Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Kuna miamala mingine lazima ufike bank, fikiria unataka kuweka fedha bank, huwezi kuweka online, utakwenda tu bank halafu ukitaka kuzitumia ndipo online banking inapofanya kazi.
Lakini pia bado zipo taasisi ambazo ili kujiridhisha kuwa umelipia huduma fulani, lazima uwapelekee pay slip, huna namna, lazima utakwenda bank.
Ni kweli teknolojia imeturahisishia sana katika ishu nzima ya utumiaji wa fedha zetu mara tuziwekapo bank
Kukosekana kwa watu bank, ni ishara kuwa watu hawana pesa za kupeleka huko, kinachopatikana kinaliwa, senti ya kuweka akiba haipo.
Uko sahihi!
Sijui wanaobisha ,wanabisha nn!
 
Hao wafia chama huwaambia lolote kila siku wao wanawaza jinsi gani ya kushinda uchaguzi tu na hawawazi maendeleo
kuna maendeleo gani zaidi ya kuwasomesha watoto wako? tumeyagundua haya wakati tulipokuwa tunafanya miamala ya kulipa ada za watoto wetu kama tulivyoelekezwa na wenye shule. nitajie shule au chuo kimoja hapa nchini ambacho kinataka wazazi walipe ada za watoto wao online au internet au tigopesa.
 
Mkuu hizo bank zitakuwa ni crdb ya mbezi goigi na nmb ya mbezi africana
 
Juzi naingia CRDB pale Mlimani City, ile namaliza kubonyeza tu kile kimashine cha kutoa namba mlangoni nikashtukia ndio namba hiyo hiyo inaitwa kwenda Counter, nikashangaa sana.
Ilibidi tu niende Counter nimwabie ndio kwanza naingia hata Slip Siajajaza bado.
 
Ingekuwa baa la njaa, maafa ya mafuriko au tetemeko la ardhi au kimbunga katrina tungepata misaada kutoka kwa mataifa rafiki, je hili tunajikwamuaje?
 
Siku hizi kila kitu ni INTERNET BANKING ndio maana foleni zimepungua. Jamani acheni UCHOCHEZI.
 
Hali ni mbaya kweli.Nakumbuka kipindi cha JK nyanya ikishuka sana tenga lilikuwa 20000 lakini hali ndo kama ilivyo hivi sasa na mfano mwingine nyama buchani kwenye mji wetu ilikuwa ukienda buchani saa 8 mchana hukuti nyama lakini sasa hivi muda wowote nyama unapata.
 
Utamuuzia nani hizo mboga zako? Nyanya zimejaa zinakosa mnunuaji.
Usimkatishe tamaa mwishowe akajiua bure!
Lakini mwaka Jana mwez 9! Kulikuwa na wimbo maarufu wa viwanda nahisi bado haujatoka, au ilikuwa ni promo ya ule wimbo uliokuwa unaitwa "wacha waisome namba"!
 
2015/10 tulikosea sana
Japo siku mpigia ila wakulaumiwa ni wale waliomuweka hapo alipo
Kuishi maisha ya kukomoana si vizuri kabisa
 
Sitii neno nitaitwa mchochezi
lengo sio kuchochea tunafuta nini kifanyike, maendeleo na maumivu hayana chama, wote tunanunua na kuuza palepale bila kujali umevaa fulana na capelo ya rangi gani.
 
ndululu anasema uchumi uko imara !
uchumi wa nani ?
aweke wazi,jamaa anajijazia akaunti wengine tunazidi kuwazika,kila siku mazishi.
 
Ngoja noti zibadilishwe utaona foleni tu. Tunajua mnazificha hela uchagoni, zitoeni kabla noti mpya hazijaingia mujini
 
Back
Top Bottom