Nini sababu ya mikoa ya Kusini kuwa salama sana kibinadamu?

Nazungumzia Lindi na Mtwara haswa!

1. Kule husikii albino amechinjwa

2. Kule husikii wenye macho mekundu wameuawa kisa ni wachawi,

3. Kule husikii wenye upanja wamepigwa nondo ili zikatumike buchani

4. Kule husikii mtu amechunwa ngozi

5. Kule ni nadra kusikia wazazi, sijui mama, kutolewa uhai ili kuleta utajiri

6. Kule ni nadra kusikia makabila au koo wamepigana na kutoana uhai (ingawa kuna makabila mengi tu na yanapishana wakati mwingine),

7. Kule ni nadra kusikia mauaji ya kinyama kwa kisa cha mapenzi au kudaiana fedha

8. Kule ni nadra kusikia babu sijui mjomba amembaka mjuu/mpwa,

9. Kule ni nadra kusikia visa vya mabinti kutupa watoto chooni,

10. kule ni nadra kusikia binadamu ananyofolewa viungo ili vikauzwe vilete utajiri

11. Kule ni kawaida mgeni ukapokelewa na kuishi kama wananchi wengine bila wasiwasi n.k.

Wakati hali ikiwa hivyo, maeneo mengine kuna utofuti sana.

-Mauaji. JF kwa siku karibia nne au tano leo zimejaa thread za mauaji tu kwa visa vya mapenzi n.k. kisa cha hivi karibuni kuripotiwa ni hicho kilichotokea Tabora

-Ubakaji

-Utupaji wa watoto

-Ushirikina, kuna maeneo wazee eti wanakaa kabisa na kufanya tambiko ambapo mgeni anauawa kama kafara (mwalimu mmoja wa sekondari alikutana na dhahama hii sehemu fulani, galifuatwa akauawa na mwili wake kuchukuliwa kwenda kufanyiwa tambiko). pia, maeneo mengine tunaona na kusikia jinsi makaburi yanavyoenda kufukuliwa na maiti kutolewa na kurudishwa ilikotoka.....wafiwa wanaamka asubuhi wanakuta wamewekewa maiti ya ndugu yao waliomzika jana uwanjani.

na vingine vingi

Wajuzi/wafuatiliaji/ wasomi; sababu kubwa haswa ya hali hii ni nini? dini au?

Karibuni kwa uelimishaji.
Nimeishi Kusini wakati flani.. kwa kweli ni Sehemu Salama sana. Wenyeji wako poa hawana Ubaguzi wala Tatizo na Mgeni wa hali yoyote ile kiuchumi.
 
Nazungumzia Lindi na Mtwara haswa!

1. Kule husikii albino amechinjwa

2. Kule husikii wenye macho mekundu wameuawa kisa ni wachawi,

3. Kule husikii wenye upanja wamepigwa nondo ili zikatumike buchani

4. Kule husikii mtu amechunwa ngozi

5. Kule ni nadra kusikia wazazi, sijui mama, kutolewa uhai ili kuleta utajiri

6. Kule ni nadra kusikia makabila au koo wamepigana na kutoana uhai (ingawa kuna makabila mengi tu na yanapishana wakati mwingine),

7. Kule ni nadra kusikia mauaji ya kinyama kwa kisa cha mapenzi au kudaiana fedha

8. Kule ni nadra kusikia babu sijui mjomba amembaka mjuu/mpwa,

9. Kule ni nadra kusikia visa vya mabinti kutupa watoto chooni,

10. kule ni nadra kusikia binadamu ananyofolewa viungo ili vikauzwe vilete utajiri

11. Kule ni kawaida mgeni ukapokelewa na kuishi kama wananchi wengine bila wasiwasi n.k.

Wakati hali ikiwa hivyo, maeneo mengine kuna utofuti sana.

-Mauaji. JF kwa siku karibia nne au tano leo zimejaa thread za mauaji tu kwa visa vya mapenzi n.k. kisa cha hivi karibuni kuripotiwa ni hicho kilichotokea Tabora

-Ubakaji

-Utupaji wa watoto

-Ushirikina, kuna maeneo wazee eti wanakaa kabisa na kufanya tambiko ambapo mgeni anauawa kama kafara (mwalimu mmoja wa sekondari alikutana na dhahama hii sehemu fulani, alifuatwa akauawa na mwili wake kuchukuliwa kwenda kufanyiwa tambiko). pia, maeneo mengine tunaona na kusikia jinsi makaburi yanavyoenda kufukuliwa na maiti kutolewa na kurudishwa ilikotoka.....wafiwa wanaamka asubuhi wanakuta wamewekewa maiti ya ndugu yao waliomzika jana uwanjani.

na vingine vingi

Wajuzi/wafuatiliaji/ wasomi; sababu kubwa haswa ya hali hii ni nini? dini au?

Karibuni kwa uelimishaji.
Kuna kaukweli kiasi bt ushirikina ,uchawi ndo home huku...misukule na chuma uletee ndo penyewe.
Pia pamoja na rasilimali kibao km bahari,gas, korosho watu wanakumbatia umasikini sana na elimu ni duni sana
 
... sidhani kama ni dini. Maana dini hizo hizo zilizoko kusini ndio hizo hizo zilizoko maeneo mengine ya nchi. Mbona hatusikii mauwaji ya kijnga kama hayo yakitokea Ulaya?
Inawezekana pia hali siyo shwari kama tunavyofikiria ila mawasialiano ndiyo yanasababisha tusipate habari nyingi za huku. Hii mikoa bado iko nyuma sana. Ila nikiri kuwa watu wa huko hawana mambo ya tamaa ya mali kama mikoa mingine. Kule mtu akipata sex na chakula anaona ameshamaliza shida zote za maisha.
 
... sidhani kama ni dini. Maana dini hizo hizo zilizoko kusini ndio hizo hizo zilizoko maeneo mengine ya nchi. Mbona hatusikii mauwaji ya kijnga kama hayo yakitokea Ulaya?
Maeneo ya pwani huwa yanastaarabika mapema zaidi kuliko bara kwa sababu ya muingiliano mkubwa na watu wa mataifa mengine na pia wana fursa ya muingiliano mkubwa na makabila mengine ya bara.
"Exposure" kubwa.
 
Back
Top Bottom