Nimekumbuka zamani

Nimekumbuka zamani

Habari za siku nyingi wanajukwaa….

Leo nimekaa nimejiwazia nikajikuta tu naona watoto wa sikuizi hawaenjoy kama ambavyo sisi zamani tulikuwa tunaenjoy,. Watoto wa saizi hawajui hata raha za kwenda likizo kwa bibi

Kwanza niseme tu kuwa bibi yetu kama wajukuu kabarikiwa nao ,. Mpaka sasa nadhani tunaweza kuwa hata tuko 50 na wengine ambao hatuwajui wanaweza kuwa hata 60 tumefika,. Imagine watoto 13 naa wote wana watoto sio chini ya wanne😄😄 ( ila hiii sio lengo la uzi ) ila mtaelewa kwanini nimesema hivi.

Kipindi kile ilikuwa likizo zote za sikukuu yaani December na ile likizo ya pasaka bibi yangu alikuwa anasisitiza wajukuu wotee tuende kumwona,. Yaani tulikuwa tunakuwa wengii kwa bibi ( kila kona unayopita ina mtu😅😅😅) ,. Na kwa vile tulikuwa wengi uharibifu kila siku kuanzia kwenye vyombo watu wanavunja,. mafundi TV sasa ndio kabisa mpaka bibi alikuwa anafungia ndani Tv zake zote hakuna kuangalia mpaka tuondoke,.

Sasa hapo ndio ile mikakati ilikuwa inaanza,. Ikikaribia likizo simu zinaanza kipigwa basi kila watu tunapangiana vitu vya kubeba,. Mie na dada angu tulikuwa tunabeba zetu TV ,. Binamu zetu wengine wa mwanza walikuwa wanabeba deki,. Wa arusha walikuwa wanabeba CD ( baasi hapo kila mtu ataagiza movie anazozitaka wao kazi yao kuzifatuta zilizotafsiriwa wanakuja na CDs Kibao ),. Wengine wa Dar ilikuwa kazi yao kubeba snacks ,.Wengine mipira midoli yaani Ili mradi tu kila mtu awe na chakubeba ….. Yaani ilikuwa tukifika kwa bibi ni kuangalia tu movie kuanzia asubuhi hadi usiku maana ilikua marufuku mtu kutoka nje ya geti😁😁😁

Usiku sasa kila watu wakishaingia chumbani kwao ni muda wa mastori hadi mida mibovu asubuhi hata hakunaa anayekumbuka alilala saa ngapi,. Kila watu wanasimulia stori za nyumbani shuleni yaani ilikuwa raha kipindi kile….

Bibi kwanza alikuwa ananunua sahani nyingi na vikombe vya plastiki kila mtu anamwandika jina kwenye sahani yake ( maana hataki kero mda wa kula zilikuwaga kelele sio za nchi hii watu wanachagua sahani maara vikombe mwisho wa siku kuvunja ),. Baaasi nguo zetu zote zilikuwa zinaandikwa majina ili akija mtu wa kufua kila mtu kambani anaenda kuanua nguo zilizoandikwa jina lake,. Ila bibi😂😂😂

Bibi alikuwa anatuambia yaani babu yenu wakati anajenga hii nyumba aliweka vyumba vikubwa kwajili yenu,. Yaani dream yake ilikuwa muwe mnakuja mnajaa kama hivi mnacheza mnampigia kelele,. Lakini kwa bahati mbaya alifariki bila kumwona mjuu wake hata mmoja ,. Yaani wote tumezaliwa akiwa kashakufa🥹🥹🥹

Kipindi kile ilikuwa hata kama likizo imekukuta mgonjwa utang’a ng’ania usafiri tu hivyo hivyo maana utajisi unyonge wenzio wote wako kwa bibi,.
Sema ndio hivyo sasa watu wenyewe wotee saizi washakuwa watu wazima ,. Wakuoa wameoa na wakuolewa wameshaolewa wengine toka waliendaga nje kusoma haawajarudi wenginee ndio hivyo yaani kwenda kwa bibi sikuizi laabda litokee tukio na hata mkienda hamui wengi na hata hao wachache kila mtu yuko busy na mambo yake yaani nyumba imepoozaaa😔😔 sio kama zamani…
Chai sana hapa.
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi michezo yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Hapo Pa kwenda kuogelea mtoni, umenikumbusha mbali mno.
 
