Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
9,347
Reaction score
20,049
Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
 
Atheist miyeyusho. Atheist gani unafunga ndoa kanisani?
Alitakiwa afunge usongo au kilemba ili tumuone ni real atheist sio?
Umesema ni mkeo!

Kama ndoa yenu ilifungwa kanisani kwa viapo hakuna Atheïst hapo.
Kuna sehemu nimeandika nimefunga ndoa kanisani?
Hao wote wana matatizo ya akili, kama wanakubali simu imetengenezwa na kuwa hivi ilivyo, vipi Dunia na vinginevyo visiwe na muumbaji ? Hizi akili wanazitumia vibaya sana, ila bishara mbaya kwao.
 
Mkuu achana na huo u-atheists ,Soma biblia Kama Una mlengo wa ukristo ina nguvu Sana , ila pia dini ya mkeo na yenyewe miyeyusho Tu , ulokole hamna kitu , watakukomba hela yote af utakuwa kama kondooo
 
Hili swali hata mimi hulifikiria!!
Hivi Kwanini atheists wengi wana asili ya ukristo ?
Nadhani sababu wakristo wapo huru zaidi kuliko Waislam.

Mkristo yupo huru kufungua kanisa lake au kuhamia kanisa jingine ama Dini

Kwa Waislam ni tofauti, ni dini ya itikadi Kali zaidi, madhehebu yao wenyewe kwa wenyewe wanapigana Vita, kufunga Ramadan wanalazimishwa, kuna nchi nyingine ukibadili dini adhabu yake ni kifo.
 
Johnny Sack, always sucks!!

Maelezo yako ya kuungaunga sasa umeanza kutembea na beats tu, enwei jikite kwenye kile unataka kusikia.
Nenda kapimwe akili unakuwaje "Atheist" ?
Kwa nini wafia dini mnakuwa na hasira hivi kwa watu ambao hawaamini Imani zenu? Kama huyo mungu yupo si ataniadhibu Mimi wewe inakuuma Nini?
 
Back
Top Bottom