kelvin complex
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 605
- 580
Habari, naomba mwenye uzoefu wa kutumia mfumo wa kupata leseni ya biashara online uitwao tausi portal unaopatikana katika tovuti ya Tamisemi, anisaidie namna ya kupata mawasiliano ya huduma kwa wateja, kwani mtandao umekuwa na changamoto ya kuchelewa kutoa control number ili kupata leseni ya biashara online, pia kila ninapojaribu kuingia kwenye account yangu unatoa message ya either bad credentials or bad gate away hali inayoashiria mfumo huu una changamoto. Nina siku zaidi ya nne tangu nijisajili lakini hali imekuwa bado changamoto
Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
====
Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais TAMISEMI mkoani Dodoma Erick Kitali, ameeleza kwamba mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri ujulikanao kama Tausi utasaidia kupunguza urasimu uliokuwepo hapo awali kwenye ukusanyaji wa mapato.
Kitali alitoa tathmini hiyo wakati wa mahojiano maalum na The Chanzo yaliyofanyika ofisini kwake mjini hapa hivi karibuni kuhusu mfumo huo unaotajwa kubuniwa na wataalam wa ndani ya nchi.
Ukipewa jina la ndege huyo mzuri anayepatikana nchini Tanzania, Tausi umebuniwa baina ya kubainika uwepo wa changamoto mbalimbali kwenye mfumo uliokuwa unatumika hapo awali, ikiwa ni pamoja na uzoefu wa mlipa kodi.
“Mfumo huu utasaidia kupunguza muda, kuondoa urasimu uliokuwepo kwa baadhi ya sehemu,” Kitali alisema kwenye mahojiano hayo. “Na sehemu nyingine tulikuwa tunaambiwa kwamba kuna rushwa tumepunguza kwa sababu hukutani moja kwa moja na mwananchi.”
Pamoja na mambo mengine, mfumo wa Tausi humsaidia mteja kufanya malipo kwa kutumia VISA, MasterCard na namba ya malipo kutoka Mfumo wa Malipo wa Kielektroniki wa Serikali (GePG).
Mfumo huo pia humsaidia mteja kujihudumia mwenyewe, hali ambayo haimlazimu tena kwenda ofisi za halmashauri kuomba, au kulipia, tozo, ushuru, leseni, faini au vibali mbalimbali badala yake anaweza kufanya mwenyewe kupitia dirisha la mteja, au Taxpayer Portal.
Kabla ya ujio wa mfumo huo, Serikali ilikuwa inatumia mfumo wa LGRCIS, au Local Government Revenue Collection Information System, ambao Kitali alisema kwenye mahojiano yake na The Chanzo kwamba ulipaswa ubadilishwe ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia.
Akizungumzia kuhusu namna wananchi walivyoupokea mfumo huo mpya, Kitali alisema mpaka sasa muitikio ni mkubwa.
“Kwa sababu wananchi walikuwa wanapata changamoto ya kupoteza muda mwingi sana kwenda kufuatilia huduma,” alisema. “Ule urahisi wa kufanya malipo mbalimbali ya Serikali umesaidia wananchi kuwa na muitikio mkubwa.”
“Umeongeza uaminifu kwa wananchi kwa Serikali yao kwa sababu wana uhakika na fedha wanayoilipa inakwenda moja kwa moja kwenye Serikali,” aliongeza Kitali. “Pia, mfumo huu umesaidia fedha zinazokusanywa [na halmashauri] zinapelekwa benki kwa wakati.”

single gallery | Kinondoni Municipal Council
kinondonimc.go.tz