Eeeh ilikuwa raha sana . Ukiambiwa uondoke kabla ya wenzako unaona umekatiliwa sana yaani. Halafu kama ni december unakuta ni kipindi cha masherehe sijui kipaimara alooo😂😂😂tulikuwa tunavamia kila nyumba unakunywa nyumba hii fanta nyingine coka nyingine mirinda. Mkirudi nyumbani mmevimbiwa😂😂😂😂
😂😂😂😂
 
Kumbe ww ni wa juzi-juzi tu hapo. Eti mnakaa kuangalia Tv. na Uncle kaleta Ps.
Hebu rudi nyuma kule enzi za redio za mbao National na Hitachi halafu kwa bibi mara nyingi kama sio zote ni huko mashambani - gari ikipita inashangliwa na watoto ...Gaaari; Gaaari. Nyie wa hapo mjini na huko kwa bibi inaonekana ni enzi za juzi hapo umeme ukikatika utawasikia watoto: Haaaaaa! kwa muda halafu ukirudi utawasikia: HUOOOOOO. Hakuna cha mvulana au msichana wote ni kelele mtindo mmoja. Huku mashambani ambako ndo kiuhalisia ndo kwa Bibi; wavulana hushirikishwa kazi za kiume - kuchunga, kuvua samaki, kurina asali, kulima na kukata vichaka kuzunguka nyumba ya bibi n.k n.k. Wasichana hushirikishwa kazi za kupika, kufua nguo, kukamua, kuuza maziwa n.k.nk.
😂😂 Mkuu kwa bibi sio lazima kuwe bush haswa, babu na bibi walihamia kijiji kilichoendelea, barabara, maji , umeme havikua shida. Kwa bibi sio lazima kuwe na shida mkuu.

Hata mleta uzi kwa bibi yake kuna bonge ya geti, tv, movies kila mtu ana expirience yake nzuri anayokumbuka.

Na hata miaka hiyo ya 80 unayoisema wewe bado walikuwepo wenzio wanaenda kwa bibi na umeme sio bush.
 
Eeeh ilikuwa raha sana . Ukiambiwa uondoke kabla ya wenzako unaona umekatiliwa sana yaani. Halafu kama ni december unakuta ni kipindi cha masherehe sijui kipaimara alooo😂😂😂tulikuwa tunavamia kila nyumba unakunywa nyumba hii fanta nyingine coka nyingine mirinda. Mkirudi nyumbani mmevimbiwa😂😂😂😂
Naona wengi story zenu zina ushua mwingi
 
bibi alikuwa anafungia ndani Tv zake zote hakuna kuangalia mpaka tuondoke,.

Sasa hapo ndio ile mikakati ilikuwa inaanza,. Ikikaribia likizo simu zinaanza kipigwa basi kila watu tunapangiana vitu vya kubeba

Awali ya yote zamani ina zama nyingi...

Leejay, hii zamani yenu inaonekana kama ni zamani ya Jakaya Kikwete hivi yenye kupigiana hadi simu ninyi wajukuu, maana nikikumbuka zamani ya simu za TTCL si kaya nyingi zilikuwa na huduma ya zile simu, na hata zikiwepo basi wazazi walikuwa wakizifungia kwenye kiboksi cha mbao chenye kikufuli au ile sehemu ya kuzungusha namba inawekwa lock...

Sisi wengine zamani zetu tulikuwa ni kwenda mtoni au mabwawani huko kuogelea na kuvua visamaki (hii tulikuwa tunapigwa marufuku sana sababu ya matukio ya kufa maji), kwenda porini kutafuta kuni, kwenda porini kuchunga mbuzi na ng'ombe lakini ukiwa mtoto lazima awepo mtu mzima sababu ya matukio ya kunyonya damu (tulikuwa tunaamini kuna nyonya damu 😅)...
 
Habari za siku nyingi wanajukwaa….

Leo nimekaa nimejiwazia nikajikuta tu naona watoto wa sikuizi hawaenjoy kama ambavyo sisi zamani tulikuwa tunaenjoy,. Watoto wa saizi hawajui hata raha za kwenda likizo kwa bibi

Kwanza niseme tu kuwa bibi yetu kama wajukuu kabarikiwa nao ,. Mpaka sasa nadhani tunaweza kuwa hata tuko 50 na wengine ambao hatuwajui wanaweza kuwa hata 60 tumefika,. Imagine watoto 13 naa wote wana watoto sio chini ya wanne😄😄 ( ila hiii sio lengo la uzi ) ila mtaelewa kwanini nimesema hivi.

