Tusizunguke mbuyu, Huyo Jamaa ni mwizi maana Kama pesa Imeingi Kwenye ac yako halafu hujui imetoka wapi ni busara kusubiri na kuona nani atakupigia, Mimi ilishanitokea siku moja hela iliingia kwangu yakutosha kiss nikasema doh, mambo yamekaa poa ila roho ikaniuma sana, nilikuwa na rafki yangu akanishauri tukaitoe fasta nikaona ni mwenye Tamaa nikampa ukweli kuwa sili jasho la mtu kwanza sijui kaipata vipi, nimekaa masaa mawili nishasahau nasikia sim inaita kupokea nasikia mama analia nikamuuliza vipi mbona walia na sikufahamu akaniambia amenitumia pesa kimakosa nikamuuliza sasa anacholia ni nini akaanza kujieleza mambo meengi nikamwambia pesa yake ipo salama cha msingi aongee na Huduma kwa Mteja wairudishe na kuanzia wakati huo sitafanya muamala wowote mpaka anijulishe kuwa amerudishiwa hela yake mama alifurahi sana, sikuona nimeshinda njaa kwasababu nimeachia pesa isiyo halali yangu, hivyo Mimi napitisha kabisa kuwa huyo mtu ni mwizi kabisa tena alaaniwe