Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Sasa kama huna uthibitisho maana yake hujui ukweli wa kile unachokisema una hakika nacho kua kipo

Mimi nimedai uthibitisho kwa anayesema mungu yupo, huna uthibitisho hivyo huwezi kuthibitisha, huwezi kuthibitisha ni kwasababu ni mungu wa kufikirika tu
Unaweza ukamuona mtu amekukonyeza(ni ukweli kabisa) ila ukashindwa kuthibitisha kuwa huyo mtu kuwa ni kweli kakukonyeza.

Ishu ni kwamba mimi naamini Mungu yupo bila ya shaka na nina sababu za kuamini,sasa wewe unataka uthibitisho kitu ambacho mie sijadai kuwa ninacho.

Juzi kati hapa kuna baba mmoja aliachiwa huru kutoka jela baada ya kukuka jela kama miaka 7 hivi kutokana na kesi ya kumbaka mwanae, alihukumiwa kifungo cha maisha ila mahakama ikaja kugundua kuwa yule mtoto aliyedai kubakwa ni kwamba alitoa ushahidi wa uongo mahakamani.
 
Hivi kwanini atheists wengi wana asili ya Ukristo?

Dini yao ina mapungufu sasa ukifikiria kwa kina unaona sio kweli,mfano;
ILI UWE PADRI UWE RIJALI ALAFU USIOE,

HAURUHUSIWI KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA ILA WANA WATOTO WA NJE YA NDOA,

HAKUNA KUACHANA NDOANI (KURUHUSU UDHINIFU BAINA YAO WAACHANAO)

Hayo ni baadhi tu na wengine kukosa uelewa

Mfano sisi Waislam tunaamini kuna siku ya mwisho na kama unapata usingiz na kupoteza fahamu then unaamka basi na kaburini hivyo hvyo tutaamshwa huo ni mfano hai
 
Mkuu hiki ulichokiandika hapa ni sawa na kusema hayupo.
Wewe kweli unajishughulisha na huu ulimwengu? Wewe umemdhahania Mungu, mimi nikakujibu hamithiliki hata kwa dhana!

Hufahamu hakuna vinavyomithilika?

Mithili maana yake ni mfano! Hamithiliki! Yaani hana mfanowe! Yaani hashahabiani. Ukiambiwa hakuna mithili yake maana yake ni kuwa hakuna kinachofanana naye. Yaani hajafanana na chochote (hamithiliki kwa chochote).

"A" hamithiliki kwa chochote, Yaani A hajafanana na chochote maana yake chochote hakijafanana na A. Kwa tafsiri nyengine A kafanana na yeye mwenyewe.

Mungu hamithiliki na chochote maana; chochote hakimithiliki na Mungu, Yaani chochote hakijafanana na Mungu! Kwa maana Mungu kafanana na yeye mwenyewe.

Picha ni mfano halisi wa kitu. Dhana yako itajikita kwa vile ambavyo tayari una taswira yake iwe ya sasa au ya baadaye. Kwenye hiyo dhana/dhahania Mungu yupo nje ya box la dhana. Kwa msingi huo huwezi ukamdhahania.

Sijui umeelewa?! Kwa sababu naona unajibu ilimradi umejibu.
KKila kitu kina chanzo" hiyo ndio universal principle so ukiitumia hii principle kutaka kupata majibu basi dhana ya ukomo hautakiwi kuiweka. Ukisema kila ktu kina chanzo isipokua mungu hapo utakua umetumia logical fallacy, vinginevyo kanuno ya kila kitu kina chanzo uiweke pembeni
Universal principle ina apply kwa nani?

Kisa wewe unakula Mungu naye anakula? Wewe unaenda haja Mungu naye anaenda haja? Wewe unafua nguo zako Mungu naye ana mavazi yake anafua? Sasa hii ni akili au ni nini?

Jambo likishindikana kwako haina maana limeshindikani kwa wengine pia. Wewe umeshindikana kuwepo bila chanzo yupo ambaye yupo bila chanzo.

Kutoa ushahidi wa jambo kwa kizingatia misingi na kanuni za kimantiki ili kupata jawabu la uhakika juu ya madai ambayo umeyaweka
Ushahidi ni namna ambayo inatumika kukanusha au kuthibitisha ukweli wa jambo linalichunguzwa.

Na mantiki maana yake ni mawazo ya binadamu ambayo hutumika katika mchakato wa kutafuta ukweli.

Ukweli ni muafaka baina ya usahihi na uhalisiya wa mambo.

Tukiambiwa nini kuthibitisha inamaanisha ni namna ambayo inatumika kukanusha au kuthibitisha ukweli wa jambo linalichunguzwa kwa kuzingatia misingi na kanuni mawazo ya binadamu ambayo hutumika katika mchakato wa kutafuta ukweli ambao ni muafaka baina ya usahihi na uhalisiya wa mambo.

Hii ndiyo maana ya kuthibitisha. Kuthibitisha ni kuendana na usahihi wa uhalisiya wa mambo. Ninyi akili yenu ilivyo mgando mnachukulia uthibitisho ni hali ambayo inabidi kinachotafutiwa ushahidi chenyewe kionekane kwa macho.

Ninyi hamjui mnachokisimamia na hamjui maana ya maneno mnayoyasimamia. Mnabaki kuendekeza ubishi na kuwa na ile hali nipo tofauti na ninyi. Kwa hakika hamkatazwi kuwa tofauti na watu ila mna ubishi ambao ni upuuzi.

Kwa muda niliyojadiliana nawe sijaona chochote ulichokiandika zaidi ya kuona hauelewi hata hicho unachokisimamia na kujenga ubishi.
 
Wewe kweli unajishughulisha na huu ulimwengu? Wewe umemdhahania Mungu, mimi nikakujibu hamithiliki hata kwa dhana!

Hufahamu hakuna vinavyomithilika?

Mithili maana yake ni mfano! Hamithiliki! Yaani hana mfanowe! Yaani hashahabiani. Ukiambiwa hakuna mithili yake maana yake ni kuwa hakuna kinachofanana naye. Yaani hajafanana na chochote (hamithiliki kwa chochote).
Sio kweli kwamba hana mfano au amithiliki na chochote maana naweza kujenga hoja kupitia vitabu vyenu ambavyo vimedai mungu alimuumba adamu kwa mfano wake

Ukisema hamithiliki na chochote na hana mfano mi nitakuuliza umejuaje hilo?
"A" hamithiliki kwa chochote, Yaani A hajafanana na chochote maana yake chochote hakijafanana na A. Kwa tafsiri nyengine A kafanana na yeye mwenyewe.
We umejuaje kwamba hajafanana na chochote?

Mungu hamithiliki na chochote maana; chochote hakimithiliki na Mungu, Yaani chochote hakijafanana na Mungu! Kwa maana Mungu kafanana na yeye mwenyewe.
Hata kisichopo nacho kina sifa hizo hizo
Picha ni mfano halisi wa kitu. Dhana yako itajikita kwa vile ambavyo tayari una taswira yake iwe ya sasa au ya baadaye. Kwenye hiyo dhana/dhahania Mungu yupo nje ya box la dhana. Kwa msingi huo huwezi ukamdhahania.
We taswira ya mungu umeipatia wapi mpaka ukajua hamithiliki na kitu chochote?

Sijui umeelewa?! Kwa sababu naona unajibu ilimradi umejibu.

Universal principle ina apply kwa nani?
Ina apply Kwa kila kitu meanwhile hakuna exception kwenye hiyo principle
Kisa wewe unakula Mungu naye anakula?
Vingapi ambavyo havili, je navyo tuviite mungu?

Na kama mungu hali utasemaje hamithiliki na kitu chochote wakati vingi tu visivyo kula vipo?
Wewe unaenda haja Mungu naye anaenda haja?
Mungu anayekalia kiti cha enzi anakosaje kua na matako?

Mungu ambaye amedaiwa kuumba binadamu kwa mfano wake ana vingi vya kufanana na huyo binadamu

Wewe unafua nguo zako Mungu naye ana mavazi yake anafua? Sasa hii ni akili au ni nini?
Kwa hiyo mungu anashinda uchi?

Au kaajiri mabeki tatu wakumfuria nguo huko juu?

Haya vingapi ambavyo havifui nguo na vipo hapa duniani, je hivyo navyo ni mungu?

Sasa utasemaje hamithiliki na kitu chochote kwasababu hafui nguo wakati hata nyani tu hafui nguo?
Jambo likishindikana kwako haina maana limeshindikani kwa wengine pia. Wewe umeshindikana kuwepo bila chanzo yupo ambaye yupo bila chanzo.
Unaonaje sheria hii ui apply kwako, kwamba jambo la kushindwa kuthibitisha mungu ana chanzo likishindikana kwako haina maana mungu hana chanzo, wewe umeshindwa kuthibitisha chanzo chake hivyo yupo anayeweza. So kuja hapa na kusema mungu hana chanzo unakua ubajihukumu kwa sheria yako mwenyewe
Ushahidi ni namna ambayo inatumika kukanusha au kuthibitisha ukweli wa jambo linalichunguzwa.
Unao ushahidi wa kuonesha mungu yupo?

Weka hapa tuuone kama ume qualify
Na mantiki maana yake ni mawazo ya binadamu ambayo hutumika katika mchakato wa kutafuta ukweli.
Kama ambavyo mawazo ya binadamu yalipowaza kuna mungu. Hayo mawazo unayachukuliaje?
Ukweli ni muafaka baina ya usahihi na uhalisiya wa mambo.

Tukiambiwa nini kuthibitisha inamaanisha ni namna ambayo inatumika kukanusha au kuthibitisha ukweli wa jambo linalichunguzwa kwa kuzingatia misingi na kanuni mawazo ya binadamu ambayo hutumika katika mchakato wa kutafuta ukweli ambao ni muafaka baina ya usahihi na uhalisiya wa mambo.
Sasa kuna jambo gani ambalo lisilo la kibinadamu ambalo haliwezekani kuthibitishwa kwa kanuni za binadamu?

Mbona mambo mengi yasio ya binadamu yanathibitishika vizuri tu?
Hii ndiyo maana ya kuthibitisha. Kuthibitisha ni kuendana na usahihi wa uhalisiya wa mambo. Ninyi akili yenu ilivyo mgando mnachukulia uthibitisho ni hali ambayo inabidi kinachotafutiwa ushahidi chenyewe kionekane kwa macho.
Wapi nimedai uthibitisho wa mungu kwa dhana ya kuonekana kwa macho?
Ninyi hamjui mnachokisimamia na hamjui maana ya maneno mnayoyasimamia. Mnabaki kuendekeza ubishi na kuwa na ile hali nipo tofauti na ninyi. Kwa hakika hamkatazwi kuwa tofauti na watu ila mna ubishi ambao ni upuuzi.
Thibitisha mungu yupo naona unajisahau sana
Kwa muda niliyojadiliana nawe sijaona chochote ulichokiandika zaidi ya kuona hauelewi hata hicho unachokisimamia na kujenga ubishi.
Hujaona nilichokiandika sasa umewezaje kujibu post ambayo haijaandikwa chochote?

Huu muda uliotumia kuelezea hisia zako na changamoto za maisha yako ungeutumia kuthibitisha mungu yupo ungekua umefanya jambo la maana sana ambalo limewashinda wengi

Thibitisha mungu yupo
 
Unaweza ukamuona mtu amekukonyeza(ni ukweli kabisa) ila ukashindwa kuthibitisha kuwa huyo mtu kuwa ni kweli kakukonyeza.
Ulichokiona kinaweza kikawa ni eye illusion na ndio maana ni ngumu kuthibitisha
Ishu ni kwamba mimi naamini Mungu yupo bila ya shaka na nina sababu za kuamini,sasa wewe unataka uthibitisho kitu ambacho mie sijadai kuwa ninacho.
Huwezi ukaamini mungu halafu ukakosa shaka
Juzi kati hapa kuna baba mmoja aliachiwa huru kutoka jela baada ya kukuka jela kama miaka 7 hivi kutokana na kesi ya kumbaka mwanae, alihukumiwa kifungo cha maisha ila mahakama ikaja kugundua kuwa yule mtoto aliyedai kubakwa ni kwamba alitoa ushahidi wa uongo mahakamani.
Ukikosa uthibitisho hutakiwi kujenga madai kwamba jambo fulani lipo kwa hakika, ukitaka sheria hiyo itumike utajikuta hata jambo la uongo unalikubali kua ni kweli as long as mtu atasema sina uthibitisho
 
Wanaoharibu dunia ni Taliban, ISIS, Alshabaab, Boko Haram, LRA, masalia na wengine wanaofanana na hawa
Yah wanatuharibia wala sibishi
Ila hao ni watu wenye maslahi binafs wala si dini hiyo dini mfano boko haram waliteka Kijiji na humu walikuwepo waislamu
Pia tukio la mashambulizi ya mabomu kule west gate kenya (if I am not mistaken) alshabaab walifanya sawa lakini walikuwa na uhakika gan pale wote sio waislamu
Fikiri tena makundi hayo hutumia sehemu za mikusanyiko kufanya mashambulizi kama sokon
Kwani kuna dini inahamasisha kuuwa wenzao?? Kama jibu ni ndyo kwenye public place unajuaje Hawa niko nao dini au dhehebu Moja??
 
Mtu unaamini katika kuto kuamini Mungu kwako unakutetea mbele za sisi tusio kujua..

Lakini huwezi kusimamia mSimamo wako mbele ya mke wako..
Inamaana ulimdanganya Tangu mwanzo..kua Wewe Ni mkirisitu kumbe uongo..

Kwanini hukuwa muwazi from the word go.
 
Ulichokiona kinaweza kikawa ni eye illusion na ndio maana ni ngumu kuthibitisha

Huwezi ukaamini mungu halafu ukakosa shaka

Ukikosa uthibitisho hutakiwi kujenga madai kwamba jambo fulani lipo kwa hakika, ukitaka sheria hiyo itumike utajikuta hata jambo la uongo unalikubali kua ni kweli as long as mtu atasema sina uthibitisho
Hebu kuwa muelewa, watu wanaosema kuna Mungu huitwa waaamini Mungu,kwa maana hiyo ni imani na hivyo ndivyo wanavyoamini.
Kwahiyo wewe unaweza usiamini hicho ambacho wanaamini au ukaamini chengine tofauti na wanachoamini wao ndivyo imani ilivyo.

Sasa hali ya mtu kuwa au kutokuwa na shaka juu ya jambo fulani haihusiani na ukweli au uongo wa hilo jambo,ndio maana unaweza ukafojishiwa ushahidi wa jambo fulani na wewe ukakubali bila kujua na ukawa huna shaka juu ya hilo jambo ila kiuhalisia hilo jambo si la kweli.
 
Kwa sababu ya elimu ndogo mkuu ndo maana tunaona mambo ya ajabu mtu kutokuamini Mungu.
Si suala la elimu,tatizo wengi mlivyo mnafikiri kutokuamini Mungu ni jambo la kiakili na la kielimu na kinyume chake ni kwamba hawana elimu ndio maana wanaamini Mungu. Wewe unasema hakuna Mungu ni uchaguzi wako tu kutokana na mtazamo wako kama ilivyo kwa mwenye kuamini na hapo haihusiani na elimu na ndio maana kwenye hayo makundi mawili kote kuna watu wenye elimu na wasio na elimu.
 
Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
Askofu wa Atheists Ni nani, katiba yenu ipi?
Je mnaamini kuwa Mungu wa manabii yupo?
Swali la 2 muhimu sana. Kama hamuamini ninyi ni wapagani au watu wa fikra fulani.
 
Hebu kuwa muelewa, watu wanaosema kuna Mungu huitwa waaamini Mungu,kwa maana hiyo ni imani na hivyo ndivyo wanavyoamini.
Kwahiyo wewe unaweza usiamini hicho ambacho wanaamini au ukaamini chengine tofauti na wanachoamini wao ndivyo imani ilivyo.

Sasa hali ya mtu kuwa au kutokuwa na shaka juu ya jambo fulani haihusiani na ukweli au uongo wa hilo jambo,ndio maana unaweza ukafojishiwa ushahidi wa jambo fulani na wewe ukakubali bila kujua na ukawa huna shaka juu ya hilo jambo ila kiuhalisia hilo jambo si la kweli.
Hiyo ni fallacy of BANDWAGON APPROACH Watu kusema wanaamini mungu kwa hoja yoyote ile hakuthibitishi kwamba ni halali au imani hiyo ni ya kweli

Imani ingekua njia sahihi ya kuaminika kujua ukweli wa jambo basi kusingekua na imani zenye kutofuatiana kati ya dini na dini.

Na kila mungu anayeabudiwa na dini yoyote angekua ni wa kweli as long as wanaomuabudu wanatumia dhana ya "imani"

Imani ingekua njia ya ya uhakika kujua ukweli wa kitu basi leo hii dini ingekua moja yenye kuabudu mungu mmoja maana wote hao wangeweza kujua mungu gani ni sahihi apaswaye kuabudiwa kwasababu ya imani
 
Back
Top Bottom