Nimkubalie?

Nimkubalie?

Mume wa mtu ni sumu dada yangu, tulia na umlee mwanao vizuri na umfunze tabia njema.

Kwanza huyo mtoto wako ni jinsia gani?????

Kama ni wa kike asije kurithi tabia ya kupenda waume wa watu kwa sababu ni hatari sana.

Vumilia na kumbuka subira yavuta heri, hivyo mwenyezimungu atakuwa ameshakuandalia mume mwema it's just a matter of time.
 
Anti ni wewe na roho yako tu. Pima ushauri uliyopewa kisha amua cha kufanya kwa mujibu wa dhamira yako na kamwe usije jutia kwa uamuzi wako kwani maisha ni safari. Isipokuwa ni vema ukatambua kuwa, kwa mujibu wa maelezo yako, yaonesha kuwa unapenda maisha ya ndoto. Na ni ndoto hizo ndizo zilizovunja ndoa yako ya awali kwani hazikukupa nafasi ya kumsamehe mumeo kwa kosa la kuzaa nje ya ndoa. Nasema ndoto kwa sababu, huenda wakati unakata shauri ya kuolewa na huyo mumeo, ulidhani kuwa ni malaika na kamwe hawezi kukosea kwenda nje ya ndoa. Pia ulisahau kuwa, mumeo hakuwa wa kwanza kutenda kosa kama hilo kwani hata vitabu vya dini vinasimulia matukio kama ya watu watakatifu kuzaa na wajakazi wao. Mpira sasa uko mikononi.
 
Dada huyo MH. ni TAPELI,
1. Njia alizotumia ni mbinu kali sana za kuhakikisha anakupata. Kukualika lunch ni mbinu nzuri ya watu wa aina hiyo kukupata vizuri tabia yako, naungana na mchangiaji mmoja aliyesema angependa kujua umri wako ili akupe mawazo yake kulingana na umri. Hujakosea kuomba msaada.
2. Mkewe kuwa "BUSY" ni mwanya mbaya ambao amekuachia wewe uujaze lakini huku akijua ni mtego mbaya kwako, je siku akiwa hayuko "BUSY" nafasi yako ni nini"
3. Inawezekana Mkewe yuko "BUSY" kuepukana na matatizo aliyonayo huyo Mh.

Nakushauri kwa kuwa ulishaonja joto la jiwe ukaweza kufikia hapo ulipo hadi sasa HUYO MH ACHANA NAYE!!!!!!

Bi Senti 50

Mtu azininiye na Mwanamke hana akili kabisa,tena afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake

Do not exploit your nature.Achana na wanataka kuwatumia watu kama viburudisho vyao.WAIT YOU WILL GET YOUR SIZE
 
Ushauri wangu mimi kama mmependana mwambie ahalalishe na akuoe. Si lazima amuache mkewe kufanya hilo.
 
natoa shukrani kwa michango yenu yote na ningejaribu kumjibu mmoja mmoja lakini kama mnavyojua ttcl yetu hii na mitandao ya kudandia.

Naomba niseme tatizo si fedha zake kwani na mimi nina za kwangu na nina uwezo wa kuishi vizuri tu. Mwanzoni nilifikiri ni mtu wa urafiki tu lakini aliponipa hizo za kunidondokea ndio nimepata na utata. Hivi nikiamua kuanza kumchunia si atanielewa vibaya na anaweza kuanza kudai "yote aliyonifanyia" mimi na mwanangu?

Au niamue kumlipa "kiaina" yaishe huku nikijua siwezi kuwa naye? Lakini pia maisha ya kuishi single muda mrefu nayo si mazuri kwani Mungu alituumba wawili wawili.

Nimeuliza hapa si mimi tu kuna mabinti wengine ambao wao hawana hata watoto lakini wanajikuta na utata huu wa kutembea na waume za watu hasa hawa waheshimiwa wetu. Au na sisi tuingie kwenye haya ya kuwakamua tu na kuwachuna?

nadhani nitafikia uamuzi na asanteni sana. Bimkubwa, nashukuru kwa ushauri wako. Umenisaidia sana.

Asanteni.
 
nadhani nitafikia uamuzi na asanteni sana. Bimkubwa, nashukuru kwa ushauri wako. Umenisaidia sana.

Asanteni.

You are most welcome my dear. Huwezi jua kwa kutulia kwako na kutokuwa mapepe kuna mtu ambaye hajaoa na atapendezwa na tabia yako.
Maamuzi ni yako lakini kumbuka pia "usiache mbachao kwa msala upitao". Huo uheshimiwa ni wa muda tu. Uliza heartache wanazopitia nyumba ndogo za watu............ hakuna mwenye hadithi yenye furaha na kama ipo basi ukweli bado haujajitenga, ukijitenga ndio pale uongo unajifichua....

Hiyo ofisi unayofanyia kazi nimeisikia kwa muda mrefu kidogo maana kuna Dada ambaye ninamfahamu toka mbali sana na enzi, yupo katika hiyo ofisi au pengine ofisi nyingine inayohusiana na hayo mambo ya waheshimiwa. Ninajua hajazaa ila anatembea na mheshimiwa mmoja hadi kujengewa nyumba. Na nisikudanganye hata kidogo, huyo dada hata afanyaje hawezi kupata mume wa kumfaa atabaki kuwa nyumba ndogo ya huyu mheshimiwa maana watu wanamjua and there is no secret under the skies. Usitake kufanana na mtu kama huyo. Ninachoelewa ofisi anayofanyia kazi huko inajulikana kama "centre ya nyumba ndogo za waheshimiwa".You are priceless my dear and you deserve the best!

we are judged by our society my dear na ni society hii hii inayotupa kula yetu. Usipotezee hadhi yako kwa kuwa unataka kufanana na hao mabinti wengine kwenye hiyo ofisi yako.
Mwambie huyo mheshimiwa frankly tena usimdanganye kwa kupepesa macho, mweleze ukweli unavyouona. He will respect you hawezi kukudai hata centi moja aliyokupa ila kama alikuwa mtu wa ovyo utamuona uhuni wake.

sometimes being different is not bad at all, it saves lives and it might save yours. Kumbuka pia kuna UKIMWI.
 
Ushauri wangu mimi kama mmependana mwambie ahalalishe na akuoe. Si lazima amuache mkewe kufanya hilo.

Kupendana huko unakosemea ni kupendana kweli au ni tamaa kwa kuwa mkewe hayupo? Je unajua kuwa kuna wake wa hao waheshimiwa walishaaibishwa na tabia za waume zao huko bungeni kiasi kwamba wanaona ni heri wakae nyumbani kuliko kwenda kuadhirika zaidi kwa tabia za waume zao?

Usimdanganye binti wa watu hakuna penzi linalogawanyika, penzi humtokea mtu mara 2 tu ktk uhai wa mtu. Na hii hutokea sequentially baada ya penzi la kwanza kufa lingine huanza muda mrefu baadaye. Yote wanayofanya watu ni kushibisha matamanio yao.

Usimdumbukize kwenye matatizo zaidi wapo waheshimiwa wengi tu ambao nyumbani kwa kunawaka moto kutokana na tabia hizi. Usimuingize kwenye matatizo yakaja yakahamia kwake akaonekana ndio sababisho ya matatizo yote kwenye ndoa ya mheshimiwa.
 
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.

Pole na tatizo/mtihani/majaribu yaliyokukumba. Kwa bahati mbaya, naona majibu mengi uliyopewa yamekaa kiutani utani. Sijui km nawe uko serious kiasi gani!

Tunaambiwa kuwa ulimi ni mjumbe wa moyo. Ulimi hutoa kauli; kauli ni maneno. K/hiyo maneno hudhihirisha kilichofichwa na moyo.

Nilichojifunza kutokana na maneno yako mwenyewe ni haya:

"Uliwatolea wengi nje" k/sbb hao hawakuwa na vigezo ulivyovitaka wewe. On the contrary, huyu "mheshimiwa" anavyo vigezo hivyo. Hebu angalia lugha yako:

Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu.

