Faida ni bora kuliko mshahara. Mshahara utakufanya uishi tu, lakini faida inaweza kukufanya uwe tajiri

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,329
8,250
Habari waungwana,

Ukiwa mwelewa na kuacha ubishi haya maneno yanaweza kubadilisha maisha yako kabisa. Siandiki maneno haya ili kukuonyesha kwamba mimi ni tajiri sana hapana. Naweza kuwa sina chochote lakini bado nikaandika kitu ambacho kitakufanya kesho uwe mtu mkubwa sana hapa duniani. Wapo watu ambao wameishia kulisoma neno FAIDA/PROFIT kwenye topic za hesabu tu ila hawajawahi kuipata wala kuionja katika maisha yao. Lakini embu soma vizuri aya inayofuata.

Unajua ni vigumu sana kupata utajiri kupitia mshahara, lakini mtu yeyote anaweza kutajirika kupitia faida. Faida ndio inaweza kubadilisha mtazamo wako wote, hata kama unaipata kwa muda wa ziada uliotenga kufanya kibiashara fulani. Hata kama unaipata kwenye kibiashara kidogo cha ujasiriamali, kikampuni cha mtandao wa masoko au kibiashara cha kutoa huduma za kuandika na kuhariri kama anachofanya Meneja Wa Makampuni kupitia kikampuni chake cha "Bright and Genius Editors".

Kinaweza kuwa kibiashara cha mafunzo, ushauri au kufundisha. Kinaweza kuwa kibiashara cha kitu unachokipenda kama vile kupaka rangi, kuandika, ufundi, kutengeneza mbao, kompyuta au kupika.

Lakini mara tu unapoanza kuwekeza muda wako wa ziada na juhudi zako katika kibiashara chako mwenyewe hata kama ni kidogo, utaona jinsi ilivyo raha kuamka asubuhi na kwenda kufanya kazi yako mwenyewe kwaajili ya kujiingizia kipato chako mwenyewe huku ukiwa unaufukuzia utajiri. Hata kama unatumia masaa machache tu kwa wiki kufanya kazi hiyo.

Kiukweli huwa inatia nguvu sana unapokwenda kufanya kikazi chako mwenyewe kila siku kwa muda wa ziada uliotenga ili upate kifaida kidogo kitachokufanya uwe tajiri badala ya kutegemea tu kazi inayokufanya uweze kuishi. Na mara tu unapoanza kuonja kifaida chako hata kama ni kidogo mtazamo wako wote unabadilika na wakati mwingine hata confidence ya kuishi hapa duniani huongezeka.

Mwisho: Kutegemea mshahara unaokufanya upate kipato kitachokuwezesha kuishi kwa mwezi tu kunakufanya wakati mwingine uwe mwoga wa mazingira ya hapa duniani. Mtu anaogopa hivi keho nikifukuzwa kazi nitaishije mimi. Hivi kesho nikitumbuliwa mimi nitaishije. Mtu anayetegemea mshahara tu hana mahali pengine pakuipata pesa yake zaidi ya mshahara. Sii hivyo tu hana mahali pengine pakuongeza kipato chake, kipato chake ni constant huku matumizi yake yanazidi kuongezeka kadri miaka inavyozidi kwenda.

Imeandikwa na Bright and Genius Editors:
Watoa huduma ya Kuandika na Kuhariri.
Email: bandg.editors@gmail.com
Phone/WhatsApp: +255747744595/+255687746471
 
Mawazo mazuri.

Main stream ambayo ni mshahara inabidi iwe chanzo Cha kuanzisha other channels. Pamoja na kuwa na bihashara ndogondogo usidharau kazi kuu inayokupa mshahara wa kuwekeza kwenye mbishe zako izo.

Vyanzo vya capita ni pamoja na mshahara, loan from ndugu ama taasisi ndondogo za kufedha, michango kutoka kwa ndugu etc.

Kikubwa kuwa na heshima ya fedha ,kujari mda, toa service au bidhaa bora na customer care. Lakin elewa pia miracles ktk maisha zipo, upatapo fursa itumie to the fullest.
 
Taarifa yako ya kuomba fund USA ambassador was scama nilichukia kuona unapost Mambo ya uongo.
Unauhakika na uchokisema au unataka kunichafua boss. Umejaribu kufutilia kwenye website ya ubalozi wa marekani? Umejaribu kuwauliza mods kwanini waliufuta. Kwa kifupi watu wengi wa jamii forum bado hawajastaaribika na wengine wamejaa wivu uskute waliomba mods afute uzi ili usisambae kwa watu wengi. Ingia ubalozi wa Marekani utakutana hilo Tangazo.
 
Mawazo mazuri.

Main stream ambayo ni mshahara inabidi iwe chanzo Cha kuanzisha other channels. Pamoja na kuwa na bihashara ndogondogo usidharau kazi kuu inayokupa mshahara wa kuwekeza kwenye mbishe zako izo.

Vyanzo vya capita ni pamoja na mshahara, loan from ndugu ama taasisi ndondogo za kufedha, michango kutoka kwa ndugu etc.

Kikubwa kuwa na heshima ya fedha ,kujari mda, toa service au bidhaa bora na customer care. Lakin elewa pia miracles ktk maisha zipo, upatapo fursa itumie to the fullest.
Pointed
 
Ajira inaweza kukufanya uwe tajiri ila ni mpaka upate cheo kikubwa, shida inakuja tupo mil 60, na vyeo vikubwa vyenye psa havizidi mil10. Hapo ndio inabidi wengine tufukuzie utajiri pembezoni mwa barabara
 
Back
Top Bottom