Nini hatima ya Ofisi ya Spika iliyojengwa Urambo?

Fanyeni utaratibu ihamishiwe makao makuu dodoma itapunguza gharama za majengo mapya ya sirikali. Na shauri muongee na rafiki zenu wa china labda wamegundua teknologia ya kuhamisha mjengo uliokamilika. Nchi hii bwana ina mambo ya ajabu ajabu, eti ofisi ndogo ya spika.
.
Na washawasha!
 
Tunajadili hili kwa sababu mzee wetu sita katutoka ila kama tutakuwa na uwanja wa ndege mkubwa na hakuna ndege ya kutua tutageuza kuwa kitu gani?
Uwanja wa mpira hapa Tanzania hakuna jambo gumu
 
Mkuu uko Nchi gani wewe? Mzee Sitta alijenga Ofisi ya Spika Jimboni mwake mpaka leo sijui huyu Mzee alikuwa anafikiri nini, lakini ndivyo Viongozi wa Afrika walivyo maana hata Gaddaffi alijenda Makao makuu ya AU kjiji kwao Siirte
kweli kabisa......mambo ya Gbadolite
 
View attachment 433171 View attachment 433169 Huyu mhe (rip) alijenga ofisi ya spika jimboni kwake urambo,inatumika kwa shughuli gani?

napendekeza ifanywe dispensary au itafutiwe matumizi mengine ya umma
Nini kilimfanya aijenge kwao? aliamini atakuwa speaker milele?
na kama alijua hata kuwa speaker milele alikuwa anasisitiza kila atakaechaguliwa kuwa speaker ajenge ofisi za speaker wa bunge kwao.
Alikuwa na matumizi mabaya ya fedha za umma,
 
Engine na Rejeta la Gari lako na Gauge Temperature ya Gari lako vikiwa juu, ina maana Gari lako lina Over Heat. Sasa jawabu na Solution yake ya haraka ni KUPOOZA ENGINE.


Kipindi cha Uspika wake ndugu Samwel John Sitta alijenga Ofisi ya Spika Jimboni Mwake Urambo ( Sijui huyu alikuwa anawaza nini)

1. Je Haukuwa Ubadhirifu wa Mali ya Uma ukizingatia sasa hivi ile ofisi haitumiki?

2. Je itakuwa ni Busara kwamba Bunge liweke kigezo cha Kuwa Mbunge wa Urambo kama kimojawapo cha mtu Kugombea nafasi ya Spika ili ile ofisi iwe inatumika?

3. Nini Hatima ya ile ofisi je itumike kama Kituo cha afya?

Wapambe wa Sitta akina Malaria Sugu, FaizaFoxy, rizt, Rejao pamoja na kutambua kwamba Mgao wa Vocha Umepungua naamini mtapata nafasi ya kuja kutoa Mawazo yenu pia.
 
Mwishoni mwa uspika wa Samwel Sitta, serikali ilijenga ofisi ya spika wa bunge Urambo Tabora ambako ni jimboni kwa spika wa wakati huo mheshimiwa Samweli Sitta. Maswali yangu ni haya:

1. Samweli Sitaa siyo spika tena. Je anaitumia ofisi hiyo au hapana? Na kama ndio anaitumia kama nani na kwa shughuli z
zipi?
2. Spika wa sasa Anna Makinda ameshaitumia ofisi hiyo mara ngapi? Na kama haitumii ni kwanini?!
3. Je utaratibu wa kujenga ofisi kwenye kila jimbo analotoka spika utaendelea?
4. Je ilikusudiwa Sitta awe spika wa kudumu mpaka kufa kwake?
5. Kama ofisi hiyo haitumiki na spika aliyepita na aliyepo ni ya nini? Inafaa kuendelea kuwepo? kwanini isigeuzwe darasa
shule au ghala la kuhifadhia asali?
maswali magumu
 
Ni ajabu na aibu urambo ni choka mbaya sasa sijui wananchi wananufaika vipi na ofisi hii labda waigeuze makumbusho ya spika inaweza kuingiza pesa kupitia utalii
 
Back
Top Bottom