Nini kinachoendelea Singida?

Nini kinachoendelea Singida?

WanaJF, salaamu.

Naomba mwenye kujua kinachoendelea mkoani Singida atujuze. Nimesema hivyo kutokana na mambo mawili ambayo yamejitokeza kwa karibuni kwa kufuatana.

1: Sherehe za Maulid mwaka huu kitaifa zilifanya mkoani Singida, na Waziri mkuu ndiye alikuwa mgeni rasmi.

2. Sherehe za Christmas, siwezi kusema kitaifa, bali Rais alikuwa Singida.

Japo kwa maelezo yake alisema alienda kusali katika kanisa hilo kwani ushindi wake ulitokana na Rosary aliyopewa na mtawa mmoja wa kanisa huko Singida.

Najiuliza hivi kweli hiyo rosary ndiyo iliyompa ushindi au ni watanzania waliompigia kura? Au kuna jambo la siri linaendelea huko?.

Nawasilisha
Samaki aliyeufunga mdomo wake huikwepa ndoano.
 
Siyo Singida tena .Baada ya ibada ya xmass Jana asubuhi ngoma ilinyooka moja kwa moja Chato by SAA kumi Jana alikuwa ndani ya Lubambagu_Chato.
 
Hata Musa na Joshua walitumiwa na Mungu Kama vyombo vya kusafirisha Waisrael kuelekea nchi ya ahadi kwa hiyo waisrael walimsikiliza Musa anD Joshua. Bikira maria alitumika nal Mungu Kama Chombo cha kumzaa Yesu na sis hatuna budi kumheshimu bikira Maria Kama chombo kitakatifu kilichotumiwa na Mungu.
Nani amuheshimu?. Tofautisha kumuheshimu mtu na kumwabudu ama kumfanya sehemu ya ibada hasa hasa karibu na Mungu au kuwa juu ya Mungu mfano kumfanya muombezi ambacho ni kinyume na Neno la Mungu. Hivi umewahi kujiuliza kwa nini Musa alizikwa Mungu na kaburi lake hakuna ajuaye lilipo?. Mungu aliwaona watu kama nyinyi mapema.
 
WanaJF, salaamu.

Naomba mwenye kujua kinachoendelea mkoani Singida atujuze. Nimesema hivyo kutokana na mambo mawili ambayo yamejitokeza kwa karibuni kwa kufuatana.

1: Sherehe za Maulid mwaka huu kitaifa zilifanya mkoani Singida, na Waziri mkuu ndiye alikuwa mgeni rasmi.

2. Sherehe za Christmas, siwezi kusema kitaifa, bali Rais alikuwa Singida.

Japo kwa maelezo yake alisema alienda kusali katika kanisa hilo kwani ushindi wake ulitokana na Rosary aliyopewa na mtawa mmoja wa kanisa huko Singida.

Najiuliza hivi kweli hiyo rosary ndiyo iliyompa ushindi au ni watanzania waliompigia kura? Au kuna jambo la siri linaendelea huko?.

Nawasilisha
Mkuu amesali krismas Singida kwa madai yake ndiko alikopewa rozari na masista. Rozari ambayo anaitumia mpaka leo kwenye sala zake binafsi.

Ni sababu ya kiroho zaidi sio kisiasa. Anaamini kwa kusali Singida anakuwa amewaheshimu wale masista waliompa rozari na kusali nae akiwa kwenye kampeni.
 
Hapo Magufuli amekosea sana.Naiheshimu IMANI yake.
Lakini kuhusisha MARIA, ROSARY katika ushindi wake, ni sawa na kusema Mungu hakukusaidia bali MARIA na ROSARY.
Maria alikufa na AKAZIKWA na biblia HAITUAMBII tumwombe Maria.
Na kama Magufuli UTAMSAHAU Mungu na KUCHANGANY MARIA! Mungu na YESU nchi hii itamshinda.
Maana Mungu HADHIHAKIWI!!
Maana pia ni Mungu MWENYE WIVU
MPE MUNGU UTUKUFU!
Mambo mengine sio lazima uyatolee maoni. Tafuta watu waliokuzidi kwenye masuala ya imani halafu wape nafasi ya kukuelimisha kiroho. Itakusaidia sana, na hautajiandikia mambo usiyoyafahamu kama ulivyofanya kwenye huu uzi.
 
