.

Ilikuwa ni njia rahisi na ya haraka ya kutuma pesa umbali mrefu mfano kutoka nchi moja kwenda nyingine, bara moja kwenda jingine n.k, ikarahisisha namna ya ku-track miamala, na ikaweza ku-maintain thamani.

Lakini kuna watu hawakuipenda taswira hii ya Crypto na uhalifu, walitaka kuionesha dunia kuwa crypto inaweza kusafishwa na kuwa njia mbadala ya malipo na ikatumiwa na kila mmoja duniani pasipo kuhusisha uhalifu.​

NIMEKUPATA, SASA CRYPTO ILIWEZA KUPENYA NA KUKUBALIKA NA WATU WENGI NJE YA WAUZA UNGA?
Wajasirimali. Kwa kutumia mbinu za kimauzo ikiwemo mbinu ya kupandikiza kitu kinachoitwa FOMO (Fear Of Missing Out), wajasiriamali wengi waliibeba agenda ya Crypto kama fursa ya kiuwekezaji. Wakawashawishi watu kuwa Crypto itakuja kuziondoa pesa za kawaida. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja tena ya kuwa na Shilingi, au Dola, au Paundi, Au Euro n.k. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja ya kuwa na mabenki kwasababu watu watakuwa wanamalizana wao kwa wao bila kuwa na haja ya uwepo wa Serikali au "Mtu kati".

Mdogo mdogo watu wakaanza kuelewa somo, uhitaji wa Bitcoin ukaanza kuongezeka. Bitcoin ikaanza kupanda thamani kwasababu wanaoihitaji wakawa wengi. Kampuni mbalimbali zikaibuka kwaajili ya kutumia fursa zitokanazo na Bitcoin. Kwa kuona mafanikio ya Bitcoin, Crypto zingine zikaanza kuibuliwa pia. Zingine zilipata umaarufu kimasihara tu mfano Dogecoin!​

NOMA SANA, NASIKIA WATU WANASEMA MLIPUKO WA KORONA ULIWEZESHA THAMANI YA CRYPTO KUPANDA, NI KWELI?
Ni kweli. Kila baada ya kipindi fulani Dunia huwa inashuhudia jambo linaibuka, linafikia kilele cha umaarufu, kisha linaporomoka ghafla na pengine linapotea kabisa. Kisha linaibuka jingine linaenda mzunguko uleule - wenyewe wanaita "Boom and bust cycles".

Hakuna watu wanaweza kumshukuru "aliyetengeneza" kirusi cha Korona kama watu wa Crypto. Maana Korona ilipelekea marufuku za watu kuzurura mitaani, kwenda makazini, kusafiri n.k. Hali hiyo ilipelekea watu kutumia muda mwingi wakiwa wamejifungia ndani. Lakini maisha ilikuwa ni lazima yaendelee; miamala ilikuwa ni lazima ifanyike. Na njia rahisi ilikuwa ni kulipa kwa njia ya mtandao. Hapo ndipo tukashuhudia crypto zikipanda thamani kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa kabla.

Watu wengi walijikuta wako majumbani, na hivyo muda mwingi walikuwa wanautumia mitandaoni. Hata manunuzi yakawa yanafanyika mtandaoni. Na kuna baadhi ya nchi raia walikuwa wanalipwa pesa kiasi kwaajili ya kujishikiza - maana yake watu wakaanza kupata pesa ambazo hawajazitolea jasho. Na kwakuwa watu walikuwa na pesa zisizo na jasho wakaanza kuzitumia hata kwa vitu "risky" kama vile kuwekeza kwenye crypto. Na tukaanza kushuhudia mtu anawekeza Dola 10 anapata Dola 100. Mtu anaweka TZS 500,000/= inapanda mpaka milioni kadhaa ndani ya muda mfupi. Tazama Bei ya Bitcoin ilivyoongezeka miezi mitatu tangu WHO walipotangaza kuwa COVID-19 ni Pandemic (Mwaka 2020).

View attachment 2473358

Hapa ndipo makampuni kibao yakaibuka. Na mengi yalikuwa yanahimiza watu kuwekeza kwenye crypto. Ilikuwa kila kona unakutana na matangazo ya Crypto. Watu maarufu duniani wakaanza kuwa ma-influencers wa Crypto. Kuna uwanja unaitwa Staples Center ambao unatumiwa na timu maarufu ya mpira wa kikapu ya LA Lakers nchini Marekani - ulibadilishwa jina na sasa unaitwa Crypto.com Arena.

Kuna tangazo moja linamhusisha muigizaji maarufu wa Marekani aitwaye Matt Damon; HILI HAPA kwenye hilo tangazo (La Crypto) anatoa ujumbe rahisi tu lakini ni mzito, kwamba "Fortune Favors The Brave." Matangazo ya hivi yalikuwa mengi sana.

Haya matangazo na hawa influencers walichokuwa wanajaribu kuwaambia watu ni kwamba; "Wekezeni kwenye crypto kabla hamjachelewa, mkiikosa hii nafasi leo mtakuja kuijutia kesho." Na karibu matangazo yote ya Crypto yanaegemea kwenye kitu kimoja - FOMO. Kwamba usiponunua crypto leo basi wewe ni mjinga, wewe hujielewi, wewe unapitwa na wakati, wewe ni mshamba, wewe ni muoga, na message zingine kama hizo.

Hii "hype" ya wakati wa pandemic ndio ilikuwa "Golden era" ya crypto. Watu wengi hawakutaka kupitwa kama ambavyo matangazo yanawashawishi. Hapa ndipo Crypto ikaingia "mainstream", ikawa habari kubwa duniani. Kila mtu akawa ni "mtaalamu" wa crypto, unapita kijiweni pale Njombe kwetu unakuta bodaboda wanaongelea biashara ya "Kucheza Bitcoin" na ikaambatana na biashara ya "Kucheza FOREX" na ikaambatana na biashara ya "Kuweka mikeka"

TUKO PAMOJA, NINI KIKAFUATA?
Well, nimeongelea mara kadhaa kuwa kampuni nyingi ziliibuka wakati huo wa pandemic. Ambacho sijasema ni kuwa hizi kampuni hazikuwa zinatengeneza crypto mpya, bali nyingi ziliingia kwaajili ya kuwawezesha watu ku-fanya miamala ya crypto. Chukulia mfano wa Benki; benki hazitengenezi pesa, bali zinawawezesha watu kutunza na kufanya miamala ya pesa.​

Kwahiyo, kampuni nyingi zilizoibuka zilikuwa ni kama "Crypto Banks".

HEH!?! BENKI TENA? MIMI NILIJUA WATUMIAJI WA CRTPTO WANAZICHUKIA BENKI? INAKUWAJE KUNAKUWA NA "BENKI" ZA CRYPTO?
Kwakweli hata mimi nashindwa kushangaa; ni ajabu na kweli. Lakini ninachojua hizi kampuni hazijiiti benki. Na wala hazisimamiwi kama benki. Lakini kiuhalisia zinafanya kazi kama benki (Rudia tena kusoma). Unaweka crypto yako, unaiacha kwa muda fulani - inazalisha faida vile vile kama ambavyo ukiweka pesa benki kwenye "savings account" zinazalisha faida.​

Nitatoa mfano mmoja: Kuna kampuni inaitwa Celsius ambayo ilikuwa inajinadi kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 1.5

View attachment 2473475

Hii kampuni ilianzishwa na mtu anaitwa Alex Mashinsky. Huyu mchizi ana historia ya utapeli-tapeli, anaongea sana na muongo muongo - ila ana nguvu ya ushawishi (Very charismatic). Kwahiyo, baada ya kupiga utapeli kwenye biashara zingine huko - akakutana na Crypto, akavutiwa na fursa zake, akaanzisha kampuni.​

ALIWEZAJE KUWASHAWISHI WATEJA?
Ni rahisi tu; alikomaa na pointi moja kwamba "Benki za kawaida zinawadanganya watu na kuwaibia pesa zao!". Hiyo ndio ilikuwa "Selling point" yake. Kwamba, "Sikieni nyie watu; Mfano una hela zako, unazipeleka benki, benki wao wakishazipokea wanazikopesha mikopo ambayo ina riba mpaka asilimia 25%, wakati huo wewe wanakupa chini ya asilimia 1% (Kwa akaunti ya kawaida). Hilo ni tatizo, kwasababu imefika mahali tunaona ni sawa na tunaendelea kuwapa pesa zetu na wao wanaendelea kutajirika wakati sisi maisha yetu yanabaki vile vile."

Baada ya kuwagonga watu na hiyo pitch, then anawaambia kuwa Celsius itafanya kinyume chake; Itachukua crypto zako, itawekeza na kuzalisha faida kubwa, kisha asilimia kubwa ya faida utachukua wewe! Kwahiyo, Celsius inakuwezesha wewe kutumia pesa zako kutengeneza pesa kirahisi kabisa!

Jamaa alikuwa anaweka videos YouTube kila wiki kama dozi. Akawa ana-tweet kinoma. Na kwasababu wakati huo watu wengi walikuwa majumbani, wameshiba, wananenepeana tu, ujumbe ukawa unawafikia barabara kabisa. Boom, wateja wakaanza kuzipeleka crypto zao Celsius. Jamaa alikuwa anahubiri injili ya Crypto kisawasawa na ikawa inawaingia watu; na watu wanaokoka kwenda kwenye Crypto kupitia Celsius kutoka benki za kawaida

KWANI FAIDA ILIKUWA NI KIASI GANI UKIWEKEZA CELSIUS?
Kama ilivyokuwa kwa crypto banks nyingi, ilikuwa ni 18%. Hii haikuhitaji kufikiria mara mbili, hakuna benki itakupa riba ya asilimia 18% kwenye akaunti ya kawaida. Na kumbuka; hii haikuwa kama hisa au cryptocurrency zenyewe ambazo unanunua ukiwa na matumaini kuwa thamani yake itapanda (Japo moyoni una uhakika itashuka ), hawa Celsius walichokuwa wanakifanya ni hivi;

Wewe unaweka crypto yako kwa kuanzia kama mtaji. Kisha baada ya hapo inakuwa ni mwendo wa kupokea 18%, huwazi suala la thamani kushuka wala nini. Inakuwa kama umepanda crypto hivi, baada ya hapo ni mwendo wa kuzivuna

Na amini usiamini, wajinga duniani hawatokuja kuisha. Watu hawakuona kuwa huu ni utapeli, bali wengi waliamini hizi ni "Hela za bure" zinazotolewa na Celsius... asalaleee!!!🥱​

EBWANAEEEE! LAKINI, WAO CELSIUS FAIDA WALIKUWA WANAITENGENEZAJE?
Hakikuwahi kueleweka, lakini kitu kimojawapo ambacho Celsius walikuwa wanakifanya; ni kuchukua pesa (crypto) za wateja, kisha wanazikopesha kwa wawekezaji wakubwa na wafanyabiashara professional, na wale wawekezaji walikuwa wanakopa kwa riba, kwahiyo wakilipa na wao Celsius wanazisukuma kwenda kwa mteja.

Namba zinagoma eh?!? Ni kweli, haiingii akilini kuwa kwa kufanya hivyo aliweza kuwahudumia wateja wote hawa zaidi ya 1.5M. Kuna mengi ambayo hatuyajui yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia.​

MH! HAKUKUWA NA WAKOSOAJI? HAKUKUWA NA WATU WA KUUANIKA HUU UTAPELI?
Walikuwepo; wanauchumi, wataalamu wa masuala ya kibenki na masoko ya mitaji n.k. Walijitahidi kwakweli kuwaelimisha watu kuwa hakuna pesa za rahisi namna hiyo katika mifumo ya kifedha. Wengi walikuwa wanawatahadharisha watu kuwa hii ni "Ponzi Sheme"

Kitu kingine kilichokuwa kinaleta hofu zaidi kwa wataalamu wa uchumi ni kwamba; Akiba ambazo watu huwa tunaweka benki huwa zinakatiwa bima, lakini kwa Celsius - akiba za watu hazikuwa na bima yoyote! Lakini kwa namna moja ama nyingine, ni vigumu sana kumshawishi mtu anaekaribia kutapeliwa kuwa atatapeliwa; huwa ni wabishi kinoma!​

SASA, IKAWAJE? CELSIUS IKAISHIAJE?
Uchumi wa dunia ukaanza kuyumba yumba, Urusi ikaivamia Ukraine, mataifa bado yalikuwa yana "hangover" ya Korona, mifumo ya ugavi ikaathirika kwa kiwango kikubwa. Benki kuu zikaanza kuongeza riba, na hiyo inamaanisha mtelezo wa kwenda juu ukawa umeishia hapo. Hisa zikaanza kuporomoka bei, na vivyo hivyo crypto nazo zikaanza kuporomoka. Ghafla watu wengi wakaacha kuziamini crypto hivyo wakaanza kuzitoa (Ku-withdraw). Bei za crypto zikawa zinashuka kama mwewe - zimetanguliza kichwa.

Hata coin inayoitwa Terra USD ambayo ilibuniwa kwa namna ambayo thamani yake inaenda sambamba na thamani ya dola, kwenye ule mporomoko nayo haikuachwa salama.

Ikawa kama muvi la kutisha vile; ghafla project nyingi za crypto zikaanza kuanguka. Wazungu wanaita "Domino effect" - kikianguka kimoja kinasababisha vingine vingi vianguke. Mabilioni ya dola yakageuka moshi ndani ya siku chache.

Kwahiyo, hata wateja wa Celsius wakawa wanataka kutoa pesa zao + riba ambayo wamejikusanyia kwa kipindi chote ambayo walikuwa hawajaichukua. Kikatokea kitu ambacho mabenki huwa yanakiogopa - "Bank run". Bank run ni pale ambapo wateja wengi wanataka kutoa pesa zao kutoka benki kwa mara moja. Mara nyingi huwa inakuwa ni dhahama kubwa kwasababu uwezekano wa kuwepo pesa za kutosha watu wote kutoa unakuwa ni mdogo sana, kiasi ambacho benki inalazimika kusitisha miamala.

