Ajira mpya: Ushauri wa kuacha Kazi

City Agent

New Member
Oct 3, 2023
2
32
Nimelazimika kuja na ID mpya kwa sababu hii

Ipo hivi, Nilimaliza Chuo 2019, nikaingia mtaani, nikasota sana kwa kutafuta mtaji kidogo, ujenzi, Supplier, kuvuka border na malori, yaani mishe nyingi sana ngumu, lakini pia Kuomba ajira bila Mafanikio kwa kipindi chote nilitembeze bahasha.

Nikaanzisha ka business kidogo mjini lakini mda mwingi ni U winga K.koo, humu wengi tuu tushafanya business, Basi Nikakubali haya ndio maisha niyabadilishe taratibu, Nikaweka ndani familia.

Ikafika hatua issue ya ajira nikaipotezea kabisa, sio kama nilikua vizuri kiuchumi, ila sikua tena na morali ya kuajiliwa, hasa kwa kua nilijua nitapelekwa sehemu ambayo sitaweza kufanya harakati zangu.

Hili jambo lilikua tofauti kabisa kwa Bi Mkubwaa, Hakuna kitu alikua akiomba Mungu siku zote kama mimi kupata Ajira, kila chance zikitoka hata kabla sijapata taarifa yeye ashajua ananipigia kuuliza nimeshaomba?
Kutomkatisha tamaa siku zote nimekua nikimuitikiaa,

Nikapata ki part time sehemu flani hivi nakula 500k, Mara Ajira zikatangazwa, Akanipigia kama kawaida, kipindi hiki nikamwambia "mama hapa nishapata ajira ngoja tuu nijishikize huku" hicho kitu alishangaa sanaa, yaaani sana, Akanisisitiza nikaitikia, ila nahisi alijua tuu sitaomba..

Akamuita Bro, kila kitu changu alikua nacho, akamuambia muombee mdogo wako, basi bwana, Mimi kweli sikuomba ila niliambiwa nimekuombea, fumba fumbua June ter 5 napigiwa Simu na Bimkubwa Akiwa anafura ambayo sijawahi muona nayo, "Mwanangu Mungu ni mkubwa Umepata Ajira", na maneo mengi sana ya kushukuru, Maombi yake yamejibiwa,

Nikwa niko surprised nami ilibidi nianze kufurahi nayee, Basi akaniambia Naomba week ijayo uende ukaripoti nitakupa nauli (nauli ni almost 75k), na ukirudi tuu uje nyumbani tuongee.

Kiuhalisia Suala la kupata nilifurahi kwa namna flani ila Baada ya hapo ndio nikaanza kuwaza Ule umbali ambao ndio sikuzote umekua ukiniwazisha nikipata ajira niatatupwa mbali...

Akanitumia 100k, nakumbuka ter 12 nikafunga Safari, Njiani nawaza huku niendako kukoje? Haya achilia mbali huu umbali jee Huko ninakoenda ni ndani kiasi gani? mishe zangu itakuaje? Familia nayo?

Basi Usiku wa giza nikaingia nikatulia pale pale stend, Asubuhi nikaulizia nikapanda gari kwenda Halmashauri, ni elf 3 kutoka hapo stend (mkoani).

Nikamaliza kila kitu mapema, nikasema hapa sirudi mpaka niione shule, Kuipata Shule tu ni elf 10 kwa boda, nikafika nikaangalia mazingira Sio mabaya sana, ni Shule kongwe ya Advance na ndio shule ya wilaya.

Kwa lugha hio, kwa Hapo shule ilipo kwenda Mkoani ni karibu zaidi ya Wilayani(halmashauri). Kesho yake nikageuza, na mawazo sana, nifanyejee? Isitoshe mpk hapo nilikua nishapigika kiuchumi, maana nilishachukua ka fremu na kuchukua ka mzigo ambako muuzaji ni mimi mwenyewe, naenda kuanzaje life?

Bila kutarajia ilikua June ter 23, napokea Muamala bank "Kiasi cha 671,000 kimewekwa kwenye account yako..."
Nikampigia mshkaji wangu nikamuuliza nimeona pesa ya kujikimu, akaniambia kiasi gani? Nilivyomuambia akasema huo ni mshahara shukuru, wamepata wachache sana, kuja kuuliza Halmashauri nzima tulipata watu Sita.

Basi Siku zikaisha nikarudi kitanzini..

Mazingira ya Nilipopanga...
Ni central kubwa lakini ya kizamani, shule ipo hapo hapo, ila pako local sana, ukabila sana nikaulizia kuhusu business kwa wafanyakazi wenzangu naambiwa hapo ukianzisha biashara kwa wewe mgeni wateja huwapati wanataka wenyeji, Uchawi kwa sanaaa lakini pia Wafanyabiashara wenzako watakuandama.

Nyumba Nzuri ni zakuunga unga, Wizi kwa sana siku ya kwanza nipo tuu ndani nafanya usafi ndani natoka nje Viatu na Fagio na Ndoo vishaenda. Ukame uliopitiliza, Vyakula ni ghali,


Mazingira ya Kazini...
Shule ni ya Advance, Haina uhaba wa walimu Nina vipindi kama vinne au tatu tuu kwa siku(kwa lugha nyingine naingia mara 2 tuu kwa siku).

Baada ya hapo Saa nane vipindi vimeisha, kinachofuatia ni Vipindi vya Ziada ambavyo Vina posho yake(buku 5 kwa kipindi au 10 kwa double).

Chai, lunch ni Jukumu la shule, na ofa ofa nyingne, wana miradi yao mingi.

Kwa ufupi mazingira ya kazini sio shida sana..


Mazingira ya Biashara.....
Kwa hapa ni magumu sana, Nikitaka kufanya hivyo basi niende mkoani, Sio mbali na shule dk kumi umefika, nauli ni buku. Ni mjini pako vizuri almost kila kitu, wafanyakazi wengi wanaishi huko na kufanya biashara zao huko.

Kwa nini nataka kuacha..
Sina furaha kabisa kuishi huku, hakunipi changamoto, Mkoani ndio pana fursa nyingi sana na wateja wapo sana, hasa kwa biashara ambayo mimi nilikua na dili nayo mjini ya electronics, nguo na viatu, ni rahisi sana kuifanya huku, lakini changamoto ni umbali wa kuja dar kuchukua mzigo kuleta, kwa uzoefu inatakiwa angalua kila baada ya week 2 niingie town, nitawezaje?

Ingekua ni sehemu unasafiri usiku, asubuhi umefika hii ningesema ijumaa nije town, jumamosi k.koo, jumapili nageuza, lakini hata kama hilo linawezekana, uhakika wa gari za usiku bado haupo, Tangu nimekuja huku nimekua wa mawazo.

Hivyo naona kabisa nikididimia, kila siku napigiwa simu na watejaa, nalazimika kila baada ya week mbili niende mjini kuweka mambo sawa halafu nirudi, Risk kubwa, gharam kubwa...

Nini napanga...
Salary yangu take home ni 670,000 as sidaiwi loan board, nimeuliza kwa Salary hii naweza pata loan mpk 34M niki force kumaliza ile 1/3, Nichukue mkopo nirudi zangu mjini ,nitawalipa hata kwa kutumia biashara, sitaki nigeuke tapeli,

Najua kuna risk pia, ila hili sidhani kama nakurupuka. Niliwaza niombe uhamisho, ila nafikiria ugumu uliopo hapo haijalishi cheti cha ndoa ninacho..

Nini kinanifanya nawaza kuacha..
Bi mkubwa, Bi mkubwa, Bi mkubwa...
Siku akisikia nimeacha, Najua sana ataumia mnoo, hataamini kua nimeacha katika nia nzuri, atahisi ni kukengeuka...,

Mshahara wangu wa pili nilimtumia 150k, akachukua 50k, 100k akarudisha akaniambia jiwekee pesa yako taratibu, umepata ajira utulie mwanangu, Yaani yeye zile hustle za Uwinga mjini, kukesha kwenye Malori usiku, mihangaiko mingi situlii kumbe alikua anaona ni kama mateso, yaani nafanya kwa kuumia, ndio maaana anasema nipumzike, nawaza 670k nitaishije na familia?

Nimewaza Niache Job, lakini asijue mtu yoyote yule ili Bi mkubwa awe na amani...

Naombeni ushauli katika hili...
Nikibaki mazingira ni kama hayo, na zaidi wife amesema ameshachoka kukaa mwenyewe, anaomba kila siku aje namkazia, hivyo kama nisipofanya maamuzi ya kuacha, mwezi huu nimruhusu aje huku.

Mshahara wa 670k, nitaugawaje kwa matumizi na maendeleo kwa watu wa 3?, Jee nimshirikishe tuu bimkubwa kuhusu hili, nioongee naye kwa undani sana?

Akilili yangu asivi..
Kaucha 70%
Kubaki 15%
Kuhama 5%.

Experience ya Hustle za mtaani, nimeziishi kwa vitendo, nyakati ngumu sana nimekutana nazo, ujenzi nimepiga mno, night shifts sana tuu, ila hua kuna mwanga na tumaini mbeleni, ila hapa ni mtihani.

Mwisho ieleweke Siichukii hii kazi, wala kufanya kwa kinyongo, Hio nayo ni kujitaftia Nuksi na mikosi,

Nikingia Darasani nafundisha vzr tuu na kwa moyo wote, mara nyingi sana wenyewe wananiomba niingie hata Usiku wachange pesa wanipe.

Pengine ningekua town nisingeacha as long napata muda. Hivyo kwa ufupi kazini sina shida, Tatizo linaanza ninaporudi Geto, Sijazoea kabisa kukaa nisubiri mda nile nilale, naona kabisa kuna bomu nalitengeneza, naona majukumu haya hapa.
 
Okay.

Mapema sana kutoa maamuzi magumu kama hayo. Na mi nashauri ubaki.

Kwanini?

Biashara ni upepo, mambo yanaweza kufeli ukaomba poa. Yeah, najua we risk taker lakini ebu hold kidogo.

Nashauri, subiri angalau mwaka mmoja (miezi 12) ujipange.

Unaweza biashara ukafanya sehemu nyingine, ambapo unaweza muweka msimamizi mwingine.
 
We mwamba unaonekana ni mtu kazi hebu fanya hvi.......
Kwa kuwa umesema kutoka hapo hadi mkoani ni mbali wa dk 10 basi fanya kuamia mkoani na uishi huko na familia yako hamishia hapo kabisaa alafu fungua biashara, ila fanya kuongeza mtaji ili safari za nenda rudi dar zipungue kwa maana utakuwa unachukua mzigo mkubwa wa kukusogeza walau miezi 2

Hiyo kazi nakushauri usiiache maana naona ni kama daraja la kukupeleka Kwenye mtaji mkubwa.

Huko unapaona hapafai kwa sababu tu ya ugeni na hujazoea mazingira we komaaa siku zote mwanzo ni mgumu daima.

Mwamba nakushauri just replicate that spirit of hard work and determination ulokuwa nayo hapa mjini daslam naamini utatoboa na kufanikiwa mwamba.....

Bro ushapata mtaji hapo komaa.....ila nakushauri usijichanganye ukachukua mkopo alafu ukaacha kazi, kama ni mtu wa kutaka kukua kibiashara kuna wakati utataka uende benki ukachukue mkopo afu ukutane na bonge moja la ban........kwa maana hutoweza kukopesheka
 
Nimelazimika kuja na ID mpya kwa sababu hii

Ipo hivi, Nilimaliza Chuo 2019, nikaingia mtaani, nikasota sana kwa kutafuta mtaji kidogo lakini pia Kuomba ajira bila Mafanikio kwa kipindi chote.

Nikaanzisha ka business kidogo mjini lakini mda mwingi ni U winga K.koo, humu wengi tuu tushafanya business, Basi Nikakubali haya ndio maisha niyabadilishe taratibu, Nikaweka ndani familia.
Ikafika hatua issue ya ajira nikaipotezea kabisa, sio kama nilikua vizuri kiuchumi, ila sikua tena na morali ya kuajiliwa, hasa kwa kua nilijua nitapelekwa sehemu ambayo sitaweza kufanya harakati zangu.

Hili jambo lilikua tofauti kabisa kwa Bi Mkubwaa, Hakuna kitu alikua akiomba Mungu siku zote kama mimi kupata Ajira, kila chance zikitoka hata kabla sijapata taarifa yeye ashajua ananipigia kuuliza nimeshaomba?
Kutomkatisha tamaa siku zote nimekua nikimuitikiaa,

Nikapata ki part time sehemu flani hivi nakula 500k, Mara Ajira zikatangazwa, Akanipigia kama kawaida, kipindi hiki nikamwambia "mama hapa nishapata ajira ngoja tuu nijishikize huku" hicho kitu alishangaa sanaa, yaaani sana, Akanisisitiza nikaitikia, ila nahisi alijua tuu sitaomba..

Akamuita Bro, kila kitu changu alikua nacho, akamuambia muombee mdogo wako,
Basi bwana, Mimi kweli sikuomba ila niliambiwa nimekuombea,
Fumba fumbua June ter 5 napigiwa Simu na Bimkubwa Akiwa anafura ambayo sijawahi muona nayo, "Mwanangu Mungu ni mkubwa Umepata Ajira", na maneo mengi sana ya kushukuru, Maombi yake yamejibiwa,

Nikwa niko surprised nami ilibidi nianze kufurahi nayee, Basi akaniambia Naomba week ijayo uende ukaripoti nitakupa nauli (nauli ni almost 75k), na ukirudi tuu uje nyumbani tuongee.

