MSAADA: Nimepata kazi Serikalini dereva ila mshahara mdogo kuliko wa Mwendokasi ninakofanya kazi sasa. Nimechanganyikiwa!

road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
2,064
3,011
Nimepata kazi Serikalini dereva mshahara 300,000/ kwa mwezi, wakati Mwendo kasi nachukua 800,000/. Nimechanganyikiwa!

Wanabodi mimi ni dereva mzoefu wa daladala kisha nikaajiriwa na Mwendokasi ambapo nakula 800,000/per month .

Wandugu kwa sasa nimevurugwa kwan baada ya interview iliyohusisha watu 760 ambao tuliomba kazi wakala wa vipimo tumepenya na kuajiriwa 57 tu.

Nimepewa barua Jana napaswa kuripoti kituon kuanzaia 2/7 sasa aisee mbona hii salary Jau!? Yaani nipo kipindi kigumu wandugu hebu wenye uzoefu nisaidieni hill!?

Kiukweli napata wakati mgumu sana barua ninayo ila naipenda ajira za Serikali tatizo hiyo salary!?

Naomba ushauri.
 
Serikalini kuna mshahara mdogo sana ila fursa nyingi ingawa inategemeana na mahala utakapokua.

Nakushauri ukubali huo wa wakala wa vipimo.

Ushauri wangu unatokana na sababu kwamba kada yako ya udereva kwenye private sector iko soo weak, muda wowote unaweza kufukuzwa kazi ukipata ajali wakati serikalini utapata ajali utapewa gari nyingine ila sio kufukuzwa.
 
Kama huko wakala wa vipimo kuna safari za nje ya mkoa basi nenda. Serikalini kuna kitu inaitwa 'per diem', madereva wanajenga kwa kuitegemea hiyo kitu. Lakini kama kazi yako itakua kuzunguka tu hapo mjini basi maisha yako yatakuwa magumu kwakweli. Lakini kwa ujumla nakushauri nenda karipoti, jungu kuu halikosi ukoko.
 
Serikalini kwa nafasi ya udereva utapata security ya ajira, Pia chunguza hiyo ofisi inasafari za kutosha unaweza pata zaidi ya laki 8 kama night huku salary usiiguse, pili serikalini ukiingia ni rahisi kuchungulia taasisi nyingine zenye safari na ukahamia kwa urahisi kwa check namba yako tu.
 
Acheni kumjaza mwenzenu ujinga...uache laki nane ukimbilie laki tatu..ukikatwa hiyo unabaki na laki mbili...ukienda huko utakula msongo wa mawazo to your entire life.

Kuhusu ishu ya perdiem wasikudanganye..perdiem inaendana na levo ya mshahara..kwa mshahara huo perdiem yako haitazidi elfu sitini..sasa upate safari ya siku tatu singida utalipwa 240,000.

Ukienda huko ulipie guest, msosi, utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.

Ushauri wangu endelea hapo hapo mwendokasi
 
Serikalini kwa nafasi ya udereva utapata security ya ajira, Pia chunguza hiyo ofisi inasafari za kutosha unaweza pata zaidi ya laki 8 kama night huku salary usiiguse, pili serikalini ukiingia ni rahisi kuchungulia taasisi nyingine zenye safari na ukahamia kwa urahisi kwa check namba yako tu.
Security ya ajira ni ujinga ambao unawaponza wengi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom