Beast of no nation
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,612
- 2,537
Kupanda kwa bei ya mafuta kunakoendelea kumesababisha ongezeko la gharama za maisha, ikiwemo bei za bidhaa mbalimbali na huduma muhimu za kijamii. Miongoni mwa athari zinazozidi kujitokeza ni changamoto ya usafiri kwa wanafunzi, hasa baada ya kuongezeka kwa nauli za daladala na vyombo vingine.
Kwa sasa, wanafunzi wengi ndani ya Jiji la Dar es Salaam wanakumbana na tatizo la kuachwa vituoni kwa muda mrefu. Daladala nyingi zinashindwa kuwapakia kwa wakati kwa madai kuwa nauli ya wanafunzi ya shilingi 200 haiendani na gharama za uendeshaji kutokana na hali ya sasa ya uchumi.
Mimi binafsi nimeshuhudia hali hii mara kadhaa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam. Kwa mfano, katika barabara ya Bagamoyo kuelekea Bunju, mara nyingi watoto hukaa vituoni kwa zaidi ya saa moja hadi mbili wakisubiri usafiri. Hali kama hiyo pia hujitokeza nyakati za jioni katika maeneo ya Kariakoo na Mbagala, ambapo wanafunzi hulazimika kusubiri kwa muda mrefu kabla ya kupata daladala.
Aidha, rafiki yangu aliyepo Morogoro amenieleza kuwa huko changamoto ni kubwa zaidi. Wanafunzi wengine hulazimika kusubiri usafiri kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa tatu bila mafanikio ya kupata daladala kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanafunzi hulazimika kulipa nauli za watu wazima au kutoa hadi shilingi 500 ili waweze kusafirishwa. Wale wasioweza kufanya hivyo huendelea kuachwa vituoni hadi pale idadi ya abiria inapopungua. Hali hii inasikitisha sana, na ndiyo maana siku hizi si jambo la ajabu kuwaona wanafunzi wakiwa bado kwenye daladala hadi majira ya usiku wakiwa wamechoka kupita kiasi.
Changamoto hii inaathiri moja kwa moja elimu ya watoto wetu. Wapo wanaochelewa kufika shuleni, kushindwa kushiriki masomo kwa ufanisi, au hata kukata tamaa kabisa. Aidha, wazazi nao hulazimika kubeba mzigo mkubwa wa gharama za usafiri katika kipindi hiki kigumu cha maisha.
Nakumbuka kusikia kuhusu mpango wa Serikali wa kuanzisha mabasi maalum kwa ajili ya wanafunzi, jambo ambalo limekuwa likisisitizwa na wadau mbalimbali wa elimu na usafiri. Hata hivyo, hadi sasa wananchi wengi hatujui mpango huo umefikia hatua gani.
Ni wakati sasa kwa Serikali kuharakisha utekelezaji wa mpango huo au kuchukua hatua za dharura kwa kuweka mabasi maalum ya wanafunzi katika majiji na miji yenye changamoto kubwa ya usafiri. Hatua hiyo itasaidia kupunguza adha wanazopitia wanafunzi kila siku na kuboresha mazingira yao ya kujifunzia.
Ukiwekwa utaratibu rafiki changamoto hii inaweza kutatuliwa hata katika ngazi za TAMISEMI kupitia ubunifu wa mipango rafiki ya kupata magari na kuyaendesha. Sio lazima hadi kusubiri Serikali Kuu au wahisani wa nje; kinachohitajika ni dhamira, maamuzi, na ubunifu katika kutafuta suluhisho la kudumu.