Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

mada ni pana sana, na mwisho wake huwa hakuna mshindi.
Aisee, hata kama ingekuwa ni kushindana au niambiwe nishindane na wajinga nyinyi, nisingeshindana sababu najua hamna hoja wala hamjawahi kuwa na hoja. Nachofanya hapa huwa nawaonyesha ni kwa namna gani mlivyo wajinga na hamfikirii mambo kiundani.
 
Tunarudi

Usione vyaelea, vimeundwa.
Aliyeviunda, na yeye aliundwa.
na
Aliyemuunda aliyeviunda, na yeye aliundwa.

Hiyo ndio chain halisi, hakuna majibu.
Kila mtu aendelee kuamini anacho kiamini.
Huu mjadala huuwezi. Namalizia kwa kukuuliza, huyo "na yeye aliundwa" yeye aliundwa na nani ?

Hizi akili mlizo pewa bure mtakuja kuulizwa kwanini hamzitumii inavyotakiwa.
 
Ndio nika
Hiyo ni limit ambayo ni lazima uijiwekee endapo utaamini uwepo wa mungu.

Hutakiwi kuhoji mungu alitokea wapi.

Mfano:
Kwenye dini ya kiislamu, ukihoji kuhusu chanzo cha mungu, unaambiwa ni kufuru na nidhambi kubwa.
Unaambiwa, we amini tu na ufuate alicho kuamrisha.
Hapo ndipo wanao pinga uwepo wa mungu wanapingana hiyo limit ya kuhoji.
Hata kwenye science kuna limit ambayo huwezi kuhoji mfano Energy, can not be created but it can be transformed into another form" huoni kama kuna vitu havina creation?
 
Kwa akili yako ya kawaida tu, unakubali ya kuwa kila kitu kina chanzo ?
Unapouliza kwa kusema "kila kitu" kina chanzo unamaanisha nini?

Nataka nijue hiyo kila kitu inakua na mipaka au haina mipaka

Maana kuna mwingine anaweza kusema kila kitu kina chanzo kwa dhana isiyo na mipaka halafu ukaja kukubaliana naye kwa baadhi ya vitu tu kua ndio vina chanzo kwa kuweka mipaka kua kitu fulani hakina chanzo

Kama ina mipaka basi swali lako la kuuliza kila kitu linakosa mantiki kwasababu kuna vitu viko nje ya dhana ambavyo navyo vilipaswa kuhusihswa ila hujataka kuvihusisha

Kama kila kitu ni neno ambalo liko openly na universal lisilo na mipaka tunaweza tukakupatia majibu

Ila kwanza tukabaliane hapo
 
Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
Ulifunga ndoa porini?
 
Bado kidogo uelewe.
"Kama hakuna kisicho na chanzo au mwanzo basi isingewezekana kupatikana chochote".

Ni kweli kabisa, ndio maana swali kama 'Mungu ametokea wapi' linazaliwa.

Maana huwezi kusema kuwa kuna mungu, alafu hutaki kusema ametokea wapi.

Wasio amini uwepo wa mungu wanasubiri kupata jibu la chanzo cha mungu.

Ila, jiulize swali...ukiacha vitu vilivyo anzishwa na binadamu, dunia na vilivyomo na vitu nje ya dunia vimeletwa na nani...?

Ukisema: Vimeletwa na Mungu, je mungu alitokea wapi...? Jibu hauna.

Ukisema: Vimezuka tu...jibu hili lina ukakasi pia.

Kazi kwako.
Amini au usiamini, live your life.
Nafikiri hujanielewa,nachosema ni kwamba wote tunajua kuwa kila kitu kina mwanzo/chanzo ila lazima kiwepo ambacho hakina mwanzo/chanzo ili ndio kiwe chanzo cha vitu vyengine vyote,ikiwa hakuna kisicho na chanzo basi tusingeweza kupata chochote.

Kwa sababu ili kitu kipatikane lazima kuwepo na kitu chengine kilichokuwepo kabla,sasa tunapotofautiana ni kwamba wewe haukubali kuwepo kisicho na chanzo/mwanzo.
 