Kwanini sababu hizo hukuziona na kwa "mheshimiwa" pia? Unajuaje kuwa naye anataka hicho hicho wanachotaka wengine? Unasema:

kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Maisha hayana definition moja. Nawe ukifikwa na sababu za kutoweza kumridhisha, atafanya nini tena? Je, alitakalo yeye si lile lile ulilodai kuwatolea nje wengine? Je, ukimkubalia, huo ndio utakuwa mwisho wa hayo majaribu? Mfano ameshakuoa, na wewe ni mjamzito – huwezi kusafiri – nani atampoza na majaribu huko njiani?

Unamuangalia sana mtu kwa nje kuliko unavyomuangalia kwa ndani, na labda hili ndilo lililokufanya usidumu na mzazi mwenzako. Kumuangalia mtu kwa nje ni kuangalia, kwa mfano, mali zake, cheo chake, umashuhuri wake, and the like.

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke?

Kwanini hukumwambia hivi: "Siwezi kuwa nawe k/sbb unae mke" badala ya kumuuliza ulivyomuuliza? Kujiamini ndiko kunakupa msimamo, dada!

Jinsi ulivyojizuia kubaki pweke, ndivyo jinsi unavyozizuia hizo "signals" – i.e., jinsi ulivyoshindwa kujizuia, ndivyo utakavyoshindwa kuzizuia "signals". Unajitutumua bila kufikia uamuzi hasa wa kufanya hivyo. Labda k/sbb umekosa will, know-what, and know-how, ambavyo vinakufanya ukose kujiamini na kutoa uamuzi makini. Angalia hatima ya kujitutumua kwako:

Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana.

… amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia

Kuendelea kwako kuwa single parent ni jitihada zako za kujitutumua tu (labda kutaka kumuonesha mzazi mwenzako kuwa unaliweza hili), lkn unaonekana hulimudu hilo. Sister, hili suala la cold competition lipo kwa kiasi kikubwa kwa wanandoa wenye mfarakano, na nadhani ukijiweka huru utagundua kuwa nawe limekuathiri. Ni hivi: unaonekana bado unampenda mzazi mwenzako (ndio maana ukaamua kubaki "single" kwa muda wote huo), ila kuna aina fulani ya kujitoa kwako kimasomaso kumuonesha kuwa huna habari naye. Sasa umeshindwa kulivumilia hilo, ndio maana unajikuta uko njia panda.

Ulizipokea "signals" kutoka kwa "mheshimiwa" tangu awali ya kisa hiki,

… amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia

… nawe ulizihisi hizo "signals" lkn ulikuwa ukiidanganya tu nafsi yako kuwa sizo wkt internally ulijua kuwa ndizo ila kwa hulka ya wanawake, ulikuwa ukisubiri tu muda wa ulimi wa "mheshimiwa" kudhihirisha contents za moyo wake.

K/hiyo, unaonekana kuwa jibu unalo, dada, lkn tu hujiamini, na umelileta suala hili k/sbb ya kutafuta tu kuungwa mkono kwa namna fulani. Hebu angalia "ati ati" zako:

kasema ati mke wake yuko busy sana … amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.

… na kumbe uliliona kuwa hili ni tatizo:

Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke

… mbona bado unaendelea kutafuta ushauri?

Na hili nalo la kuliona suala lako ni muhimu lkn …

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi.

USHAURI WANGU:

· Usikurupuke kutoa jibu. Jipe muda kumchunguza na kujichunguza wewe mwenyewe km kweli ulitakalo ndilo hilo. Ukimpa jibu la haraka huenda hiyo the so-called "ndoa" ikachukua indefinite time, na hivyo kuhalalisha uhawara – hapo utakuwa umelamba "Joker".
· Suala la ukewenza linaendana na imani ya mtu. Kabla ya ushauri mwingine, hivi wewe dada ni dini gani?
· Usiangalie mambo ya nje ya mtu, km mali, cheo, umaarafu, … k/sbb hivyo huenda vikaondoka, na ukabaki unajuta. Angalia mambo ya ndani ya mtu, km uaminifu, kujali, upendo wa kweli (unconditional love), ushirikiano, uvumilivu, … kadri Alivyokujaalia Mungu. Kipimo cha kwanza ni kumwambia kuwa huwezi kutoa jibu la haraka k/sbb hukuwa na mpango wa kuolewa. Hapo utaona uvumilivu na upendo wake kwa kiasi fulani.
· Ichunguze ndoa yake.

