Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Ndoa imefungwa bila kuhusika imani na huyo mwanamke akaona ni sawa hakuna shida(sijajua mafundisho ya imani ya huyo mwanamke inazungumziaje suala hili) sasa iweje tena ndoa ivunjike kisa imani hali ya kuwa hazikuhusika katika kuwaonganisha wao wawili na kuwa wanandoa?
Mungu wetu husamehe, akifanya toba akamwomba Mungu amsamehe kwa kuamua mambo yake bila kumshirikisha na kumwomba amwonyeshe suluhu kadri ya mapenzi yake Mungu atafanya

Hakuna kosa kubwa kwake muumba lisilosameheka tukifanya toba
 
Huko kusema Mungu hayupo,ndio ushahidi wa uwepo wa Mungu,kwasababu huwezi kusema hakuna ,ila ni kuweko kwake,ndio kukawa hakuna,kama hayupo ,kusingekuwako na hayupo,il yupo,ndio ikawepo hayupo.
ok, mimi nasema hakuna nyani mwenye mabawa
hakuna tambi yenye miguu
pia hakuna bruce lee aliezaliwa tanga

kwa logic yako, hivyo vyote ni ushahidi kwamba vipo..

kusema kitu hakipo, hakimaanishi kipo
hakipo maana yake hakuna ushaidi kipo; nafasi yake inaweza kuchukuliwa na kitu chochote ikiwemo nothing

kama sio 1, aimaanish number inayofuata ni mbili, yaweza kuwa 8 au 0.
possibilities are endless
 
Yap huo ni mfumo wa maisha na sio dini

Elements za dini unazijua?

Kwa mujibu wa uislam dini ni moja tu uislam je unakubaliana na hoja hiyo?

Kwa mujibu wa uislam wasio na dini wote ni makafir

Duniani kuna maelfu ya dini na maelfu ya miungu, so kwa mujibu wako dini hizo zote zinatambulika kwenye uislam kwasababu?
Kwa mujibu wa Uislam dini zipo nyingi ila inayokubalika kwa Mungu ni Uislam.

Kwenye Quran wametajwa wa aina 3 kuna Makafir, Yahudi na Wanaswara.

Kafir hana tofauti na mpagani.
Yahudi ni wayahudi.
Naswara ni wakristo.
Yahud na Naswara kwa lugha nyengine wameitwa Ahlul Kitaab.

Dini ni mfumo wa maisha. Unaweza ukawa ni mfumo sahihi na usiwe sahihi.
 
Hauwezi kusema wewe na nani?

Kwani nani kasema atheism ina base kwenye kuamini au kutokuamini??

Nimesema atheism ni lack of belief, hizo habari za kuamini na kutiamini hapo ziningiaje?
Ok kwahiyo atheism ni lack of belief ila sio kwamba atheist haamini?ndio unavyokusudia si ndivyo?
 
Mungu wetu husamehe, akifanya toba akamwomba Mungu amsamehe kwa kuamua mambo yake bila kumshirikisha na kumwomba amwonyeshe suluhu kadri ya mapenzi yake Mungu atafanya

Hakuna kosa kubwa kwake muumba lisilosameheka tukifanya toba
Hoja yangu huyo mke hana sababu ya kuleta utata pindi akijua mumewe hana dini.
 
"Kwa mujibu wa uislam"

As long as umesem kwa mujibu wa uislam basi hiyo ni boundary kwamba wasio waislamu haiwahusu maana siyo haiko katika muktadha wa universal

Ushawahi jiulize kwa mujibu wa hizo dini zingine zinauchukuliaje uislam?

Ushawahi kujiuliza kwa mujibu wa dini zingine zinajichukuliaje kama ni dini za haki au la?

Kwani dini gani ambayo imejinasibu kwa mujibu wa mafundisho yake kua sio dini ya haki na kuitaja dini yako kua ndio ya haki?

Sasa ukitaka tufanye hitimisho kwa kutumia keyword "kwa mujibu wa dini husika" kuangalia dini ipi ni ya haki tutapata ukweli, kweli hapo?
Kwa muktadha huo ndiyo Mungu kaweka siku ya hukumu. Ulimwengu haujaja kwa bahati mbaya na vilivyomo havipo kwa bahati mbaya.

Mtaenda kukutana naye aliyewaleta na atahukuku hizo ikhtilafu baina yenu. Atakayekuwa sahihi atajulikana asiyekuwa sahihi atajulikana pia.
 
Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
Screenshot_20210103-175401.png
 
Nani ulimuona kauliwa kwa kuachs uislamu.katika uislamu ukiacha kuswali swala tano,sio muislamu tena,na wapo wengi tu hawaswali swala tano,na wanatoka katika familia za kiislamu,hata huko arabuni,hapa Afrika,uliona nani kapewa adhabu.
Hapa ndo waislam huwa mnapoteza credibility..maana Hata vitu vilivyo wazi mnajaribu kuficha..Capital purnishment ya apostacy inajulikana wala sio siri lakini mko humu mnapotosha umma....Rashin Soodmand mfano mmoja huo aliyeuliwa kisa Dini.Kuanzia baba ake
 
inategemea na madai ya mwenye dini
kama unasema mungu wako anaishi mawinguni, basi tuoneshe
kama unasema mungu wako ni ng'ombe na afanya mazingaombwe basi tuoneshe

kama unasema mungu wako haonekani, asikiki, apimiki; basi ndugu kesi yako haina ushahidi
kwani mi ninaweza sema nina billioni moja, ila azipimiki, asioneki, na wala azishikiki

pointi yangu ni kwamba: mwenye madai ndio mtoa ushuhuda
emu tupe ushahidi wa mungu: na hakikisha ushahidi wa kisayansi
labda ulimwona, alipimwa sehemu, alipigwa picha..nk.

ushahidi ni juu yako

lasivyo, karibu nyumbani kwangu ninauza farasi mwenye mabawa na rangi ya kijani asilia; lakini sina ushahidi
ivyo inabidi uniamini..😂🤣
Wewe ndio umefikia point ya kudai ushahidi na ndio maana nikakuuliza huo una idea ya huo ushahidi unatakiwa uweje? Sasa mimi naona humu unadai ushahidi sasa ndio ungenieleza wewe swali nililokuuliza na sio kuniambia inategemea na madai ya mwenyewe dini wakati nakuona wewe ukiudai huo ushahidi kwa hivyo una idea huo ushahidi unatakiwa uweje.
 
Hapa ndo waislam huwa mnapoteza credibility..maana Hata vitu vilivyo wazi mnajaribu kuficha..Capital purnishment ya apostacy inajulikana wala sio siri lakini mko humu mnapotosha umma....Rashin Soodmand mfano mmoja huo aliyeuliwa kisa Dini.Kuanzia baba ake
Waislamu wapo kila pembe ya dunia na wanabadili hata hapa jirani na kwangu kuna jamaa kabadili dini kafuata dini ya mkewe kawa mkristo kutoka uislamu ila hakuna hata aliyemgusa kisa kabadili dini.
 
Kwa mujibu wa Uislam dini zipo nyingi ila inayokubalika kwa Mungu ni Uislam.

Kwenye Quran wametajwa wa aina 3 kuna Makafir, Yahudi na Wanaswara.

Kafir hana tofauti na mpagani.
Yahudi ni wayahudi.
Naswara ni wakristo.
Yahud na Naswara kwa lugha nyengine wameitwa Ahlul Kitaab.

Dini ni mfumo wa maisha. Unaweza ukawa ni mfumo sahihi na usiwe sahihi.
Dini ni mfumo wa maisha ila sio kila mfumo wa maisha ni dini...Inshort ili iwe dini lazima ihusishe imani ya vitu supernatural sasa huwezi kuwa na mfumo wa kibepari ikaitwa dini
 
Waislamu wapo kila pembe ya dunia na wanabadili hata hapa jirani na kwangu kuna jamaa kabadili dini kafuata dini ya mkewe kawa mkristo kutoka uislamu ila hakuna hata aliyemgusa kisa kabadili dini.
Hapa bongo Kuna Sharia?Hii ni nchi ya kiislam?mbona mnajitoa ufaham ili kutetea upuuzi?

Nchi yoyote ikishaanza kuwa na muslim majority ndo haya mambo yanakuwepo..ila wakiwa wachache they are the most peaceful people you can find
 