Tunaanza kuzikataa dini kwanza, then taratibu tutafika huko. Dini zimeletwa ili kumfanya binadamu afuate vigezo na masharti, ila ni upuuzi ambao hauna maana yoyote.
Ninapoona watu wanagombana kisa dini huwa najiuliza ina maana Mungu ndiyo karuhusu haya yote

Anyway mi naamini Mungu yupo ila hizi dini ndiyo sasa nimeanza kuwa na mashaka nazo sana kwa kweli
 
we jamaa unachukulia JF imejaa vichwa panzi eti?Kama ni ivo Basi hakuna muislam duniani maana mtu akinywa pombe ameacha uislam,akizini ameacha uislam,akiiba ameacha uislam asiposwali asubuhi ameacha uislam.
Hapa tunaongea Kutoamini tena katika Uislam either kwa kubadili dini au kuwa atheist.
Najua uarabuni wapo wengi ila wanaishi kwa mficho hamna anayejitangaza na msikitini wanahudhuria wasishtukiwe....Mimi naweza kukutajia Atheists 20 wanaoishi marekani wewe nitajie Atheist mmoja anayeishi publicly Saudia au Pakistan au Afghanistan au Iran
Katika uislamu,yapo mambo ukifanya unatoka nje ya waislamu,na hivyo hivyo yapo mambo ukifanya yanakurudisha katika uislamu,kwa mfano ulitenda kosa,halafu wewe mwenyewe,ukaomba msamaha kwa Mungu,lakini usilirudie tena kosa hilo.Kwa hiyo kuacha uislamu na kurudi katika uislamu ni wewe na Mungu wako.
Hivi wewe katika akili yako,unafikiri waarabu wote ni waislamu duniani?Wapo waarabu wakristo,wapo waarabu atheist,wapo waarabu waislamu,na wao katika nchi za kiarabu.Wewe unachukulia sheria ya nchi ya kiarabu na sheria ya dini ya kiislamu.Zipo nchi za kiarabu,zimejiwekea sheria zao za nchi,kuwa watu wawe ni dini sina fulani tu.Huko ulaya unakosema,wacha kuwa atheist,zipo nchi za ulaya,ukiwa dhehebu lisilokuwa la nchi hiyo,unakosa stahiki nyingi tu.
1.Wataka kuniambia hujawahi kusikia kuwa maelfu ya wayahudi,waliuliwa Ujerumani na Hitler,kwa kukusanywa na kuchomwa moto,au wewe wajuwa kuwa Ujerumani ni uarabuni.
2.Wataka kuniambia hujawahi kusikia vita vya waprotestant na wakatoliki,Ireland ya Kaskazini?Ireland,ukiwa protestant,unaonekana hufai,au wafikiri Ireland ni uarabuni.
3.Hujawahi kusikia jinsi wakristo na waislamu,wasivyotakiwa china.
4.Wataka kuniambia hukuwahi kusikia kama Israel hawathamini dini za uislamu na ukristo .
5.Hujawahi kusikia,Ufaransa,inapiga vita waislamu kuvyaa mavazi ya kiislamu?Na mpaka waislamu wanavyujiwa heshima,na wanaofanya hivyo hawashitakiwi.
6.Wataka kuniambia hujawahi kusikia kuwa Uingereza,wanathamini Uangalikhana,kuliko dhehebu lolote la kikristo wala kiislamu.
 
Aisee, hata kama ingekuwa ni kushindana au niambiwe nishindane na wajinga nyinyi, nisingeshindana sababu najua hamna hoja wala hamjawahi kuwa na hoja. Nachofanya hapa huwa nawaonyesha ni kwa namna gani mlivyo wajinga na hamfikirii mambo kiundani.
Thank you
 
Kwanza unajitengenezea Sheria then unaniulizia nani aliyeivunja akaadhibiwa.
Tuanze kwanza na hiyo Sheria uliyoitengeneza Wapi imeandikwa asiyeswali swala tano sio muislam?
Lazima uelewe kila kikundi chochote cha watu,wanaunda umoja wao wana katiba yao,ya kuendesha kikundi husika.Kwa mfano viko vikundi,vimeweka masharti fulani,usipoyafuata umeshajitoa uanachama,kwa mfano hujahudhuria vikao vitatu vya chama,bila maelezo yoyote ya kuridhisha,tayari uwanachama huna.Zipo dini,usipohudhuria katika nyumba zao za ibada,tayari umeshatoka katika dini hiyo,hata ukifariki hawakuziki.
Na katika uislamu una kitabu cha Qur'an na muongozo wa Mtume Muhammad,katika uislamu mtume anasema "Tofauti kati ya muislamu na asiye muislam ni SWALA",USIPOSWALI HUNA UISLAMU.
 
Easiest way

Tupe uthibitisho uliokufanya ujue mungu yupo kisha tuupime kama ume qualify
Sasa hapo swali langu utakuwa umelikwepa na msingi wa hilo swali ni kutaka kuondoa hili tatizo la mtu kujaribu kutoa yale anayoona ni uthibitisho wa kuwepo Mungu ila nyie mkambwambia kuwa sio uthibitisho.

Kwahiyo nilichokiona mie kuwa kuna tatizo kwenye hichi kinachoitwa uthibitisho wa kuwepo Mungu,hapo ndio tatizo lililopo kwa maana naona haijafahamika huo uthibitisho unatakiwa kufananaje?
 
Katika uislamu,yapo mambo ukifanya unatoka nje ya waislamu,na hivyo hivyo yapo mambo ukifanya yanakurudisha katika uislamu,kwa mfano ulitenda kosa,halafu wewe mwenyewe,ukaomba msamaha kwa Mungu,lakini usilirudie tena kosa hilo.Kwa hiyo kuacha uislamu na kurudi katika uislamu ni wewe na Mungu wako.
Hivi wewe katika akili yako,unafikiri waarabu wote ni waislamu duniani?Wapo waarabu wakristo,wapo waarabu atheist,wapo waarabu waislamu,na wao katika nchi za kiarabu.Wewe unachukulia sheria ya nchi ya kiarabu na sheria ya dini ya kiislamu.Zipo nchi za kiarabu,zimejiwekea sheria zao za nchi,kuwa watu wawe ni dini sina fulani tu.Huko ulaya unakosema,wacha kuwa atheist,zipo nchi za ulaya,ukiwa dhehebu lisilokuwa la nchi hiyo,unakosa stahiki nyingi tu.
1.Wataka kuniambia hujawahi kusikia kuwa maelfu ya wayahudi,waliuliwa Ujerumani na Hitler,kwa kukusanywa na kuchomwa moto,au wewe wajuwa kuwa Ujerumani ni uarabuni.
2.Wataka kuniambia hujawahi kusikia vita vya waprotestant na wakatoliki,Ireland ya Kaskazini?Ireland,ukiwa protestant,unaonekana hufai,au wafikiri Ireland ni uarabuni.
3.Hujawahi kusikia jinsi wakristo na waislamu,wasivyotakiwa china.
4.Wataka kuniambia hukuwahi kusikia kama Israel hawathamini dini za uislamu na ukristo .
5.Hujawahi kusikia,Ufaransa,inapiga vita waislamu kuvyaa mavazi ya kiislamu?Na mpaka waislamu wanavyujiwa heshima,na wanaofanya hivyo hawashitakiwi.
6.Wataka kuniambia hujawahi kusikia kuwa Uingereza,wanathamini Uangalikhana,kuliko dhehebu lolote la kikristo wala kiislamu.
Maneno ef moja point sifuri....Hujajibu hoja yangu wala hujaleta hoja yoyote
 
ok, mimi nasema hakuna nyani mwenye mabawa
hakuna tambi yenye miguu
pia hakuna bruce lee aliezaliwa tanga

kwa logic yako, hivyo vyote ni ushahidi kwamba vipo..

kusema kitu hakipo, hakimaanishi kipo
hakipo maana yake hakuna ushaidi kipo; nafasi yake inaweza kuchukuliwa na kitu chochote ikiwemo nothing

kama sio 1, aimaanish number inayofuata ni mbili, yaweza kuwa 8 au 0.
possibilities are endless
Hayo yote wasema wewe peke yako,hukuyakuta ulipozaliwa ul,sio wengi wanasema hivyo.Ingekuwa hayo unayosema,yalisemwa,na wewe ukayakuta,ulipozaliwa,ndio yanakuwepo.
 
Sasa hapo swali langu utakuwa umelikwepa na msingi wa hilo swali ni kutaka kuondoa hili tatizo la mtu kujaribu kutoa yale anayoona ni uthibitisho wa kuwepo Mungu ila nyie mkambwambia kuwa sio uthibitisho.

Kwahiyo nilichokiona mie kuwa kuna tatizo kwenye hichi kinachoitwa uthibitisho wa kuwepo Mungu,hapo ndio tatizo lililopo kwa maana naona haijafahamika huo uthibitisho unatakiwa kufananaje?
Uthibitisho gani ulioutoa ambao watu wameukataa ukakupa jibu kua kuna tatizo?

Wewe unakubali mungu yupo kwa uthibitisho upi, uweke hapa tuujadili usianze kutubashiria majibu as if upo vichwani mwetu
 
Ninapoona watu wanagombana kisa dini huwa najiuliza ina maana Mungu ndiyo karuhusu haya yote

Anyway mi naamini Mungu yupo ila hizi dini ndiyo sasa nimeanza kuwa na mashaka nazo sana kwa kweli
Kwani mbona Mungu karuhusu vitu vingi tu,wapo watu wanahoji kama kweli Mungu yupo anaruhusu vp watoto wadogo wazaliwe wakiwa na ulemavu na mfano wa hayo,ila wewe hayo hayajakufikirisha we yamekufikirisha ya dini.
 
Hapa ndo waislam huwa mnapoteza credibility..maana Hata vitu vilivyo wazi mnajaribu kuficha..Capital purnishment ya apostacy inajulikana wala sio siri lakini mko humu mnapotosha umma....Rashin Soodmand mfano mmoja huo aliyeuliwa kisa Dini.Kuanzia baba ake
Ndio nikakuambia huwa mnachanganya uislamu na muislamu.Aliyesema kuhusu Rushd ni Muislamu sio uislamu.Pia huwa mnachanganya sheria ya nchi ya kiarabu na uislamu,au nchi ya Uajemi na uislamu.
 
Uthibitisho gani ulioutoa ambao watu wameukataa ukakupa jibu kua kuna tatizo?

Wewe unakubali mungu yupo kwa uthibitisho upi, uweke hapa tuujadili usianze kutubashiria majibu as if upo vichwani mwetu
Point yangu hapa sio kuujadili uthibitisho wangu na wala hakuna niliposema nina huo uthibitisho.
 
Point yangu hapa sio kuujadili uthibitisho wangu na wala hakuna niliposema nina huo uthibitisho.
Kama wewe hutaki tujadili uthibitisho wako tutakua na hakika gani ya kwamba unajua kua mungu yupo kwa uthibitisho?
 
Hapa bongo Kuna Sharia?Hii ni nchi ya kiislam?mbona mnajitoa ufaham ili kutetea upuuzi?

Nchi yoyote ikishaanza kuwa na muslim majority ndo haya mambo yanakuwepo..ila wakiwa wachache they are the most peaceful people you can find
Sasa hoja ya kwamba kwenye uislamu hakuna uhuru watu wanauliwa ukibadili dini au kuwa atheist inakuaje ikiwa kumbe hicho kitu kinafanyika kwa nchi zenye kufuata sharia tu? Hizo nchi za kufuata sharia ni chache kuliko nchi ambazo hazifuati sharia na kuna waislamu wengi tu mfano Tanzania,kwahiyo hoja yangu ni kupinga madai ya kwamba et waislamu huogopa kubadili dini au kuwa atheist kwa sababu ukifanya hivyo unauliwa wakati kumbe penye kufanyika hivyo ni baadhi tu ya nchi chache.
 
Kama wewe hutaki tujadili uthibitisho wako tutakua na hakika gani ya kwamba unajua kua mungu yupo kwa uthibitisho?
Bado hapo unanijadili mimi binafsi,nishasema hakuna nilipodai kuwa nina uthibitisho wa kuwepo Mungu kwahiyo usielekeze nguvu kwangu mimi binafsi.
 
Back
Top Bottom