Yashanikuta,bahati nzuri haikuwa pesa kubwa nikapotezea baada ya niliyemtumia kuingia mitini!
Kuna siku nikiwa chuo,nilikuwa nimepigika kinoma na rafiki yangu!Hatukuwa na hata mia ya kula mchana!Ilikuwa jmos,basi tukawa tumelala tu hostel kila mtu akihangaika na simu kucheki ndugu wa kututoa kwenye majanga!Mimi nilikuwa nimepiga mzinga watu kama watatu hivi!Nikawa nasubiri,ghafla 100,000/= ikaingia!Kilichofuata nikamshtua jamaa twende tukale mzigo umeingia!Kwa njaa niliyokuwa nayo hata sikuangalia nani katuma,nikaenda kutoa 30,000 tukaenda kula!Tukiwa katikati ya msosi,nikapigiwa simu na mama mmoja akaniambia amekosea kutuma hela!Daah nilisinyaa!Ikabidi nimueleze hali halisi bila kuficha!Nikamuomba nimrudishie 70,000 ikiyokuwepo kwny simu then nikipata nitamtumia kiasi kilichobaki!Huyo mama hakuamini,akasema mwanangu basi tu usitume hata hiyo 70,000!Itakusaidia na usome kwa bidii!Mpaka leo huyo mama tunawasiliana na kujuliana hali!
Ukikosea kutuma pesa basi fanya kama umepoteza tu,usiihesabie kabisa!Halafu mtu huwezi muanika kisa ameingia mitini na hela uliyomtumia kimakosa!