Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

na kama upinzani wa kweli utatoka ndani ya Chama Cha Mafisadi na huo utakuwa ndio mwisho wake. alama za haya kutokea zinaanza kuonekana, angalia kauli za msuya, sumaye, warioba na butiku utajua

Mkuu Ochu,

Sijakupata hapa unamaanisha ndio itakuwa mwisho wa CCM au upinzani, kama hutajali fafanua.
 
Mkamap,

Nakubaliana kabisa kuhusu haki ya msingi ya kila mtanzania ni pamoja na kukubali kuwa na affiliation ya chama au kukataa. kama CCM wameona kuwa haki ya msingi ya watanzania walioko nje ni pamoja na kuwapa matawi ya CCM nafikiri sitakuwa nimekosea kuwa wanakandamiza kwa namna moja au ingine haki ya msingi ya kupiga kura. Tukifocus kuwa matawi ni ya kuwasaidia wananchi walioko nje katika mambo mengine pamoja na kugombea uongozi wakirudi vile vile itakuwa bora kama wataruhusiwa kupiga kura huko waliko. Idea ya wananchi wa nje kupiga kura iliishawakilishwa kwa balozi aliyepita na hakuona umuhimu wa kufuatilia wala kutoa feedback ya swala zima linaendelea vipi. Itakuwa jambo la busara wala sio kwa CCM tu ila kwa chama chochote ambacho kitasimamia maslahi ya watanzania walioko nje kupiga kura. Na changamoto vile vile inaweza kuwa kwa watanzania walioko nje kusukuma hii idea kwa ajili ya maslahi yao.

Nafikiri ccm ndio mpango Lakini yawezekana wanasita kutokana na MAKELELE ya wapinzani maana wakifanya hivyo wapinzani watasema ni move ya kuiba kura.
ccm wakianzisha uraia wa nchi mbili wapinzani wanaibuka na kusema ni njisi ya kuficha mafisadi na kuuza nchi.
Dugu yangu mambo pale ni magumu sana kila ukitaka kufanya jambo la maana jamaa wanakushika shati .
 
Kubwajinga,

Nafikiri utakuwa hujakosea kuwa pamoja na kwamba mabadiliko yanaweza kuletwa na nguvu waliyonayo CCM, wapinzani pia wana nafasi yao katika kubadilisha sura ya Tanzania na kama hawatafanya hivyo sidhani kama wananchi watawasamehe kwa kushindwa kutimiza their end of the bargain.

GM,

Wapinzani wana nafasi kubwa sana katika mageuzi kama yakitokea ndani ya CCM, lakini itategemeana sana na mambo mawili makubwa;
  1. Je CCM watabadilika katika mfumo gani. Watavunjika vipande vipande au watazaliwa upya. Hii ni muhimu sana kwa upinzani kwani kama CCM wakijibadilisha vizuri ndani yao na kukubalika, basi wanaweza wakakaa madarakani mpaka sunami lingine lije. Hili ndio ninaloona kuwa rahisi kutokea na dawa yake ni moja tu kwa wapinzani kuungana kiukweli-ukweli.
  2. Lingine ni kwa vyama vyenyewe vya upinzani kuwa viko katika hali gani kupokea mageuzi na demokrasia ya kweli? Je wana tofauti gani na CCM hasa kimiundo na demokrasia ndani yake? Hii ni muhimu sana pale CCM itakapovunjika vipande vipande na kuhitaji mwokotaji wake. Kwa hali ya njaa na siasa za TZ hili bado ni gumu kidogo lakini bado linawezekana. Kama ikitokea, basi ni vile vyama tu vyenye mvuto wa demokrasia halisi, no matter how small they are, ndio vitakavyofaidika. Sidhani kama mtu atakimbia CCM kwa kukosa demokrasia halafu akakimbilia chama kingine ambacho nacho kina mizengwe ndani yake kama ya mzee Makamba.
 
