Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Hii ni habari ya kweli kabisa. Uongo mimi nauchukia kama ukoma.

Kama huamini kuna wachawi, sikiliza vizuri: Hivi majuzi, walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano yenye saruji. Sio mzaha, nakwambia.

Sijawahi kuhisi uzito huo kamwe. Haraka sana nilitambua ni wachawi wanaotumiwa na mapepo kujaribu kunidhuru. Nikaanza kuwakemea kwa Jina la Yesu - kwa sauti ndogo, lakini yenye mamlaka watoke na kuniachia. Instantly, waliniacha na mgandamizo ule ukatoweka. Jina la Yesu lina nguvu sana. Ukilitamka, wachawi wanapigwa kipigo kikali sana na kukimbia. Hii ni mojawapo ya faida za kuokoka. Unatembea kifua mbele bila kuogopa wachawi.

Yakobo 4:7-10
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, na muomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainu

Wacha kumpakazia Yesu , hakuna mahali Yesu aliagiza watu watumie jina lake kwa jambo lolote . Wacha Kufuru
 
Mimi pia juzi walikuja ila niliwafanya kitumbaya sana maana mmoja alivyonikalia namimi siku fanya kosa, siwanakujaga bila nguo , sinikamuotea aisee nikamkata bonge la ndole lenye kucha ,aisee aliruka huyooo na game ikaishia hapo ,kumsumbua Yesu saa nyingine niukosefu wa adabu tu.
 
Hiyo ni Sleep paralysis inatokana haswa na mtindo mbovu wa maisha.

Kutokuwa na utaratibu maalumu wa kula, Uchovu mwingi, Stress, Kulala chali na kuchelewa kulala ni moja ya visababishi.
Sidhani kama watakuelewa hapa🥱🥱🥱
 
Mpaka sasa umejibu swali langu kwa asilimia 98% aiseee oky ...
Ngoja nimalizie hizi mbili..
Mkuu nilianza kuvutiwa sana na maneno yako mazri ambayo ulinambia baada ya kuanzisha nyuzi yangu ya kuota ndoto ya ajabu kama unakumbuka..

Swali je kwa kijana mwenzako kama mimi ambaye nahitaji huduma ya maombi kutoka kwako naweza kuipata hiyo hudumu.. hata kama hutoi ila niseme ukweli nimevutiwa na maombi yako wewe naomba nikukabizi kichwa changu...

Je naweza kuombewa na wewe.. nje ya jf
Sasa unataka kuwa mvuvi wa watu😂😂😂😂😂
 
Wacha kumpakazia Yesu , hakuna mahali Yesu aliagiza watu watumie jina lake kwa jambo lolote . Wacha Kufuru
Jagina
Soma Marko 16: 15-18 Imeandikwa hivi:
[Yesu] akawaambia, Nendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona."

Luka 10:17
“Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, Bwana[Yesu], hata pepo wanatutii kwa Jina lako.”
 
MKUU 🤣🤣

Sawa tunaamini katika KRISTO lakini kuna vitu sio shetani wala nini ni mwili wako tu ndio unayafanya hayo kaka.

Kuna kitu kinaitwa "KUPARALAIZ USINGIZINI" hii inatokana vitu vifuatavyo.
1. Kulala vibaya - umejikunjakunja

2. Oxygen debt - washa feni elekeza upande mwingie yaan upepo usikuguse dorect acha hewa iwepo ndani inazurula

3. Mazingira unayolala yaangalie pia.

UKIONA BADO YAPO BASI PIGA GOTI ITA YESU AJE AOKOE JAHAZI.
 
Jagina
Soma Marko 16: 15-18 Imeandikwa hivi:
[Yesu] akawaambia, Nendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona."

Luka 10:17
“Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, Bwana[Yesu], hata pepo wanatutii kwa Jina lako.”

Hizo aya ulizoleta hayo si maneno ya Yesu , soma vizuri , imeanza na, [Yesu] akawaambia , yaani huyo ni mtu anatuhadithia tu hatujui kwamba ni kweli au la na mtu huyo hata hajulikani ni nani kwa hiyo injili inaitwa Injili kama alivyotuhadithia Marko , hilo jina la marko limewekwa tu hapo na huyo marko wenyewe si mwanafunzi wa Bwana Yesu .

lete maneno Mimi Yesu nimewaagiza mtumie jina langu kwa matatizo yenu , na hakuna kwani hiyo ni shirki kuomba mtu badala ya Mungu. Yesu hawezi kuruhusu hivyo hata siku moja
 
Sidhani kama watakuelewa hapa🥱🥱🥱
pilato93
Tunamuelewa vizuri sana. Ibn Unuq anafikiri sayansi inaweza kuelezea kila kitu. Muulize: Yesu aliwezaje kugeuza maji yakawa divai? Aliwezaje kutembea juu ya bahari? Aliwezaje kubariki mikate mitano na samaki wawili tu akawalisha watu 5,000 na vipande vikabaki? Akikupa majibu ya kisayansi uni-tag
 
Leo watu elfu 5 wanalisha mtu 1
 
Hizo aya ulizoleta hayo si maneno ya Yesu , soma vizuri , imeanza na, [Yesu] akawaambia , yaani huyo ni mtu anatuhadithia tu hatujui kwamba ni kweli au la na mtu huyo hata hajulikani ni nani kwa hiyo injili inaitwa Injili kama alituhadithia Marko , hilo jina la marko limewekwa tu hapo na huyo marko wenyewe si mwanafunzi wa Bwana Yesu .

lete maneno Mimi Yesu nimewaagiza mtumie jina langu kwa matatizo yenu , na hakuna kwani hiyo ni shirki kuomba mtu badala ya Mungu. Yesu hawezi kuruhusu hivyo hata siku moja
Kama hukubaliani na andiko hilo. Na hili je?
Luka 10:17–19
Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

Hapo wanaposema "wanatutii kwa Jina lako," ni nani anaambiwa kama si Yesu?
Aliyesema "nimewapa amri ya kukanyaga nyoka" ni nani kama si Yesu?

Wewe kama unabishi, acha sisi tuendelee kulitumia Jina la Yesu kuyachapa mapepo.
 
Leo watu elfu 5 wanalisha mtu 1
Youbettersleep
Ni siku za mwisho hizi, manabii wengi wa uongo wametokea na kuwadanganya wengi. Kwahiyo usishangae watu 5000 wakimlisha mtu 1
Mathayo 24:4-28
Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi...Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi..."
 
Lete ushahidi wa Yesu kuagiza watu watumie jina lake kwa mambo au matatizo yao
Ushahidi gani tena unaotaka zaidi ya ushuhuda huu nilioandika katika uzi huu? Kama Yesu angekuwa hajaagiza tutumie Jina lake unafikiri hao wachawi wangekimbia? Si wangeninyonga?
 
Mimi pia juzi walikuja ila niliwafanya kitumbaya sana maana mmoja alivyonikalia namimi siku fanya kosa, siwanakujaga bila nguo , sinikamuotea aisee nikamkata bonge la ndole lenye kucha ,aisee aliruka huyooo na game ikaishia hapo ,kumsumbua Yesu saa nyingine niukosefu wa adabu tu.
Hahaa, hao walikuwa waigizaji tu au ndio hizo Sleep Paralysis anazosema Ibn Unuq .
Wachawi wenye mapepo halisi huwezi kuwaona kwa macho, mkuu, wala huwezi kuwafukuza bila Jina la Yesu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom