Nini kilikusaidia kupata kazi?

Nini kilikusaidia kupata kazi?

Kiukweli sehemu nyingi siku hizi ni connection japo zipo pia ofisi ambako wapo fair unabebwa na CV yako na kujiamini tu (kujibu kwenye interview). I'll share my experience kidogo:
JOB 1: After 1st degree nilijiendeleza na post grad na kabla sijamaliza nilihangaika kutafuta kazi bila kupata .Hatimaye nikapata kwenye Taasisi fulani hivi.Najua walinipa coz mkuu wa hapo anafahamiana na mama lakini najua pia I was qualified enough for the Job (so hapa walinipa kishkaji out of 50 candidates nilipata mimi).

JOB 2: Job two nilipata kupitia mtandao wa Zoom jobs...nilikua tu nachoka kukaa job one nikawa bahatisha bahatisha mitandaoni nikaona kazi iloendana na qualifications zangu nikaomba na nikapata. It was a prestigious International NGO.
Sikua na mjomba wala shangazi wala Danga [emoji3][emoji3] Iikua mimi na Mungu wangu na CV yangu no connection at all.

JOB 3: Three years and a few months later I landed my 3rd Job...again through Zoom jobs....I must have outgrown my 2nd job so nikawa nazurula mtandaoni nikakutana na kazi ilonivutia na NGO nyingine tena nzuri. Wenye ma NGO ni wazungu....na mie sina mjomba,shangazi wala shosti mzungu. Nikaomba kazi kwa CV tu bila connection. Nilifuata maelekezo yao nikaweka vigezo walivyotaka kwenye application. One week later I was interviewed and I got the job.

JOB 4 : Again CV....and a little connection!

C Plus Plus nnachojaribu kukuonyesha sio kila kazi lazima uwe na connection ila a good CV....Andika CV vizuri (Format ya CV iwe nzuri, Good writing skills inasaidia kwenye Covering letter na experience nzuri as per job requirements) hayo mengine unamwachia Mungu (Pray).
Usichoke ku browse mitandao kuona kazi mpya zinazotoka.Pia hakikisha kazi unayoomba unaimudu as in iwe ni kazi ambayo ukipewa unafanya ila usione kwasabu tu unataka kutoka mtaani....omba kazi ambayo hata ukiitwa interview inaonyesha kua una experience nayo.
Lakini pia unapopata nafasi ya kuitwa interview hakikisha unafanya background check ya Taasisi/Shirika uliloitwa.I Mie hua kibidi naingia LinkedIn kuangalia profile za management team (probably ndio watakao ku-interview) ili angalau niwaelewe career wise na niwape kile wachotaka.
Best of luck....keep trying your breakthrough is around the corne6[emoji173]

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Katika maisha na mafanikio kwa ujumla bahati pia ina play a very big role. Sijui umesomea nini exactly na level of confidence na power ya kujieleza uliyo nayo ila kimsingi naona utakuwa ni mtu mwenye zali sana katika maisha. Kuna watu wana qualifications za hali ya juu ila kupata kazi still ni kipengele na interview kibao washaenda.
 
Omba Mungu sana, kuajiriwa hakuna ujanja, ni Mwenyezimungu akiamua tu unapata, kuna jamaa yangu mmoja hivi alijitolea Kinyerezi 2, miezi 10 hakupata ajira, kipindi anajitolea akaitwa tena kujitolea TPA(seap program) mwaka mzima uliisha na ajira zikitoka yupo pale lkn alikuwa hapati ajira, ingawa alikuwa analipwa 1M kwa nwezi. juzikati ajira za TBA wakaitwa watu 280 huku wakiwa wanatafuta mtu mmoja akachukuliwa yeye (Mechanical Engineer 2).

Kuna mdogo wangu kamaliza mwaka huu AUTOMOBILE ENGINEERING, kapata kazi TOTAL bila connection walienda kuomba kurecruit watu wa automobile wanamchukua kisa ana gpa nzuri, kuna jamaa humu jamii forum, nilimkonect tu mahala wanatafuta maintenance engineer haikuchukua hata week 2 akaitwa kazini, na niliwapa watu wengi email watume maombi lkn ye aliitwa faster. .

Ukisikia mtu kapata kazi wala sio ujanja wake, bali nimuda tu umefika.
Ndio maana mie huwa naona mafanikio ni game of chance. Kuna muda tu Mungu anaamua kukunia nazi basi unachomoka kimaisha.
 
Mimi hata sielewi, niliambiwa tu nenda kwa baba yako mdogo mengine atakwambia huko huko. Nilipata ajira nikiwa na 19yrs hata barua ya kuomba kazi nakumbuka aliniandikia mzee.
Hahahahah hio ndio tafsiri ya Connection.
 
Omba Mungu sana, kuajiriwa hakuna ujanja, ni Mwenyezimungu akiamua tu unapata, kuna jamaa yangu mmoja hivi alijitolea Kinyerezi 2, miezi 10 hakupata ajira, kipindi anajitolea akaitwa tena kujitolea TPA(seap program) mwaka mzima uliisha na ajira zikitoka yupo pale lkn alikuwa hapati ajira, ingawa alikuwa analipwa 1M kwa nwezi. juzikati ajira za TBA wakaitwa watu 280 huku wakiwa wanatafuta mtu mmoja akachukuliwa yeye (Mechanical Engineer 2).

Kuna mdogo wangu kamaliza mwaka huu AUTOMOBILE ENGINEERING, kapata kazi TOTAL bila connection walienda kuomba kurecruit watu wa automobile wanamchukua kisa ana gpa nzuri, kuna jamaa humu jamii forum, nilimkonect tu mahala wanatafuta maintenance engineer haikuchukua hata week 2 akaitwa kazini, na niliwapa watu wengi email watume maombi lkn ye aliitwa faster. .

Ukisikia mtu kapata kazi wala sio ujanja wake, bali nimuda tu umefika.
Inaonesha jamaa alikuwa intern ila anakula stipend ambayo hata vijana wengine waliopo kwenye mikataba rasmi hawapati.
 
Wengi wanajifanyaga wana connections za kazi ila hawana kitu mkuu. Trust me. Wengi wao wakiona wameshindwa wanakupiga chenga badala ya kuwa wakweli.

Mtu aliyenipa kazi yangu ya kwanza mwaka 2013 mkoani Iringa mshahara take home 750,000/= alikuwa ni mtu wa kipato cha chini saaaana sema aliniomba CV yangu kisha akampa ndugu yake aliyekuwa anafanya kazi BANK.
Ndio maana ya mtu anayeweza kukusaidia kukuondoa topeni ni yule ambaye humatarajii siku zote.
 
Binafsi ni juhudi tu katika field yangu ya kwanza, pia na Bahati naweza kusema. Field yangu nilijituma sana na kama Bahati, aliyekua assistant wa boss alikua mlevi na mzembe mno kazini kiasi kwamba jumatatu kuja kazini kwake lilikua jambo zito, either apoteze simu au aje ananuka pombe siku nzima, kupitia tabia zake nikaonekana nafaa sana, hata nilipomaliza chuo sikufanyiwa interview wala kuombwa japo CV nilipewa contract na mshahara mzuri nikiwa fresh from school....
Then baadae baada ya hiyo kampuni kufunga kazi zake TZ nikatuma CV kampuni moja kiutani tu siku hiyo hiyo nikaambiwa at my favourate time nifike ofisini kwao, nikajua interview, kufika wananimbia tunegotiate mshahara na niwambie lini nitaanza kazi, baada ya hapo tukakubaliana hadi leo Niko nao na tunategemeana....
Sijawahi fanya interview yeyote wala kuombwa cheti chochote zaidi ya kuaminiwa, na nalipwa mshahara unaojitosheleza na kazi zangu zinaheshimika. Kiufupi huwa najiona ni mwenye Bahati tu mana sijawahi kutumia utaalamu au namna yoyote zaidi ya Bahati tu.
Bahati ina play role kubwa sana kwenye mafanikio ya mtu binafsi. Kuna watu hawajawahi kuteseka na kazi na wanabadili kazi kama pea za viatu 😅 huku mwengine hata field attachment tu hapati.
 
MUNGU ni mwema
Baada ya kumaliza chuo July 2016 nilijiapiza kwamba nisingerudi mkoani hadi nitoboe lakini nilijiwekea ukomo wa miezi nane tu kama ningechemka kupata upenyo basi ningehamishia mashambulizi mkoani hivyo nililipia kodi miezi sita kwani miwili ilikuwa ndani ya mkataba.

