Nimemkopea pesa kwa mtu hataki kurudisha

Nimemkopea pesa kwa mtu hataki kurudisha

Pole sana mkuu tena sana,.kumuamini mtu moja kwa moja ni gharama mtu akiwa ana uhitaji anajinyongeza kiasi wenye mioyo yetu ya imani tunaingia king,ila nimejiunza kitu MALI BILA DAFTARI HAIENDI BILA HABARI hivyo kama una kaushahidi kidogo kitumie kumshtaki ila kama huna kabisa cjui itakuwaje maana watu wa hivi ni matapeli tuu na hashindwi kukuruka kama akijua huna hata ushahidi wowote...

Pole sana M ndefu bhana usawa huu..
Asante mkuu. Na kweli alifanikiwa kuniingiza king..
 
Mkuu mwandikie barua mwambie unamdai milion 5 then akikujibu kwa maandish kuwa unamdai one m ndo itakuwa hati ya makubaliano ya kukoposhena
 
Mkuu mwandikie barua mwambie unamdai milion 5 then akikujibu kwa maandish kuwa unamdai one m ndo itakuwa hati ya makubaliano ya kukoposhena
Mkuu barua zama hizi si ataona namuigizia?
 
Duh, yaani ww mwenyewe huna uwezo wa kumkopesha ila umeweza kwenda kujitia kitanzi kwa kumkopea! Akili nyingine banah, Nenda polisi.
 
Nenda Polis utasaidiwa,ila ujifunze kutomwamin Mtu sababu,hasa hawa wenye sifa ya kukopa kopa ovyo na maden full
 
We are sailing in the same boat! kuna rafik angu kabsaaa alkuja nikamkopesha 200,000/- alisema angenirudishia kesho sas iyo kesho ni mwez saiz na amekaa kimya tu. Yaan nafikiria cjui nimfanye nin
We are in the same boat.

Kuna mdada mmoja alikuja kwangu akanambia nimpatie laki mbili, ambayo angerudisha baada ya Mwezi....Aisee hadi sasa ni zaidi ya miezi miwili sijapata hiyo hela.

Nafikiria hata niende kwa sangoma[emoji24] [emoji24] ...it kills me when i think of the situation.
 
Njia nzuri ya kumpoteza rafiki na pesa ni kumkopesha. Huyo harudishi mpaka uchukue hatua nzito sana.
Kwa sasa nimejifunza kutumia maneno SINA HELA, kinyume na hapo nitakuwa natoa hela kama msaada sio kama mkopo.
 
Kuna mtu alikuja ana shida nimsaidie million moja atarudisha baada ya siku 3, nilimuamini nikamwambia sina ila nitamtafutia. Nikaipata kwa mtu nikampatia, ila sasa toka aseme anairudisha mpaka leo zimepita week 3 kila siku ananiletea story kuwa anatafuta ananiletea nyumbani ila haleti, juzi nilikutana na mtu akawa ananiambia huyo mdeni ni tapeli ameshaomba hela kwa watu wengine na aliniambia hivyo bila kujua na mimi nimeshampatia pesa. Sielewi hiyo hela naipataje na mimi sina hiyo hela kusema ntailipa mara moja tu. Nisaidieni nifanye nini huyu mtu arudishe pesa ya watu.
'Any decision you make in life you are responsible for it' Tuanzie hapo Ilitakiwa kwavile unamkopea mungeli andikishana 'Vinginevyo unatakiwa umfugie mbwa wa kizungu' na kuchukua kitu chake/mali uka uze ili upate angalau kiasi fulani
 
Mi najua siku hizi watu hawalipi madeni, mtu akiomba nimkopeshe laki Nampa tu elf kumi imsaidie kuelekea kutafuta kwingine
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
akiomba 10000
utampa ngapi sasa
 
Katika maisha jifunze kitu kimoja kabla ya kukopesha mtu. Rafiki na asiye Rafiki.

1. Je akishindwa kulipa urafiki wenu utapotea?
2. Je akishindwa kulipa maisha yako yatatetereka kwa sababu ya hiyo pesa?
3. na mwisho wa siku akishindwa kukulipa utamchukia yeye au ndugu zake?

Kama jibu ni ndiyo katika mojawapo ya hayo maswali matatu, basi mshauri aende Benki.
 
Back
Top Bottom