Nimkubalie?

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,667
2,000
natoa shukrani kwa michango yenu yote na ningejaribu kumjibu mmoja mmoja lakini kama mnavyojua ttcl yetu hii na mitandao ya kudandia.

Naomba niseme tatizo si fedha zake kwani na mimi nina za kwangu na nina uwezo wa kuishi vizuri tu. Mwanzoni nilifikiri ni mtu wa urafiki tu lakini aliponipa hizo za kunidondokea ndio nimepata na utata. Hivi nikiamua kuanza kumchunia si atanielewa vibaya na anaweza kuanza kudai "yote aliyonifanyia" mimi na mwanangu?

Au niamue kumlipa "kiaina" yaishe huku nikijua siwezi kuwa naye? Lakini pia maisha ya kuishi single muda mrefu nayo si mazuri kwani Mungu alituumba wawili wawili.

Nimeuliza hapa si mimi tu kuna mabinti wengine ambao wao hawana hata watoto lakini wanajikuta na utata huu wa kutembea na waume za watu hasa hawa waheshimiwa wetu. Au na sisi tuingie kwenye haya ya kuwakamua tu na kuwachuna?

nadhani nitafikia uamuzi na asanteni sana. Bimkubwa, nashukuru kwa ushauri wako. Umenisaidia sana.

Asanteni.

Kama walivyosema wengi jibu unalijua. Wewe ulishafanyiwa na unajua chungu yake sasa kwa nini unataka kujiingiza huko? Hauna haja ya kumchunia wala kumchukia maana yeye kama mwanaume yeyote katupa ndoana yake na kuna kupata na kukosa. Ukimtema, mteme kiungwana na kama ni muungwana kweli basi uhusiano wenu utakomaa zaidi maana mipaka itakuwa inajulikana kwa wote. Hawezi kukudai chochote maana alifanya yote kwa mapenzi yake. Na kudai kunaweza kumlipukia maana haitakuwa siri tena kuwa alitoa kwa malengo gani.

Ukiamua kumshukuru kiaina, ufanye ukijua kuwa na wewe utajulikana tu. Kama vile wewe ulivyomstukia mwenzio (au tatizo lilikuwa ni yeye kuzaa na sio kuwa na uhusiano nje?). Upete ukijua kuwa kama itatokea siku akatokea anayekutaka na yuko huru patakuwa na kazi! Jamaa dizaini hii ni ving'ang'anizi ile mbaya.

Lakini nina wasiwasi. Is this for real? Maana kwa simulizi zako kama jamaa anapitia humu atakuwa ameishajijua!

Asante.
 

Mswahilina

Senior Member
Apr 7, 2008
171
0
natoa shukrani kwa michango yenu yote na ningejaribu kumjibu mmoja mmoja lakini kama mnavyojua ttcl yetu hii na mitandao ya kudandia.

Naomba niseme tatizo si fedha zake kwani na mimi nina za kwangu na nina uwezo wa kuishi vizuri tu. Mwanzoni nilifikiri ni mtu wa urafiki tu lakini aliponipa hizo za kunidondokea ndio nimepata na utata. Hivi nikiamua kuanza kumchunia si atanielewa vibaya na anaweza kuanza kudai "yote aliyonifanyia" mimi na mwanangu?

Au niamue kumlipa "kiaina" yaishe huku nikijua siwezi kuwa naye? Lakini pia maisha ya kuishi single muda mrefu nayo si mazuri kwani Mungu alituumba wawili wawili.

Nimeuliza hapa si mimi tu kuna mabinti wengine ambao wao hawana hata watoto lakini wanajikuta na utata huu wa kutembea na waume za watu hasa hawa waheshimiwa wetu. Au na sisi tuingie kwenye haya ya kuwakamua tu na kuwachuna?

nadhani nitafikia uamuzi na asanteni sana. Bimkubwa, nashukuru kwa ushauri wako. Umenisaidia sana.

Asanteni.

Uamuzi wa Busara ni kumsamehe na kumrudia Mzazi mwenzako au kuamua kuishi kama mseja. Kuwa hawara ni kujidhalilisha na kupata UKIMWI.
 

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
424
195
Bwana wasikutishe,we kama unaamua kumpa Tunda we toa kama unaona gozi piga chini kwani hadi sasa utakuwa unajua nini ni nini.Kana ka nsungu aligusia mambo ta Sex na Love so hapo inabidi upime je wewe una nia gani na huyo jamaa..kama masilahi yako yakifikiwa basi you can go on...
 

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,271
1,195
After climbing a great hill, someone only finds there are more hills to climb onwards..
 

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,398
1,250
Nashindwa kuelewa mantiki ya huyu bibiye anaeuliza swali hili. Anadai aliachana na mumewe kutokana na tabia ya mume huyo kutembea nje ya ndoa. Sasa kuna faida gani kuachana na mume aliyetembea nje ya ndoa, na sasa unataka ukatembee nje ya ndoa na mwanamume mwingine anayetembea nje ya ndoa? Kulikuwa na mantiki gani ya kumwacha mume yule?
 

