Nitatoa zawadi ya 200,000

Nitatoa zawadi ya 200,000

Kichefuchefu cha kutetea wezi na majambazi kila uchao kinazidi, tunakunywa maji mengi kuzuia kutapika, lakini inashindikana hadi tunatapika sasa.
Hivi nikuulize wewe mwenye dalili zote za kihalifu, hiyo sim card# ya simu yako mnaimiliki watu wangapi?
Mtu asemeje hadi umsapoti kuwa kadhulumiwa Kitapeli cha kiaminifu?
Ndiyo nyie mnaodai hata mwizi akikamatwa hatakiwi kuitwa mwizi, bali ni mtuhumiwa hadi atiwe hatiani na mahakama. Na mahakama inahukumu kosa ama tendo la wizi na haimuiti huyo aliyepatikana na hatia ya wizi kuwa ni mwizi. Itamfunga bila kumuita mwizi, akifika jela haitwi mwizi, bali anaitwa mfungwa.
Sasa mwizi huwa ni nani?
WaTz tumezoea blahblah za kishenzi sana na upotoshaji wa lugha kwa uwazi bila ya soni.
Kwa hiyo kumuita mtu mwenye tabia za ukwapuaji kuwa ni mwizi ni kumharibia brand!
Kweli jf linakada zote
Wengi wanadhani kwamba mwizi hadi awe ameshikilia kisu ama bunduki na kupora, huyo ndie mwizi.
Humu watoto wengi, na wengi hawajajua changamoto za makosa kama haya
 
Ukimpata kazi ya kumminya kende ili afunguke naiomba, ,, hana adabu ,,bora anagerudisha ht nusu ya pesa, ,pole mkuu
 
Pole sana mkuu mwenyew hayo yalisha nitokea saana, ila ya maramwisho nilikosea nikamtumia mtu pesa ndefu kidogo. nahisi hata uliotuma wewe haifikii. nikawasiliana nae huku nikimuomba anirudishie pesa yangu, sim akazima na laini akatupa. sikutaka kujisumbua, nikajisogeza Bariadi. hapakupita wiki 2 pesa amerudisha yeye mwenyewe. nimeshangaa tu mtu kanipigia namba ngeni... nikaletewa pesa japo alikua tayari alisha tumia kama Nusu. ila yoote amelipa, pole sana
ama kweli..
 
huo ni kuchafuana brand!una uhakika gani kama ndio yeye?kosa ni kako au lake?kwa nini umejipa kazi ya polisi na mahakama?kama sio yeye uko tayari kumlipa fidia?achaupuuzi
umefikaje huko
calm down kidogo, fikiria tena then andika upya
 
Hahaahaaaaa.....
Asante mkuu, mimi shida yangu kubwa ni kumpata tu.
Nikimpata kwangu yatosha, kwani kiukweli yawezekana pesa amesha tumia
Ukishampata unataka umfanye nini?umwambie nini?
 
hahahha haya mambo bwana nilikosea nkamtumia jamaa mkwanja flan badae nkamcheki anirudushie alicho nijibu nilicheka peke yangu kwa upole alinambia

"bro nna dhiki ya kufa mtu, nkisema ntakurudishia ni uongo nisamehe sana bro."
, nimecheka sanaaa
 
Anatafutwa kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao. Pia namba alio tumia kupokelea pesa haipatikani.
Kwa mujibu wa maelezo kadhaa.... Inasemekana anaishi maeneo ya kimara Dar.
Kama nilivyo toa angalizo kwamba zawadi ya 200,000 itatolewa kwa yeyote atakae toa informations zake na exactly location anayo patikana naomba ani PM.
Nimeambatanisha picha na machache niliyo yapata kuhusu mtu huyu.
Asanteni.View attachment 492396View attachment 492397View attachment 492398
rb unayo na kibali cha kumripoti.au unataka kutumia.utekaji.
unajua sheria ya kumtangaza mtu kupitia mtandao bila kibali kuna vifungu vitakufunga
 
rb unayo na kibali cha kumripoti.au unataka kutumia.utekaji.
unajua sheria ya kumtangaza mtu kupitia mtandao bila kibali kuna vifungu vitakufunga
Haya ndio matatizo ya kusoma threads bila kuikamilisha.
Mkuu....
Naona unajaribu kudandia treni kwa mbele
 
Haya ndio matatizo ya kusoma threads bila kuikamilisha.
Mkuu....
Naona unajaribu kudandia treni kwa mbele
nimedandia sawa.tangaza mtu kwenye mitandao bila kibali.uone jela ina kuita hata kama unakosa
 
Back
Top Bottom