Nitamuita Shujaa wa Taifa Mbunge yeyote atakayependekeza kodi kwa Wabunge

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,396
12,979
Kwa kweli wananchi wa Tanzania hasa wafanyakazi wa serikali wamesota sana kwa miaka 6 iliyopita. Kuiishi miaka yote hiyo bila kuongezewa mshahara wakati ghalama za maisha zikiendelea kupanda kwa kweli siyo mchezo.

Hapa lazima tuwapongeze hawa wafanyakazi. ingekuwa nchi za wenzetu has kama za ndugu zetu kule Bondeni naamini kabisa wangeitisha Kunji za kufa mtu. Thanks God, this is Bongoland!

Straight to the point. Naona Wabunge wetu safari hii wamekuja na mapendekezo ya Uzalendo pamoja na ile kodi ya kidogo iliyoitwa na Mh. Zungu kuwa ni ya Uzalendo, ile ya makato ya siku kila uki-recharge voucher. Ni wazo zuri, ila kwa nini hatokei Mbunge mmoja akapendekeza makato kwenye mishahara na marupurupu yao manono. Mimi nitamuita SHUJAA WA TANZANIA.

Kwanini miaka yote hii hatokei walau Chizi moja tu humo mjengoni akaja na wazo hili; kila moja wetu anajua kuwa halitakubaliwa lakini litampa ushujaa mleta hoja.
 
Ni chanzo kipya cha mapato, hawawezi kukiona kwakuwa ki nguoni mwao.
 
Mkuu wanasiasa wetu ni WABINAFSI mnoo na wapo hapo walipo ili kujinufaisha na ndio maana wapo tayari kwa lolote ili mradi tu wapate hayo madaraka.

Mfumo wetu ni wa kinyonyaji mnooo inakuwaje watu Elimu sawa mmoja unamlipa 12M na mwingine laki 5.
Kuna watu wapo hapo kazi yao kubwa ni kuchekesha tu na kuchangamsha bunge. Imagine wakina Msukuma, Mlinga, the Big Sex Payers nao wanalamba 12 m kila mwezi.
 
Ila hii kitu inauma jamani.
Na akimaliza anachukua pensheni ambayo hata hajaichangia.

Muda huo kuna mwalimu anasahisha mitihani ya mkoa mzima kwa wiki mbili kaondoka na laki na nusu 😢😢😢

Wabunge ni wanafiki na wabinafsi sana! Inabidi wanaharakati waanzishe wao kuishinikiza serikali ipeleke muswada wa kupunguza mipunga ya ubunge maana ni kufuru ,nimeona Mwanaharakati Dr Cyril Christopher amelianzisha.

Mafao ya Mil 250 anapewa bila kukatwa(Kuchangia) aisee wabunge wametudharau sana.
 
Wabunge ni wanafiki na wabinafsi sana! Inabidi wanaharakati waanzishe wao kuishinikiza serikali ipeleke muswada wa kupunguza mipunga ya ubunge maana ni kufuru ,nimeona Mwanaharakati Dr Cyril Christopher amelianzisha.

Mafao ya Mil 250 anapewa bila kukatwa(Kuchangia) aisee wabunge wametudharau sana.
Na hiyo mil 250 miaka mitano tu ya ubunge wengine wakistaafu hiyo miaka 60 anapata ml 80 tena kwa kuisotea... sio fair kabisa sio fair.

Maslahi ya wengine serikali haina hela ya kwao mpunga upo wanasiasa wanatukosea sana.
 
Wabunge ilitakiwa wakatwe kati ya 20% to 25% kwa kila mapato yao.

Kwa namna hii wangekuwa na feeling ya what it take ku-earn then kabla fedha haijaungia mfukoni, TRA inakata kutoka kwenye pay yao.

Otherwise tuna watu ambao hawana hisia za nini wafanyakazi wa nchi hii wanapitia.
 
Back
Top Bottom