Dodoma: Maombi ya leseni ya biashara kupitia njia ya mtandao (online) Kuna usumbufu mkubwa sana kuliko kwenda manispaa physically

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,737
Ninazungumza haya nikiwa Nina wiki Sasa imekata leseni ya biashara sijapata, Tena siyo leseni mpya nimetuma maombi ya kurenew leseni yangu ya Zamani lakini kilichotokea mpaka nimechoka.

Sasa sijajua kinachoendelea ni Nini hapo wakati kabla ya serikali kuelekeza wafanyabiashara waombe kupitia online, mwanzo walikua wanapata kiurahisi kuliko huu mfumo waliouanzisha.

Nakumbuka nilichukua leseni manispaa kiurahisi pamoja na kupanga foleni ilinichukua masaa matatu control namba ilitoka nikalipia Kisha niliondoka na leseni yangu ndani ya masaa matatu.

Huu mfumo wa online haswa hapa dodoma nahisi wanaohusika nao wanajisahau sana/WANAFANYA kazi kwa mazoea na ndiyo maana Hawa "approve" documents kwa wakati ili watu wapate leseni wafanye Mambo mengine.

Maoni Yangu : serikali/wahusika watafute njia nzuri ya uwajibikaji ili kuepusha kelo Kama hizi kwa wateja haiwezekani mtu afatilie leseni wiki nzima Tena ana renew na documents zote zipo hapa kutakua na urasimu siyo BURE.
 
Hayo ndiyo mambo ya serikali yako na mtandao wake wa hovyo wa TAUSI.

Yaani unaweza ukafikiri labda hayo malipo ya yenyewe ya leseni yanamnufaisha mfanyabiashara anayehangaishwa na huo mfumo wa mpya.
 
Hayo ndiyo mambo ya serikali yako na mtandao wake wa hovyo wa TAUSI.

Yaani unaweza ukafikiri labda hayo malipo ya yenyewe ya leseni yanamnufaisha mfanyabiashara anayehangaishwa na huo mfumo wa mpya.
Hakika mkuu huu mfumo haswa hapa dodoma umenisikitisha sana.
 
Hata mie nina wiki nafuatilia jiji ilala. Tena Ilala jiji, watumishi hawana majibu kama wako kazini. Wako kama vile wako Manzese.
 
Ukiwa kwenye jiji la Dar Es Salaam na una shida ya Leseni ya Biashara kupitia mfumo wa TAUSI usisite kunicheki nitakusaidia.

Lakini pia ukihitaji:-
✓Kusajili jina la kampuni
✓Kusajili kampuni
✓TIN
✓Business proposal & Plan zilizonyooka.

Dm ipo widely Open 24/7.
 
Hata mie nina wiki nafuatilia jiji ilala. Tena Ilala jiji, watumishi hawana majibu kama wako kazini. Wako kama vile wako Manzese.
HATARI SANA MKUU, HAWA JIJI HUWA WANAIFANYA SERIKALI KAMA YA BIBI YAO.
 
Ukiwa kwenye jiji la Dar Es Salaam na una shida ya Leseni ya Biashara kupitia mfumo wa TAUSI usisite kunicheki nitakusaidia.

Lakini pia ukihitaji:-
✓Kusajili jina la kampuni
✓Kusajili kampuni
✓TIN
✓Business proposal & Plan zilizonyooka.

Dm ipo widely Open 24/7.
Acha uongo. Ina maana hao wote wanaolalamika wajinga. Wewe ndio mwerevu. Usije ukawa ndio unatoa leseni pori.
 
Acha uongo. Ina maana hao wote wanaolalamika wajinga. Wewe ndio mwerevu. Usije ukawa ndio unatoa leseni pori.
Sikulaumu,.najua kuishi kwako kwenye jamii iliyojaa wizi na utapeli, ndiyo kunafanya uchukulie kila unayemuona ni mtu wa namna hiyo.

NB: Hakuna sehemu nimesema kwamba Mimi ni mwerevu kuliko watu wote.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom