Wakuu habari,
Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.
Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine
Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.
Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.
Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.
Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?