MUNGU ni mwema
Baada ya kumaliza chuo July 2016 nilijiapiza kwamba nisingerudi mkoani hadi nitoboe lakini nilijiwekea ukomo wa miezi nane tu kama ningechemka kupata upenyo basi ningehamishia mashambulizi mkoani hivyo nililipia kodi miezi sita kwani miwili ilikuwa ndani ya mkataba.
Hustle zikaanza rasmi nikawa nimejiwekea utaratibu wa kusambaza CV tatu kila siku ila approach yangu haikuwa kuacha reception, kabla ya kwenda kampuni husika nilikuwa nasoma Company profile ili kujua viongozi wakubwa kama Operation manager,HR manager au hata Mkurugenzi hivyo nikifika hapo namwambia secretary nimekuja kumuona mtu fulani nina shida ya kiofisi hii mbinu sio rahisi kama huna confidence na haifanyi kazi sehemu zote kwani kuna wakubwa kutokana na majukumu yao hawapendi kuonana na mtu ambate hakuwa na appointment nae, binafsi ilinisaidia sana kwenye kujenga kujiamini kwani niliweza kukutana na watu wakubwa physically na kuongea nao japo waliishia kuniambia CV niache kwa HR hivyo sikuwahi kuitwa popote kwa ajili ya interview ama ajira.
Kuna muda sikuwa na nauli basi jua likawa langu na mvua pia ilikuwa kawaida kutoka mtongani hadi posta kwa mguu yani mvua ikinyesha bahasha inachanika mara CV zimeloa inabidi shughuli siku hiyo iishie hapo.
2.Connection
Siku moja nikiwa kwenye daladala naelekea mikocheni nilipigiwa simu na kaka yangu akaniambia nimtumie CV yangu haraka sana nikamuomba kondakta anishushe ilala nikaingia internate cafe chap nikafanikisha, nauli ikawa imekata ikabidi nirudi getto kwa mguu, aisee ndugu usiniulize nilkuwa nakula nini kama tu nauli ilikuwa inanishinda mimi nilikuwa naloweka mchele nakula nalala nisingeweza kupika sina gesi wala mkaa ila MUNGU ni mwema yamepita japo yanaweza kujirudia so ni suala la kuendelea kuwa mwaminifu kwa MUNGU.
December 1,2016 nikiwa getto nimejilaza natafakari nilipokea Call kutoka Benk fulani wakinialika kwenye interview ila natakiwa nikafanyie mkoani aisee ilikuwa jumatatu na natakiwa jumatano niwe huko nilipagawa basi nikamjulisha bro akaniambia poa ntakuchangia nauli uende nilimshukuru sana, nilijiandaa vizuri mno nilifika eneo la tukio tulikuwa watu kumi na tano na walitakiwa watu wanne tu mm ndiye niliyekuwa mtu wa kwanza aisee nilipiga interview kwa hasira hadi Manager akaacha kuandika marks akaanzisha mjadala kwa kiswahili finally akasema nahitaji kufanya kazi na wewe tuka shake hands nikaondoka kesho asubuhi nikapigiwa simu kuwa nimepata kazi natakiwa nipeleke nyaraka zote ikiwemo vyeti, picha nk ilikuwa ni kazi ya uwakala wa mauzo (sales agent) na walikuwa wanahitaji watu wa diploma tu ila naambiwa wengi walikataa coz ni kazi ngumu na haina maslahi kiivyo,,,,nilijisemea nitafanya kazi hii kwa nguvu zangu zote ndani ya mwaka mmoja sitakuwa hapa tena.
Recruitment process ilichukua muda kidogo tuliitwa kuanza kazi mwezi wa kwanza 2017, aisee nilikuwa napambana sana na strategy zangu zilikuwa poa sana basi baada ya miezi miwili kukatokea shortage ya mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa anaenda maternity basi wakatangaza fixed term opportunity wengi tulifanya application pamoja na wengine tuliowakuta pale baada ya interview namshukuru MUNGU pia nikatoboa wakaniambia nitafanya for six months akirudi mwente nafasi yake kutakuwa na mawili aidha kurudi kwenye nafasi yangu ya awali ama kama kutakuwa na chance nyingine watanipa nikakubali na nikajiapiza kuwa ndani ya hii miezi sita ntafanya kazi ambapo wao watahangaika kufikiria wanipeleke wapi,,,,,yule Dada alirudi nikapigiwa Simu na HR kuwa rasmi wananipa permanent contract na natakiwa kwenda kureport mwanza ndiko kitakuwa kituo changu cha kazi kama bank teller, safari yangu rasmi ikaanzia hapo namshukuru sana Kaka yangu na yule Manager kwa kuniamini kwani MUNGU amekuwa mwema napanda vyeo kila mwaka na mm nimekuwa mibaraka kwa vijana wengine kuwapatia nafasi ndani na hata nje ya taasisi. Wazungu wanasema "Success is where lucky meets good preparation" niamini mimi connection haitafanya kazi kama ww mwenyewe binafsi hautakuwa na maandalizi mazuri kuchukua fursa zitakazo kuwa mbele yako.
Kikubwa zaidi muombe sana MUNGU bila kuchoka, weka juhudi kubwa pale unapopewa nafasi ndogo, kuwa mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu na heshima inalipa sana.