Hakiya nani jamani nyie, leo mwenzenu nilishikwa na butwaa kukuta ndani ya Bank hakuna ile misululu wa watu niliyoizoea kuikuta siku zote niendapo bank.
Nilikwenda kulipia ada za watoto wangu kwenye bank mbili tofauti zilizopo jijini Dar mitaa ya New Bagamoyo Rd. Nilikwenda kwenye matawi ya Bank maarufu na makongwe hapa nchini zilizoko mbembezoni mwa barabara ya New Bagamoyo Road.
Nilichokikuta mule ndani sikutaka kuyaamini macho yangu baada ya kukuta hakuna wetaja wanaohudumiwa.
Nilipotoka ofisini nilikwishajiandaa na foleni ndefu za benki zile. Baada ya kuona hamna watu Nilisimama kwanza karibu na kile kitufe nilichozoea kubonyeza ili kupata coupon ya kuhudumiwa, nilidhani kuwa labda kuna tangazo linalokataza watu wasiingie ndani ya benk kwa wakati ule ambalo mimi sikuliona huko nje, hivyo nilitaka kutoka nje nikaangalie kama kuna tangazo kama hilo, lakini mhudumu alidakia karibu.
Tawi lile lina tellers (counter) 7 lakini ilikuwa imefunguliwa teller moja tu. Mhudumu akaniita na kuniuliza nikusaidie nini nikamwambia naomba form ya kutuma ada ya shule, akanambia hakuna kujaza form njoo tu moja kwa moja nikuhudumie, we taja tu account number ya shule.
Wakati ananihudumia nikamuuliza kulikoni leo kuko hivi, akasema hali ni mbaya hivi sasa, tunasubiri tu labla mwisho wa mwezi ndo watu wanakuwa wengi kidogo, hatujui na sisi hatima yetu itakuwaje.
Nilipomalizana na bank ile nikaenda bank ile nyingine kutuma ada kwa mtoto mwingine, loo huko pia hali nikaikuta mbaya zaidi, sikukuta kabisa mhudumu kwenye madirisha (tellers) ya kuhudumia wateja, wahudumu walikuwa wanafanya kazi nyingine.
Nikajiuliza maswali mengi mwenyewe kama vile
1. Ni kweli watanzania wengi walikuwa mission town?
2. Ni kweli uchumi wetu utakuwa?
3. Ni kweli mishahara ya watumishi inawafikisha mwisho wa mwezi? na kama haiwafikishi hizo siku zitakazobaki watafanyaje?
4. Nini kifanyike ili watu wengi waende kupata huduma za kibenki kama zamani?