Mengine baadae, km nitapata muda, au wengine wataendeleza.
 
Kama huna matatizo ya kuwa mke wa pili, basi mwambie kwamba kama ana nia ya kukuoa uko tayari kumpa uroda lakini usimpe kila anapotaka lazima akuoe kwanza ndio apate uroda kila anapoutaka. Vinginevyo mwambie akatafute uroda kwingine...🙂
 
BTW hata heading ya post yako inaonyesha wazi ushafanya uamuzi!!! duh?
 
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.

Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.

Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.

Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.

Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.

asanteni and I'm out.

Mmmh dadangu,sijui mwenzangu uko ktk dini gani,ila maneno ya Mungu yanatufundisha,"ndoa na iheshimiwe na watu wote".Najua huyo asiyeheshimiwa(maana ameshindwa kuhehimu mke wake mwenyewe na ndoa yake mwenyewe)anajaribu kukuvuta kwa ahadi mbovu za hutapata shida wwe na mtoto wako,ila dada usikubali.

Hehimu ndoa at leat for the sake of your fellow woman.DO NOT BECOME A HOME BREAKER!

Wewe menyewe umesema ndoa yako ilikufa kwa sbb ya mambo km haya haya.Je na watoto wa mwenzio waje baki na brocken family sbb yako?You are a mother,so I hope you understand what I mean.Be brave and show a motherly heart!

Kaa na huyo asiyeheshimiwa,tell him on his face kwamba he should respect his own marriage!Utakua umemsaidia na atakuheshimu kwa hilo
 
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.

Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.

Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.

Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.

Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.

asanteni and I'm out.

Mmmh dadangu,sijui mwenzangu uko ktk dini gani,ila maneno ya Mungu yanatufundisha,"ndoa na iheshimiwe na watu wote".Najua huyo asiyeheshimiwa(maana ameshindwa kuheshimu mke wake mwenyewe na ndoa yake mwenyewe)anajaribu kukuvuta kwa ahadi mbovu za hutapata shida wwe na mtoto wako,ila dada usikubali.

Heshimu ndoa at leat for the sake of your fellow woman.DO NOT BECOME A HOME BREAKER!

Wewe menyewe umesema ndoa yako ilikufa kwa sbb ya mambo km haya haya.Je na watoto wa mwenzio waje baki na brocken family sbb yako?You are a mother,so I hope you understand what I mean.Be brave and show a motherly heart!

Kaa na huyo asiyeheshimiwa,tell him on his face kwamba he should respect his own marriage!Utakua umemsaidia na atakuheshimu kwa hilo
 
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.

Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.

Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.

Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.

Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.

asanteni and I'm out.

Kwa ushauri wangu, bado mumeo wa ndoa ambaye unasema amezaa nje ya ndoa yenu anakupenda. Wewe ndiye mkewe, msamehe mumeo, mlee watoto wenu.
Ukimkubalia huyu kigogo sijui kama utakuwa umefanya jambo la busara, sanasana utakuwa UMEKWEPA MAJIVU UKAKANYAGA MOTO.
 
Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.

...Between these quotes...

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.

...unapata majibu lukuki pamoja na methali kibao mfano;

Mtenda akitendewa,hujihisi kaonewa (imagine ulivyojiskia ex husband wako alivyofanya, na mke wa huyo kibosile atavyojiskia).

kosa si kosa, ila kosa kurudia kosa (kama alofanya ex husband wako mpaka akazaa nje, na kuvunjika ndoa yenu).

Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu ('unataka' hatarisha ndoa ya mw'mwenzio sasa baada ya machungu ya ilokuwa ndoa'ko kuisha si ndio eeh?).

...Yaonekana wewe ni mwanamke msomi/mwenye wadhifa wako mzuri tu, "pick up lines" kama hizi alizotumia huyu mheshimiwa zinatia kinyaa kwa mtu wa umri wako kumkubalia, maneno kama hayo 'hudanganyiwa' wanafunzi na ma house maids.

kumkubalia au kumkatalia maamuzi ni yako, muhimu ukumbuke ukimkubalia Consequenses zake mama mnh, pima mwenyewe.

Kumbuka; the light at the tunnel end may be the headlamp of oncoming train!!!!
 
Bibi 50 centi, sijui nikuite DADA YANGU au MDOGO WANGU maana umri wako siufahamu!! Mimi ni mwanamke mwenzako NILIYEOLEWA na tena mwenye watoto WATATU na mzoefu wa miaka mingi katika ndoa. Naamini nakuzidi umri, na hivyo tafadhali MDOGO WANGU huyo bwana na viofa ofa vyake mwambie kwa uwazi na macho makavu kuwa "ulichopendekeza, samahani siwezi". Mkatae aende zake akalee watoto wake na huyo mke wake aliye BUSSY, tafadhali kabisa mwanamke mwenzangu huyo mwanamme asikufanye wewe kibanda cha kituo cha DALADALA cha mtu kupumzika akisubiri gari, yaani wewe uwe safety valve yake wakati mkewe akiwa bussy. Natamani ningemfahamu huyo bwana nimpashe maneno yake. Ukihitaji [/U]ushauri zaidi tuma PM kwangu na nitakuwa nawe sambaba kukupa ushauri wa kusambaratisha mitego ya huyo bwana.
 
Wakina mama moto moto moto humu...Jamani upweke mgumu huyu Bi 50 cent ukiona kafikia hatua ya kuomba ushauri ni ujue kashavumilia vya kutosha...na kwa uelewa wangu mdogo huwa mara kwa mara mtu ambaye anaomba ushari kwa mtizamo huu huwa anao uamuzi tayari...

Kukaa bila bwana ni shida jamani...walioko kazini mbali na waume zao ni issue sembuse huyu ambaye hana kabisa....

Anyway dada thats is ur call unaweza kwenda kupima nae..mkapata majibu ndio mkaanza mapenzi lakini dont put him kwenye moyo sana kwani kukuacha inaweza kuwa ni kitu rahisi sana kwake..ingawa najua kwa wadada ni ngumu sana kufanya mapenzi bila kuwa na upenda kwa mwenzie.

Ila sasa utafanyaje hawa wanao kushauri wako kwenye mahusiano ya thabiti...wewe hauko na ni muhitaji wa kuwa humo...as long usizae nae tu ndio la muhimu sana we lea huyo uliye nae..kwa sasa.

Utasubili milele what if asipotokea wa kufa na kuzikana?

Usije sema sijakwambia mchana mwema its ur call.

Buswelu.[/COLOR]
 
Hakuna dili hapa, wewe mwenyewe unajua mbichi na mbivu harafu unauliza nile ndizi zipi. We kama mzinifu endelea badala ya kusumbua watu hapa JF. We mpaka umeweka mazingira ya ukaribu na huyo mheshimiwa ulitegemea nini???

Umeachana na mme wako kwa sababu eti kazaa nje ya ndoa yenu, na je wewe unataka kufanya nini sasa ukijua kuwa pia huyo mheshimiwa yupo kwenye ndoa??? Nyie ndiyo wale wale sizitaki mbichi hizi huku unazipenda.

Achana na umalaya badala yake mrudie mmeo, umsamehe na muendelee na maisha badala ya kuanza kuingilia ndoa za wenzako.

Ahsante kwa kunielewa.
 
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.

Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.

Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.

Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.

Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.

asanteni and I'm out.

Hivi wewe Dada, umeshawahi kujiuliza kuwa ni kwa nini Mumeo alizaa nje ya Ndoa yenu?
Wewe ndiye una matatizo, Mrudie Mumeo mara moja; Kama hutaki Endelea na huyo mwenye mke na watoto wake utapata zawadi ya HIV/UKIMWI ambayo itakupeleka kuzimu mapema na kumuacha mtoto wako akiwa yatima asiye na mama mzazi.
Lakini usijali wewe kufa tu, mtoto atalelewa na babae.
 
Back
Top Bottom