Ni mnyororo Mtamu sana unaomuunganisha mwanadamu na Mungu wake anaposali. Anapanda kufuatana na hizo kete anaposali . kutoka karne moja hadi nyingine. Karibu ujifunze nawe utakuwa karibu na Mungu wako na mafanikio ya kuwa karibu naye utayaona na utatusimulia. Mungu awe nawe upate kuwa karibu naye uweze kuhubiri Amani ndani ya familia zetu na hata Taifa zima.
Upagan tu
 
mkoa wa singida ni miongoni mwa mikoa maskini na kame, kwenda kwao kunaufanya mkoa kubustika kiaina, sio mbaya, kwa kuwa ni mkoa wangu, niwaaombeni msiwe na wivu, na ningependa na mwaka mpya aulie singidani, msijali zamu yenu itafika tu
 
Mambo mengine sio lazima uyatolee maoni. Tafuta watu waliokuzidi kwenye masuala ya imani halafu wape nafasi ya kukuelimisha kiroho. Itakusaidia sana, na hautajiandikia mambo usiyoyafahamu kama ulivyofanya kwenye huu uzi.
Mkuu ninayafahamu. Niliwahi kutaka kujiunga na Seminary niwe Padre. Macho yangu yakafunguka.
Najua mbivu na mbichi.
Siandiki tu hivi hivi.
Rais Magufuli akitaka NCHI HII ibarikiwe kweli kweli ASIMAME katika imani ya kweli ya KRISTO Yesu isiyo na UDINI bali wokovu wa kweli.

AKICHANGANYA changanya mara Rozari mara SANAMU nchi hii itaingia katika UMASKINI mkubwa.
Ninajua MADHARA ya kuchanganya Mungu na vitu kama hivyo ni Heri tumwambie mapema kwa heshima kuwa Mzee hiyo si njia nzuri!
 
Watu mnamambo,mbona Pm alikuwa Ar karibu wiki nzima hamkuhoji? Sgd nayo ni Tanzania! Kila siku mnataka wawe kwenu kwani sgd nao si wapo waliowachagua? Kuna mambo binafsi ya mtu nayo tuhoji humu? Tujadili mambo ya msingi nasi hoja nyepesi kama hizi.
 
Ukitaka kuijua Historia ya Kanisa Katoliki soma kuanzia Karne ya kwanza sio kuanzia mwaka 1854.
Hili ni Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume na Papa wake wa Kwanza ni Mtakatifu Petro ambaye alikabidhiwa majukumu hayo na Yesu Kristo.
Kanisa lilivunjavunja imani za himaya ya kirumi na wengi wao walimkubali Yesu kuwa ni Masiha hivyo wakabatizwa wakiwemo vigogo wa dola hiyo.Hayo mambo sio mageni na yapo hata leo.
Kama unaiamini Biblia lazima ulikubali na Kanisa Katoliki kwa sababu ndilo lililofanya jitihada za kukusanya machapisho mbalimbali na kuyakubali baadhi na mengine kuyatupa.waliyoyakubali waliyaweka pamoja kama kitabu ambacho Kinajulikana kama Biblia(Maktaba).
Kuhusu Bikira Maria,Kwa Mtu yeyote anayemkubali kwamba Yesu ni Mungu haoni shaka ya kumheshimu Bikira Maria maana hata Malaika wa Mbinguni wanamkubali.
Mkuu Farudume. Kwanza kabisa napenda post zako. Nitakujibu hivi,
1.PETRO HAKUWA Pope wa kwanza wa Kanisa. Petro alikuwa na MKE hata mimi kabla sijafunguliwa macho niliamini kama wewe.

2.Biblia HAIKUANDIKWA na Wakatoliki kama unavyodai infact WALIJARIBU sana kutaka KUHARIBU manuscripts nyingi wakichoma moto WAKIITAFUTA biblia waiharibu, Mungu akailinda.
Ukitaka kujua sana tafadhali google "Roman Catholic church and INQUISITION"
Utaelewa na hata kuhuzunika.
Pia kama una nafasi angali kwenye YOUTUBE "God's wrath on Lisbon 1755" Katika documentary hiyo ambayo wiki hii ilikuwa ikionyeshwa katika CHENELI ya NATIONAL GEOGRAPHIC .Wanasayansi walishindwa kuelewa tukio hilo wakaliita God's wrath/ "Hasira za Mungu"
Hasira hizo ziliushukia Mji mkuu wa Ureno. kwa siku moja. TEMEMEKO, TSUNAMI na MOTO mitaani na BAADAYE WAUAJI vitu vinne SIKU MOJA.
URENO ambayo ilikuwa DEEP Catholic nation itakupa Picha kamili. Kuhusu hoja yako uliyoileta.

3.NIPE TAIFA la KIKATOLIKI duniani LILILOBARIKIWA ukianzia na ITALY ambako ndo makao makuu ya dini. Kabla hawajaingia EU hela yao LIRA haikuwa na THAMANI katika soko la fedha za kimataifa ilikuwa ni kama yetu.
Zunguka Ulaya, na bara la AMERIKA nenda Mshariki ya mbali ya ASIA UFILIPINO nk. Halafu uniambie HIYO ROZARI kama iliwasaidia. NI UMASKINI tu!!!
 
Sina maana hiyo. Ninacho takakujua ni kwa nini matukio haya mawili ambayo viongozi wa juu wa serikali walishitiki yafanyikie mkoa mmoja tena kwa kufuatana.
Coincidences do happen in life !
 
Nafurahi sana kuona na mikoa iliyokuwa "imetelekezwa" mara hii walau inakumbukwa
 
Back
Top Bottom