Wewe ndio umefikia point ya kudai ushahidi na ndio maana nikakuuliza huo una idea ya huo ushahidi unatakiwa uweje? Sasa mimi naona humu unadai ushahidi sasa ndio ungenieleza wewe swali nililokuuliza na sio kuniambia inategemea na madai ya mwenyewe dini wakati nakuona wewe ukiudai huo ushahidi kwa hivyo una idea huo ushahidi unatakiwa uweje.
sasa ndugu, we unasema kuna mungu. ukiulizwa una ushahidi, unauliza ushahidi gani.
aileti maana

tuseme mimi niseme wewe umeua mtu; polisi akadai ushahidi; mimi nikamuuliza ushahidi gani?
hili swali alidhilishi kuwepo kwa ukweli kwenye dai langu.
kwani, kama nilikuona umeua mtu, basi nitasame "nilimuona kaua mtu"
au, kama nilisikia umeua mtu, nitasema "nilisikia kaua mtu"
siwezi kumuuliza polisi ni aina gani ya ushaidi anataka, kwani jukumu la kutoa ushahidi ni ya yule anayedai

mimi nasema, mpaka sasa, HAKUNA USHAHIDI WA KUWEPO KWA MUNGU ULIOTOLEWA NA WAUMINI WOTE WA DINI ZOOOOTE!

nyie ndo mnapaswa kunipa ushahidi wa madai yenu: "kwanzia kufufuka, mbingu, shetani, malaika, pepo..nk.)

done
 
Swali langu lipo wazi kabisa kwamba huo ushahidi unaoutaka unajua unafananaje au una idea ya ushahidi wa kuwepo Mungu unavyotakiwa kuwa? Nimekupa mfano wa mie kutaka mtu kunipa ushahidi wa kuwa kweli kaoa,nikasema kwa haraka nitategemea kuoana cheti cha ndoa. Kama huna idea ya huo ushahidi unaweza ukaletewa ushahidi na ukakataa au ukaletewa kisicho ushahidi ukakubali.

Sasa wewe sema huyo Mungu ambaye wewe unataka ushaidi wake je huo ushahidi unafikiri unatakiwa uweje? Hata huko mahakamani sio kila ushahidi unakubalika au kutambulika.

Unataka kusikia sauti ya Mungu?
Kuoneshwa Mungu? Au vp ambavyo wewe unaona yapaswa Mungu kuthibitishwa?

Kwa sababu wapo watu wamejaribu kutoa ushahidi ila mmeona kuwa si ushahidi na ndio mnasema kuwa hakuna mtu aliyeweza kutoa ushahidi,sasa mie nimeona tatizo lipo kwenye huo ushahidi wenyewe ndio maana nikauliza hilo swali.
 
Hii point ila huwa inanipa maswali hadi nahisi kuchanganyikiwa na huwa naachana nayo. Huyo mwumbaji wa dunia yeye nani alimwumba???? Nikijibiwa hili vizr nakuwa mchungaji mwaka huu😇😇
Mahesabu wanayopiga viumbe ndiyo wanamkadiria kwa mahesabu hayo hayo aliyewaumba.

Wao wana wameumbwa, yeye hayupo kama uumbaji wake, yeye yupo tofauti na uumbaji wake. Yeye hang mwanzo wala mwisho, na ndivyo alivyokuwa, na ndivyo alivyo na ndivyo atakavyokuwa. Yeye yupo tofauti na uumbaji wake.

Wagiriki wana mtizamo mzuri wa kujifunza kuhusu utokeaji wa mungu. Laiti Mungu angelikuja kama sisi viumbe vyake kwa neno "kuumbwa" basi ulimwengu usingelikalika. Ungelisambaratika na kanuni zinazoongoza ulimwengu wetu zingelikuwa zenye kubadilika badilika.

Kwa sababu kila mungu angelitaka kuonyesha ukuu wake. Ulimwengu ungeligawanyika. Kungelikuwa na ukoloni wa ulimwengu 1 kuonyesha umwamba kwa ulimwengu mwengine.

Ugiriki imani yao hapa kale hapakuwa na kitu. Wakatokea Titans. Wakatokea miungu ambao wao walitokana na Titans. Kilichotokea ni vita baina yao kwa sababu Titans walijua zao lao lilikuwa linakuja kuwapindua na kusimika ukuu wa uungu. Vita ikapigwa!

Zeus ambaye ni zao laTatans ambao wao wanamuita ndiye aliyeumba binadamu baadaye akatengeneza silaha ya kuwadhibiti hao Titans na kuwalaani na wakatupwa gerezani.

Zao la Titans ambao ndiye likawa miungu iliyoweka huu ulimwengu lilikuwa ni la watatu. Zeus, Poseidon na Hades. Baada ya kushinda vita dhidi ya Titans ulimwengu uliyoumbwa uligawanywa kimamlaka. Lakini mbeleni walikuwa wanatofautiana.

Laiti Mungu angelitokea kwa tunavyopiga mahesabu ya makadirio kunasibisha uwepo wake na utokeaji wetu basi Mbinguni na ardhini kusingelikalika.
 
Back
Top Bottom