Kipindi kile ilikuwa likizo zote za sikukuu yaani December na ile likizo ya pasaka bibi yangu alikuwa anasisitiza wajukuu wotee tuende kumwona,. Yaani tulikuwa tunakuwa wengii kwa bibi ( kila kona unayopita ina mtu😅😅😅) ,. Na kwa vile tulikuwa wengi uharibifu kila siku kuanzia kwenye vyombo watu wanavunja,. mafundi TV sasa ndio kabisa mpaka bibi alikuwa anafungia ndani Tv zake zote hakuna kuangalia mpaka tuondoke,.

Sasa hapo ndio ile mikakati ilikuwa inaanza,. Ikikaribia likizo simu zinaanza kipigwa basi kila watu tunapangiana vitu vya kubeba,. Mie na dada angu tulikuwa tunabeba zetu TV ,. Binamu zetu wengine wa mwanza walikuwa wanabeba deki,. Wa arusha walikuwa wanabeba CD ( baasi hapo kila mtu ataagiza movie anazozitaka wao kazi yao kuzifatuta zilizotafsiriwa wanakuja na CDs Kibao ),. Wengine wa Dar ilikuwa kazi yao kubeba snacks ,.Wengine mipira midoli yaani Ili mradi tu kila mtu awe na chakubeba ….. Yaani ilikuwa tukifika kwa bibi ni kuangalia tu movie kuanzia asubuhi hadi usiku maana ilikua marufuku mtu kutoka nje ya geti😁😁😁

Usiku sasa kila watu wakishaingia chumbani kwao ni muda wa mastori hadi mida mibovu asubuhi hata hakunaa anayekumbuka alilala saa ngapi,. Kila watu wanasimulia stori za nyumbani shuleni yaani ilikuwa raha kipindi kile….

Bibi kwanza alikuwa ananunua sahani nyingi na vikombe vya plastiki kila mtu anamwandika jina kwenye sahani yake ( maana hataki kero mda wa kula zilikuwaga kelele sio za nchi hii watu wanachagua sahani maara vikombe mwisho wa siku kuvunja ),. Baaasi nguo zetu zote zilikuwa zinaandikwa majina ili akija mtu wa kufua kila mtu kambani anaenda kuanua nguo zilizoandikwa jina lake,. Ila bibi😂😂😂

Bibi alikuwa anatuambia yaani babu yenu wakati anajenga hii nyumba aliweka vyumba vikubwa kwajili yenu,. Yaani dream yake ilikuwa muwe mnakuja mnajaa kama hivi mnacheza mnampigia kelele,. Lakini kwa bahati mbaya alifariki bila kumwona mjuu wake hata mmoja ,. Yaani wote tumezaliwa akiwa kashakufa🥹🥹🥹

Kipindi kile ilikuwa hata kama likizo imekukuta mgonjwa utang’a ng’ania usafiri tu hivyo hivyo maana utajisi unyonge wenzio wote wako kwa bibi,.
Sema ndio hivyo sasa watu wenyewe wotee saizi washakuwa watu wazima ,. Wakuoa wameoa na wakuolewa wameshaolewa wengine toka waliendaga nje kusoma haawajarudi wenginee ndio hivyo yaani kwenda kwa bibi sikuizi laabda litokee tukio na hata mkienda hamui wengi na hata hao wachache kila mtu yuko busy na mambo yake yaani nyumba imepoozaaa😔😔 sio kama zamani…
Ndio maisha mkuu, Sasa Mimi ndio nilikaa kwa Bibi ,ndio nilikuwa nawapokea binamu zangu,dada zangu,wakiondoka kurudi Town nilikuwa napwaya kweli,ila nabaki na manguo kibao hadi nayagawa kwa wasiokuwa nazo!Hili
Ilaaa😂😂😂😂,. Ngoja wajuzi waje kukujibu mkuu
Nyeto zipo kitambo Mkuu,Tena wanyama walikuwa wanapiga nyeto balaa!
 
Nyie mlikuwa wa kishua
Sisi ukienda kwa bibi mtachota maji mtoni mtachanja kuni
Mtaenda shamba
Kukamua ng'ombe na kusafisha zizi
Michezo yetu ilikuwa rede,kombolela n.k
Mambo ya cd hatukuwa nayo ni mwendo wa VHS zile mnaangalia kwaya za kkkt Mkichoka mnaweka za kinaijeria au Neriaaa
 
Back
Top Bottom