Nitatoa zawadi ya 200,000

Nitatoa zawadi ya 200,000

Mkuu...
Huyu jamaa nilimtumia pesa kwa bahati mbaya nikiwa nafanya malipo kwa watu kadhaa.... Sasa baada ya kuwalipa wengine wote, nikapata sim toka kwa jamaa mmoja akiulizia malipo yake. Nami nikamjibu kwamba tayari nimefanya malipo kwa watu wote, lakini nikaamua kurudi kuhakiki kama nilikua sahihi.... Toba... , nikakuta nimezituma kwa Venance Chiwalala.
Hapo nikaamua kumpigia sim na kumtaarifu kuhusu kilicho tokea king makosa kwa kumtumia pesa asio stahiki, kisha huyu jamaa akakubali na akaniahidi kuirudisha baada ya muda mchache, nami bila hiyana nikamwambia achukue 50,000 kwakua amekua muungwana.
Baada ya kuona muda unapita, ndipo nikaamua kumpigia tena na jamaa akawa amezima sim.
Hajapatikana kwenye namba ile hadi leo.
Hapo nikaamua kwenda toa taarifa police kuhusu tukio lile, na nikafungua kesi ya kuibiwa kwa njia ya mtandao.
Hapo bila kuchelewa nikaanza kufanyia kazi jambo hili na nikapata informations zake kadhaa
sasa huo ndo wizi???yan uzembe wako uje udhalilishe watu
mm mwenyewe ungekosea kwenye namba yangu nisingekurudishia hata na usawa wenyewe huu
 
Mkuu Ushimen nimemcheki kijana Facebook yake naona yupo tu anatamba ila Instagram ndio kaweka Private!

Nahisi kumpata ni rahisi ila kuipata hela ndio inaweza kuwa ngumu!

Halafu dogo anafanana na Bashite nahisi wana undugu!
Hahaahaaaaa.....
Asante mkuu, mimi shida yangu kubwa ni kumpata tu.
Nikimpata kwangu yatosha, kwani kiukweli yawezekana pesa amesha tumia
 
matapeli kama hawa nikumjaza busha tu la mgongoni atarudisha mwenyew maan kakosa uungwana umeambiwa uchukue 50,000 ya bila jasho bado hujaridhika khaa
 
Unaonekana una njaa ya hatari....
Anyway, naomba nikupuuze tafadhali
no vitu vingne jarbu kutumia common sense leo umepost pics za mtu humu kwa jina alosajiria line
tz kuna watu kibao wanatumia line ambazo hazisajiliwa jina lake kama mm hapa
je mwenye hio pics akikufungulia kesi ya uzalilishaji utakua umeonewa??na ushafikiria odds za kishndwa na utaoteza shilling ngap zaidi???
 
  • Thanks
Reactions: y-n
POLE SANA MKUU HUU NI UJINGA WETU WENYEWE SISI WATANZANIA KWA KUKUBARI, KUITUMIAKIA MITANDAO ISIYO WAJARI WATEJA WAKE....MITANDAO YOTE YA SIMU ILIYOPO TANZANIA INAENDESHWA KITAPELI TAPELI SANA...NAMUOMBA MUNGU AKUPE SUBIRA JUU YA TATIZO LILILOKUPATA MKUU...
 
Asante mkuu
 
Mkuu pole sana,pamoja na yote ni kweli kafanya kosa kukubali kuirudisha na kushindwa kufanya hivyo.

Nimejifunza kitu ktk uzi huu sisi binadamu tuna tamaa sana ya vitu visivyohalali yetu.

Fanya hivi km atakana kuwa siyo yeye baada ya kumpata ,muache usipoteze muda na pesa nyingne kwaajili yake,watu km hawa wapo ktk jamii, Hakika naiman ktk pilika pilika zako utapata zaidi na Mungu akusimamie ktk kazi zako.
 
Ulikosea mkuu Ilibid punde baada ya kugundua kuwa umetuma pesa kimakosa ilibid upige simu huduma kwa wateja wenyewe wange izuia hiyo pesa km angekuwa bado hajaitoa pole sana mkuu
 
Mkubwa pole sana na usawa wenyewe huu aiseee pole sana.

Ila mdogo siyo muungwana tu kama ulimpa na offer.

But next time na ndiyo njia sahihi ya kufanya kama unajua umefanya kosa la kutuma ktk simu ya MTU mwingine unatakiwa upige haraka sana kwa service provider ili aiblock hiyo pesa na kukurudishia ktk simu yako.

Kwa kumuachia ulimpa temptation na akaingia tamaa kweli.
 
Pole mkuu, jaribu kwenda kanisani hapo na hiyo picha bila shaka unaweza kupata taarifa nyingi zaidi kumhusu yeye
 
Mkuu pole sana,pamoja na yote ni kweli kafanya kosa kukubali kuirudisha na kushindwa kufanya hivyo.

Nimejifunza kitu ktk uzi huu sisi binadamu tuna tamaa sana ya vitu visivyohalali yetu.

Fanya hivi km atakana kuwa siyo yeye baada ya kumpata ,muache usipoteze muda na pesa nyingne kwaajili yake,watu km hawa wapo ktk jamii, Hakika naiman ktk pilika pilika zako utapata zaidi na Mungu akusimamie ktk kazi zako.
Asante kwa ushauri wako mkuu
 
Duuuh ...! pole sana ila uwezekano wa kumpata huyu mtu upo mkubwa. Hyo inatokea mara kwa mara
 
Ulikosea mkuu Ilibid punde baada ya kugundua kuwa umetuma pesa kimakosa ilibid upige simu huduma kwa wateja wenyewe wange izuia hiyo pesa km angekuwa bado hajaitoa pole sana mkuu
Asante mkuu.
Hii nilichelewa kugundua kama nimetuma kimakosa baada ya niliepaswa kumtumia kuanza kuniulizia fungu lake.
Ndipo nilipo Fanya kuhakiki nq nikajikuta tayari nimesha kosea.
Sikupoteza muda kuwapigia jamaa wa mtandao ndipo wakanijibu kwamba jamaa amesha zitoa.
Ndipo nilipo amua kuongea nae kiungwana, na akakubali kuirudisha na baada ya muda akatoweka
 
Pole mkuu, jaribu kwenda kanisani hapo na hiyo picha bila shaka unaweza kupata taarifa nyingi zaidi kumhusu yeye
Asante kwa ushauri mkuu, nitajaribu pia
 
Back
Top Bottom