Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Hakiya nani jamani nyie, leo mwenzenu nilishikwa na butwaa kukuta ndani ya Bank hakuna ile misululu wa watu niliyoizoea kuikuta siku zote niendapo bank.

Nilikwenda kulipia ada za watoto wangu kwenye bank mbili tofauti zilizopo jijini Dar mitaa ya New Bagamoyo Rd. Nilikwenda kwenye matawi ya Bank maarufu na makongwe hapa nchini zilizoko mbembezoni mwa barabara ya New Bagamoyo Road.

Nilichokikuta mule ndani sikutaka kuyaamini macho yangu baada ya kukuta hakuna wetaja wanaohudumiwa.

Nilipotoka ofisini nilikwishajiandaa na foleni ndefu za benki zile. Baada ya kuona hamna watu Nilisimama kwanza karibu na kile kitufe nilichozoea kubonyeza ili kupata coupon ya kuhudumiwa, nilidhani kuwa labda kuna tangazo linalokataza watu wasiingie ndani ya benk kwa wakati ule ambalo mimi sikuliona huko nje, hivyo nilitaka kutoka nje nikaangalie kama kuna tangazo kama hilo, lakini mhudumu alidakia karibu.

Tawi lile lina tellers (counter) 7 lakini ilikuwa imefunguliwa teller moja tu. Mhudumu akaniita na kuniuliza nikusaidie nini nikamwambia naomba form ya kutuma ada ya shule, akanambia hakuna kujaza form njoo tu moja kwa moja nikuhudumie, we taja tu account number ya shule.

Wakati ananihudumia nikamuuliza kulikoni leo kuko hivi, akasema hali ni mbaya hivi sasa, tunasubiri tu labla mwisho wa mwezi ndo watu wanakuwa wengi kidogo, hatujui na sisi hatima yetu itakuwaje.

Nilipomalizana na bank ile nikaenda bank ile nyingine kutuma ada kwa mtoto mwingine, loo huko pia hali nikaikuta mbaya zaidi, sikukuta kabisa mhudumu kwenye madirisha (tellers) ya kuhudumia wateja, wahudumu walikuwa wanafanya kazi nyingine.

Nikajiuliza maswali mengi mwenyewe kama vile
1. Ni kweli watanzania wengi walikuwa mission town?
2. Ni kweli uchumi wetu utakuwa?
3. Ni kweli mishahara ya watumishi inawafikisha mwisho wa mwezi? na kama haiwafikishi hizo siku zitakazobaki watafanyaje?
4. Nini kifanyike ili watu wengi waende kupata huduma za kibenki kama zamani?
Ulitaka bank pawe PEUSI kiongozi??
 
Hacha uwongo halo mbaya wewe,unataka utuaminishe wayanzania kwa maana ya Wateja wa benki wangapi wanaweza kufanya online banking.acha kuwa na kichwa kikubwa ubongo mdogo
Mwadila huyo yuko kazini mkuu achana naye, atakuharibia siku tu.
 
Kuna miamala mingine lazima ufike bank, fikiria unataka kuweka fedha bank, huwezi kuweka online, utakwenda tu bank halafu ukitaka kuzitumia ndipo online banking inapofanya kazi.
Lakini pia bado zipo taasisi ambazo ili kujiridhisha kuwa umelipia huduma fulani, lazima uwapelekee pay slip, huna namna, lazima utakwenda bank.
Ni kweli teknolojia imeturahisishia sana katika ishu nzima ya utumiaji wa fedha zetu mara tuziwekapo bank
Kukosekana kwa watu bank, ni ishara kuwa watu hawana pesa za kupeleka huko, kinachopatikana kinaliwa, senti ya kuweka akiba haipo.
Good!
 
Dah,umenivunja moyo!
Pole sana ndg Kilimba kwa kuvunjwa moyo. Mimi naomba nikutie moyo ktk shughuli ya kilimo cha mbogamboga unachotarajia kukianza ili kupunguza ukali wa maisha. Katika kutafuta pesa kamwe usiruhusu walioshindwa na waoga kukurudisha nyuma ktk mipango yako. Fahamu kuwa biashara inayohusu chakula cha binadamu kamwe huwa hakikosi wanunuzi, labda kiwe ktk hali hafifu. Hivi nikisema kuwa kuna watu wanaishi vizuri kwa kutegemea kilimo cha mbogamboga naeleweka? Shime Kilimba chukua jembe, tafuta mbegu bora na maji ya kumwagilia usisahau mbolea ya samadi. Kuza mboga za viwango halafu tafuta wanunuzi, uone kama mfuko wako haujajaa kipato cha ziada ama la. Usisahau kumshukuru Mungu kwa kipato hicho. Kila la kheri.
 
Mkuu hali ya uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja ni tete kuliko tunavyoaminishwa na makasuku wa CCM.
 
Pole sana ndg Kilimba kwa kuvunjwa moyo. Mimi naomba nikutie moyo ktk shughuli ya kilimo cha mbogamboga unachotarajia kukianza ili kupunguza ukali wa maisha. Katika kutafuta pesa kamwe usiruhusu walioshindwa na waoga kukurudisha nyuma ktk mipango yako. Fahamu kuwa biashara inayohusu chakula cha binadamu kamwe huwa hakikosi wanunuzi, labda kiwe ktk hali hafifu. Hivi nikisema kuwa kuna watu wanaishi vizuri kwa kutegemea kilimo cha mbogamboga naeleweka? Shime Kilimba chukua jembe, tafuta mbegu bora na maji ya kumwagilia usisahau mbolea ya samadi. Kuza mboga za viwango halafu tafuta wanunuzi, uone kama mfuko wako haujajaa kipato cha ziada ama la. Usisahau kumshukuru Mungu kwa kipato hicho. Kila la kheri.
Nashukuru Sana!
 
Kuna miamala mingine lazima ufike bank, fikiria unataka kuweka fedha bank, huwezi kuweka online, utakwenda tu bank halafu ukitaka kuzitumia ndipo online banking inapofanya kazi.
Lakini pia bado zipo taasisi ambazo ili kujiridhisha kuwa umelipia huduma fulani, lazima uwapelekee pay slip, huna namna, lazima utakwenda bank.
Ni kweli teknolojia imeturahisishia sana katika ishu nzima ya utumiaji wa fedha zetu mara tuziwekapo bank
Kukosekana kwa watu bank, ni ishara kuwa watu hawana pesa za kupeleka huko, kinachopatikana kinaliwa, senti ya kuweka akiba haipo.

Kuna watu huwa wanaongea ili mradi tu waonekane wajanja. Utalipaje ada ya chuo au shule online?
 
Hawa wanasiasa si wakuwaamini kila walisemalo. Kwa sasa wimbo wao ni maisha magumu. Kwangu mimi maisha yamekuwa rahisi tukianzia na nyumba za kupanga zimepungua bei siyo kama mwaka jana, vyakula bei iko chini sana, nyanya ndio usiseme, viwanja, vifaa vya ujenzi kama cement bei inaendelea kupungua. Huduma za afya na elimu kwa sisi walalahoi zinaboreshwa, Service charge kwenye umeme hatulipi tena. Mtaani kwangu tumeletewa maji ya bomba na imepunguza gharama ya maji ya kununua kutoka elfu sitini kwa mwezi na sasa nalipia elfu kumi tu kwa mwezi. Nyinyi wanasiasa mnaotafuta umaarufu hayo maisha magumu ni kwa akina nani? Ni bora maisha yawe magumu kwa wachache(mafisadi) na yawe nafuu kwa watu wengi(walalahoi). Gharama za mahitaji muhimu ya watu wengi kama yako chini mimi sioni tatizo.
 
Ushauri :+. Nimefanya biashara ya mazao ufuta na mbaazi Ila sikupata fedha kama miaka mingine hasa mbaazi ndio kabisa nimekula hadi hasara sasa mwaka huu tujitahidi kufanya kilimo kwaajiri ya kula
 
Niwaelimishe kidogo hayo mnyoyaona ndio tafsiri halisi ya mabadiliko. Huwezi kubadili mambo au jambo ukategemea vitu vibaki vile vile tunapita katika transition period tu pinguzeni mihemko
pinguzeni ,,,,,,,,,, sasa nimeelewa wewe ukada unakusumbua.
 
Back
Top Bottom