Hustle zikaanza rasmi nikawa nimejiwekea utaratibu wa kusambaza CV tatu kila siku ila approach yangu haikuwa kuacha reception, kabla ya kwenda kampuni husika nilikuwa nasoma Company profile ili kujua viongozi wakubwa kama Operation manager,HR manager au hata Mkurugenzi hivyo nikifika hapo namwambia secretary nimekuja kumuona mtu fulani nina shida ya kiofisi hii mbinu sio rahisi kama huna confidence na haifanyi kazi sehemu zote kwani kuna wakubwa kutokana na majukumu yao hawapendi kuonana na mtu ambate hakuwa na appointment nae, binafsi ilinisaidia sana kwenye kujenga kujiamini kwani niliweza kukutana na watu wakubwa physically na kuongea nao japo waliishia kuniambia CV niache kwa HR hivyo sikuwahi kuitwa popote kwa ajili ya interview ama ajira.

Kuna muda sikuwa na nauli basi jua likawa langu na mvua pia ilikuwa kawaida kutoka mtongani hadi posta kwa mguu yani mvua ikinyesha bahasha inachanika mara CV zimeloa inabidi shughuli siku hiyo iishie hapo.

2.Connection
Siku moja nikiwa kwenye daladala naelekea mikocheni nilipigiwa simu na kaka yangu akaniambia nimtumie CV yangu haraka sana nikamuomba kondakta anishushe ilala nikaingia internate cafe chap nikafanikisha, nauli ikawa imekata ikabidi nirudi getto kwa mguu, aisee ndugu usiniulize nilkuwa nakula nini kama tu nauli ilikuwa inanishinda mimi nilikuwa naloweka mchele nakula nalala nisingeweza kupika sina gesi wala mkaa ila MUNGU ni mwema yamepita japo yanaweza kujirudia so ni suala la kuendelea kuwa mwaminifu kwa MUNGU.

December 1,2016 nikiwa getto nimejilaza natafakari nilipokea Call kutoka Benk fulani wakinialika kwenye interview ila natakiwa nikafanyie mkoani aisee ilikuwa jumatatu na natakiwa jumatano niwe huko nilipagawa basi nikamjulisha bro akaniambia poa ntakuchangia nauli uende nilimshukuru sana, nilijiandaa vizuri mno nilifika eneo la tukio tulikuwa watu kumi na tano na walitakiwa watu wanne tu mm ndiye niliyekuwa mtu wa kwanza aisee nilipiga interview kwa hasira hadi Manager akaacha kuandika marks akaanzisha mjadala kwa kiswahili finally akasema nahitaji kufanya kazi na wewe tuka shake hands nikaondoka kesho asubuhi nikapigiwa simu kuwa nimepata kazi natakiwa nipeleke nyaraka zote ikiwemo vyeti, picha nk ilikuwa ni kazi ya uwakala wa mauzo (sales agent) na walikuwa wanahitaji watu wa diploma tu ila naambiwa wengi walikataa coz ni kazi ngumu na haina maslahi kiivyo,,,,nilijisemea nitafanya kazi hii kwa nguvu zangu zote ndani ya mwaka mmoja sitakuwa hapa tena.

Recruitment process ilichukua muda kidogo tuliitwa kuanza kazi mwezi wa kwanza 2017, aisee nilikuwa napambana sana na strategy zangu zilikuwa poa sana basi baada ya miezi miwili kukatokea shortage ya mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa anaenda maternity basi wakatangaza fixed term opportunity wengi tulifanya application pamoja na wengine tuliowakuta pale baada ya interview namshukuru MUNGU pia nikatoboa wakaniambia nitafanya for six months akirudi mwente nafasi yake kutakuwa na mawili aidha kurudi kwenye nafasi yangu ya awali ama kama kutakuwa na chance nyingine watanipa nikakubali na nikajiapiza kuwa ndani ya hii miezi sita ntafanya kazi ambapo wao watahangaika kufikiria wanipeleke wapi,,,,,yule Dada alirudi nikapigiwa Simu na HR kuwa rasmi wananipa permanent contract na natakiwa kwenda kureport mwanza ndiko kitakuwa kituo changu cha kazi kama bank teller, safari yangu rasmi ikaanzia hapo namshukuru sana Kaka yangu na yule Manager kwa kuniamini kwani MUNGU amekuwa mwema napanda vyeo kila mwaka na mm nimekuwa mibaraka kwa vijana wengine kuwapatia nafasi ndani na hata nje ya taasisi. Wazungu wanasema "Success is where lucky meets good preparation" niamini mimi connection haitafanya kazi kama ww mwenyewe binafsi hautakuwa na maandalizi mazuri kuchukua fursa zitakazo kuwa mbele yako.