Miwani

Senior Member
Feb 25, 2008
181
195
Mama, kama uliachana na mumeo kwa sababu ya kuzaa nje na ukuweza kumsamehe iweje sasa uwaletee wenzio shida. Unafikiri huyo mke wake akisikia kuwa mumewe anakidosho nje naye si atavunja ndoa yake na kwa hiyo tatizo la kuvunjika kwa zoa kuongezeka. Kama ulivyochukizwa kwa kitendo cha mumeo hivyohivyo usiwafanyie na wenzako hivyo
 

Kipanga

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
678
0
... dada hilo ni kanya boya achana na hilo dude na kama ameshakwambia ana mke na watoto sioni nafasi ya kupendwa sana sana unatafutwa kurogwa na mwenye mume. Tulia omba mungu utapata kitu cha kweli na cha uhakika hayo ma-advertise ya kusafiri na yuko busy yatakurudia siku moja. Si ujanua wanaume akila mzigo anatambaa na moto wake!!!
 
Mar 26, 2008
6
0
Kwa mtazamo wangu mi naona "mchane mbavu"..huyo anataka kukutumia tu pale anapojisikia na vile vile ana mke na watoto!Hakuna future hapo.. subiri ambaye hajaoa au kama jasiri na unaona unataka kuondoa upweke kwa kuolewa tafuta wa kukuoa..
 

rutashobya

Member
May 2, 2008
6
0
Wewe ni mtu mzima, unajua kila kitu, kwani unataka kutuambia kwamba hukuwahi kutembea na mwanaume yeyote ila mme wako tu? Je kama ulishawahi unatuuliza nini, tumia mbinu ile ile unayotumia kwa wanaume wako wengine.
 

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,635
2,000
Kwanini hukumwambia hivi: “Siwezi kuwa nawe k/sbb unae mke” badala ya kumuuliza ulivyomuuliza? Kujiamini ndiko kunakupa msimamo, dada!

Watu wengine hawapendi maendeleo ya wengine. Kuwa na mke haijalishi my friend. Watu huoa hata wanne ebo?

Wewe sister kama mmeachana na jamaa fresh angalia tu usawa wa mbele. Huyu aweza kuwa mchumba.Labda kama hutaki mchumba aliyeoa. Ila ninahisi kumpata fresh itakuwa ngumu. Labda umpate aliyeachika , japo hata mimi ningeachika ningechagua msichana .
 

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
dadangu, inategemea utaamua kutumia akili au utashi au hisia kufanya maamuzi.
Kama uliwakatalia wote hao kabla, huyu kakupa nini? Lazima kuna cha zaidi.
mi navyoona unahitaji company wakati kama huu wakati akili yako inapopingana nguvu za vishawishi.
Hivi ulikuwa unafikiri kumkataa mwanaume ni kishawishi? La hasha dada!!
Kishawishi ni kumkataa mwanaume ambaye unamtamani. Mwili wote unauma, kila kitu anachosema unaona kama ukweli na kizuri, hapo ndio uko kwenye kishawishi manake unashawishika.
Sasa kama wewew huwezi kushinda vishawishi basi ndio hivyo tena. Endelea tu.
Lakini kama unataka support ya upweke na liwazo wakati unapigana na kishawishi tupo wakina dada JF.
Nakuusia tu, kuwa unaweza kuvishinda, ni kuamua tu, msaada ni kukaa mbali na kishawishi, mwili hauna nguvu sana, hivyo tumia akili kaa mbali, futa namba ya simu. badili vitu vyote vinavyowakutanisha.
Anyway, kama ukikuwa unadhani inawezekana ukwa nae comfortably kwa zaidi ya miaka 10, si kweli, uhusiano utakwisha mapema tu na utabaki mpweke.
 

TanzActive

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
366
225
Unajua kwanini anakutaka?? kwa kuwa kipya hakinyemi......,baadaye akikupata atalelkea kwenye kipya kingine .Kumbuka kwa kuwa huna ndoa naye utakuwa ndio basi tena afadhali ya mkewe wa ndoa akienda anrudi tena!!!! utaumizwa tena kisha uchukie wanaume kweli kweli !!! achana na huo ujinga !!!
 

Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
587
225
Mpe tu tundi lakini tumia kinga! Usikubali kuwa wa kudumu lakini mchune kisawasawa maana hawa waheshimiwa wanakula hela zetu bila kuzifanyia kazi. Akipatikana wa kuwachuna, mie naona ni bora ili wazipunguze kidogo. This advise is nonetheless without prejudice, and is given without any fiducial commitment!
 

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,285
2,000
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.

Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.

Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.

Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.

Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.

Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k

Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.

asanteni and I'm out
.

Kuna mtu aliniambia kuwa adui ya mwanamke siyo mwanaume bali mwanamke mwenzake.
Ukimkubali halafu akakupa miwaya, usije ktk baraza kuomba ushauri jinsi ya kupona.
Angalia maisha ya mwanao (Innocent) kwanza kisha mengine yatafuata.....

......May be you look attractive, can i see you?????
 

Chief

JF-Expert Member
Jun 5, 2006
2,428
2,000
Mimi ningekushauri u-make up na mume wako kama mlikuwa mmeoana. Of course, kama anajutia kwa dhati kosa alilolifanya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom