Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Nimeshangaa kukuta Benki ni kweupe

Inategemea na bank yako
Kuna banks wanachaji a minimal fee
Nyingine ni free
Kulikoni upoteze muda wako kwenye foleni, parking, ujambazi etc ni bora ulipe tu hiyo fee ndogo
Ushauri tu
Hahahahaha naona unazidi kuchanja mbuga kulikimbia swali la mkuu
 
Mtoa mada,hii hali mimi wikend iliyopita nilikumbana nayo mahali,tena kwenye tawi la benk kubwa sana hapa nchini,nikamuuliza mteja mwenzangu Je tawi hili huwa halina foleni?akasema aaah watu wamepungua labda mwisho wa mwezi
nenda ile benki pale magomen usalama uone foleni
 
Kuna ndugu humu alisema yeye hii hali alishaizoea kitambo na akajiingiza ktk UJASIRIAMALI wa KUUZA KILA KILICHO MBELE YAKE.
 
Hahahahaaa interesting.
Ni kama magari tu vile, kila moja huingia kwa wakati wake barabarani na kutengeneza foleni.
Kwann unafikiri suala la ukata limekuwa gumzo kwa kila mwana jamvi?

Inategemea unamuuliza nani. Mimi binafsi naona ni kawaida sababu sijaona impact yoyote kwa upande wangu tangia utawala uliopita hadi sasa
Kamshahara kangu ni kale kale tena nashukuru kodi Ya nyumba imepungua
Matumizi yangu ni yale yale
Sasa huo ukata labda ni kwa wafanya biashara
Ila ninachoma ndizi kuongeza kipato na wateja ni walewale na sijaona mabadiliko yoyote hadi sasa
 
Mdau,ile benk wateja wake wakubwa ni wafanyakazi,na ukumbuke malipo mengi ya serikali hupitia pale hata ya vyeti vya kuzaliwa vya watoto,kingine foleni ya pale ni ya msimu,yaani mwisho wa mwezi.Pamoja na hayo foleni imepungua bado
nenda ile benki pale magomen usalama uone foleni
 
Inategemea unamuuliza nani. Mimi binafsi naona ni kawaida sababu sijaona impact yoyote kwa upande wangu tangia utawala uliopita hadi sasa
Kamshahara kangu ni kale kale tena nashukuru kodi Ya nyumba imepungua
Matumizi yangu ni yale yale
Sasa huo ukata labda ni kwa wafanya biashara
Ila ninachoma ndizi kuongeza kipato na wateja ni walewale na sijaona mabadiliko yoyote hadi sasa
Kamshahara!!! ni heri yako una kamshahara kale kale kanakusukuma, sasa yule fundi ujenzi, rangi, umeme, randa, mama ntilie, mpiga matofali, muuza cement, bomba, rangi, tiles, n.k watafanya kazi gani ili kupata pesa kama hakuna tajiri anayehitaji kujengewa nyumba, kuchongewa madirisha na milango, kuwekewa tiles, kupigiwa rangi, kufanyiwa wiring, kuwekewa bomba za maji, kupauliwa? mama ntilie atamuuzia nani chakula kama hakuna wabeba zege site? mwenye duka la vyakula atamuuzia nani kama mama ntilie hapiki kwa kukosa wateja site? hakuna viwanda, hakuna mashamba makubwa ya mifugo wala mazao ambayo yanaweza kuajiri watu wengi na kupata pesa, wakapata wapi pesa sasa za kwenda kununulia vitunguu vya mkulima na bidhaa zitakazozalishwa kutoka "viwandani"? Pesa kule vijinini zitakwendaje kama nyanya hazina bei huku mjini?

Nadhani tunahitaji mjadala mpana hapa, na ikumbukwe kuwa kosa hapa sio la serikali hii ya awamu ya tano bali hata wao wamelikuta tatizo hili. Watanzania tulikuwa hatulipani mishahara bali tulikuwa tunapeana posho ambazo hazifiki tarehe 10 ya mwezi, hivyo kila mfanyakazi alikuwa anaishi kwa mission town, kila mtu aliruhusiwa na mfumo kuwa mwizi wa kitu fulani ili ajalizie siku za mwezi zilizobakia. Wako waliokuwa wanaiba muda wa waajiri, wako waliokuwa wanaiba pesa kwa njia za udanganyifu, wako waliokuwa wanaiba vitu halisi kama vile mafuta ya magari na vifaa vya kazi vya waajiri wao, na wako waliokuwa wanakula rushwa za aina mbalimbali. Serikali zilizopita zote zilikuwa zinalifahamu hilo wakati wa kupanga kima cha mishahara ya watumishi wake. Walikuwa wanafahamu kuwa kima cha chini cha mshahara hakimfikishi mtumishi japo hata siku 5 lakini hawakushangaa kwanini mtumishi anafika mwisho wa mwezi pamoja na matanuzi juu na baa zinajaa na TBL inasifiwa kuongoza kwa ulipaji kodi, kumbe kodi ile ni pesa zilizokuwa zikiibwa serikalini hukohuko. Kosa la awamu hii ya tano ni kuiziba mianya yote ya wizi bila kutoa njia mbadala ya kuwafanya watumishi wafike mwisho wa mwezi, wanunue nyanya za wakulima, wanunue chakula cha mama lishe wadogo, n.k. Haisemi watu watauzia wapi na nani atanunua bidhaa za wakulima na wafugaji. Mipango yetu ya maendeleo haikuendana na ongezeko la idadi ya watu, sasa watu ni wengi na uchumi ni kidogo tutafanya nini sasa?. mfano, Wakati ule tunapata uhuru tulikuwa wachache na mkoloni alituachia mapesa mengi, badala kupanga maendeleo yetu tukasema Tanzania haiko huru mpaka bara lote la Afrika liwe huru, hivyo ilitugharimu sana kazi hii ya kuikomboa Afrika na tukasahau maendeleo ya watu wetu. Marais waliopita wamemuachia Magufuli kazi kubwa sana ambayo haikustahili kuwa yake. Nadhani taifa lingeachwa lizalishe watu wachache wenye uwezo mkubwa wa kulima mashamba makubwa kwa njia za kisasa yanayoweza kulisha watanzania wote na kutoa ajira kwa watanzania badala ya kila mwananchi kudai ardhi ya kulima vituguu debe moja. Kwanjia yoyote ile taifa lizalishe watu wengi kama akina Mengi, Dewji, Rostam, na wawekezaji wengine ili watanzania walio wengi wapate ajira humo na sio kila mtu anakuwa na kiwanda cha kuprocess tomato sauce. Serikali isimamie ukutozaji kodi tu na kuwalipa watumishi wake mishara itakayowafanya watoe huduma safi kwa wateja.
 
Wasioweza maisha haya wachukue majembe wakalime vijijini
Ardhi ipo Ya kumwaga. Ujanja ujanja usiokuwa na tija hauna nafasi in the future
Tibadilike
Only the fittest will survive
Sounds harsh but that the reality
 
Hivyooo!! nipe darasa, inakuweje hivyo, shule imeagiza ada zote zilipiwe bank fulani na ikatoa Account na jina la bank halafu wanasema mtoto aje na Original Pay in Slip shuleni kudhibitisha malipo. Nambie hiyo automation yako unayosema ningefanyaje ili nipate hiyo Pay in Slip inayotakiwa na mwalimu Mkuu?
Wa kukurupuka hao hujawafahamu? wao hakuna kutafari anapoteza muda likija kichwani analiweka hadhari bila kutafari kama linafaa ama la wasikuumize kichwa.
 
Back
Top Bottom