Nini plan B baada ya vifurushi vya internet kupanda bei?

Dr Dre

JF-Expert Member
May 23, 2015
2,556
2,585
kama kichwa kinavyosema binafsi naamini JF ina watu wenye maujuzi yao, embu tupeane ABC ya njia mmbadala zenye unafuu baada ya serikali ya wanyonge kunyonga wanyonge wao kwa bei zisizovumilika za vifurushi vya internet.

NB:natoa onyo kwa maana kuna watu watataka kuutumia huu uzi kama sehemu yao ya kutapeli watu.
 
Kama upo Dar maeneo ya Kariakoo, Mjini posta, Msasani, Peninsular, Upanga, Kinondoni ya Morocco, Mikocheni, Masaki, O'bey, n.k Kuna fiber za kutosha kama zuku, Raha, Gofiber, n.k

Fibre ni internet ya waya, unavutiwa waya hadi sehemu ulipo nyumbani kwako, ni internet ya waya lakini kuna kifaa utapewa kinaitwa wireless router, hiki kifaa kitakuwezesha utumie internet kwa wifi ya simu au laptop ama vifaa vingine vyenye wifi.

Kwa mfano internet ya fibre ya zuku inapatikana kino, kariakoo, msasani, peninsular, upanga,n.k utalipia elf 70 kwa mwezi (kifurushi cha chini) au zaidi (kuna vifurushi vina speed kali sana hivi ni kama watumiaji ni wengi na vina speed kali sana) pia hapo hapo utakuwa umelipia na channel za zuku utazocheki kwa kingamuzi.

A.10 Mbps = 69,000,
B.20 Mbps = 99,000
C.40 Mbps = 129,000
D.100 Mbps = 249,000.

Tukumbuke Mbps (Megabits per second) sio na zile megabytes ambazo huwa tunadownload, zile huwa na herufi kubwa ya "MB", ukitaka kujua unaweza kudownload MB ngapi kwa sekunde, hapa kilinganishi ni kwamba 1 Mbps ni sawa na MB 0.125 kwa hio mfano kifurushi A cha 10 Mbps ukifanya hesabu unapata uwezo wa kudownliad MB 1.25 kwa sekunde moja, ukija kifurushi B ni MB 2.5 kwa sekunde, n.k japo speed hushuka pale mnapokuwa watumiaji wengi mnaanza kugawana speed.

Utaweza kutumia internet bila kikomo, speed ni nzuri hata kwa kifurushi cha chini cha elf 70 ambacho unaweza kudownload mb 1 (nasikia sikuhizi ni 2) kwa sekunde, ni speed nzuri hata videos utaangalia bila kukwama na hata kwenye kudownliad utaweza kudownload muvi hata ya GB 1 kwa takribani dakika 18 tu, kitu kizuri zaidi ni hakuna kikomo, hakuna mambo ya ukifikisha gb kadhaa speed inashuka. Makampuni mengi gharama za vifaa na kuletewa waya wa internet hadi kwako ni bure ikiwa utalipia bando la mwezi au miezi kadhaa.

Changamoto ni kwamba haipo kila sehemu Dar na pia inabidi uwe mazingira ya nyumbani au ofisini ili kutumia wifi ya kifaa chao.

Kwa waliopo nje ya maeneo hayo au mikoani TTCL nao wana fibre sema nasikia ni gharama.

Kiukweli ni pigo kubwa, saizi wasanii wasahau kupata views nyingi kama zamani huko youtube, Internet ilikuwa silaha yetu kwa kuinua wasanii ila kwa hali hii jumna bovu limewaangukia
 
ngoja waje wajuzi ,

hivi wale naowaona insta wanasema wanaunga vifurushi ni matapeli kama wale wengine au ?
kutokana na vifurushi kuwa affordable hata sjawahi kufikiria kuwachek hao watu lakini hivi sasa itabidi tu,lamda kama kuna mtu alishawahi kuwachek atuambie hapa
 
  • Thanks
Reactions: Lee
kama kichwa kinavyosema binafsi naamini JF ina watu wenye maujuzi yao, embu tupeane ABC ya njia mmbadala zenye unafuu baada ya serikali ya wanyonge kunyonga wanyonge wao kwa bei zisizovumilika za vifurushi vya internet.

njia ya kwanza nayoijua mimi ni yourfreedom hii ni VPN ambayo unalipia plan ya 1 month online wanakupa free internet for 1month ,sema ubaya wa hii ni kuwa haipo smooth ,yaani huwa ina tabia ya kupoteza connection mara kwa mara hivyo kulazimu mtu kuswitch kila mara.
NB:natoa onyo kwa maana kuna watu watataka kuutumia huu uzi kama sehemu yao ya kutapeli watu.

Kwa kweli hivi vifirushi na majanga sana
 
Kama upo dar kuna maeneo kama kariakoo kuna zuku fibre ya nyumbani, utalipia elf 70 kwa mwezi na utaweza kutumia internet bila kikomo, speed ya kudownload ni mb 2 kwa sekunde,,,,,,bila kikomo

Kiukweli ni pigo kubwa, saizi wasanii wasahau kupata views nyingi kama zamani huko youtube, Internet ilikuwa silaha yetu kwa kuinua wasanii ila kwa hali hii jumna bovu limewaangukia
hii ina effect kubwa sana hata mapato serikalini yatokanayo na mitandao ya simu pia yatapungua sana ,sisi tuliokua tukitegemea mitandao kulisha familia zetu napo hali ni mbaya ,wasanii ndio usiseme ,hapa kilichobaki ni kutafuta tu plan b
 
Kama upo dar kuna maeneo kama kariakoo kuna zuku fibre ya nyumbani, utalipia elf 70 kwa mwezi na utaweza kutumia internet bila kikomo, speed ya kudownload ni mb 2 kwa sekunde,,,,,,bila kikomo

Kiukweli ni pigo kubwa, saizi wasanii wasahau kupata views nyingi kama zamani huko youtube, Internet ilikuwa silaha yetu kwa kuinua wasanii ila kwa hali hii jumna bovu limewaangukia
hiyo fibre ni kariakoo tu au ni maeneo yote
 
1617352454509.png
 
Kwanini tutafute plan B? Kwanini tusiulize mamlaka husika kwanini wamepandisha gharama namna hiyo? Sababu ni nini? Kwa umoja wetu itaelewaka tu kuliko kujinyongesha
tunaotegemea data katika kazi zetu tumebaki mdomo wazi mkuu hatujui tuanzie wapi, halafu mkuu hili swala lipo kisiasa zaidi ukihoji utajibiwa kisiasa tu bila mabadiliko yoyote na mwisho wa siku wananchi wataona ni kawaida na maisha lazima yaendelee.
 
Ndio shida yetu Watanzania tunaridhika mapema lakini waziri alipaswa kuliongelea hili sababu aliahidi vitashuka matokeo vimepanda, kama kazi imemshinda aseme wapo wataalam wanaweza kufit.
 
Plan B ni kununua kifurush cha buku; mb zake tumia kufungua email, labda site za habar na kujifunza kidogo. Fb tumia free, unaeza ingia gharama kidogo kwa kudownload game nzur ili zikupotezee andas ya kuingia kwe mitandao km twita nk.

Epuka kuangalia status wasap

Usisahau kupitia na humu coz wala hutumii mb nying.
 
kama kichwa kinavyosema binafsi naamini JF ina watu wenye maujuzi yao, embu tupeane ABC ya njia mmbadala zenye unafuu baada ya serikali ya wanyonge kunyonga wanyonge wao kwa bei zisizovumilika za vifurushi vya internet.
NB:natoa onyo kwa maana kuna watu watataka kuutumia huu uzi kama sehemu yao ya kutapeli watu.
Tafta sehemu zenye free WiFi nyonga maisha
 
Back
Top Bottom