Hotuba ya Mlimani - Hotuba Maarufu zaidi kuwahi kutolewa Duniani

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
HOTUBA MAARUFU ZAIDI KATIKA BIBLIA
(SERMON ON THE MOUNT)

images (12).jpeg


Yesu alipoanza Huduma ya kueneza neno la Mungu alikusanya wanafunzi wake 12 na akatoa Hotuba maarufu zaidi katika biblia nzima na hajawahi mtu yeyote katika biblia kutoa Hotuba kama ile kuanzia Mwanzo mpaka ufunuo hakuna Hotuba zaidi ya hiyo.

Hotuba hiyo inaitwa Hotuba ya mlimani , inakadiriwa alitumia masaa zaidi ya mawili na nusu kuimaliza Hotuba hivyo.Ni hotuba iliyochukua sura Tatu katika kitabu cha Mathayo (5-7)

SERMON ON THE MOUNT ( Mathayo 5-7)

Hotuba hii Yesu alielezea Mpango wake wote hapa duniani , akieleza wazi atakachokifanya mpaka atakapomaliza kazi , alisema kila kitu kilichomleta.

Yesu alipoona makutano wanamfuata kutoka pande zote akaamua kupanda mlimani ili sauti yake iweze wakifikia wote

Mathayo 4:25

[25]Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani

Mathayo 5:1-2
[1]Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;
[2]akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,

YESU ANATAJA SIFA 8 ZA WAFUASI WAKE WANAVYOTAKIWA KUWA NAZO

Tabia 8 za Mkristo

Mathayo 5:3-10

[3]Heri walio maskini wa roho;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
[4]Heri wenye huzuni;
Maana hao watafarijika.
[5]Heri wenye upole;
Maana hao watairithi nchi.
[6]Heri wenye njaa na kiu ya haki;
Maana hao watashibishwa.
[7]Heri wenye rehema;
Maana hao watapata rehema.
[8]Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
[9]Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
[10]Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Alianza kwa kuzitaja sifa 8 za watakaoingia Mbinguni (Raia Wa Mbinguni) kisha alipomaliza hotuba yake alianza kuitafsiri alipokuwa akifundisha mitaani , mpaka anakufa ndani ya miaka mitatu akawa amefafanua kila kipengele cha hotuba ya mlimani

Leo nitaelezea sifa moja

HERI WENYE MOYO SAFI

[8]Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.

Yesu anasema watakaofanikiwa kumuona Mungu ni wale wenye Moyo safi tu.Kuwa na moyo safi ndio kuwaje?

Moyo safi ni moyo ule uliomuelekea Bwana pasipo kuzongwa na nia zingine ,umpende Bwana kwa moyo wote pasipo kuwa vuguvugu.

Mwandishi Wa zaburi aliuliza ni nani atakaye panda mlima Wa bwana akaonane naye?

Zaburi 24:3-4
[3]Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
[4]Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili,
Wala hakuapa kwa hila.

Yesu akaja akajibu swali hili lililoulizwa kwenu kwenye zaburi miaka mingi sana iliyopita kwa kasema

"Mathayo 5:8
[8]Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
"

Nabii Ezekiel alionyeshwa na Mungu jinsi agano jipya litakavyokuwa ,jinsi Mungu atakavyotupa moyo safi

Ezekieli 36:25-26
[25]Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.
[26]Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Agano jipya litafanyiko na Maneno ya Bwana yatawekwa mioyoni mwetu

Yeremia 31:31-33
[31]Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
[32]Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.
[33]Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

Yesu anawaambia mafarisayo waliowachafu Wa mioyo yao ,wasafishe mioyo yao kwanza ,moyo ukiwa safi hata tabia mbaya zitakoma ,maana kilicho ndani ya moyo ndio kinachotokeza kwa nje ,kwahiyo mzizi Wa dhambi upo moyoni ,hivyo waung'oe.

Mathayo 23:25-29
[25]Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
[26]Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.
[27]Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.
[28]Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.
[29]Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,

Kuwa na moyo safi ni kutokuwa na nia mbili ,yani mguu mmoja kwa Mungu na mmoja duniani , moyo umuelekee Mungu wote

Yakobo 4:8
[8]Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Nabii Yeremia anasema agano jipya litakavyokuwa , anatoa unabii kuwa ni agano la moyo ya watu wenye njia moja

Yeremia 32:39
[39]nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao;

Nabii Ezekieli anasema kuna agano litakuja , agano jipya ,ambapo Mungu atadili na mioyo ,ambapo atatupa moyo mpya

Ezekieli 11:19
[19]Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

Mtume Paulo anawaambia Wakorinto wamhudumu Mungu pasipo kuvutwa na vitu vingine , yani kuwa na moyo unamuelekea Bwana pasipo kuchanganya na mambo mengine yasiyofaa

1 Wakorintho 7:35
[35]Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.

Moyo Wa binadamu una mambo ya uongo kiasi kwamba sio rahisi kuyajua hivyo moyo ndio matatizo ya dhambi yanapoanzia

Yeremia 17:9
[9]Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Yesu anafafanua hotuba ya mlimani kuwa katika moyo mambo yote mabaya ambayo Musa aliyaandika kama ni dhambi ndio yanapoanzia ,kwahiyo tukiusafisha moyo tutaachana na dhambi

Mathayo 15:19
[19]Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

Yesu anasema dhambi ipo ndani ya moyo , nje ya moyo Wa mtu hakuna dhambi hivyo tukisafisha Moyo tutakuwa tumemalizana na dhambi maana mizizi ya dhambi zote ipo moyoni

Marko 7:15,21-23
[15]Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu.
[21]Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
[22]wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
[23]Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Yesu anatuambia kuwa neno lake ndio linalosafisha moyo ,hivyo kwa kuwa na neno la Mungu moyo husafishika na Roho Wa Mungu hujenga makazi

Yohana 15:3
[3]Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

Mjini Wa Yerusalemu mpya watu watamuona Mungu uso kwa uso,na Yesu anasema watakaomuona ni wale kwenye moyo safi

Ufunuo wa Yohana 22:3-4
[3]Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;
[4]nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.

Heri kwenye moyo safi ,maana nao watamuona Mungu.

Amen.
 
Hizo heri nane ni tabia za kimasikini ambazo matajiri walizikataa na ndio ivo wakatoboa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom