Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Habari wakuu,

Nahitaji ushauri kidogo hapa. Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kufanyia kazi popote pale, na hata kuhamia yalipo makao makuu ya shirika kama nikitaka (Houston, Texas, USA), lakini pia nikitaka naweza kubaki hapa hata Tanzania nikaendelea kufanya kazi remotely, nikawa naenda USA mara mbili tu kwa mwaka. Nikiamua kuhamia USA, maana yake wako tayari kuni sponsor VISA ya H-1B.

The tricky part ni kwamba mshahara ni ule ule, vyovyote vile nitakavyoamua. Jiji ambalo makao makuu ya jamaa yapo ni Houston, jimbo la Texas. Mimi nina familia ya mke na watoto wawili, ofa yao ya mshahara ni USD 7,500 kwa mwezi. Wamenipa muda wa wiki mbili nifanye maamuzi kisha niwaatarifu ili waandae mkataba wangu kulingana na maamuzi nitakayokuwa nimeyafanya.

Kufanya kazi na kuishi USA kiujumla limekuwa ni jambo ambalo nimelitamani sana kwa muda mrefu kusema ukweli, shida ni hapo kwenye maslahi naona kuhamia USA with the same income ambayo naweza pia ipata kwa kubaki hapa bongo ni kama nitakuwa nimerudi nyuma sana, kwa sababu USD 7,500 kwa maisha ya Marekani sio pesa nyingi kihivyo, kulinganisha na bongo ambako unaishi ki-don kweli kweli kwa hiyo pesa.

Najua humu JF kuna wazoefu wa kuishi USA, na pia kuna watu wana exposure za kutosha kiujumla, nikaona sio mbaya nikaja hapa kuomba ushauri.

UPDATE 01/02/2024: Napenda kuwapatia update kuwa nimefanya uamuzi kuhusiana na hili suala.
Nimeamua kuwa nitabakia hapa hapa BONGO, baada ya kuchakata ushauri wenu, pamoja na insights kutoka sehemu mbalimbali. Nimeonelea kuwa itakua na faida zaidi kwangu nikiendelea kubaki hapa hapa, mpango ni kuweza ku save as much as possible, na kufanya investiments za long term na short term hapa hapa nchini. Hivyo, nimeshasaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utawezesha hilo. Nawashukuruni nyote kwa mawazo yenu.
 
Screenshot_20240123-121413_1.jpg
Screenshot_20240123-121413_1.jpg
 
Indeed hiyo sio pesa ya kutisha US hasa kwenye mji kama Houston, ila there's truckload more that the US offers kulinganisha na Ileje (Bongo yote ni Ileje tu).

Nenda nje kapate exposure, ongeza ujuzi, elimu na maarifa. It's easier to scale up ukiwa nchi ya maziwa na asali-US kuliko Ileje. Utadouble hiyo amount within a short period of time. Ushajiuliza ukibaki bongo afu ukapoteza hiyo kazi ni wapi pengine utapata kazi kama hiyo? US zipo kibao ni wewe tu.

Badilisha mazingira huko mbeleni ukiamua kurudi Ileje it's up to you ila at least jaribu maisha upande wa pili. Usiinyime familia fursa.
 
Ninajua unasema ukweli ila nina amini...kuna mahali hakupo sawa...

Mshahara wa 7500 kwa Us ni hela ndogo sana...ukihamia us tena makao makuu...lazma huo mshahara uwe mara mbili au tatu...

Kwa kukushauri...

Baki bongo utanishkuru na uwekeze kweli kweli achana na bata kabisa labda kama uko 20's

Nina rafki angu mmoja nahisi ni inteligence wa us ila ni mbongo analipwa dola 9elf...anaishi kitajiri sana
Ofice nyumbani na kila kitu hapa bongo wako wawili tu

Baki hapa....us utaenda tu ukiperfome na ukivumilia na utaenda na mshahara sahihi
 
Back
Top Bottom