Bi. Senti 50
JF-Expert Member
- Apr 17, 2007
- 287
- 12
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.
Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.
Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.
Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.
Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.
Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k
Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.
asanteni and I'm out.