Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,154
- 137,162
Obama hajasoma level ya Ph.D, ila technically ni Juris Doctor kwa sababu ana degree ya sheria. Degree ya Sheria Marekani ni Juris Doctor (J.D)Kwa hiyo angependa maujiko angejiita Dr. Obama.
Nchi kama Marekani, si ma doctor wote wana Ph.D. Kunda ma doctor wengine wana Ed.D (Doctor of Education) au Psy.D (Doctor of Psychology)
Jamii zilizoendelea kielimu, kama mtu hayupo katika kazi za kufundisha au research, kujiita Dr. inaonekana ulimbukeni.
Watu kama Waziri wa Ulinzi wa zamani wa Marekani Robert Gates, ana Ph.D, lakini alikuwa anaitwa tu Defense Secretary, Robert Gates. Kwa sababu mtu kuwa na doctorate si kitu cha ajabu.
Watu wengine ambao wana Ph.D lakini mara nyingi husikii wakiitwa "Dr" ni Condoleeza Rice na Susan Rice.
Kuhusu tofauti ya Dr na Professor, inategemea na mfumo wa nchi.
Kwa Marekani, Professor ni mtu anayefundisha chuo Kikuu tu. Nakumbuka wakati naanza chuo, kuna Professor mmoja tulimuita Dr., tukifikiri ni Dr., akatusahihisha kwamba yeye hajafanya doctorate degree yake bado, kwa hiyo tusimuite Dr. yeye ni Profesa tu.
Lakini kwa Tanzania, nilivyoona, ni kwamba, U Profesa ni cheo fulani, kwa hiyo kuna watu wengi wenye doctorate zao ni ma Doctor so and so, lakini hawajafikia cheo cha u Profesa.
Hata Chelsea Clinton ana PhD. Lakini sijawahi ona popote akiitwa Dr. Clinton...

.