Je, wajua Wakristo huwasindikiza Waislamu Kufunga Ramadhan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tutafunga siku 40, vipi Waislamu Mtatusindikiza?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi

Hili ni bandiko la swali kuwa

Je, wajua kuwa sisi Wakristo huwa tunanawasindikizaga ndugu zetu Waislamu kufunga swaumu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tunaanza safari ya kufunga kwa siku 40, vipi nyie wenzetu Waislamu, je mtatusindikiza kama ambavyo sisi tunavyo wasindikizaga?​


Leo ni siku ya Jumatano ya Majivu, Ash Wednesday ambayo ni kisheria cha mwanzo wa kufunga siku 40 kwa Wakristu kote duniani kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyofunga siku 40 Jangwani kabla ya kusulubiwa kwa mateso, na kufa msalabani siku ya Ijumaa Kuu ambapo Jumapili Alfajiri alifufuka katika wafu, akakaa na sisi duniani kwa siku 40 nyingine kisha akapaa mbinguni. Toka huko atarudi tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu na ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Naomba kulianza bandiko hili lina sehemu 3.
  1. Sehemu ya kwanza ni sala ya Kanuni ya Imani
  2. Sehemu ya Pili ni Maana ya Jumatano ya Majivu
  3. Sehemu ya Tatu ni Mastori ya Pasco na Umuhimu wa kufunga.

Sehemu ya Kwanza​

Sala ya Kanuni ya Imani​

Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi
Mwumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu,mwana wa pekee wa Mungu.
Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa Mungu,mwanga kwa mwanga,Mungu kweli kwa Mungu kweli.
Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba,
ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.
Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.
Akapata mwili kwa uwezo wa roho mtakatifu kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu.
Akasulibiwa pia kwa ajili yetu sisi
Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,akafa akazikwa.
Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
Akapaa mbiguni, amekaa kuume kwa baba
Atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa na mwisho
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu Bwana mleta uzima atokaye kwa Baba na Mwana anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana aliyenena kwa vinywa vya manabii.
Nasadiki kwa Kanisa moja,Takatifu Katoliki la mitume
Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu.
Na uzima wa milele ijayo.
Amina.

Sehemu ya Pili

Maana ya Jumatano ya Majivu, hii ni C&P
Kutoka IFAHAMU JUMATANO YA MAJIVU
UTANGULIZI
Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa. Ni ishara ya kuanza kwa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu ili kuichukua aibu yetu. Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu.

KWA NINI TUNAPAKWA MAJIVU?
Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa kisakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13

KWA NINI MAJIVU YAPAKWE KATIKA PAJI LA USO NA SI PENGINEPO?
Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

MANENO ANAYOTAMKA PADRE YANA MAANA GANI?
Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.
Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

MAJIVU HUTOKA WAPI?
Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

KWA NINI TUNATUMIA MATAWI YA JUMAPILI YA MATAWI?
Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

KANISA LIMEKATAZA NINI SIKU YA JUMATANO YA MAJIVU?
Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

NANI ANALAZIMA KUFUNGA SIKU YA JUMATANO YA MAJIVU NA KWARESMA?
Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

TUNAPOSEMA KUJINYIMA WAKATI WA KWARESMA TUNAMAANA GANI?
Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

MWISHO
Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema

Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.
Sehemu ya Tatu: Mastori ya Pasco
Dini mbili Kuu duniani ni Wakristo na Waislamu, hakuna sensa yoyote iliyowahi kufanyika duniani kuestablish Wakristu ni wangapi na Waislamu ni wangapi hivyo hakuna data nani ni wengi zaidi ya wengine. Kwa Tanzania enzi za sensa za mkoloni waliwahesabu hadi makabila na dini, kuna wakati Waislamu wslikuwa wengi Tanganyika baadaye Wakristu wakawa wengi, tulipuungana na Zanzibar na kwa Tanzania, sensa ya mwisho yenye swali la dini Waislamu wakawa wengi.