Kiuhalisia Suala la kupata nilifurahi kwa namna flani ila Baada ya hapo ndio nikaanza kuwaza Ule umbali ambao ndio sikuzote umekua ukiniwazisha nikipata ajira niatatupwa mbali...

Akanitumia 100k, nakumbuka ter 12 nikafunga Safari, Njiani nawaza huku niendako kukoje? Haya achilia mbali huu umbali jee Huko ninakoenda ni ndani kiasi gani? mishe zangu itakuaje? Familia nayo?

Basi Usiku wa giza nikaingia nikatulia pale pale stend, Asubuhi nikaulizia nikapanda gari kwenda Halmashauri, ni elf 3 kutoka mkoani..
Nikamaliza kila kitu mapema, nikasema hapa sirudi mpaka niione shule, Kuipata Shule tu ni elf 10 kwa boda, nikafika nikaangalia mazingira Sio mabaya sana, ni Shule kongwe ya Advance na ndio shule ya wilaya..
Kwa lugha hio, kwa Hapo nilipo, Mkoani ni karibu zaidi ya Wilayani(halmashauri)

Kesho yake nikageuza, na mawazo sana, nifanyejee? Isitoshe mpk hapo nilikua nishapigika kiuchumi, maana nilishachukua ka fremu na kuchukua ka mzigo ambako muuzaji ni mimi mwenyewe, naenda kuanzaje life?

Bila kutarajia ilikua June ter 23, napokea Muamala bank "Kiasi cha 671,000 kimewekwa kwenye account yako..."
Nikampigia mshkaji wangu nikamuuliza nimeona pesa ya kujikimu, akaniambia kiasi gani? Nilivyomuambia akasema huo ni mshahara shukuru, wamepata wachache sana..

Basi Siku zikaisha nikarudi kitanzini..

Mazingira ya Nilipopanga...
Ni central kubwa lakini ya kizamani, shule ipo hapo hapo, ila pako local sana, ukabila sana nikaulizia kuhusu business kwa wafanyakazi wenzangu naambiwa hapo ukianzisha biashara kwa wewe mgeni wateja huwapati lakini pia Wafanyabiashara wenzako watakuandama...
Nyumba Nzuri ni zakuunga unga,
Wizi kwa sana siku ya kwanza nipo tuu ndani nafanya usafi ndani natoka nje Viatu na Fagio na Ndoo vishaenda..
Ukame uliopitiliza, Vyakula ni ghali,


Mazingira ya Kazini...
Shule ni ya Advance, Haina uhaba wa walimu Nina vipindi kama vinne tuu kwa siku(kwa lugha nyingine naingia mara 2 tuu kwa siku)..
Baada ya hapo Saa nane vipindi vimeisha, kinachofuatia ni Vipindi vya Ziada ambavyo Vina posho yake(buku 5 kwa kipindi au 10 kwa double)
Chai, lunch ni Jukumu la shule, na ofa ofa nyingne, wana miradi yao mingi.
Kwa ufupi mazingira ya kazini sio shida sana..


Mazingira ya Biashara.....
Kwa hapa ni magumu sana, Nikitaka kufanya hivyo basi niende mkoani, Sio mbali na shule dk kumi umefika, nauli ni buku.., Ni mjini pako vizuri almost kila kitu, wafanyakazi wengi wanaishi huko na kufanya biashara zao huko.

Kwa nini nataka kuacha..
Sina furaha kabisa kuishi huku, hakunipi changamoto, Mkoani ndio pana fursa nyingi sana na wateja wapo sana, hasa kwa biashara ambayo mimi nilikua na dili nayo mjini ya electronics, nguo na viatu, ni rahisi sana kuifanya huku, lakini changamoto ni umbali wa kuja dar kuchukua mzigo kuleta, kwa uzoefu inatakiwa angalua kila baada ya week 2 niingie town, nitawezaje? Ingekua ni sehemu unasafiri usiku, asubuhi umefika hii ningesema ijumaa nije town, jumamosi k.koo, jumapili nageuza, lakini hata kama hilo linawezekana, uhakika wa gari za usiku bado haupo, Tangu nimekuja huku nimekua wa mawazo
Hivyo naona kabisa nikididimia, kila siku napigiwa simu na watejaa, nalazimika kila baada ya week mbili niende mjini kuweka mambo sawa halafu nirudi, Risk kubwa, gharam kubwa...

Nini napanga...
Salary yangu take home ni 670,000 as sidaiwi loan board, nimeuliza kwa Salary hii naweza pata loan mpk 34M au zaidi ya hapo niki force kumaliza ile 1/3, Nichukue mkopo nirudi zangu mjini ,nitawalipa hata kwa kutumia biaashara, sitaki nigeuke tapeli,
Najua kuna risk pia, ila hili sidhani kama nakurupuka
Niliwaza niombe uhamisho, ila nafikiria ugumu uliopo hapo haijalishi cheti cha ndoa ninacho..

Nini kinanifanya nawaza kuacha..
Bi mkubwa, Bi mkubwa, Bi mkubwa...
Siku akisikia nimeacha, Najua sana ataumia mnoo, hataamini kua nimeacha katika nia nzuri, atahisi ni kukengeuka...,

Mshahara wangu wa pili nilimtumia 150k, akachukua 50k, 100k akarudisha akaniambia jiwekee pesa yako taratibu, umepata ajira utulie mwanangu, Yaani yeye zile hustle za Uwinga mjini, mihangaiko mingi situlii kumbe alikua anaona ni kama mateso, yaani nafanya kwa kuumia, ndio maaana anasema nipumzike, nawaza 670k nitaishije na familia?
Nimewaza Niache Job, lakini asijue mtu yoyote yule ili Bi mkubwa awe na amani...


Naombeni ushauli katika hili...
Nikibaki mazingira ni kama hayo, na zaidi wife amesema ameshachoka kukaa mwenyewe, anaomba kila siku aje, hivyo kama nisipofanya maamuzi ya kuacha, mwezi huu anakuja huku..
Mshahara wa 670k, nitaugawaje kwa matumizi na maendeleo kwa watu wa 3?, Jee nimshirikishe tuu bimkubwa kuhusu hili, nioongee naye kwa undani sana?

Akilili yangu asivi..
Kaucha 70%
Kubaki 15%
Kuhama 5%.

Experience ya Hustle za mtaani, nimeziishi kwa vitendo, nyakati ngumu sana nimekutana nazo, ujenzi nimepiga mno, night shifts sana tuu, ila hua kuna mwanga na tumaini mbeleni, ila hapa ni mtihani.

Mwisho ieleweke Siichukii hii kazi, wala kufanya kwa kinyongo, Hio nayo ni kujitaftia Nuksi na mikosi, Nikingia Darasani nashusha Nondo vzr tuu, mara nyingi sana wenyewe wananiomba niingie hata Usiku wachange pesa wanipe..
Pengine ningekua town nisingeacha as long napata muda...
Hivyo kwa ufupi kazini sina shida, Tatizo linaanza ninaporudi Geto, Sijazoea kabisa kukaa nisubiri mda nile nilale, naona kabisa kuna bomu nalitengeneza.
mzazi anaona mbali ndugu asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na.....jamii forum🤣😅😆😁😄😀😃
 
Mawazo yote ni sawa ni ishu tu ya game of chance wapo waliopiga chini kazi wakatoboa wapo waliopiga chini ikala kwao
 
Samahani sijaweza kuisoma yote nimeishia hapo kwenye kuanzisha biashara.

Ushauri wangu (mimi siyo muajiriwa nitakupa tu ushauri kama raia wa kawaida) omba ruhusa njoo Dar unakopanga kuchukua mzigo pitia kwenye maduka wanamouza bidhaa husika kisha chukua namba zao za simu rudi kituo chako cha kazi fanya biashara kwa njia ya kuaminiana na hawa watu ukitaka mzigo unaandika order unalipa kwa simu au bank mzigo unapelekwa transporter siku mbili tatu umefika dukani maisha yanaenda.

Mimi nina wateja zangu wapo Kigoma walikuja mara moja tu kufunga mzigo wa bidhaa ninazouza miaka minne nyuma mpaka leo tunafanya biashara kwa njia ya kuaminiana hata sura zao sizikumbuki tena,tumia njia hii hope itakusogeza sababu hata ungekuwa na nafasi siyo rahisi kila wiki useme unafata mzigo mwenyewe sababu kuna gharama za nauli malazi etc
 
Umeongea mengi Ila
1.usiache Kaz esp kama ya serikali tafuta alternatives
2.Jipe mudaa ulichakate hko wazo vizur..unaonekana bado mtto kwenye maisha na kwenye biashara
3.usiache kazin..kazi ya kuajiriwa ndo basic ya kwanza au mtaji mkuu ukitaka ufanye biashara za maaana
 
Back
Top Bottom