Nini maana ya Professor na Doctor(PhD)?

Mr the dragon

JF-Expert Member
Apr 14, 2017
1,919
3,645
Habari zenu wadau wa JF.

Hivi Ni vigezo gani hutumika mpaka mtu aitwe Proffesor au Doctor.Doctor ninayemzungumzia ni yule mwenye PHD sio hospitali.

Nimeuliza hivi kwa sababu, Tanzania mtu yeyote mwenye shahada ya uzamivu huitwa Doctor(Dr).

Lakini nimesoma biography ya Barrack Obama na Hillary Clinton na nikagundua wamesoma mpaka level ya PHD lakini sijawahi kusikia wanaitwa Doctor tofauti na hapa kwetu.

Mfano rais wetu John Pombe Magufuli ana PHD anaitwa Doctor.Obama pia ana PHD na aliwahi kufundisha Chuo kikuu ila sikuwahi kusikia akiitwa Doctor au Proffesor.

Hii imekaaje ndugu wa JF naomba kuelimishwa.
 
professor niliwahi kusikia ni yule ambae amefanya utafiti UNIQUE sana juu ya jambo fulani, ambalo halikuwahi kufanywa hapo nyuma sana

Na amevumbua jambo ambalo lililkuwa likisumbua sana watu kwa kulifanyia utafiti wa kina

mi najua kidoogo hivyo kuhusu Professor
 
PhD ni Shahada ya Uzamivu, yaani mtu anabobea au kuzamia katika Kaeneo fulani kidogo kataaluma take na wanaitwa madaktari wa falsafa. Uprofesa ni daraja la juu la wanataaluma, kuanzia mhadhiri mzaidizi, hadi profesa. Na vyeo hivyo vinapanda kwa kusomea na kufanya machapisho kwenye majarida ya kisayansi
 
Swali niliokuwa najiuliza mfano Obama alikuwa na PHD lakini sikuwahi kuona au kusikia jina lake likianzia Dr kama ilivyo kwa Kikwete,Magufuli etc, ambao majina yao yanaanzaga na Dr
Doctor/Doctorate of Philosophy wanaoipata wanaitwa madocta (ila sio wa binadamu, bali ni wa kwenye degree ya 3) kibongo bongo level ya mwisho ya degree

hiyo nadhani labda wengine wanaweka kwa ajili ya cheo/wadhifa na hata sifa saa nyingine kama wale INJINIA lazima jina lake aanze na ENG. mwanzoni
 
PhD ni Shahada ya Uzamivu, yaani mtu anabobea au kuzamia katika Kaeneo fulani kidogo kataaluma take na wanaitwa madaktari wa falsafa. Uprofesa ni daraja la juu la wanataaluma, kuanzia mhadhiri mzaidizi, hadi profesa. Na vyeo hivyo vinapanda kwa kusomea na kufanya machapisho kwenye majarida ya kisayansi
Nimekuelewa, but kinachonitatiza nimetolea mfano Obama ana PHD lakini sikuwahi kusikia au kusoma akiitwa Doctor.

Utofauti upo wapi?
 
Nyerere alitunukuwa PhD nyingi tu za heshima na vyuo mbalimbali lkn sikuwahi msikia akiitwa doctor Nyerere. Hii doctor kwa viongozi ilipamba moto sana enzi za Kikwete tena ilipambishwa moto na watu wa chama tawala, hao si unajua tena kwa kusifia mtu akiwa Ikuku unaweza dhani ktk nchi hakuna anayeweza kuja kuongoza zaidi yake. Katika harakati za uchaguzi fulani kulikuwa na professor Lipumba, Doctor Slaa na ndugu Kikwete. Kuvuta mfanano wa wagombea zikapekuliwa degree za kutunukiwa za Kikwete ghafla zikaanza kupaishwa naye akaanza kuitwa doctor Kikwete. Ameondoka Ikulu hii Doctor naona kama inasahaulika ktk kum-address. Wamarekani hawahitaji hiyo sifa kuonekana kiongozi anajua ndo maana akina Obama wahawakuhitaji kuitwa madoctor
 
Hii inasound kuwa na ukweli fulani.Naweza kukubaliana na hiyo sababu.

Kumbee ni sisi waafrika na masifa yetu
 
Habari zenu wadau wa JF.

Hivi Ni vigezo gani hutumika mpaka mtu aitwe Proffesor au Doctor.Doctor ninayemzungumzia ni yule mwenye PHD sio hospitali.

Nimeuliza hivi kwa sababu, Tanzania mtu yeyote mwenye shahada ya uzamivu huitwa Doctor(Dr).

Lakini nimesoma biography ya Barrack Obama na Hillary Clinton na nikagundua wamesoma mpaka level ya PHD lakini sijawahi kusikia wanaitwa Doctor tofauti na hapa kwetu.

Mfano rais wetu John Pombe Magufuli ana PHD anaitwa Doctor.Obama pia ana PHD na aliwahi kufundisha Chuo kikuu ila sikuwahi kusikia akiitwa Doctor au Proffesor.

Hii imekaaje ndugu wa JF naomba kuelimishwa.
Obama hajasoma level ya Ph.D, ila technically ni Juris Doctor kwa sababu ana degree ya sheria. Degree ya Sheria Marekani ni Juris Doctor (J.D)Kwa hiyo angependa maujiko angejiita Dr. Obama.

Nchi kama Marekani, si ma doctor wote wana Ph.D. Kunda ma doctor wengine wana Ed.D (Doctor of Education) au Psy.D (Doctor of Psychology)

Jamii zilizoendelea kielimu, kama mtu hayupo katika kazi za kufundisha au research, kujiita Dr. inaonekana ulimbukeni.

Watu kama Waziri wa Ulinzi wa zamani wa Marekani Robert Gates, ana Ph.D, lakini alikuwa anaitwa tu Defense Secretary, Robert Gates. Kwa sababu mtu kuwa na doctorate si kitu cha ajabu.

Watu wengine ambao wana Ph.D lakini mara nyingi husikii wakiitwa "Dr" ni Condoleeza Rice na Susan Rice.

Kuhusu tofauti ya Dr na Professor, inategemea na mfumo wa nchi.

Kwa Marekani, Professor ni mtu anayefundisha chuo Kikuu tu. Nakumbuka wakati naanza chuo, kuna Professor mmoja tulimuita Dr., tukifikiri ni Dr., akatusahihisha kwamba yeye hajafanya doctorate degree yake bado, kwa hiyo tusimuite Dr. yeye ni Profesa tu.

Lakini kwa Tanzania, nilivyoona, ni kwamba, U Profesa ni cheo fulani, kwa hiyo kuna watu wengi wenye doctorate zao ni ma Doctor so and so, lakini hawajafikia cheo cha u Profesa.
 
Nimekusoma vizuri.

Nilichokielewa zaidi ni kwamba Kuna tofauti Kati ya nchi na nchi.

Sema Tanzania Kuna ka harufu kakupenda maujiko.
 
Back
Top Bottom