Kikubwa zaidi muombe sana MUNGU bila kuchoka, weka juhudi kubwa pale unapopewa nafasi ndogo, kuwa mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu na heshima inalipa sana.
Naomba nafasi kama kijana mwenzio pia, nimesoma BA in Microfinance&Enterprise development
 
Pole sana mdogo wangu. Nilikuwa kama wewe mwaka 2009 mpaka 2012 ila yote yamepita na imebaki kuwa historia.

Ninakuombea kwa Mungu wewe pamoja na vijana wengine wanaohangaika kupata kazi kuwa ipo siku utakuwa na pesa nyingi sana mdogo wangu.
Amina...🙏🙏🙏
 
Katika maisha na mafanikio kwa ujumla bahati pia ina play a very big role. Sijui umesomea nini exactly na level of confidence na power ya kujieleza uliyo nayo ila kimsingi naona utakuwa ni mtu mwenye zali sana katika maisha. Kuna watu wana qualifications za hali ya juu ila kupata kazi still ni kipengele na interview kibao washaenda.

Bahati tu na Mungu

CV yangu hakuna mahali naweza tuma nisiitwe, NASEMA HAKUNA TZ HII UTUMISHI SIJAWAHI OMBA KAZI NISIITWE

Ishu kwangu ni Kujieleza, yaani hapo huwa nakua kama kuku aliemwagiwa maji. Kiingereza kinanisalitigi sana

Ila Mungu mwema siku nafanya usaili wa Oral wakaniuliza kiswahili maswali kama 4
 
Acha tu mkuu, nilienda kwenye interview moja tena benk, tumefanya round one tulikuwa kama 300 hvi, tukatokea 10 kati ya wale 300, interview ilikuwa ya round w tu ndo mana walikata kutoka 300 mpaka kumi kupunguza idadi ya wanaoenda round ya 2 ambayo ni mwisho

Tulipoenda tulikuwa wanaume 2 na wanawake 8

Interview ikaendelea, ilipofika zamu yangu wakauliza maswali mpaka ya siasa, nkajibu

Mwisho wakaniambia eti nina mwili mdogo sitoiweza nafasi nanayoiomba mana nafasi hiyo chini yake kuna watu wengine wazima na wakubwa sana kimwil hivyo hawataniheshimu

Najuta kuwa na mwil mdogo, nilitaman Mungu aniumbe upya, mpaka leo npo mtaani zaid ya 5 yrs sasa
Kwani ilikuwa kazi ya kubeba zege au?
kwa sababu hizo Rais wa nchi inabidi awe Giant
 
Acha tu mkuu, nilienda kwenye interview moja tena benk, tumefanya round one tulikuwa kama 300 hvi, tukatokea 10 kati ya wale 300, interview ilikuwa ya round w tu ndo mana walikata kutoka 300 mpaka kumi kupunguza idadi ya wanaoenda round ya 2 ambayo ni mwisho

Tulipoenda tulikuwa wanaume 2 na wanawake 8

Interview ikaendelea, ilipofika zamu yangu wakauliza maswali mpaka ya siasa, nkajibu

Mwisho wakaniambia eti nina mwili mdogo sitoiweza nafasi nanayoiomba mana nafasi hiyo chini yake kuna watu wengine wazima na wakubwa sana kimwil hivyo hawataniheshimu

Najuta kuwa na mwil mdogo, nilitaman Mungu aniumbe upya, mpaka leo npo mtaani zaid ya 5 yrs sasa
That was so unproffesional of them you applied for the job because you had the qualifications they needed. Kwenye Tangazo la kazi hawakuweka physique appearance kama moja ya vigezo vya kupata kazi (ah waliweka?) kwangu mimi huo ni unyanyapaa....and I swear nnavyopenda kucheza na sheria ninge wa sue [emoji1][emoji1] Yani ungekua na mwanasheria mzuri mbona hiyo ni kesi na wangekulipa....

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom