Nimemkopea pesa kwa mtu hataki kurudisha

Nimemkopea pesa kwa mtu hataki kurudisha

Dada mtu humjui, hela huna ila unaitafuta kwa ajili yake, serious?????
Wenzio 20 tu wanalizwa we million utalipwa???? Duh pole
Nilivyokua namjua sikuhisi anaweza kuwa mbabaifu ndo tatizo. Nimekoma lakini. Hawa usiowadhania ndo wanakuaga hivi, nina rafiki angu wa zaidi ya miaka 6 ila hata aje na shida kiasi gan akiniambia nimkopeshe siwez maana najua hatanilipa, nikimpaga hela huwa nampa tu bila kuweka akilini atanilipa siku moja. Huyu nae sikua nimemjua sasa nishamjua.
 
Hakuna aiseee.. hata buku kama ilikua kwenye mahesabu yako halafu ukampa mtu akazingua kurudisha itakuuma...
Nimefundshwa mahali ukikutana na mtu kama hasiyetaka kulipa deni, unampotezea. Unaangalia ustaarabu mwingine wa kupata hiyo pesa.
 
Mkuu wewe una Moyo wa kishujaa na kipekee. Unakopa kusudi umkopeshe mtu mwingine?
 
Mfalme Sulemani anasema katika kitabu chake cha Mithali 17:18"Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na
mtu; Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake".
 
Nilimuamini tu sababu nilijua ni mtu anaejulikana na inasemekana ana pesa nikaona hataleta uswahili.
Kwa dunia hii ya Leo ambayo pesa ndio imekuwa chanzo cha matatizo mengi ni makosa makubwa sana kumuamini mtu kiasi hicho hata kama anamiliki mgodi.

Unapomkopesha mtu hela bila kuweka mazingira yoyote yanayokuhakikishia kurudi kwa pesa hiyo ni sawa na kufanya gambling tu haijalishi mtu huyo financial status aliyonayo iko vipi.

Sasa kwa sababu ulimkopesha kienyeji na hataki kukulipa basi itabidi wewe uingie gharama kwa kuwashirikisha polisi ukitumia huo ushaidi mdogo ulionao wa phone messages!.

Siku nyingine ujifunze kuwa mchoyo au kama ni kumkopesha mtu, Fanya ukiwa na back up plan.
 
Pole sana mkuu tena sana,.kumuamini mtu moja kwa moja ni gharama mtu akiwa ana uhitaji anajinyongeza kiasi wenye mioyo yetu ya imani tunaingia king,ila nimejiunza kitu MALI BILA DAFTARI HAIENDI BILA HABARI hivyo kama una kaushahidi kidogo kitumie kumshtaki ila kama huna kabisa cjui itakuwaje maana watu wa hivi ni matapeli tuu na hashindwi kukuruka kama akijua huna hata ushahidi wowote...

Pole sana M ndefu bhana usawa huu..
 
Kwa dunia hii ya Leo ambayo pesa ndio imekuwa chanzo cha matatizo mengi ni makosa makubwa sana kumuamini mtu kiasi hicho hata kama anamiliki mgodi.

Unapomkopesha mtu hela bila kuweka mazingira yoyote yanayokuhakikishia kurudi kwa pesa hiyo ni sawa na kufanya gambling tu haijalishi mtu huyo financial status aliyonayo iko vipi.

Sasa kwa sababu ulimkopesha kienyeji na hataki kukulipa basi itabidi wewe uingie gharama kwa kuwashirikisha polisi ukitumia huo ushaidi mdogo ulionao wa phone messages!.

Siku nyingine ujifunze kuwa mchoyo au kama ni kumkopesha mtu, Fanya ukiwa na back up plan.
Nashukuru kwa ushauri..
 
Back
Top Bottom