Wewe kweli unajishughulisha na huu ulimwengu? Wewe umemdhahania Mungu, mimi nikakujibu hamithiliki hata kwa dhana!
Hufahamu hakuna vinavyomithilika?
Mithili maana yake ni mfano! Hamithiliki! Yaani hana mfanowe! Yaani hashahabiani. Ukiambiwa hakuna mithili yake maana yake ni kuwa hakuna kinachofanana naye. Yaani hajafanana na chochote (hamithiliki kwa chochote).
Sio kweli kwamba hana mfano au amithiliki na chochote maana naweza kujenga hoja kupitia vitabu vyenu ambavyo vimedai mungu alimuumba adamu kwa mfano wake
Ukisema hamithiliki na chochote na hana mfano mi nitakuuliza umejuaje hilo?
"A" hamithiliki kwa chochote, Yaani A hajafanana na chochote maana yake chochote hakijafanana na A. Kwa tafsiri nyengine A kafanana na yeye mwenyewe.
We umejuaje kwamba hajafanana na chochote?
Mungu hamithiliki na chochote maana; chochote hakimithiliki na Mungu, Yaani chochote hakijafanana na Mungu! Kwa maana Mungu kafanana na yeye mwenyewe.
Hata kisichopo nacho kina sifa hizo hizo
Picha ni mfano halisi wa kitu. Dhana yako itajikita kwa vile ambavyo tayari una taswira yake iwe ya sasa au ya baadaye. Kwenye hiyo dhana/dhahania Mungu yupo nje ya box la dhana. Kwa msingi huo huwezi ukamdhahania.
We taswira ya mungu umeipatia wapi mpaka ukajua hamithiliki na kitu chochote?
Sijui umeelewa?! Kwa sababu naona unajibu ilimradi umejibu.
Universal principle ina apply kwa nani?
Ina apply Kwa kila kitu meanwhile hakuna exception kwenye hiyo principle
Kisa wewe unakula Mungu naye anakula?
Vingapi ambavyo havili, je navyo tuviite mungu?
Na kama mungu hali utasemaje hamithiliki na kitu chochote wakati vingi tu visivyo kula vipo?
Wewe unaenda haja Mungu naye anaenda haja?
Mungu anayekalia kiti cha enzi anakosaje kua na matako?
Mungu ambaye amedaiwa kuumba binadamu kwa mfano wake ana vingi vya kufanana na huyo binadamu
Wewe unafua nguo zako Mungu naye ana mavazi yake anafua? Sasa hii ni akili au ni nini?
Kwa hiyo mungu anashinda uchi?
Au kaajiri mabeki tatu wakumfuria nguo huko juu?
Haya vingapi ambavyo havifui nguo na vipo hapa duniani, je hivyo navyo ni mungu?
Sasa utasemaje hamithiliki na kitu chochote kwasababu hafui nguo wakati hata nyani tu hafui nguo?
Jambo likishindikana kwako haina maana limeshindikani kwa wengine pia. Wewe umeshindikana kuwepo bila chanzo yupo ambaye yupo bila chanzo.
Unaonaje sheria hii ui apply kwako, kwamba jambo la kushindwa kuthibitisha mungu ana chanzo likishindikana kwako haina maana mungu hana chanzo, wewe umeshindwa kuthibitisha chanzo chake hivyo yupo anayeweza. So kuja hapa na kusema mungu hana chanzo unakua ubajihukumu kwa sheria yako mwenyewe
Ushahidi ni namna ambayo inatumika kukanusha au kuthibitisha ukweli wa jambo linalichunguzwa.
Unao ushahidi wa kuonesha mungu yupo?
Weka hapa tuuone kama ume qualify
Na mantiki maana yake ni mawazo ya binadamu ambayo hutumika katika mchakato wa kutafuta ukweli.
Kama ambavyo mawazo ya binadamu yalipowaza kuna mungu. Hayo mawazo unayachukuliaje?
Ukweli ni muafaka baina ya usahihi na uhalisiya wa mambo.
Tukiambiwa nini kuthibitisha inamaanisha ni namna ambayo inatumika kukanusha au kuthibitisha ukweli wa jambo linalichunguzwa kwa kuzingatia misingi na kanuni mawazo ya binadamu ambayo hutumika katika mchakato wa kutafuta ukweli ambao ni muafaka baina ya usahihi na uhalisiya wa mambo.
Sasa kuna jambo gani ambalo lisilo la kibinadamu ambalo haliwezekani kuthibitishwa kwa kanuni za binadamu?
Mbona mambo mengi yasio ya binadamu yanathibitishika vizuri tu?
Hii ndiyo maana ya kuthibitisha. Kuthibitisha ni kuendana na usahihi wa uhalisiya wa mambo. Ninyi akili yenu ilivyo mgando mnachukulia uthibitisho ni hali ambayo inabidi kinachotafutiwa ushahidi chenyewe kionekane kwa macho.
Wapi nimedai uthibitisho wa mungu kwa dhana ya kuonekana kwa macho?
Ninyi hamjui mnachokisimamia na hamjui maana ya maneno mnayoyasimamia. Mnabaki kuendekeza ubishi na kuwa na ile hali nipo tofauti na ninyi. Kwa hakika hamkatazwi kuwa tofauti na watu ila mna ubishi ambao ni upuuzi.
Thibitisha mungu yupo naona unajisahau sana
Kwa muda niliyojadiliana nawe sijaona chochote ulichokiandika zaidi ya kuona hauelewi hata hicho unachokisimamia na kujenga ubishi.
Hujaona nilichokiandika sasa umewezaje kujibu post ambayo haijaandikwa chochote?
Huu muda uliotumia kuelezea hisia zako na changamoto za maisha yako ungeutumia kuthibitisha mungu yupo ungekua umefanya jambo la maana sana ambalo limewashinda wengi
Thibitisha mungu yupo