Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Mie sijui hao wengine watafanyaje,ila mie nimeazimia kuanza kilimo cha bustani:vitunguu na mbogamboga!
Hali ni mbayaaa!
Kauli kama hizi zinawafedhehesha Wakulima. Yaani hali ikiwa mbaya ndio ukalime? Wanaolima siku zote hali zao zikoje.. Pumbavu!
 
Inategemea na bank yako
Kuna banks wanachaji a minimal fee
Nyingine ni free
Kulikoni upoteze muda wako kwenye foleni, parking, ujambazi etc ni bora ulipe tu hiyo fee ndogo
Ushauri tu
Mbona unaruka ruka kama mwanamke anatongozwa? Toa maelezo utapataje stakabadhi ya malipo iwapo utafanya malipo on line? Acheni kujifanya mnajua sana kumbe ni v......za
 
Hakiya nani jamani nyie, leo mwenzenu nilishikwa na butwaa kukuta ndani ya Bank hakuna ile misululu wa watu niliyoizoea kuikuta siku zote niendapo bank.

Nilikwenda kulipia ada za watoto wangu kwenye bank mbili tofauti zilizopo jijini Dar mitaa ya New Bagamoyo Rd. Nilikwenda kwenye matawi ya Bank maarufu na makongwe hapa nchini zilizoko mbembezoni mwa barabara ya New Bagamoyo Road.

Nilichokikuta mule ndani sikutaka kuyaamini macho yangu baada ya kukuta hakuna wetaja wanaohudumiwa.

Nilipotoka ofisini nilikwishajiandaa na foleni ndefu za benki zile. Baada ya kuona hamna watu Nilisimama kwanza karibu na kile kitufe nilichozoea kubonyeza ili kupata coupon ya kuhudumiwa, nilidhani kuwa labda kuna tangazo linalokataza watu wasiingie ndani ya benk kwa wakati ule ambalo mimi sikuliona huko nje, hivyo nilitaka kutoka nje nikaangalie kama kuna tangazo kama hilo, lakini mhudumu alidakia karibu.

Tawi lile lina tellers (counter) 7 lakini ilikuwa imefunguliwa teller moja tu. Mhudumu akaniita na kuniuliza nikusaidie nini nikamwambia naomba form ya kutuma ada ya shule, akanambia hakuna kujaza form njoo tu moja kwa moja nikuhudumie, we taja tu account number ya shule.

Wakati ananihudumia nikamuuliza kulikoni leo kuko hivi, akasema hali ni mbaya hivi sasa, tunasubiri tu labla mwisho wa mwezi ndo watu wanakuwa wengi kidogo, hatujui na sisi hatima yetu itakuwaje.

Nilipomalizana na bank ile nikaenda bank ile nyingine kutuma ada kwa mtoto mwingine, loo huko pia hali nikaikuta mbaya zaidi, sikukuta kabisa mhudumu kwenye madirisha (tellers) ya kuhudumia wateja, wahudumu walikuwa wanafanya kazi nyingine.

Nikajiuliza maswali mengi mwenyewe kama vile
1. Ni kweli watanzania wengi walikuwa mission town?
2. Ni kweli uchumi wetu utakuwa?
3. Ni kweli mishahara ya watumishi inawafikisha mwisho wa mwezi? na kama haiwafikishi hizo siku zitakazobaki watafanyaje?4. Nini kifanyike ili watu wengi waende kupata huduma za kibenki kama zamani?
Shukuru umeweza kupata hiyo pesa ya kuwalipia wanao shule. Kuna jamaa alikuwa anapeleka watoto wake wote kwa Santa schools sasa hivi analia. Soon atawapeleka
Kanumba. Unaambiwa watu wengi waliokuwa na mishe ni wale walioshughulika na viongozi wa chama na serikali. Sasa tunaisoma namba wote.
 
Mbona unaruka ruka kama mwanamke anatongozwa? Toa maelezo utapataje stakabadhi ya malipo iwapo utafanya malipo on line? Acheni kujifanya mnajua sana kumbe ni v......za

Once a transaction is posted it can immediately be reflected in that school's account (in real time)
Unless huyo headmaster ni mbabaishaji na hiyo shule ni mangumashi
Mbadilike na kwenda na wakati na teknolojia na msiachwe nyuma
Thanks
 
acheni kupeana moyo kwa mambo ya kipuuzi,mnapinga kwa ujinga tu,hebu niwaulize hayo mambo ya kutumia mitandao tameanza mwezi huu?au mwaka huu?maisha yamekua magumu kama sio kwako basi kwetu.
Hao ni pipa na mfuniko,wanaona watu wote humu hatuna akili na wao tuu ndio waojua kutumia hiyo automation.
 
Niwaelimishe kidogo hayo mnyoyaona ndio tafsiri halisi ya mabadiliko. Huwezi kubadili mambo au jambo ukategemea vitu vibaki vile vile tunapita katika transition period tu pinguzeni mihemko
 
huu uchochezi sasa,gavana keshasema mambo ni safi kabisa, mororoooooo
 
Siku hizi watu wanafanya miamala kwa njia ya simu..... Benki tunaenda kwa dharura tu....
 
Hakiya nani jamani nyie, leo mwenzenu nilishikwa na butwaa kukuta ndani ya Bank hakuna ile misululu wa watu niliyoizoea kuikuta siku zote niendapo bank.

Nilikwenda kulipia ada za watoto wangu kwenye bank mbili tofauti zilizopo jijini Dar mitaa ya New Bagamoyo Rd. Nilikwenda kwenye matawi ya Bank maarufu na makongwe hapa nchini zilizoko mbembezoni mwa barabara ya New Bagamoyo Road.

Nilichokikuta mule ndani sikutaka kuyaamini macho yangu baada ya kukuta hakuna wetaja wanaohudumiwa.

Nilipotoka ofisini nilikwishajiandaa na foleni ndefu za benki zile. Baada ya kuona hamna watu Nilisimama kwanza karibu na kile kitufe nilichozoea kubonyeza ili kupata coupon ya kuhudumiwa, nilidhani kuwa labda kuna tangazo linalokataza watu wasiingie ndani ya benk kwa wakati ule ambalo mimi sikuliona huko nje, hivyo nilitaka kutoka nje nikaangalie kama kuna tangazo kama hilo, lakini mhudumu alidakia karibu.

Tawi lile lina tellers (counter) 7 lakini ilikuwa imefunguliwa teller moja tu. Mhudumu akaniita na kuniuliza nikusaidie nini nikamwambia naomba form ya kutuma ada ya shule, akanambia hakuna kujaza form njoo tu moja kwa moja nikuhudumie, we taja tu account number ya shule.

Wakati ananihudumia nikamuuliza kulikoni leo kuko hivi, akasema hali ni mbaya hivi sasa, tunasubiri tu labla mwisho wa mwezi ndo watu wanakuwa wengi kidogo, hatujui na sisi hatima yetu itakuwaje.

Nilipomalizana na bank ile nikaenda bank ile nyingine kutuma ada kwa mtoto mwingine, loo huko pia hali nikaikuta mbaya zaidi, sikukuta kabisa mhudumu kwenye madirisha (tellers) ya kuhudumia wateja, wahudumu walikuwa wanafanya kazi nyingine.

Nikajiuliza maswali mengi mwenyewe kama vile
1. Ni kweli watanzania wengi walikuwa mission town?
2. Ni kweli uchumi wetu utakuwa?
3. Ni kweli mishahara ya watumishi inawafikisha mwisho wa mwezi? na kama haiwafikishi hizo siku zitakazobaki watafanyaje?
4. Nini kifanyike ili watu wengi waende kupata huduma za kibenki kama zamani?

Mi nitakujibu number moja:

Mission town wanatoa pesa wapi? Je wanaiba? Hapana, wapo between wanafanya udalali etc, now waki pata pesa wanajenga, wanajisomesha, mizunguko ya pesa inasonga.
Hata USA pana mission town. This is more than that. Vibarua waliopo tu wanazurua nao walikuwa mission town?
 
Jishauwe tu uone kama mwakani hautawaandikisha hao wajukuu Nyerere day school.
 
Kwa kweli watu hatupendi mabadiliko, kwanza haya ya kusema fedha za mission town ndizo zilikuwa zinaendesha maisha yetu sio kweli, zilikuwa fedha za madawa ya ya kulevya, magendo, wizi na ubadhirifu zilizokuwa zimesambaa. Kwa kweli kama tunaitakia nchi yetu mema hayo sio maisha tunayotaka kuwafundisha watoto wetu, wajukuu au vitukuu, ni maisha fake na sijuwi tungeishia wapi, kuna bwana mmoja hapa kajitahidi mno kutuelezea sisi, kwamba kufanya miamala sio lazima uende benki, bado tunabisha, unaenda benki kwa swala muhimu mno, labda ku update details zako au kama kweli muamala uliotakiwa kuufanya electronically umeshindikana, ila bado tunabisha ili kupata nafas ya kwenda kushinda benki, pia foleni zilizokuwapo huko nyuma kwenye services zetu tusishangae zikipunguwa, haya ndio maisha tunayotakiwa kuishi, foleni kidogo au kutokuwepo kabisa!
[HASHTAG]#hapakazi[/HASHTAG] tu! mbona hatukubali?!
Simbanking, Mpesa, Tpesa, Emoney hata Airtel money ndio future...
Tunaenda shangaa benki au sehemu zingine za huduma kwa ajili ya nini?! Kwanini twapenda poteza muda wetu bila sababu?! Tubadilike..
Pia kama ulizoea kuishi maisha yaliyo juu ya kipato chako badilika, wala sio shida, ni kwenda na hali, wengine wala! Twaona kawaida kama sio maisha safi tu..
 
Hapo nimeona mengi
-benki hazitoajiri tena
-redundancy lazima ziwepo
-baadhi ya benki zitafutika
kwenye hili duara la tz
-mikopo ndo isahaulike.
-uwekaji wa pesa benki
hautokuwepo.

Maoni yangu ule utafiti urudiwe wiki mbili zijazo.
 
" NATAKA WALIOISHI KAMA MALAIKA WAISHI KAMA MASHETANI " Na wala siyo walioishi kama shetani waishi kama malaika , Hapa kazi tu !
Walioishi kama malaika ndio waliokuwa na hali nzuri, sasa wanatakiwa waishi kama shetani katika hali mbaya, je waliokuwa katika hali mbaya tayari ya ushetani, nafikiri watakuwa marehemu sasa. Roho yake usuuzike.
 
Back
Top Bottom