Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 80,836
- 93,617
Anza na kodi mshahara wa Rais kwanza awe mfanoView attachment 1822510
View attachment 1822511
1. Mpango wa kupinga tofauti kubwa ya kipato baina ya wabunge na watumishi wa serikali (hasa walimu, madaktari na wanajeshi) utaanza kwa kusambaza jumbe, picha na video, ili kuwajulisha watumishi husika juu ya tofauti iliopo. Nitaandaa jumbe hizo kwa lugha inayotafakarisha.
2. Ifahamike, ninapinga ni utofauti wa kipato baina ya wabunge na watumishi kwa sababu malipo yao yanatokana na kodi za watanzania. Wenye mamlaka waamue kupunguza utofauti huu kwa kushusha malipo ya wabunge au kuwaongezea watumishi wengine. Wataaua wenye maamuzi. Lakini tofauti iliyopo sasa haikubaliki.
3. Sambamba na kusambaza jumbe hizo, nitaandaa 'online petition' kwa watu wote wanaoguswa waweze kutia saini. Pia nitaandika barua (nakala ngumu) kwenda kwa waziri mkuu ambaye ndo kiongozi wa shughuli za serikali bungeni kueleza jambo hili.
4. Kabla ya kuifikisha barua kwa w/mkuu, nitaisambaza kokote ninapoweza ili watumishi husika watie sahihi zao.
Hili ni zoezi endelevu lisolokoma (Continuous & endless). Mbinu ya mwisho itakuwa ni kuitisha mgomo wa watumishi kupinga tofauti hii kubwa ya mgawanyo wa kodi za watanzania.Hakuna sababu zozote za msingi za utofauti mkubwa wa malipo ya wabunge na watumishi wengine yanayotokana na kodi za wananchi. Katika nchi zinazojitambua, hili jambo halipo.
5. Nakaribisha maoni. Nitapokea yale yatakayosaidia mpango huu na kupuuza yale ya kukwamisha.
Watu wa video graphics, cartoonists na yyt anayeona anaweza kufanya kazi hii (overtly or covertly), anicheki kwa 0713933736 (whatssap and sms tu).