Kwamba Upinzania na Mageuzi ya kweli kuletwa na CCM!!!!

La hasha!

Hizi ni ndoto za walevi wa Siasa potofu za Ki CCM.
Upinzani wa kweli utatoka kwa Watanzania wenye nia na dhamira ya kujenga nchi yao.
Ni uongo mkubwa tena ni upotoshaji wa ukweli kuleta na kutetea dhana kwamba upinzani wa kweli utatoka CCM.

CCM ni chama Mfu kilichovunja nguzo zote muhimu za kukisetiri chama chochote cha kisiasa Duniani na kubakiwa na nguzo fikirivu isiyo weka mizizi yeyote ndani na nje ya chama, nguzo ya Fedha.

Ukitoa Ngawira hakuna CCM wanabakia hayawani wenye roho za kinyang'au waliotayari kutumia makucha yao marefu na midomo yao yenye meno marefu na ya kuchongoka.

CCM kama kundi la kisiasa limemeza matapishi yake ya mwaka 1967,ni Mbadala wa Ukoloni na Kansa katika mwili wa Tanzania.

CCM ni Mbweha halisi katika ngozi za binadamu.

Viongozi wa CCM, wanachama wa CCM, mashabiki wa CCM na wapambe wa wana CCM wote wako hapo na wanafanya hayo wafanyayo kwa sababu ya fedha au kwa mategemeo ya kupata fedha au chochote kile chenye maslahi binafsi kiuchumi au cha kuwawezesha kupooza hamu zao za kimwili.

Suala la kujenga nchi, au kujenga chama chao wenyewe kwao wana CCM limepitwa na kupewa kisogo kama ilivyo pitwa na kupewa mgongo siasa ya ujamaa na kujitegemea na mjomba wake Azimio la Arusha.

Upinzani wa kweli kamwe hauwezi kutoka katika chama Mfu na kilichojaa uoza, yaani chama cha CCM. Upinzani wa kweli utatoka kwa Watanzania walio Sturbon na walioshinda vishawishi vingi, Watanzania wawekao maslahi ya taifa mbele, Watanzania wenye Nia Dhamira na Mwelekeo Chanya wa kuiendeleza nchi yao, Watanzania wenye utu na wasio na kutu.

Macho yetu, masikio yetu na matumaini yetu sisi wanasiasa wa mwituni hayako ndani ya mduara wa Kinyang'au wa CCM,Matumaini yetu yako nje ya mduara huo haramu.

Matumaini yetu yako juu ya kizazi kipya chenye mawazo mapya cha uzao usio na damu iliyo hirimishwa ya Ki CCM. Kizazi hicho kilikuwepo kabla ya Uhuru, kilikuwepo siku ya Uhuru na kipo leo hii miongoni mwa Mamillioni ya Watanzania.
 
Nafikiri ccm ndio mpango Lakini yawezekana wanasita kutokana na MAKELELE ya wapinzani maana wakifanya hivyo wapinzani watasema ni move ya kuiba kura.
ccm wakianzisha uraia wa nchi mbili wapinzani wanaibuka na kusema ni njisi ya kuficha mafisadi na kuuza nchi.
Dugu yangu mambo pale ni magumu sana kila ukitaka kufanya jambo la maana jamaa wanakushika shati .

Mkamap,

Well stated here, I do agree with you then.
 
Hongera Wana-CCM wa Missouri chama ni chenu mna kila haki ya kukijenga mnavyojua.
 
GM,

Wapinzani wana nafasi kubwa sana katika mageuzi kama yakitokea ndani ya CCM, lakini itategemeana sana na mambo mawili makubwa;
  1. Je CCM watabadilika katika mfumo gani. Watavunjika vipande vipande au watazaliwa upya. Hii ni muhimu sana kwa upinzani kwani kama CCM wakijibadilisha vizuri ndani yao na kukubalika, basi wanaweza wakakaa madarakani mpaka sunami lingine lije. Hili ndio ninaloona kuwa rahisi kutokea na dawa yake ni moja tu kwa wapinzani kuungana kiukweli-ukweli.
  2. Lingine ni kwa vyama vyenyewe vya upinzani kuwa viko katika hali gani kupokea mageuzi na demokrasia ya kweli? Je wana tofauti gani na CCM hasa kimiundo na demokrasia ndani yake? Hii ni muhimu sana pale CCM itakapovunjika vipande vipande na kuhitaji mwokotaji wake. Kwa hali ya njaa na siasa za TZ hili bado ni gumu kidogo lakini bado linawezekana. Kama ikitokea, basi ni vile vyama tu vyenye mvuto wa demokrasia halisi, no matter how small they are, ndio vitakavyofaidika. Sidhani kama mtu atakimbia CCM kwa kukosa demokrasia halafu akakimbilia chama kingine ambacho nacho kina mizengwe ndani yake kama ya mzee Makamba.

Kubwajinga,

Mkuu, I think time will tell!
 
Katiba ya CCM inasemaje kuhusu "ufunguzi" wa matawi nje ya Tz?
Msajili wa Vyama anasemaje kuhusu hilo? CCM ya Marekani, UK, India ndio hiihii tuliyonayo hapa BONGO?
 
Wildcard,

I wish I could answer you on this, ukweli ni kwamba sijawahi iona katiba ya CCM maishani na inakuwa vigumu kukujibu, labda kama wewe au mtu yeyote ana katiba anaweza kutusaidia na swala hilo.
 
Katiba ya CCM inasemaje kuhusu "ufunguzi" wa matawi nje ya Tz?
Msajili wa Vyama anasemaje kuhusu hilo? CCM ya Marekani, UK, India ndio hiihii tuliyonayo hapa BONGO?

Katiba ya CCM haisemi lolote kuhusiana na matawi nje ya nchi kama ilivyo sheria ya vyama vya siasa. kwa kuwa sheria hiyo inafanyiwa marekebisho, naamini kuwa hili no moja ya masuala yatakayoelezwa kwenye sheria mpya
 
Katiba ya CCM inasemaje kuhusu "ufunguzi" wa matawi nje ya Tz?
Msajili wa Vyama anasemaje kuhusu hilo? CCM ya Marekani, UK, India ndio hiihii tuliyonayo hapa BONGO?

Mkuu WildCard katiba ya CCM inasema hivi

SEHEMU YA TATU
VIKAO VYA CCM
FUNGU LA 1:
VIKAO VYA SHINA
21. Kikao cha mwanzo kabisa cha CCM kitakuwa
ni kikao cha Shina. Hapa ndipo kila
mwanachama atadhihirisha uanachama wake
kwa kutekeleza kwa vitendo wajibu wake wa
uanachama. Aidha hapa ndipo alama
zinazokitambulisha Chama kama vile bendera,
zitakapoanzia kutumika.
22. (1) Kutakuwa na aina zifuatazo za Mashina:-
(i) Mashina ya Ndani ya Nchi:-
(a) Mashina yaliyoundwa katika maeneo
ya makazi.
(b) Mashina maalum yaliyoundwa katika
Ofisi za CCM, Jumuiya za Wanainchi
zinazoongozwa na CCM na Taasisi
nyingine za CCM.
(c) Mashina ya Wakereketwa/Maskani
yaliyoundwa na Wana CCM katika
maeneo husika, baada ya kupata
idhini ya Kamati ya Siasa ya Wilaya.
(ii) Mashina ya Nje ya Nchi:-
Mashina yaliyoundwa Nje ya Nchi
katika maeneo wanakoishi wanachama
16 Katiba ya Chama Cha Mapinduzi
Shina
Aina za Mashina
wa CCM, baada ya kupata idhini ya
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

(2) Ili Wanachama waweze kuunda Shina,
idadi yao isiwe chini ya watano.
(3) Kila Shina la eneo la makazi au lililo nje ya
nchi na kila Shina Maalum litachagua
Kiongozi wa Shina kwa mujibu wa utaratibu
uliowekwa ambaye atajulikana kama Balozi
wa Shina. Aidha kila Shina la Wakereketwa/
Maskani litachagua Kiongozi wa Shina kwa
utaratibu uliowekwa ambaye atajulikana
kama Mwenyekiti wa Shina la
Wakereketwa au la Maskani.
 
Kwamba Upinzania na Mageuzi ya kweli kuletwa na CCM!!!!

La hasha!

Hizi ni ndoto za walevi wa Siasa potofu za Ki CCM.
Upinzani wa kweli utatoka kwa Watanzania wenye nia na dhamira ya kujenga nchi yao.
Ni uongo mkubwa tena ni upotoshaji wa ukweli kuleta na kutetea dhana kwamba upinzani wa kweli utatoka CCM.

CCM ni chama Mfu kilichovunja nguzo zote muhimu za kukisetiri chama chochote cha kisiasa Duniani na kubakiwa na nguzo fikirivu isiyo weka mizizi yeyote ndani na nje ya chama, nguzo ya Fedha.

Ukitoa Ngawira hakuna CCM wanabakia hayawani wenye roho za kinyang'au waliotayari kutumia makucha yao marefu na midomo yao yenye meno marefu na ya kuchongoka.

CCM kama kundi la kisiasa limemeza matapishi yake ya mwaka 1967,ni Mbadala wa Ukoloni na Kansa katika mwili wa Tanzania.

CCM ni Mbweha halisi katika ngozi za binadamu.

Viongozi wa CCM, wanachama wa CCM, mashabiki wa CCM na wapambe wa wana CCM wote wako hapo na wanafanya hayo wafanyayo kwa sababu ya fedha au kwa mategemeo ya kupata fedha au chochote kile chenye maslahi binafsi kiuchumi au cha kuwawezesha kupooza hamu zao za kimwili.

Suala la kujenga nchi, au kujenga chama chao wenyewe kwao wana CCM limepitwa na kupewa kisogo kama ilivyo pitwa na kupewa mgongo siasa ya ujamaa na kujitegemea na mjomba wake Azimio la Arusha.

Upinzani wa kweli kamwe hauwezi kutoka katika chama Mfu na kilichojaa uoza, yaani chama cha CCM. Upinzani wa kweli utatoka kwa Watanzania walio Sturbon na walioshinda vishawishi vingi, Watanzania wawekao maslahi ya taifa mbele, Watanzania wenye Nia Dhamira na Mwelekeo Chanya wa kuiendeleza nchi yao, Watanzania wenye utu na wasio na kutu.

Macho yetu, masikio yetu na matumaini yetu sisi wanasiasa wa mwituni hayako ndani ya mduara wa Kinyang'au wa CCM,Matumaini yetu yako nje ya mduara huo haramu.

Matumaini yetu yako juu ya kizazi kipya chenye mawazo mapya cha uzao usio na damu iliyo hirimishwa ya Ki CCM. Kizazi hicho kilikuwepo kabla ya Uhuru, kilikuwepo siku ya Uhuru na kipo leo hii miongoni mwa Mamillioni ya Watanzania.

Madela-Wa-Madilu,

Naona umefikisha ujumbe wako ila nafikiri siyo haki kuwafikiria kuwa CCM wote ni mbweha, wapo wenye uchungu na nchi yao ambao wewe au mimi tunaweza kuwajua au tusiwajue. sina Mpango wa kuwatetea CCM hata kidogo wao kama chama au wanachama wa CCM walioko hapa watajitetea kwa kadiri ya mtizamo wao, ila kuwajumuisha wote kuwa ni Mbwewa na ni watu wanaotafuta pesa au dili za pesa sio haki wapo kweli ambao wana tabia au description uliyoitoa tena wengi tu. Whomever the hat fit, let them wear it, ila sio kila mwanachama wa CCM.
 
Asante kwa quotation mkuu Masatu, lakini WildCard aliuliza kuhusu Matawi, na si Mashina
 
Shukran mkuu Mpita njia, what abt this one;

FUNGU LA II
VIKAO VYA TAWI
31. (1) Kutakuwa na aina nne za Matawi ya CCM
kama ifuatavyo:-
(a) Matawi ambayo yameundwa vijijini
ambayo yataitwa Matawi ya Vijijini.
(b) Matawi ambayo yameundwa katika
maeneo wanayoishi watu mijini
ambayo yataitwa Matawi ya Mitaani.
(c) Matawi maalum ambayo yameundwa
kwenye Ofisi za CCM, Taasisi za CCM,
na Taasisi nyingine zinazoongozwa na
CCM.
(d) Matawi ambayo yameundwa nje ya nchi
yenye wana-CCM wengi wanaoishi
katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo
na ambao wana Mashina yao. Matawi
haya yatafunguliwa kwa idhini ya Kamati
Kuu.
 
Asante kwa quotation mkuu Masatu, lakini WildCard aliuliza kuhusu Matawi, na si Mashina

Mpita Njia,

Heshima mbele mkuu,

Naona hii kazi kweli kweli hapa katika mtizamo wa chama matawi na mashina tofauti yake nini, au katika mtizamo wowote wa utaratibu wa kawaida ambao hauhusu chama chochote tofauti ziko wapi? mtu yeyote anayeweza kufafanua hili anakaribishwa.
 
Masatu,

Naona post moja umeweka mashina na ingine ukawepa matawi nafikiri umeweka matawi ikiwa ni katika kujibu hoja ya Mpita njia, is it safe to assume kuwa matawi na mashine yanamaanisha kitu kile kile?
 
Gm

Matawi na mashina ni vitu viwili tofauti kama jina lilivyo tofauti. Shina ni nganzi ya chini kabisa na tawi ni ngazi ya juu yake
 
Hakuna upinzani wa kuletwa na ccm wala nini.
ccm hao hao wanajuwa cha kufanya ili wawatetee wananchi...Walitumie bunge na si kuleta unafiki wa kuhama vyama.
Upinzani ni ushetani...Na ndio maana hata shetani mwenyewe alikuwa mpinzani wa Mungu na akatupwa duniani na kulaaniwa kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Kama hao wabunge wa ccm walipitisha bajeti na hawakuuliza maswali kuhusiana na mikataba mibovu...Hata kama wakihamia ahera na kufungua chama hakuna kitakachobadilika.
Ukweli ni ukweli tu...Ndio maana halisi ya nguruwe na lipstick.
Huwezi kumbadilisha mtu eti kwa kigezo cha kubadilisha chama!
THUBUTU!
SHEITWAN NI SHEITWAN TUUUU.....HATA MBINGUNI HUWA ANAHUDHURURIA...KUMBUKENI KESI YA AYUBU.
 
Hakuna upinzani wa kuletwa na ccm wala nini.
ccm hao hao wanajuwa cha kufanya ili wawatetee wananchi...Walitumie bunge na si kuleta unafiki wa kuhama vyama.
Upinzani ni ushetani...Na ndio maana hata shetani mwenyewe alikuwa mpinzani wa Mungu na akatupwa duniani na kulaaniwa kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Kama hao wabunge wa ccm walipitisha bajeti na hawakuuliza maswali kuhusiana na mikataba mibovu...Hata kama wakihamia ahera na kufungua chama hakuna kitakachobadilika.
Ukweli ni ukweli tu...Ndio maana halisi ya nguruwe na lipstick.
Huwezi kumbadilisha mtu eti kwa kigezo cha kubadilisha chama!
THUBUTU!
SHEITWAN NI SHEITWAN TUUUU!

Mkuu JMushi1,

Nguruwe na lipstick hapo kazi kweli kweli, LOL
 
Back
Top Bottom