Nisaidieni hii hesabu ya makato kuhusu kodi ya TRA maana nahisi nahujumiwa

Vladmir Putini

JF-Expert Member
Mar 22, 2022
777
1,442
Wakuu habari za muda huu.

Kuna kampuni hivi jina niipe jina la X imefilisika, kwa hiyo ikabidi wafanyakazi wasitishiwe mikataba yao (redandacy).

Hivyo basi kwa sababu hilo suala liko kisheria (kupunguzwa kazini) ikanibidi na mimi niwemo kwenye orodha ya wanaopunguzwa kazini.

Sheria zote zimefatwa za watu kupunguzwa kazini, kwa hiyo ikabidi kila mwajiriwa alipwe kiasi flani cha pesa ili aachane na kampuni totally.

Niweke wazi tu bila kuficha hesabu yangu ilipigwa ikaja kama 2.7 milion hivi ambayo natakiwa nilipwe ili niachane na hiyo kampuni.

Kilichinifanya nije hapa ni hayo makato yatakayokatwa kutoka kwenye hiyo 2.7 milion ndiyo yamenikimbiza nikamwacha mwajiri mezani kwa kuhisi ananiibia.

Sasa wale wenye ujuzi na makodi ya TRA naombeni mnisaidie kujibu maswali yafuatayo.

1. Ni kodi asilimia ngapi (%) ambayo mwajiriwa hukatwa na TRA kutoka mshahara wake ?

2. Je, kisheria mtu anaepunguzwa kazini (anapoteza ajira) kwa kustishiwa mkataba, stahiki zake anazolipwa na aliyekuwa mwajiri wake zinapaswa kukatwa kodi pia ?

3.Kwenye hii 2.7 milion mwajiri amenambia kodi ni zaidi ya laki 5 na nusu, imenibidi nipate wazimu nimwache mezani niondoke kwanza.

Maana nimejipigia hesabu ya haraka haraka tu, kipindi nalipwa laki 5, kodi ya TRA ilikuwa inalipwa 14,000 tu.

Hivyo nikafikiri labda 2.7 milion ina laki tano tano kama 5 hivi na point.

That means kodi ya TRA ingekuwa 14,000 × 5 = almost 70,000 elfu.

So nilidhani labda kwenye 2.7 milion kodi ya TRA ingekuwa labda 90 elfu mpaka laki moja.

Sasa mwajiri ananambia kwenye 2.7 milion kodi ya TRA ni laki 5 na 78 elfu, je ni sawa hii au naibiwa .
 
Ni kweli lazima utakatwa kodi sababu kodi inakatwa kwenye mapato yatokanayo na ajira, uwekezaji na bishara. hiyo laki 5 bado hesabu siyo sawa sababu inatakiwa kinachozidi 1,000,000/= unazidisha mara 30% jumlisha 128,000/= shilingi kwa maana 2,700,000/= toa 1,000,000/= sawa na 1,700,000 mara 30% unapata 500,000/= jumlisha 128,000/= inakuja 628,000/=

Mapato kwa MweziKiwango cha Kodi
Mapato yasiyozidi Sh.270,000Hakuna Kodi
Mapato yanayozidi Sh.270,000 lakini hayazidi Sh. 520,0008% ya mapato yanayozidi sh. 270,000
Mapato yanayozidi Sh. 520,000 lakini hayazidi Sh. 760,000Sh.20,000 + 20% ya mapato yanayozidi Sh.520,000
Mapato yanayozidi Sh. 760,000 lakini hayazidi Sh. 1,000,000Sh.68,000 + 25% ya mapato yanayozidi Sh760,000
Mapato yanayozidi Sh.1,000,000Sh.128,000 + 30% ya mapato yanayozidi Sh. 1,000,000
 
Ni kweli lazima utakatwa kodi sababu kodi inakatwa kwenye mapato yatokanayo na ajira, uwekezaji na bishara. hiyo laki 5 bado hesabu siyo sawa sababu inatakiwa kinachozidi 1,000,000/= unazidisha mara 30% jumlisha 128,000/= shilingi kwa maana 2,700,000/= toa 1,000,000/= sawa na 1,700,000 mara 30% unapata 500,000/= jumlisha 128,000/= inakuja 628,000/=

Mkuu ulichokisahau hapo ni kuwa kabla ya kufanya calculation ya kiasi kwanza unatoa kiasi ambayo mfanyakazi anapaswa kuchangia kwenda kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF etc). Ikiwa alikuwa hana mfuko wa hifadhi ya jamii ndio itakwenda kama ulivoelezea

Kodi yake itakuwa ((1,700,000 - NSSF deduction)x30%) + 128000)
 
asante sana kwa kuliweka vizuri zaidi kiongozi
 
Wakuu habari za muda huu.

Kuna kampuni hivi jina niipe jina la X imefilisika, kwa hiyo ikabidi wafanyakazi wasitishiwe mikataba yao (redandacy).

Hivyo basi kwa sababu hilo suala liko kisheria (kupunguzwa kazini) ikanibidi na mimi niwemo kwenye orodha ya wanaopunguzwa kazini.

Sheria zote zimefatwa za watu kupunguzwa kazini, kwa hiyo ikabidi kila mwajiriwa alipwe kiasi flani cha pesa ili aachane na kampuni totally.

Niweke wazi tu bila kuficha hesabu yangu ilipigwa ikaja kama 2.7 milion hivi ambayo natakiwa nilipwe ili niachane na hiyo kampuni.

Kilichinifanya nije hapa ni hayo makato yatakayokatwa kutoka kwenye hiyo 2.7 milion ndiyo yamenikimbiza nikamwacha mwajiri mezani kwa kuhisi ananiibia.

Sasa wale wenye ujuzi na makodi ya TRA naombeni mnisaidie kujibu maswali yafuatayo.

1. Ni kodi asilimia ngapi (%) ambayo mwajiriwa hukatwa na TRA kutoka mshahara wake ?

2. Je, kisheria mtu anaepunguzwa kazini (anapoteza ajira) kwa kustishiwa mkataba, stahiki zake anazolipwa na aliyekuwa mwajiri wake zinapaswa kukatwa kodi pia ?

3.Kwenye hii 2.7 milion mwajiri amenambia kodi ni zaidi ya laki 5 na nusu, imenibidi nipate wazimu nimwache mezani niondoke kwanza.

Maana nimejipigia hesabu ya haraka haraka tu, kipindi nalipwa laki 5, kodi ya TRA ilikuwa inalipwa 14,000 tu.

Hivyo nikafikiri labda 2.7 milion ina laki tano tano kama 5 hivi na point.

That means kodi ya TRA ingekuwa 14,000 × 5 = almost 70,000 elfu.

So nilidhani labda kwenye 2.7 milion kodi ya TRA ingekuwa labda 90 elfu mpaka laki moja.

Sasa mwajiri ananambia kwenye 2.7 milion kodi ya TRA ni laki 5 na 78 elfu, je ni sawa hii au naibiwa .
Pole sana ila usipate tabu tena siku nyingine,unachukua Gross salary yako unatoa(10%)ya mshahara kwa ajili ya NSSF alafu iliyobakia unaingia hoogle andika PAYE CALCULATOR TRA itakuletea kiwango unachostahili kukatwa kwa kodi,alafu utachukua Gross salary-NSSF-PAYE=NET PAY/TAKE HOME, japo nafikiri pesa ya mkono wa kwaheri kama imetolewa huwa haikatwi
 
Mkuu ulichokisahau hapo ni kuwa kabla ya kufanya calculation ya kiasi kwanza unatoa kiasi ambayo mfanyakazi anapaswa kuchangia kwenda kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF etc). Ikiwa alikuwa hana mfuko wa hifadhi ya jamii ndio itakwenda kama ulivoelezea

Kodi yake itakuwa ((1,700,000 - NSSF deduction)x30%) + 128000)
safi hesabu nzuri
 
Back
Top Bottom