Baada ya hapo Mwalimu Nyerere akafuta maswali ya udini, sensa zote zilizofuatia hakuna tena kujua idadi nani ni wengi, ila baada ya Awamu ya kwanza zikaanza kelele za marginalisation ya dini fulani mara, mara ... kwa vile hili sii jukwaa la siasa hayo tuyaache ila sio wengi wanaofahamu kuwa Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba Mmoja, Ibrahim na Sheria ya Mungu kwa hizi dini zote mbili Wakristo na Waislamu ni sheria moja ile ile ya Musa amiliyoshushwa kwenye Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ndani ya Biblia Takatifu na Tourat ndani ya Quran Tukufu, na si wengi wanafahamu kuwa Yesu Kristo wa kwenye Biblia aliyezaliwa na Bikira Maria kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndiye yule yule Nabii Issa Bin Maryam wa kwenye Quran Tukufu.

Hili la Wakristu na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja, Jielimishe zaidi hapa "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

Baada ya kumaliza Shule ya sekondari nikajiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari TSJ, kilichopo Ilala Sharrif Shamba
Hapo TSJ, kila chumba wanakaa wanafunzi wawili na mko free kujichagua wanafunzi mnao endana, hivyo mimi mwaka wa kwanza nikakaa chumba kimoja na Innocent naomba nisitaje majina ya pili maana mambo ya ujana ni maji ya moto!.

Hapo TSJ ni chuo kidogo chenye madarasa mawili tuu, mwaka wa kwanza na mwaka wa pili, hivyo mabweni pia yalikuwa mawili tuu, bweni la wanaume wanaume likiitwa Ngorongoro na Bweni la Wanawake likiitwa Serengeti nadhani yalikuwa just 30 metres apart.

Kama ilivyo kwa wanaume, wanawake nao wanachaguana marafiki, wanakaa chumba kimoja. Wanyama wa Ngorongoro walikuwa na kibarua kimoja cha kuwinda wanyama wa Serengeti!.

Sasa ili kupata rahisi wa mahindi, nyinyi Simba wawili wa Ngorongoro lazima muwinde swala wawili wa chumba kimoja cha Serengeti ili muweze kufanya exchange bila kulazimika kupigana exile za muda mrefu wa usiku.

Hivyo ikatokea room mate wangu Inno akapenda kaswala fulani Tanga Line kule Serengeti kakikiitwa Suzy na room mate wa Suzy ni katoto kamoja ka familia ya kitajiri huko Moshi kakiitwa Joy!.

Mimi nikipigwa exile na Inno, nakwenda Serengeti ku buzz buzz chumbani kwa Suzy, na huyo Joy, sasa katika hizo buzz buzz unakuja kujikuta umepitiliza!.

Mwaka uliofuata Inno akachaguliwa kuwa president wa chuo, miongoni mwa privileges za president ni kupewa a single room ya pekee yako hivyo Inno akahamia chumba cha pekee yake, na mimi nikamkaribisha mwanafunzi Muislamu Abou!.

Inno baada ya kuwa na single room japo aliendelea na Suzy ila ukiwa kijana sana na una uhuru sana, ni changamoto, haswa inaporokea viswala ni vingi na vina katisha katisha!. Inno akaanza ku riot mara.. mara... Suzy hakukubali!, binti wa Kitanga akipenda ni amekwenda!, Inno si yuko pekee yake single room, kwenye zile riot za hapa na pale, si Inno akapotea njia akapita Tanga line nyingine!, kachuo kadogo, wanawake 50 wanaume 50! Unaweza kupita mahali ikawa siri, lakini mtu huwezi kupitia Tanga line mbili zote zipende na iwe siri!.

Kwa vile kwa Inno Suzy ndio alikuwa ametangulia na Inno yuko single, Suzy akaamua kukaba hivyo ni kila siku atalinda goli, na kila akilinda goli, kule room kwa Suzy kuna vacancy mimi naitwa Joy anaogopa kubaki peke yake!. Mwisho wa siku Suzy akaamua kuhamia jumla. Joy akamkaribisha Joy mwingine na kule Serengeti kuliwa na Mwanamke mmoja wa Kizanzibari akiitwa Untie Ummy akavikungwi vile vibinti mambo ya Kizanzibari!, Msukuma mimi kwisha habari yangu nikawa naamkia Serengeti kila uchao!. Let me cut shot this long story short, mwisho wa masoko, Inno alimuoa Suzy, Mimi nikamuoa Joy, yuko jamaa wa wa Madiba anaitwa Stan akamuoa Jane, jamaa mmoja wa Lesotho Kotso akamuoa Mgulwa, nadhani kungewa na survey ni chuo gani nchini Tanzania kinaongoza kwa kutengeneza couples ziizoishia kuoana rasmi tena ndoa za kanisani from ni TSJ!. Mimi kwenye harusi yangu Inno na Suzy ndio best man na matron!.

Tukiwa TSJ, Untie Ummy aka organize a trip ya darasa zima kutembelea Zanzibar, mimi ndio mara yangu ya kwanza kupanda boti, kuvuka maji na kufika Zanzibar. Trip ikaangukia mwezi wa Ramadan hivyo Aunt Ummy akalazimisha wote lazima kufunga!. Zanzibar mwezi Mtukufu hotel zote zinafungwa mchana isipouwa za Kitalii na hakuna kula hadharani hata kama ni Mkristu!. Na mwezi huo, Kyle Zanzibar hata ile biashara ya usiku ya dada zetu wale, inasimama!. Mimi nilivyo mpekuzi ndipo nikagundua kumbe pia sio Waislamu wote wanafunga mwezi mtukufu, wale ambao hawawezi kufunga kwa sababu mbalimbali kuna sehemu inaitwa Chimbo unaingia na kula kwa kificho, jioni unafuturu kama kawaida as if umefunga!. Hata zile huduma za wale dada zetu za usiku, japo zinasitishwa mwezi Mtukufu, kule chimbo zipo unasema tuu ulipo, uletewe kwa kificho!.

Baada ya kuanza kuishi chumba kimoja na Abou, kumbe Abou kwao Swala 5!. ulipofika mwezi mtukufa wa Ramadhan Abou anafunga na jioni kunikaribisha kwao Ilala kufuturu, mimi sifungi lakini futari ya kwa Mama Abou pale Ilala tamu balaa haswa hayo mapochopocho!.

Nikaanza kujifunza kufunga mara moja moja!. Kiukweli unapofunga kweli na kufuturu na Waislamu, unajisikia vizuri sana hivyo nikawa nafunga more often.

Tulipomaliza TSJ mimi na Abou tukaajiriwa RTD siku moja, tangapangiwa nyumba moja Ilala Bungoni, nyumba ya Dada mmoja akifanya kazi ATC akiitwa Da Mwajuma, akishindwa na wadogo zake mabinti watatu, Zena, Halima na Rahema.

Da Mwajuma akamuachia nyumba mdogo wake Halima, yeye na Rehema wakahamia Masaki ya kupitia Msasani Mwisho, huko amejenga, hivyo hapo Ilala tukawa tunaishi mimi na Abou Flat moja, next door ni Halima Mchuka. Hivyo mwezi mtukufu wa Ramadhani mimi nikawa nafunga kweli kuwasindikiza Abou na Halima, na Halima kwa Bagamoyo hivyo futari yake sio mchezo!, ikawa kufururu ni ama kwa Halima, ana Ilala Flat kwa Mama Abou ama tunaalikwa Msasani kwa Da Mwajuma. NB. Halima nae tukamvuta RTD na akawa mtangazaji mahiri Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu! na Kwanini Hatuna Watangazaji wa Kike wa Mpira Miguu?. Tanzania Alijitokeza Mmoja, Halima Mchuka, Leo ni Miaka 10 Toka Afariki, Kwanini Hana Mrithi? na hata baada ya miaka 10 Tribute to Halima Mchuka: Miaka 10 Baada ya Kifo Chake, Her Legacy Still Lives On!, Bado Ndiye "The One and Only" Mtangazaji wa Kike wa Mpira Bongo!.

Mwaka 1995 nikaacha kazi RTD na kujiunga na DTV, ni TV ya kina Dewji Waislamu wa Ismailia, Shia Ithnasher, siku ya kumbukumbu ya Imam Husein ni live ya siku nzima!, ama kriketi. DTV ndio kituo cha kwanza kuonyesha live ya World Cup na mbio za magari za Formula One!. Hiyo live ya World Cup 1994 ilileta mambo!. Ushindani kuonyesha World Cup kati ya ITV na DTV. DTV wakashinda, Tajiri wa ITV akaripoti kwa Mchagga mwenzake Lyatonga, kuwa Wahindi wa DTV wanataka kununua!. Mchagga na Wahindi!. Mrema akatoa amri wakamatwe walazwe central indefinitely hakuna kesi wala kufikishwa mahakamani!. Ndugu wakamwendea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Silvanus Adel, akamuulizia IGP ushahidi wa kuwashikilia, akaambiwa hakuna, Katibu Mkuu akaamrisha waachiwe!. Mrema moja kwa moja kwa Rais Mwinyi!, kesho yake Silvanus Adel hana kazi!. Wahindi selo!, na kiukweli walisota!.

Nikiwa DTV canteen inafungwa mwezi mtukufu, niliendelea kufunga. 1996 nikapata tenda ya Masai Studio ku host Kitimoto. Wakurugenzi wa Masai ni Jove mgoa na Ally Oki . Mshauri wa Masai Studio ni Sheik Omar Jabir, mwanzilishi wa kwanza wa video studio nchini Tanzania JO Traders yeye na Omar Oki baba yake Ali Oki.

Hapa sasa mwezi Ramadan ni kila siku futari mahali, ofisi mzima ya Masai Studio lazima kufuturu mara kwa Mzee Jabir, mara kwa Sheikh Kassin Bin Jumaa, mara kwa Sheikh Nurdin Husein, mara kwa Sheikh Said Comerean, usikute kuna siku nilifuturishwa kwa kina faiza foxy bila kujua ndio maana Faiza ananijua. Ningekuwa sijaoa nakuapia Walahi ningesilimu na ningepewa mke maana mitaa ya Mohamed Said, pale Gerezani nimepita sana!.

Kila baada ya futari tunakwenda TCC Club, Gymkana or Dar Brotherhood kwenye mechi za usiku za Five a side!.
Nilikuwa naletewa kenzo na balaghashia za Oman, ilibaki kupata tuu sigda!, nikajikuta ni mimi mwenyewe bila kulazimishwa na mtu, mwezi Mtukufu wa Ramadan nafunga japo sio mwezi mzima!. End of mastori ya Pasco
Ndipo nikagundua kufunga kuna faida nyingi, achilia kufunga kwa ibada, kufunga hata bila ibada ni very beneficial to the body. Mwili unapumzika kufanya metabolism wakati wote hivyo kurelax na kufanya detoxification kuondoa sumu mwilini.

Tofauti ya Kufunga Kikistu na Kiislamu.
Kama nilivyo eleza mwanzo Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, na sheria ya Mungu ni sheria moja ile ile ya Musa, Waislamu wanaendelea kuifuata kama ilivyo, Kiislamu kufunga ni nguzo ya Kiislamu ni lazima.

Yesu alipokuja, hakuja kuitengua Tourat ya Musa, amekuja kuikamilisha, hivyo kufunga Kikistu sio lazima ni unapojisikia.

Kufunga kwa Waislamu ni hakuna kula chochote unakaa na njaa kuruhusiwi hata kunywa maji, ila rukhsa kumeza mate, kufunga kwa Wakristo ni ukozidiwa njaa, unaweza kula kidogo, ukizidiwa kiu unaweza kunywa kidogo.

Kufunga kwa Kiislamu ni kufunga kula tuu kunywa na kutokufanya dhambi ikiwemo kumega 'tunda!' kwa wenye ndoa zao baada ya kufuturu, unashushia chakula cha usiku ikiwemo kumega tunda!. Kufunga kwa Wakristo unaweza kufunga kitu chochote lakini starehe zote haziruhusiwi ikiwemo kumega 'tunda', hakuna cha wenye ndoa zao wala cha nini!, ndio maana wakati wa kipindi cha kwaresma hakuna sherehe yoyote wala ndoa yoyote ya Katoliki maana haiwezi kuwa consummated!

Kufunga kwa Kiislamu ni kufunga tuu chakula, lakini kufunga kwa Wakristo kuna room ya selectivity unachagua kufunga tuu kunywa pombe, au kuvuta sigara au starehe yoyote, mfano kwenda out, kufunga muziki, kufunga kuagalia TV, kufunga mitandao ya kijamii etc.

Kufunga kwa Waislamu kufungulia kunaitwa kufuturu na kunaendana na kuchomoza kwa jua ndio mwanzo wa kufunga na kuzama kwa jua ndio time ya kufuturu, kufunga kwa Wakristo hawana muda maalum wa kuanza wala muda maalumu wa kufungua na kufuangua kwetu hakuitwi kufuturu.

Kufunga kwa Waislamu kuna muda wa kula daku lakini kufunga kwa Wakristo hakuna daku, hivyo kuna baadhi ya Waislamu kwao mwezi mtukufu ni kubadili tuu masaa ya chakula cha milo mitatu, badala ya kula breakfast asubuhi lunch mchana na dinner usiku, ni breakfast anakula saa 12:30 jioni, wakati wa kufuturu, lunch anakula saa 5:00 usiku baada ya tarawea na dinner anakula saa 10:00 alfajir hivyo mchana wake ndio unakuwa usiku na usiku ni mchana.

Kufunga Kiislamu ni hadharani watu wote lazima wajue umefunga na ukikaribishwa chakula popote unasema uko kwenye swaumu, kufunga Kikistu ni siri, huruhusiwi kumwambia mtu yoyote kuwa umefunga na ukikaribishwa chakula popote unasema tuu asante, uko ok bila kusema umefunga.

Kufunga Kiislamu mdomo lazima ubaki mkavu usipake mafuta ili uonekane umefunga, uso unatakiwa kuonyesha huzuni or being serious all the time. Kufunga Kikistu unatakiwa kupaka mafuta mdomoni ili watu wasijue, kuwa umefunga, unatakiwa ku smile wakati wote na kuonyesha furaha na sio huzuni au kukunja uso.

Kufunga kwa Kiislamu ukifika muda wa kufururu ni lazima ufungulie na kufuturu na hakuna kufunga siku ya Idi, kufunga kwa Wakristo ni sio lazima kufungulia ukiweza kufunga two days, three days, 7 days, 40 days kama Yesu, unafunga. Unaweza kufunga foods only ukawa unakunywa maji tuu, hii inaitwa water fast, unaweza kufunga vyakula vyote ukawa ùnakunywa fresh juice only, inaitwa juice fast, unaweza kufunga vyakula vya nyama na starch ukawa unakula mboga mboga only, na kwa wale wanaofunga na ku meditate kuna wanaofunga kila kitu na kula hewa tuu, yaani breath, hawa wanaitwa, breathpeteriann wanafunga na kula hewa tuu!. Hawa ni ma master with full body control hakuna kuingiza kitu mwilini na hawatoi kitu mwilini wanakuwa wame stop all bodily metabolism processes hata chooni hawaendi wala perisperision process inakuwa stopped!

Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Radhani Waristo Tunawasindikiza Waislamu, Vipi Wenzetu Kwaresma, mtatusindikiza?

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan baa na clubs hazijai, hata sisi Wakristo kwa kutambua wenzetu Waislamu wamefunga, sisi nasi tunapunguza starehe, baadhi ya bendi za muziki wa dansi zinakuwa likizo hazi perform.

Hata sisi Wakristo walaji wa kitimoto, wakati wa mwezi mtukufu tunapunguza kula mauzo yanashuka.

Hata sisi Wakristo tunatumia zile bidhaa za wale wadada zetu wa ile biashara ya usiku, tunapunguza kununua, hivyo bidhaa zinawadodea, hivyo hata wadada Kikristu hawapeleki bidhaa sokoni!

Je, Kwaresma Ina Hadhi Sawa na Ramadan?
Je wajua kuwa ni mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadan tuu ndio unao fahamika rasmi kiserikali na kitaasisi mbalimbali utasikia viongozi wa kisiasa, kiserikali, taasisi na watu mbalimbali wakifuturisha, huku nyumba za matajiri zikifurika masikini kila Ijumaa ambapo matajiri hao hutoa sadaka kwa masikini, lakini kiukweli Kwaresma ni kama haitambuliki rasmi!, sijawahi kusikia ikizungumzwa popote hivyo Kwaresma ni ipo kama ipo ipo na funga yetu sisi Wakristo kuonekana kama funga zuga!, why funga ya Wakristo haipewi Umuhimu kama funga ya Waislamu?.

Ndugu Zetu Waislamu, Mtatusindikiza?
Vipi ndugu zetu Waislamu, sisi ndugu zenu wa baba mmoja Wakristo leo tumeanza mfungo wa Kwaresma ambapo tunafunga siku 40, vipi mtatusikiziza kama sisi tunavyowasindikizaga?

Nakutakia Kwaresma Njema.

Paskali.
 
Mkuu ndoa huwa inafungwa kipindi cha kwaresima ambacho hakiruhusiwi ni sherehe tu baada ya kutoka kufunga ndoa.
Rejea ndoa ya marehemu Mrema nakumbuka walifunga ndoa kipindi kama hiki hiki cha kwaresima.
Anyway hongera Kwa nondo zako.
 
Hii kwaresma zaidi inawahusu wakatoliki, huko kwingine kama FPCT, TAG na EAGT walikuwa na mifungo yao mwezi mzima kuombea mambo yao na taifa kwa Mungu. Sasa waunganishe na hii kwaresma hizo afya zao zitaharibika kwa njaa. Kwanza kwaresma kwa wapentekoste haipo.
 
Mwislamu hawezi kumsindikiza mkristo kufunga,abadan(kamwe)

Sunagogi ni misikiti ya wayahudi,angalia kamusi ya biblia nyuma.

Nia yangu hapa ni kukupiga msasa kuwa yesu hakua Kristo.

Screenshot_20230222-111721.jpg
 
Kwanza kuna vitu umeandika vya uongo, kama hujui, na ofcourse hujui swaumu ya kiislam usiiongelee mzee acha kuwalisha watu matango pori. Umesema unatakiw et uonekane upo serious huo ni uongo. Na mengine mengi.

Alaf unasema kwaresma kufunga wakristo sio lazima kama ya waislam ambao wao ni lazima kwa muislam balekh, na alaf hata akifunga kwaresma hatakiw mtu yyt kujua. Alaf unadai itambulike? Why? Kama ni siri kwann itambulike?? Ifanyeni isiwe siri ili itambulike.

Ya waislam ni mwez mahsus umewekw kwa ajili ya kufunga ndio maana unatambulika dunia nzima, na bila shaka ww mwenyew ni shahidi wapo ambao sio waislam wanaupa heshima kwa sababu ni mwez ambao upo dhahir je ungefanywa mwezi wa siri ungepewa iyo heshima unayopewa saizi ?

Mtu anatakiw ajue upo ktk ibada ya swaum ambayo huwez kula, ukimficha kutomwambia kama umefunga atakulazimisha ule. Why umfiche umefunga?
Mtu ukimwambia mara moja tu 'mm nmefunga' harudii tena kukukaribosha chakula na anaheshim lkn je umwambie tu asante?

Alaf Uislam na Ukristo ni dini Mbili tofaut, ni Imani tofaut, kwaio kamwe huwezi kulinganisha. Uislam sio dini ya mseto. Unatak mambo ya mseto kafanye ktk vyama vya siasa, au unganeni wakristo na wahindu na wengin ila ktk ibada za kiislam hakuna mambo ya mseto. Tunashirikiana ktk mambo mengin ya kijamii kisiasa kitamafun, mila desturi, ujirani, lkn kamwe sio katika ibada. Nyinyi mna dini yenu, na sisi tuna dini yetu.
 
Mkristo anafunga saa 12 jion/saa 1 usiku mpaka kesho saa 12/saa 1 usiku ndiyo anakula hapo hajanywa maji.
Muislamu anaacha kula kuanzia saa 10 usiku mpaka saa 1 usiku. Kuanzia saa 1 usiku mpk saa 10 anakula tu.
Ratiba ya kula mchana yeye anakula saa 9 usiku au saa 10. Ila mkristo akila saa 1 usiku mpk kesho hakuna kunywa maji wala kula kitu chochote.

Muislamu huwa hafungi ila anabadilisha ratiba ya kula.
 
Mkristo anafunga saa 12 jion/saa 1 usiku mpaka kesho saa 12/saa 1 usiku ndiyo anakula hapo hajanywa maji.
Muislamu anaacha kula kuanzia saa 10 usiku mpaka saa 1 usiku. Kuanzia saa 1 usiku mpk saa 10 anakula tu.
Ratiba ya kula mchana yeye anakula saa 9 usiku au saa 10. Ila mkristo akila saa 1 usiku mpk kesho hakuna kunywa maji wala kula kitu chochote.
Muislamu huwa hafungi ila anabadilisha ratiba ya kula
Na hata hamfungi hivo hayo ni maneno tu ya kujimwambafai, mkristo gan afunge hivo (kwanza nyiny si mnatakiw mfunge siku 40 bila kula wala kunywa, wewe unaweza?) Mwenzako nchi jiran juz kati aliaga dunia. Na mkrsto akijitahd sana atafunga siku 2 au 3 na hivo akibanwa sana na kiu anakunywa maji na njaa ikimbana sana anakula kidoooogo (iyo ndo funga gani?), au utaskia mtu anasema anafunga aina flan t ya chakula, hiyo pia sio funga vile vile.

