Utumishi na TAMISEMI, huu ni mkakati maalum kuzuia maombi ya uhamisho kwa watumishi wa umma?

Ntemii

JF-Expert Member
May 25, 2022
290
525
Tangu kuanzishwa na kufunguliwa kwa mfumo wa watumishi portal ess.utumishi.go.tz na kuunza kutumika rasmi mnamo tarehe mosi ya mwezi september.

Ukiwa na lengo la kupokea na kushughulikia maombi ya uhamisho kwa watumishi wa umma,ambapo lengo ni kupunguza urasimu na kuondoa paper work na kurahisisha uchakataji wa maombi hayo.

Watumishi wa umma walihamasika na wengi wamejisajiri katika mfumo huu ambao pia unawapa nafasi za kupata taarifa mbalimbali ikiwamo upatikanaji wa salary slips pamoja na kuomba mikopo online ukiachilia mbali maombi ya uhamisho,hakika mfumo huu umekua na msaada.

Hoja yangu ni hii hivyo ningeomba wahusika watupatie majibu.

Mfumo tangu kunzishwa kwake umekua na matatizo lukuki hasa upande wa uhamisho kwa watumishi,kuna wakati mfumo una load muda mrefu bila mafanikio yoyote.

Mfumo kupoteza taarifa za watumishi waliomba maombi ya kubadilishana baina yao (incoming exchange request),hivyo kushindwa kuendelea na maombi kati ya watumishi wanaohitaji uhamisho wa kubadilishana.

Wasimamizi wa watumishi kushindwa kuchakata maombi (request approval)hasa ngazi za halmashauri wakiwa na sababu kwamba wao hawajui kutumia mfumo na hawana mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo huo.

Pia ili kupata msaada kupitia changamoto za kimfumo mawasiliano yaliyotolewa na ofisi ya utumishi namba zao hazipatikani ama nyingine kuita siku nzima bila mafanikio,barua pepe nayo hazijibiwi.
IMG_4118.jpg



IMG_4120.jpg

Je hii ni mbinu mpya ya ofisi ya utumishi na tamisemi kuzuia maombi ya uhamisho kwa watumishi wanao teseka kupata uhamisho ambao ni haki yao kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi.

Maombi kwa njia ya barua yamepigwa marufuku,maombi kwa njia ya mtandao nayo vikwazo ni vingi,je ni nini hatma ya watumishi hawa.

Mawaziri wa wizara husika sikieni kilio chetu.
 
Back
Top Bottom