Nini hatima ya Ofisi ya Spika iliyojengwa Urambo?

Hizi siasa ngumu sana kuzielewa ndugu yangu. Mi nilienda Urambo mwaka 2010 nikaikuta hiyo ofisi cha kushangaza hakuna activity zozote zinazoashiria kuwa hiyo ofisi iko active.
Ilikua ni bad expenditures kwa government kujenga hiyo ofisi. Maswali yako ni ya msingi sana kwa upande wa pili wa shilingi. Wasiwasi wangu ni kwamba haya maswali hata yakipelekwa bungeni hakuna majibu ya msingi yatakayotolewa. Tugange yajayo
kweli mkuu
 
Kipindi cha Uspika wake ndugu Samwel John Sitta alijenga Ofisi ya Spika Jimboni Mwake Urambo ( Sijui huyu alikuwa anawaza nini)

1. Je Haukuwa Ubadhirifu wa Mali ya Uma ukizingatia sasa hivi ile ofisi haitumiki?

2. Je itakuwa ni Busara kwamba Bunge liweke kigezo cha Kuwa Mbunge wa Urambo kama kimojawapo cha mtu Kugombea nafasi ya Spika ili ile ofisi iwe inatumika?

3. Nini Hatima ya ile ofisi je itumike kama Kituo cha afya?

Wapambe wa Sitta akina Malaria Sugu, FaizaFoxy, rizt, Rejao pamoja na kutambua kwamba Mgao wa Vocha Umepungua naamini mtapata nafasi ya kuja kutoa Mawazo yenu pia.
Naambiwa ni ofisi ya MBUNGE
 
Rais Jakaya Kikwete atembelea Urambo na Ofisi Mpya ya Mbunge na Spika wa Bunge Samwel Sitta iliyogharimu Millioni 170





IMG_8568.JPG
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Aliyesimamam ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta.

IMG_8564.JPG
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta (Kushoto) ambaye pia ni Spika wa Bunge. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

IMG_8583.JPG
Rais Jakaya Kikwete akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

IMG_8456.JPG
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge akiwakaribisha waheshimiwa wabunge mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege Urambo kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Kushoto ni Mbunge wa Mafia Mhe. Abdukarim Shah.
Duuh Kikwete nae sijui alikua anafikiria nini kwenda kuzindua hii ofisi? looh!!
 
Nachoka kuwaza matumizi na tija ya kuwepo kwa hiyo ofisi kule Urambo. Hivi alioidhinisha ule ujenzi alikua na akili ya kufikiri vya kutosha kweli?

Iundwe sheria itakayotumika pindi mtu au watu wanapofanya makosa pindi wawapo na madaraka ya kutoa maamuzi ya jambo flani likija kugundulika lilifanywa kinyume cha sheria au kifisadi au kwa interest flani basi wahusika wachukuliwe hatua.
 
zimekuwa ofisi za ma VEO, WEO na ofisi za CCM hata Tanesco na maji, Ofisa kilimo, mifugo wapo hapo. in
 
Kuna mmoja anajenga uwanja wa ndege wa kimataifa huko kijijini kwao hana tofauti na huyu.
 
Spika wa kudumu!
Akili za African leaders!

Hajui kesho hayupo,hata airport anaweza weka kijijini kwake
 
Back
Top Bottom