Celsius ikasitisha miamala . Hiyo ilikuwa ni mwezi wa sita. Na kuna utani mtaani kuwa, kwenye ulimwengu wa crypto ukisikia wametangaza kuwa wamezuia kufanya miamala kwa muda basi ujue ndo mazishi hayo. Ni nadra sana kwenye crypto wakasitisha miamala kisha wakaruhusu baada ya muda, sikumbuki kama imewahi kutokea.

Tangazo la Celsius za kusitisha miamala likazidi kuutikisa ulimwengu wa crypto. Bei zikazidi kushuka kwa kasi ya 6G. Wiki chache baadae Celsius ikatangaza kuwa imefilisika. Watu wakabaki njia panda - crypto zao watapa au hawazipata tena? Well, mpaka leo haijulikani ni nini kitatokea.​

PHEW! KWAHIYO SASA INAKUWAJE; KWANI INA MAANA WATU HAWAKUJUA KUWA CRYPTO NI KAMA KAMARI?
Watu wengi waliowekeza kwenye crypto kwa ushawishi wa ma-influenza na matangazo na mwisho wa siku wakapoteza pesa zao - huwa wanajihisi wametapeliwa. Kwamba wakati wanawekeza huwa wanaahidiwa usalama wa pesa zao, na uhakika wa faida. Wengi wamepoteza akiba zao za maisha, wengine wamepoteza mitaji yao ambayo waliiwekeza wakitumaini itakua mikubwa ili wawekeze zaidi n.k. Na kuonesha hali ilivyo mbaya, wapo wengi waliojinyonga kwasababu ya kupoteza pesa katika uwekezaji wa crypto.

Wengi wanawalaumu watu maarufu kwa kutumika vibaya kuwashawishi watu kuingia kwenye biashara ambazo mwisho wake huwaumiza watu wa hali ya chini.​

ENHE, ULISEMA CRYPTO KUNA AHADI HAIJATIMIZA - NI AHADI IPI HIYO?
Crypto ilidizainiwa kuwa mbadala wa mifumo ya kibenki; mifumo ambayo kuna "mtu" anasimamia na kufanya maamuzi juu ya pesa za watu. Nimeeleza kilichotokea kabla ya anguko la uchumi la 2008. Maamuzi mabovu ya watu wa benki yalipelekea watu kupoteza pesa zao. Crypto ilitengenezwa ili hilo lisitokee tena, lakini kama ulivyoona, yanatokea yale yale ambayo watu wa crypto walikuwa wanayakwepa.

Kwahiyo; ahadi ambayo haijatimia ni ahadi ya crypto kuwa mbadala wa pesa za kawaida ambazo zinazimamiwa na serikali na kuratibiwa na mabenki na taasisi za fedha kwa sheria na kanuni mbalimbali. Mijadala inaendelea kuhusu kama kweli crypto itaweza kuleta suluhisho la mapungufu yaliyopo katika mifumo ya kibenki. Kuna watu wanaona cryto ni utapeli tu na ni suala la muda kabla haijapotea kabisa, na kuna watu wanaona crypto ndio pesa ijayo. Inawezekana wote wapo sahihi, acha tuendelee kuishi.​

SO, CRYPTO IMEKUFA AU?
Ni mapema sana kulisema hilo. Ni kweli crypto imepoteza thamani kubwa, lakini bado kuna watu wanaendelea kuwekeza. Na sio kampuni zote za crypto zimekufa, kuna zingine bado zinaendelea kuwahudumia wateja mpaka sasa tunavoongea.

Kuna watu wapo katika ulimwengu wa crypto sio kwaajili ya faida au hasara; wao wanavutiwa na namna crypto ilivyoundwa na inavyofanya kazi. Na wanatumia teknolojia ambayo ni msingi wa crypto kuleta mapinduzi mengine ya teknolojia.

Na kama ambavyo wakati intaneti inaingia, kampuni nyingi zilikufa - lakini zile chache zilizopenya zimekuwa ni kampuni kubwa sana duniani hivi sana. Inaweza kutokea hivyo hata kwenye crypto. Yote kwa yote crypto haionekani kuwa ni kitu kinachoweza kupotea ghafla, bado tunayo sana; na baadhi yetu tuna shauku ya kujua ni nini kitafuata baada ya hapa.

Kama ni shabiki wa masuala ya crypto unaweza pia kufuatilia kilichotokea kwa kampuni ya Quadriga CX na FTX.​

Naweka kipaza sauti chini.

Mimi... ninashukuru.
Umeongea madini mazuri .mimi najihusisha na crypto ila kuna baadhi ya vitu ninejifunza hapa .uko vizuri sana umechambua vizuri sana Big up
 
Asante sana mkuu!
 
Jamaa anonymous hatokaa ajulikane kabisa, kajikusanyia Bitcoin zake zenye thaman ya Dollar million 1 alafu katulia hazitoi wala haongezi

Anaejulikana ni mtu wa kwanza kufanya nae transaction ila yeye hajulikani,
We ana biticoin milion moja zenye thamani ya dola tilioni 48.
Huenda labfa jamaa alikufa kama yuko alive kwanini huwa hazimove
 
crypto imegeuka kuwa ponzi aka Jatu au desi kwa sasa.

kupelekea watu kuunda coin na kuipaisha haraka ili wavune na kukimbia.

fanyia malipa tu kama coin usdt hayo mengine utakuja kuchanganyikiwa.
 
Just imagine, unaweka ela yako kwa mtu ambaye humjui/taasisi ambayo huijui(crypto), ambapo siku wakiamua kuzima data na kupotea. Hujui utawapata wapi. Hawa crypto ni sawa na mjasiliamali mmoja ivi, ana ela zake, sasa anataka kuzizungusha.. Ngoja nikupe kisa hiki kama hujawai kukisikia.

Jamaa ana mtaji wa kama 50M, anaanzisha biashara ya kuuza na kununua Paka( hawa paka ndio bidhaa, unaweza ukaiita crypto), huyu jamaa akaja tanzania (au ndio tuite duniani), akatangaza kuwa ananunua paka. Paka mmoja ananunua kwa elfu 20, na anahitaji jumla ya paka 500, hivyo watu wakaingia mtaani kusaka paka, wakatimia 500, wakapeleka kuuza, wakapata jumla tsh. 10M. Huyu jamaa akawakusanya hao paka kwenye yadi yake mahali, akawaficha huko. Baada ya wiki kadhaa, akatoa tangazo tena, akasema ananunua paka kwa shilling elfu 30 awamu hii.. Anahitaji paka 500, watanzania wakafurahi sanaaaa wakanogewa na biashara hii bila hata kuhoji.. Chezea ela wewe!. Basi raia wakaingia msituni kusaka paka, wakapatikana hao paka 500, jamaa akawapa ela yao 15M, kumbuka kwenye mtaji wake wa 50M, amebakiwa na 25M. Baada ya muda akatangaza kwa mara ya 3, anahitaji paka 500, atanunua kila paka kwa shillingi elfu 50, Dah safari hii wananchi wakasaka kweli kweli paka, kwa sababu walikuwa wanakaribia kuisha nchini.. Ila bahati nzuri, wakafanikiwa kupata hao 500. Jamaa akawachukua akatoa millioni yao 25M.
Kwaio Jamaa akawa amefanikiwa kukusanya jumla ya paka wapatao 1500, kwa kutoa kitita cha shillingi 50Mil.
Sasa huyu jamaa, akafungua kampuni kwa jina lingine kabisa, ili watu wasijue kama ni yeye, akawaweka paka wote (1500) kwenye hiyo kampuni,, kampuni ikatangaza kuwa inauza paka. Paka mmoja ni tsh elfu 60.

