Mikoa ya Kusini wanalalamikia sana ng'ombe

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,826
Changamoto ya ufugaji inaonekana ni kero sana kwa mikoa ya Kusini kwani wamang'ati na wamasai wameruhusiwa na Serikali ya awamu ya tano kufanya ufugaji popote hivyo wanaharibu sana mashamba na vyanzo vya maji.

Serikali ingeweka utaratibu mikoa ya Kusini iachwe izalishe chakula Kaskazini wangeachwa wafuge huko na mbona sheria ya kufuga nje ya maili tano haifuatwi. Kuanzia wilaya ya Kilwa mpaka Masasi huko chini karibu na Msumbiji wafugaji wamejichukulia maeneo wanakata miti na kulima. Tusipochukua hatua sasa tutakuja kushtuka hali imekuwa mbaya.
 
Back
Top Bottom