hilo moja, pili, kama waislam hawafungi wanabadilisha ratiba ya kula (kama vile kwako ni kitu simple) basi na ww jaribu sio mwez mzima, Laa, jaribu wiki 1 tu, ukae kuanzia saa 10 alfajir usile kitu uend na mishe zako kama kawaida uje ule saa 1 jion jarb hata kawiki kamoja tu siku 7.

Tatu, Uislam ni dini iliyokamilika, kama ambavyo na ww utasema ukristo ni dini iliyokamilika, uislam una mafundisho yake, na pia ukristo una mafundisho yake, (ambayo kiasilimia bas wakristo weng hawayafati, kwasbb haya make sense, mfano mzuri ni huo wa kufunga 40 days bila kula chcht wala kunyw chcht, ww mwnyw ni shahid wa nafs yako wakriat wangap unaowafaham wewe wanafunga hata robo tu ya izo siku 40 ambazo ni 10 days, wangapi?

Kwaio uislam umetoa mafunzo yake jins gan wafuasi wake wafunge, na ukiristo pia umetoa mafundisho yake jinsi vp watu wake wafunge.

Kwavile ni dini 2 tofaut hatutegemei mafundisho ya hiz dini mbili yatafanana kwa namna yyt.

Sasa ukisema waislam hawafungi unakosea, wao wanafunga kwa mujib wa mafundisho yao. Wewe unatak wafunge kwa mujib wa mafundisho yenu kitu ambach nyie wenyew mnashindwa haiwezekani hiyo mzee.

Wapo sahihi kwa mujib wa mafundish ya Kiislam.

Na ww funga vyvyt vile ulivofundishw kwa mujib wa mafundisho yenu.

Maelezo ni mengi ila nahis umenielewa na kamwe hutarudia kusema waislam hawafungi wanabadilish mda wa kula.

Lkn pia sitoshangaa hata ukirudia maana binadam ubishi ni maumbile yetu.

Karibu.
 
Na hata hamfungi hivo hayo ni maneno tu ya kujimwambafai, mkristo gan afunge hivo (kwanza nyiny si mnatakiw mfunge siku 40 bila kula wala kunywa, wewe unaweza?) Mwenzako nchi jiran juz kati aliaga dunia. Na mkrsto akijitahd sana atafunga siku 2 au 3 na hivo akibanwa sana na kiu anakunywa maji na njaa ikimbana sana anakula kidoooogo (iyo ndo funga gani ???), au utaskia mtu anasema anafunga aina flan t ya chakula, hiyo pia sio funga vile vile.

hilo moja, pili, kama waislam hawafungi wanabadilisha ratiba ya kula (kama vile kwako ni kitu simple) basi na ww jaribu sio mwez mzima, Laa, jaribu wiki 1 tu, ukae kuanzia saa 10 alfajir usile kitu uend na mishe zako kama kawaida uje ule saa 1 jion jarb hata kawiki kamoja tu siku 7.

Tatu, Uislam ni dini iliyokamilika, kama ambavyo na ww utasema ukristo ni dini iliyokamilika, uislam una mafundisho yake, na pia ukristo una mafundisho yake, (ambayo kiasilimia bas wakristo weng hawayafati, kwasbb haya make sense, mfano mzuri ni huo wa kufunga 40 days bila kula chcht wala kunyw chcht, ww mwnyw ni shahid wa nafs yako wakriat wangap unaowafaham wewe wanafunga hata robo tu ya izo siku 40 ambazo ni 10 days, wangapi ????

Kwaio uislam umetoa mafunzo yake jins gan wafuasi wake wafunge, na ukiristo pia umetoa mafundisho yake jinsi vp watu wake wafunge.

Kwavile ni dini 2 tofaut hatutegemei mafundisho ya hiz dini mbili yatafanana kwa namna yyt.

Sasa ukisema waislam hawafungi unakosea, wao wanafunga kwa mujib wa mafundisho yao. Wewe unatak wafunge kwa mujib wa mafundisho yenu kitu ambach nyie wenyew mnashindwa haiwezekani hiyo mzee.

Wapo sahihi kwa mujib wa mafundish ya kiislam

Na ww funga vyvyt vile ulivofundishw kwa mujib wa mafundisho yenu.

Maelezo ni mengi ila nahis umenielewa na kamwe hutarudia kusema waislam hawafungi wanabadilish mda wa kula.

Lkn pia sitoshangaa hata ukirudia maana binadam ubishi ni maumbile yetu.

Karibu.
Yesu ni mwana wa Mungu aliweza kufunga siku 40 bila kula, aliweza kufa na kufufuka. Wewe mwenye damu na nyama huwezi.
Ukila saa 12 jioni mpaka kesho saa 12 hautakiwi kula chochote bila maji. Na wala huwezi kumjua mkristo amefunga. Ndiyo maana unasema tunajimwambafy.

Mathayo 6:16-18
Neno: Bibilia Takatifu
Mafundisho Kuhusu Kufunga
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.
17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu
18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni
 
Yesu ni mwana wa Mungu aliweza kufunga siku 40 bila kula, aliweza kufa na kufufuka. Wewe mwenye damu na nyama huwezi.
Ukila saa 12 jioni mpaka kesho saa 12 hautakiwi kula chochote bila maji. Na wala huwezi kumjua mkristo amefunga. Ndiyo maana unasema tunajimwambafy.

Mathayo 6:16-18
Neno: Bibilia Takatifu
Mafundisho Kuhusu Kufunga
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.
17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu
18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni
Sasa hayo ni mafundisho yenu mzee ya kanisani kwenu au ya dini yenu.

Sasa mbona unataka na waislam wafunge kwa kufuata sheria zenu ?? Au waislam ni wakirisito wenzenu ? Au mna shea biblia ?

Kua na akili basi we lijamaa.

Nyie fungeni mnavofunga, waacheni waislam wafunge wanavofunga unataka wafuate biblia yako ausio.

Alaf mnajidai waislam wanataka kila mtu awe kama wao ila nyinyi mnajisahau.
Acheni kujifanya wajuaji sana wazew.
 
Sasa hayo ni mafundisho yenu mzee ya kanisani kwenu au ya dini yenu.

Sasa mbona unataka na waislam wafunge kwa kufuata sheria zenu ?? Au waislam ni wakirisito wenzenu ? Au mna shea biblia ?

Kua na akili basi we lijamaa.

Nyie fungeni mnavofunga, waacheni waislam wafunge wanavofunga unataka wafuate biblia yako ausio.

Alaf mnajidai waislam wanataka kila mtu awe kama wao ila nyinyi mnajisahau.
Acheni kujifanya wajuaji sana wazew.
Kila mtu anapaswa kufuata Biblia.Hiyo ni amri.
 
Mkristo anafunga saa 12 jion/saa 1 usiku mpaka kesho saa 12/saa 1 usiku ndiyo anakula hapo hajanywa maji.
Muislamu anaacha kula kuanzia saa 10 usiku mpaka saa 1 usiku. Kuanzia saa 1 usiku mpk saa 10 anakula tu.
Ratiba ya kula mchana yeye anakula saa 9 usiku au saa 10. Ila mkristo akila saa 1 usiku mpk kesho hakuna kunywa maji wala kula kitu chochote.
Muislamu huwa hafungi ila anabadilisha ratiba ya kula
Kweli kuwa uyaone! yaani wewe unaefunga kwa kujichagulia tu unajifananisha na ufungaji wa muislamu ambae ana utaratibu kamili wa kufunga!

Mungekaa kimya ingekuwa bora kwenu!
 
Hivi mkuu na wewe pia una mtazamo finyu wa kidini? coz mengi uliyo andika hapo ni uongo na biasness ya imani yako!

Pili nikurahisishie tu, imani ya dini imefungamana na kweli na uongo kulingana na hiyo imani yenyewe. Kweli ya Uislamu ni uongo kwa Ukristo, vice versa is true. With all due respect, Waislamu hatuwezi kujumuika na nyinyi katika maswala yenu kwa kuwa yanakinzana na imani yetu. The same should have been with u guys kama kweli mngekuwa na imani na utaratibu kamili katika dini yenu.
 
Back
Top Bottom