Baada ya siku kadhaa kupita, yule jamaa akatangaza kununua paka tena, (kumbuka yeye anatangaza kununua kwa wananchi tuu, na sio kutoka kampuni yoyote au taasisi, akidai lengo ni kuwawezesha wananchi), na sharti ni lazima paka wakusanywe watimie idadi anayoitaka ndio anatoa mpunga..
Akatangaza safari hii kununua paka 1500, kwa kila paka ananunua kwa elfu 80.
Wananchi wakazama msituni, wakakuta paka wameisha, ikabidi waende kwenye kampuni ile inayouza paka kwa elfu 60, wakijua kuwa watanunua hao paka kwa elfu 60, alafu wao watauza kwa elfu 80 na kupata faida ya elfu 20.

Basi, wakaenda kununua wale paka wote 1500 ambapo kwa kila paka ni elfu 60, (kwaio ile kampuni iliuza wale paka wote na kupata pato la shillingi 90Millions.
Kilichotokea sasa, kUMBUKA ILE KAMPUNI NI YA YULE YULE JAMAA ANAENUNUA PAKA.. so,baada ya kuhakimisha ameuza paka wotee na kupata millioni 90, akafunga kampuni AKATOWEKA, Wananchi wana paka mkononi, wanaenda kumuuzia mnunua paka HAYUPO, KATOWEKA. wanarudi kwenye kampuni,, HAIPO IMETOWEKA..

SO, WANANCHI WAKABAKIA NA MA PAKA YAO(bitcoins), kama urembo, wasishindwe kupata fedha...

Naomba kuwasilisha
 
Huu mfano naujua. Sina uhakika kama practically unawezekana, lakini mantiki yake naielewa.

Lakini huu mfano hau-apply kwa Bitcoin yenyewe kama Crypto, bali unaweza ku-apply kwa "Crypto Banks" au "Crypto Exchanges". Hizi Crypto exchanges zinamilikiwa na kusimamiwa na watu, lakini crypto yenyewe kama Bitcoin hakuna anaeimiliki - kwa kiingereza tunasema ni de-centralized.

Hata huyu anaeitwa Satoshi Nakamoto yeye ni Mvumbuzi wa Bitcoin, lakini sio mmiliki wa Bitcoin wala hawezi "Kui-control" Bitcoin. Na sio Satoshi Nakamoto tu, bali hakuna mtu yeyote, wala serikali yoyote, wala taasisi inayoweza kumiliki na ku-control crypto.

Satoshi sio wa kwanza kuja na concept ya Crypto, bali yeye alisaidia kutatua changamoto ambayo watangulizi wake walishindwa kuitatua, ambayo hiyo ndio imefanikisha kulifanya wazo la Crypto liwe viable. Ni kweli, waleti yake ina 5% ya Bitcoin zote - ila hajawahi kuzitoa wala kufanya muamala wowote tangu mwaka 2009. Mara ya mwisho alituma ujumbe kuwa "Nimeingia kwenye mambo mengine" mwaka 2010, tangu hapo hajasikika tena na wala waleti yake haijawahi kufanya muamala wowote.

Kwahiyo, crypto hazina wamiliki na haiwezekani kuzimiliki, bali zina waanzilishi. Makampuni mengi yanayowatapeli watu yanatumia utapeli ule ule ambao unatumika kutapeli pesa za kawaida; mfano hii kampuni niliyoielezea kwenye uzi - Celsius, na nyingine inaitwa Quadriga CX, na nyingine inaitwa FTX.

BOTTOM LINE
Shida sio crypto, shida ni kampuni zinazofanya biashara ya kutunza, na kufanikisha miamala ya crypto.
 
NB: Uzi ni mrefu, kinoma 👽

Uchumi wa dunia umekuwa ukidorora kwa miezi (Kama sio kwa miaka) kadhaa sasa, na mdororo huo umeathiri pia thamani ya cryptocurrencies kwa kiwango cha kutisha. Watu wamepoteza mabilioni ndani ya muda mfupi, kiasi ambacho wengine wamechukua maamuzi magumu ya kujiondoa duniani kwasababu walichotarajia, hakikutimia.

Hii imezua maswali juu ya ahadi iliyotolewa na wavumbuzi + chawa wa Crypto - kwamba sarafu za Crypto ni pesa ambazo ziko nje ya mifumo ya kawaida ya kibenki, kwahiyo ni salama na "stable" zaidi kwasababu hakuna mtu, wala kampuni, wala mamlaka ya serikali inayoweza kuzi-control. Lakini, uhalisia unaonesha crypto imeanza kwenda kwa kutumia mifumo ile ile ya kawaida ya kibenki ambayo waanzilishi na mashabiki kindakindaki wa crypto walikuwa wanaikwepa.

Nimeona si vibaya nikaweka uzi wangu juu ya kinachoendelea katika ulimwengu wa crypto. Asomaye na afahamu; Mimi pia ni mtumiaji wa crypto, huku niliko tunaendesha programu ambayo kwa 95% pesa zake zipo katika crypto na mpaka sasa tumeshafanya miamala ya zaidi ya TZS 25M. Lakini uamuzi wangu wa kuleta uzi huu ni kutokana na kwamba sijaona mtu alieiongelea crypto kama ambavyo nitafanya hapa. Karibu!​

KWANI, HALI YA CRYPTO IKOJE KWA SASA?
Mpaka Disemba 2022, crypto zilikuwa zimepoteza wastani wa asilimia 60 ya thamani zake. Hizi hapa chini ni crypto maarufu zaidi duniani, acha zitusaidie kupata uelewa wa pamoja wa hali ilivyo kwa sasa;​
  1. Terra: Imepoteza asilimia 100% ya thamani yake.
  2. Solana: Imepoteza asilimia 93% ya thamani yake.
  3. AMP: Imepoteza asilimia 93%
  4. Cardano: imepoteza asilimia 80%
  5. Ether: Imepoteza asilimia 67%
  6. Bitcoin: Imepoteza asilimia 63%
  7. Dogecoin: Imepoteza asilimia 55%
Kwa pamoja hizi crypto zote unazozisikia, katika ubora wake zilikuwa na thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Trilioni 3. Na sasa zina thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 1 kwa ujumla, maana yake kuna Trilioni 2 zimeyeya!​

DUH! LAKINI SI NDIO HALI YA UCHUMI ILIVYO? KAMA UCHUMI WA DUNIA UNAPOROMOKA KWANINI UNADHANI CRYPTO ZISINGEPOROMOKA?
Well, Crypto zilibuniwa ili zije kuwa mbadala wa masoko ya fedha ya kawaida. Waanzilishi wa Crypto walikuwa wanazipigia debe kama mbadala wa fedha za kawaida ambazo zinasimamiwa na benki kuu za nchi mbali mbali. Kwahiyo, matarajio ni kwamba fedha za kawaida zinapoporomoka kimbilio liwe ni crypto, ila ndo kama hivyo hali imekuwa tofauti.​

MH! SIJAELEWA BADO - FAFANUA ZAIDI.
Ok, twende kwenye Historia kidogo: Asili ya crypto ni kipindi kifupi kilichofuatia baada ya anguko la uchumi wa dunia la mwaka 2008. Katika anguko lile tulishuhudia kifo cha moja ya benki kubwa duniani iliyofahamika kama Lehman Brothers ambayo imekuwepo duniani kwa miaka 158! Ulikuwa ni msiba mkubwa.

Mabenki wakati huo yalifanya ujinga ambao watu hatutarajii wasomi wa benki waufanye kwa kutumia pesa zetu ambazo tunawapelekea watutunzie. Mabenki yaliwakopesha sana watu ambao hawastahili kukopeshwa, mabenki yalikuwa yamelegeza vigezo vya kukopa, ili raia wakope sana. Ilitokea hivyo kwasababu benki kuu zilikuwa zimepunguza riba; mfano - Marekani ilipunguza riba kutoka 6.5% mwaka 2000 mpaka 1% mwaka 2003%.

Ukiona Benki Kuu ya nchi yoyote inatangaza kupunguza riba ujue lengo ni kuifanya pesa iwe rahisi kupatikana kwa raia wa kawaida, hali ambayo ina-boost uchumi uliosinyaa. Kwahiyo watu wakakopa sana kwasababu riba ni ndogo, wengine wakachukua nyumba za mikopo, watu wakanunua magari kwa wingi n.k.

Ili kuchochea moto zaidi, Federal Reserve ya Marekani ikapunguza hitaji la kiwango cha chini cha mtaji ambacho benki zinatakiwa kuwa nacho (Kwa benki tano kubwa za Marekani). Lengo lilikuwa ni kuzihamasisha hizi benki zichukue "risk" zaidi ya kuwakopesha raia. Matokeo yake hizi benki zika-leverage mitaji yake kwa zaidi ya mara 30 hadi 40. Maana yake benki nazo zilikopa kwa zaidi ya 30 ya uwezo wake ili nazo zikopeshe!

Waneni husema hakuna hali ya kudumu; eventually Federal Reserve ya Marekani ikaanza kupandisha riba mwaka 2004 ambapo ilipanda mpaka asilimia 5.25 iliyodumu mpaka mwaka 2007. Mdogo mdogo mabenki yakajikuta yana orodha ndefu za wadaiwa sugu ambao hawana uwezo wa kurejesha mikopo kwasababu walikopa wakati riba iko chini sana, na sasa wanatakiwa kulipa wakati riba iko juu sana. Vivyo hivyo wale waliokopa nyumba, ikawa ni mtihani mzito kwenye kuzilipia, na kuziuza ikawa haiwezekani kwasababu zilikuwa zinaporomoka thamani yake siku hadi siku (Housing Bubble).

Hatimae Benki ya Uswisi ikawa ya Benki kubwa ya kwanza kutangaza hasara, ambapo ilitangaza kuwa imepata hasara ya Dola za Kimarekani Bilioni 3.4 kutokana na 'mikopo ya kimchongo'. Benki kuu mbalimbali duniani zikajaribu kuokoa jahazi kwa kumwaga pesa kwenye mabenki ili kuzuia mporomoko wa uchumi, lakini kama wasemavyo "La kuvunda halina ubani". Mabenki mengi tayari yalikuwa yamevuka mstari mwekundu; yakawa yanashindwa kukadiria kiasi cha hasara ambacho watapata kutokana mikopo mingi ya kimchongo waliyonayo kwenye hesabu zao.

Februari 2008 Serikali ya Uingereza ikalazimika kuitaifisha benki ya Northen Rock. Machi 2008 moja ya Benki kubwa ya uwekezaji duniani iitwayo Bear Stearns ambayo ilikuwa ni mhimili wa Wall Street kuanzia mwaka 1923 nayo ikatangaza kufilisika, ambapo ikanunuliwa na benki ya JP Morgan Chase kwa thumni za dola! Fahamu kwamba Wall Street ni kama center ya masuala ya uuzaji na ununuzi wa hisa duniani. Ikafuata IndyMac Bank nayo ikafariki, na ndiposa mwezi Septemba 2008, Lehman Brothers ika-rest in pieces.​

ENHE, KWAHIYO? HAYO YANAHUSIANA VIPI NA KUANZISHWA KWA CRYPTO?
Anguko la uchumi la mwaka 2008 liliwaumiza wananchi wengi wa kawaida (Rudia tena kusoma neno "Wananchi wengi wa kawaida"). Wengi walipoteza ajira zao, wengi walipoteza nyumba zao, na wengi walipoteza akiba zao. Hasira ziliwapanda wananchi hawa wa kawaida kwasababu, baada ya 2008 benki nyingi ziliweza kusimama tena kwa kuwa zilipata pesa(Bailout) kutoka serikalini (Ambazo ni kodi za wananchi). Kwa wengi ilionekana si sahihi kwa serikali kuwapa pesa za walipa kodi watu ambao walizichezea pesa za wavuja jasho. Ikaonekana kama Serikali na mabenki lao moja - kuwanyonya wananchi kwaajili ya kujineemesha wao.

Japo kwa ujumla kitendo cha serikali kuingilia kati kwa kutoa pesa kwa mabenki kilisaidia kuurudisha uchumi mahali pake, lakini kwenye akili za raia wengi ilionekana ni kama serikali ilikuwa inawazawadia watu wa benki badala ya kuwaadhibu kwa uzembe uliogharimu uchumi wa dunia.

Anguko la uchumi la 2008 lilionesha udhaifu wa mifumo ya kibenki na Serikali. Hapo ndipo watu wakaanza kufikiria kuanzia mfumo ambao utakuwa ni mbadala wa mfumo huu mbovu uliopo.​

OK, KWAHIYO HAPO NDIPO TUKASIKIA BITCOIN IMEVUMBULIWA SI NDIO?
Yap! Bitcoin kama Crypto ya kwanza kabisa, iliingia kama sarafu ambayo hakuna wa kuidhibiti. Ni pesa mtandao, sarafu ya kidijitali ambayo kila muamala wake unarekodiwa katika Kitabu cha kimtandao cha kumbukumbu kinachofahamika kama "Blockchain". Vijana wengi wakaipokea Bitcoin kwa mikono na miguu yote, wakaingia wazima wazima kwasababu walikuwa wamechoshwa na sarakasi zinazofanywa na mabenki na serikali.

Bitcoin ilionekana ni pesa inayomlinda mtu dhidi ya Serikali. Kivipi? Utaniuliza. Well, Serikali inaweza kuzisimamia na kuzidhibiti pesa zako zilizopo benki - mfano inaweza kuzuia usizitoe, inaweza kuongeza tozo, inaweza kuongeza riba, inaweza kupunguza riba, inaweza kuzibadilisha, na inaweza ikafanya maamuzi ambayo yanaathiri thamani yake. Lakini hakuna kitu serikali inaweza fanya kwenye Bitcoin, na sarafu mtandao zingine.

Kwahiyo, maono ya waanzilishi wa Crypto ni kuwa na jamii ambayo watu wanaweza kufanya miamala kwa kutumiana pesa, kununua na kuuziana vitu wao kwa wao pasipo kuingiliwa na/au kuitegemea mamlaka ya serikali yoyote ile au taasisi binafsi yoyote ile duniani.​

AISEE! SASA NDOTO HIYO ILITIMIA?
Mwanzoni mambo yalienda vizuri kabisa. Lakini usisahau kuwa, watu wa mwanzo kabisa kuikimbilia Bitcoin kwa wingi walikuwa ni wahalifu, hususani wauza madawa ya kulevya.

Kulikuwa na soko mtandaoni linaitwa Silk Road ambalo kwa asilimia kubwa lilikuwa linategemea crypto. Mtu alikuwa ananunua madawa ya kulevya kule Silk Road, halafu mzigo unamfikia mpaka mlangoni kwake na yeye analipia kwa Bitcoin. Ukawa ni mfumo ambao watu wanauamini na kuutumia kwa malipo ya biashara haramu.

Ilikuwa ni njia rahisi na ya haraka ya kutuma pesa umbali mrefu mfano kutoka nchi moja kwenda nyingine, bara moja kwenda jingine n.k, ikarahisisha namna ya ku-track miamala, na ikaweza ku-maintain thamani.

Lakini kuna watu hawakuipenda taswira hii ya Crypto na uhalifu, walitaka kuionesha dunia kuwa crypto inaweza kusafishwa na kuwa njia mbadala ya malipo na ikatumiwa na kila mmoja duniani pasipo kuhusisha uhalifu.​

NIMEKUPATA, SASA CRYPTO ILIWEZAJE KUPENYA NA KUKUBALIKA NA WATU WENGI NJE YA WAUZA UNGA?
Wajasirimali. Kwa kutumia mbinu za kimauzo ikiwemo mbinu ya kupandikiza kitu kinachoitwa FOMO (Fear Of Missing Out), wajasiriamali wengi waliibeba agenda ya Crypto kama fursa ya kiuwekezaji. Wakawashawishi watu kuwa Crypto itakuja kuziondoa pesa za kawaida. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja tena ya kuwa na Shilingi, au Dola, au Paundi, Au Euro n.k. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja ya kuwa na mabenki kwasababu watu watakuwa wanamalizana wao kwa wao bila kuwa na haja ya uwepo wa Serikali au "Mtu kati".

Mdogo mdogo watu wakaanza kuelewa somo, uhitaji wa Bitcoin ukaanza kuongezeka. Bitcoin ikaanza kupanda thamani kwasababu ya demand kubwa. Kampuni mbalimbali zikaibuka kwaajili ya kutumia fursa zitokanazo na Bitcoin. Na kwa kuona mafanikio ya Bitcoin, Crypto zingine zikaanza kuibuliwa pia. Zingine zilipata umaarufu kimasihara tu mfano Dogecoin🐶!​

NOMA SANA, NASIKIA WATU WANASEMA MLIPUKO WA KORONA ULIWEZESHA THAMANI YA CRYPTO KUPANDA, NI KWELI?
Ni kweli. Kila baada ya kipindi fulani Dunia huwa inashuhudia jambo linaibuka, linafikia kilele cha umaarufu, kisha linaporomoka ghafla na pengine linapotea kabisa. Kisha linaibuka jingine linaenda mzunguko uleule - wenyewe wanaita "Boom and bust cycles".

Hakuna watu wanaweza kumshukuru "aliyetengeneza" kirusi cha Korona kama watu wa Crypto. Maana Korona ilipelekea marufuku za watu kuzurura mitaani, kwenda makazini, kusafiri n.k. Hali hiyo ilipelekea watu kutumia muda mwingi wakiwa wamejifungia ndani. Lakini maisha ilikuwa ni lazima yaendelee; miamala ilikuwa ni lazima ifanyike. Na njia rahisi ilikuwa ni kulipa kwa njia ya mtandao. Hapo ndipo tukashuhudia crypto zikipanda thamani kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa kabla.

Watu wengi walijikuta wako majumbani, na hivyo muda mwingi walikuwa wanautumia mitandaoni. Hata manunuzi yakawa yanafanyika mtandaoni. Na kuna baadhi ya nchi raia walikuwa wanalipwa pesa kiasi kwaajili ya kujishikiza - maana yake watu wakaanza kupata pesa ambazo hawajazitolea jasho. Na kwakuwa watu walikuwa na pesa zisizo na jasho wakaanza kuzitumia hata kwa vitu "risky" kama vile kuwekeza kwenye crypto. Na tukaanza kushuhudia mtu anawekeza Dola 10 anapata Dola 100. Mtu anaweka TZS 500,000/= inapanda mpaka milioni kadhaa ndani ya muda mfupi. Tazama Bei ya Bitcoin ilivyoongezeka miezi mitatu tangu WHO walipotangaza kuwa COVID-19 ni Pandemic (Mwaka 2020).

View attachment 2473358

Hapa ndipo makampuni kibao yakaibuka. Na mengi yalikuwa yanahimiza watu kuwekeza kwenye crypto. Ilikuwa kila kona unakutana na matangazo ya Crypto. Watu maarufu duniani wakaanza kuwa ma-influencers wa Crypto. Kuna uwanja unaitwa Staples Center ambao unatumiwa na timu maarufu ya mpira wa kikapu ya LA Lakers nchini Marekani - ulibadilishwa jina na sasa unaitwa Crypto.com Arena.

Kuna tangazo moja linamhusisha muigizaji maarufu wa Marekani aitwaye Matt Damon; HILI HAPA kwenye hilo tangazo (La Crypto) anatoa ujumbe rahisi tu lakini ni mzito, kwamba "Fortune Favors The Brave." Matangazo ya hivi yalikuwa mengi sana.

Haya matangazo na hawa influencers walichokuwa wanajaribu kuwaambia watu ni kwamba; "Wekezeni kwenye crypto kabla hamjachelewa, mkiikosa hii nafasi leo mtakuja kuijutia kesho." Na karibu matangazo yote ya Crypto yanaegemea kwenye kitu kimoja - FOMO. Kwamba usiponunua crypto leo basi wewe ni mjinga, wewe hujielewi, wewe unapitwa na wakati, wewe ni mshamba, wewe ni muoga, na message zingine kama hizo.

Hii "hype" ya wakati wa pandemic ndio ilikuwa "Golden era" ya crypto. Watu wengi hawakutaka kupitwa kama ambavyo matangazo yanawashawishi. Hapa ndipo Crypto ikaingia "mainstream", ikawa habari kubwa duniani. Kila mtu akawa ni "mtaalamu" wa crypto, unapita kijiweni pale Njombe kwetu unakuta bodaboda wanaongelea biashara ya "Kucheza Bitcoin" 😝😆😆 na ikaambatana na biashara ya "Kucheza FOREX" na ikaambatana na biashara ya "Kuweka mikeka" 😎​

TUKO PAMOJA, NINI KIKAFUATA?
Well, nimeongelea mara kadhaa kuwa kampuni nyingi ziliibuka wakati huo wa pandemic. Ambacho sijasema ni kuwa hizi kampuni hazikuwa zinatengeneza crypto mpya, bali nyingi ziliingia kwaajili ya kuwawezesha watu kufanya miamala ya crypto. Chukulia mfano wa Benki; benki hazitengenezi pesa, bali zinawawezesha watu kutunza na kufanya miamala ya pesa.​

Kwahiyo, kampuni nyingi zilizoibuka zilikuwa ni kama "Crypto Banks".

HEH!?! BENKI TENA? MIMI NILIJUA WATUMIAJI WA CRYPTO WANAZICHUKIA BENKI? INAKUWAJE KUNAKUWA NA "BENKI" ZA CRYPTO?🤔
Kwakweli hata mimi nashindwa kushangaa; ni ajabu na kweli. Lakini ninachojua hizi kampuni hazijiiti benki. Na wala hazisimamiwi kama benki. Lakini kiuhalisia zinafanya kazi kama benki 🤓 (Rudia tena kusoma). Unaweka crypto yako, unaiacha kwa muda fulani - inazalisha faida vile vile kama ambavyo ukiweka pesa benki kwenye "savings account" zinazalisha faida.​

Nitatoa mfano mmoja: Kuna kampuni inaitwa Celsius ambayo ilikuwa inajinadi kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 1.5

View attachment 2473475

Hii kampuni ilianzishwa na mtu anaitwa Alex Mashinsky. Huyu mchizi ana historia ya utapeli-tapeli, anaongea sana na muongo muongo - ila ana nguvu ya ushawishi (Very charismatic). Kwahiyo, baada ya kupiga utapeli kwenye biashara zingine huko - akakutana na Crypto, akavutiwa na fursa zake, akaanzisha kampuni.​

ALIWEZAJE KUWASHAWISHI WATEJA?
Ni rahisi tu; alikomaa na pointi moja kwamba "Benki za kawaida zinawadanganya watu na kuwaibia pesa zao!". Hiyo ndio ilikuwa "Selling point" yake. Kwamba, "Sikieni nyie watu; Mfano una hela zako, unazipeleka benki, benki wao wakishazipokea wanazikopesha mikopo ambayo ina riba mpaka asilimia 25%, wakati huo wewe wanakupa chini ya asilimia 1% (Kwa akaunti ya kawaida). Hilo ni tatizo, kwasababu imefika mahali tunaona ni sawa na tunaendelea kuwapa pesa zetu na wao wanaendelea kutajirika wakati sisi maisha yetu yanabaki vile vile."

Baada ya kuwagonga watu na hiyo pitch, then anawaambia kuwa Celsius itafanya kinyume chake; Itachukua crypto zako, itawekeza na kuzalisha faida kubwa, kisha asilimia kubwa ya faida utachukua wewe!🥳 Kwahiyo, Celsius inakuwezesha wewe kutumia pesa zako kutengeneza pesa kirahisi kabisa!

Jamaa alikuwa anaweka videos YouTube kila wiki kama dozi. Akawa ana-tweet kinoma. Na kwasababu wakati huo watu wengi walikuwa majumbani, wameshiba, wananenepeana tu, ujumbe ukawa unawafikia barabara kabisa. Boom, wateja wakaanza kuzipeleka crypto zao Celsius. Jamaa alikuwa anahubiri injili ya Crypto kisawasawa na ikawa inawaingia watu; na watu wanaokoka kwenda kwenye Crypto kupitia Celsius kutoka benki za kawaida 🤪​

KWANI FAIDA ILIKUWA NI KIASI GANI UKIWEKEZA CELSIUS?
Kama ilivyokuwa kwa crypto banks nyingi, ilikuwa ni 18%. Hii haikuhitaji kufikiria mara mbili, hakuna benki itakupa riba ya asilimia 18% kwenye akaunti ya kawaida. Na kumbuka; hii haikuwa kama hisa au cryptocurrency zenyewe ambazo unanunua ukiwa na matumaini kuwa thamani yake itapanda (Japo moyoni una uhakika itashuka 🤣), hawa Celsius walichokuwa wanakifanya ni hivi;

Wewe unaweka crypto yako kwa kuanzia kama mtaji. Kisha baada ya hapo inakuwa ni mwendo wa kupokea 18%, huwazi suala la thamani kushuka wala nini. Inakuwa kama umepanda crypto hivi, baada ya hapo ni mwendo wa kuzivuna 🤑🤑🤑🤑

Na amini usiamini, wajinga duniani hawatokuja kuisha. Watu hawakuona kuwa huu ni utapeli, bali wengi waliamini hizi ni "Hela za bure" zinazotolewa na Celsius... asalaleee!!!🥱​

EBWANAEEEE! LAKINI, WAO CELSIUS FAIDA WALIKUWA WANAITENGENEZAJE?
Haijawahi kueleweka, lakini kitu kimojawapo ambacho Celsius walikuwa wanakifanya; ni kuchukua pesa (crypto) za wateja, kisha wanazikopesha kwa wawekezaji wakubwa na wafanyabiashara professional, na wale wawekezaji walikuwa wanakopa kwa riba, kwahiyo wakilipa na wao Celsius wanazisukuma kwenda kwa mteja. Lakini "Common sense" inagoma kukubaliana na hili.

Namba zinagoma, haiingii akilini kuwa kwa kufanya hivyo waliweza kuwahudumia wateja wote hawa zaidi ya 1.5M. Kuna mengi ambayo hatuyajui yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia.​

MH! KWANI HAKUKUWA NA WAKOSOAJI? HAKUKUWA NA WATU WA KUUANIKA HUU UTAPELI?
Walikuwepo; wanauchumi, wataalamu wa masuala ya kibenki na masoko ya mitaji n.k. Walijitahidi kwakweli kuwaelimisha watu kuwa hakuna pesa za rahisi namna hiyo katika mifumo ya kifedha. Wengi walikuwa wanawatahadharisha watu kuwa hii ni "Ponzi Sheme"

Kitu kingine kilichokuwa kinaleta hofu zaidi kwa wataalamu wa uchumi ni kwamba; Akiba ambazo watu huwa tunaweka benki huwa zinakatiwa bima, lakini kwa Celsius - akiba za watu hazikuwa na bima yoyote! Lakini kwa namna moja ama nyingine, ni vigumu sana kumshawishi mtu anaekaribia kutapeliwa kuwa atatapeliwa; huwa ni wabishi kinoma!

Usiniulize Serikali huwa hazioni au la, kwasababu hata mimi sijui!​

SASA, IKAWAJE? CELSIUS IKAISHIAJE?
Uchumi wa dunia ukaanza kuyumba yumba, Urusi ikaivamia Ukraine, mataifa bado yalikuwa yana "hangover" ya Korona, mifumo ya usambazaji wa bidhaa duniani ikaathirika kwa kiwango kikubwa sana. Benki kuu zikaanza kuongeza riba, lengo ni kuwafanya watu wasitumie akiba zao ovyo na hiyo inamaanisha mtelezo wa kwenda juu ukawa umeishia hapo. Watu badala ya kununua hisa, wakaanza kuziuza kwa kasi, hisa zikaanza kuporomoka bei, na vivyo hivyo crypto nazo zikaanza kuporomoka. Ghafla watu wengi wakaacha kuziamini crypto hivyo wakaanza kuzitoa (Ku-withdraw). Bei za crypto zikawa zinashuka kama mwewe.

Hata coin inayoitwa Terra USD ambayo ilibuniwa kwa namna ambayo thamani yake inaenda sambamba na thamani ya dola, kwenye ule mporomoko nayo haikuachwa salama.

Ikawa kama muvi la kutisha vile; project nyingi za crypto zikaanza kuanguka kwa pamoja ndani ya muda mfupi. Wazungu wanaita "Domino effect" - kikianguka kitu kimoja kinasababisha vingine vingi vianguke. Mabilioni ya dola yakageuka moshi ndani ya siku chache.

Kwahiyo, hata wateja wa Celsius wakawa wanataka kutoa pesa zao pamoja na riba ambazo wamejikusanyia kwa kipindi chote na ambazo walikuwa hawajazichukua. Kikatokea kitu ambacho mabenki huwa yanakiogopa , kinaitwa "Bank run". Bank run ni pale ambapo wateja wengi wanataka kutoa pesa zao zote kutoka benki kwa mkupuo. Mara nyingi huwa inakuwa ni dhahama kubwa kwasababu uwezekano wa kuwepo pesa za kutosha watu wote kutoa kwa mara moja unakuwa ni mdogo sana, kiasi ambacho mara nyingi ikitokea "Bank Run" benki huwa zinalazimika kusitisha miamala.

Basi buana, Celsius ikasitisha miamala. Hiyo ilikuwa ni mwezi wa sita mwaka jana. Kuna utani mtaani kuwa, kwenye ulimwengu wa crypto ukisikia wametangaza kuwa wamezuia kufanya miamala kwa muda basi ujue ndo mazishi hayo. Ni nadra sana kwenye crypto wakasitisha miamala kisha wakaruhusu baada ya muda, sikumbuki kama imewahi kutokea.

So, tangazo la Celsius la kusitisha miamala likazidi kuutikisa ulimwengu wa crypto. Bei zikazidi kushuka kwa kasi ya 6G. Na hatimae wiki chache baadae Celsius ikatangaza kuwa imefilisika🤒. Watu wakabaki njia panda - crypto zao watapata au hawazipata tena? Well, mpaka leo haijulikani ni nini kitatokea.​

PHEW! KWAHIYO SASA INAKUWAJE; KWANI INA MAANA WATU HAWAKUJUA KUWA CRYPTO NI KAMA KAMARI?
Watu wengi waliowekeza kwenye crypto kwa ushawishi wa ma-influenza na matangazo na mwisho wa siku wakapoteza pesa zao - huwa wanajihisi wametapeliwa. Kwamba wakati wanawekeza huwa wanaahidiwa usalama wa pesa zao, na uhakika wa faida. Wengi wamepoteza akiba zao za maisha, wengine wamepoteza mitaji yao ambayo waliiwekeza wakitumaini itakua mikubwa ili wawekeze zaidi n.k. Na kuonesha hali ilivyo mbaya, wapo wengi waliojinyonga kwasababu ya kupoteza pesa katika uwekezaji wa crypto.

Wengi wanawalaumu watu maarufu kwa kutumika vibaya kuwashawishi watu kuingia kwenye biashara ambazo mwisho wake huwaumiza watu wa hali ya chini.​

ENHE, ULISEMA CRYPTO KUNA AHADI HAIJATIMIZA - NI AHADI IPI HIYO?
Crypto ilidizainiwa kuwa mbadala wa mifumo ya kibenki; mifumo ambayo kuna "mtu" anasimamia na kufanya maamuzi juu ya pesa za watu wengine. Na kwasababu ni mtu mmoja au kikundi cha watu wachache ndio kimepewa mamlaka ya kusimamia pesa za watu wengi - uwezekano wa makosa kufanyika ni mkubwa. Nimeeleza kilichotokea kabla ya anguko la uchumi la 2008. Maamuzi mabovu ya watu wa benki yalipelekea watu kupoteza pesa zao. Crypto ilitengenezwa ili kuzuia hilo lisitokee tena, lakini kama ulivyoona, yanatokea yale yale ambayo watu wa crypto walikuwa wanayakwepa.

Kwahiyo; ahadi ambayo haijatimia ni ahadi ya crypto kuwa mbadala wa pesa za kawaida ambazo zinazimamiwa na serikali na kuratibiwa na mabenki na taasisi za fedha kwa sheria na kanuni mbalimbali. Mijadala inaendelea kuhusu kama kweli crypto itaweza kuleta suluhisho la mapungufu yaliyopo katika mifumo ya kibenki. Kuna watu wanaona cryto ni utapeli tu na ni suala la muda kabla haijapotea kabisa, na kuna watu wanaona crypto ndio future. Inawezekana wote wapo sahihi, inawezekana wote wanaota ndoto za Abunuwasi, sisi acha tuendelee kuishi.​

SO, CRYPTO IMEKUFA AU?😪
Ni mapema sana kulisema hilo. Ni kweli crypto imepoteza thamani kubwa, lakini bado kuna watu wanaendelea kuwekeza. Na sio kampuni zote za crypto zimekufa, kuna zingine bado zinaendelea kuwahudumia wateja mpaka sasa tunavoongea.

Kuna watu wapo katika ulimwengu wa crypto sio kwaajili ya faida au hasara; wao wanavutiwa na namna crypto ilivyoundwa na inavyofanya kazi. Na wanatumia teknolojia ambayo ni msingi wa crypto kuleta mapinduzi mengine ya teknolojia.

Kama ambavyo wakati intaneti inaingia, kampuni nyingi zilikufa (Dot Com Bubble) lakini zile chache zilizoweza kupenya zimekuwa ni kampuni kubwa sana duniani hivi sana. Inaweza kutokea hivyo hata kwenye crypto, tumeshuhudia kampuni kubwa za Crypto zinafilisika, lakini chache bado zinaukaza mwendo. Ni nani ajuaye pengine tukivuka hapa Crypto itasimama tena. Yote kwa yote crypto haionekani kuwa ni kitu kinachoweza kupotea ghafla, bado tunayo sana; na baadhi yetu tuna shauku ya kujua ni nini kitafuata baada ya hapa.

Homework: Fuatilia kuhusu Quadriga CX na FTX, kuna mengi utajifunza kuhusu crypto.​

Naweka kipaza chini.

Mimi... ninashukuru.
Well narrated ingawa nimepita Kama robo tatu ivi
 
Back
Top Bottom