Nimekumbuka zamani

Nimekumbuka zamani

Wakubwa walikuwa wanasema ni watu...

Kama ni 2014 kwenda nyuma basi ndio maana sijaona ni zamani ya ambayo mimi naiona zamani...
Kwamba watu wananyonyana damu looh😄,.

Kuna wale wengine chinja chinja eti wanakata vidude vya wanaume,. Ila wazazi walijua kututishia enzi zile
 
Siku zinasogea saaana aisee,. Ila maisha ya kuishi ndugu wengi pamoja ni raha sana
Hapa ndio uwa nawasifu wahindi na waarab, kuna namna hata bond inaimarika sana koo ikiwa pamoja, huwezi sikia sijui wamepigana kwenye michongo tofauti na sisi, unamuweka mtoto wa mjomba kwenye michongo ambaye mlikuwa mnawasiliana tu kwenye simu, lazima ukae.

Siku hizi kwa bibi ni mjini hawapati tena uzoefu kama huu, nashukuru mi kwetu angalau kwa mbinde uwa tunaonana kiukoo ingawa ndio hivyo babu na bibi walishatangulia.
 
Wewe hujafaidi kitu asee kama Kwa bibi yenu kulikuwa na geti na Tv huko sio vijijini ni mjini huko.

Raha ya kufaidi mwe huru sio kufungiwa kwenye geti. Hizo movie hata kwenu unaweza kuzitafta ukapata tu.

Sisi tulikuwa tunaenda Kwa bibi kijijini Tena miaka hiyo hata CD hazikuwepo

Kwanza wajukuu maximum ni 25 Hivi
Kwa bibi kulikuwa ng'ombe wengi zaidi ya 100!!

Babu alikuwa mkarimu mno na bibi pia.....tukifika tu tunachinja wenyewe mbuzi kubwa la kuchoma tu yaani linaishia juujuu tu kwenye shikome😂

Muda huo Kuna nyama za kubanika zimeshakauka mpaka basi zinaitwa ng'homele kisukuma ni mwendo wa kukata na kuloweka kwenye maji ya chumvi Kisha unakula...

Maziwa sio ya kuuliza ni muda wowote tu unajipimia ....basi wajomba kesho yake mnaenda nao kuchunga pamoja na kuwinda huko mnakutana Watoto shazi mnawinda sungura,digidigi na ndege kama kware ama kanga kama ni masika pamoja na kuchoma uyoga mnakula!!!(Hivi vitu vyote mjini huwezi pata hata ukiwa milionea)

Mkirudi kutoka machungani kulikuwa na bwawa mnaenda kuogelea weee acha tu hapa sio wanawake au wanaume mnaoga mtakavyo maana tulikuwa wadogo wakubwa ndo walikuwa hawaogi...

Mkirudi mtakula mpaka mnakula Tena. Siku ya sikukuu tulikuwa tunaenda kununulia juice cola zile zinaweka kwenye chupa za soda tulikuwa tuna nunua shilingi5 Hadi kumi!!

Michezo ilikuwa mingi sana kuumizwa ilikuwa sehemu ya michezo pia.

Kuna siku hamuendi kuwinda ni Tour ya kusaka matunda pori na kumletea bibi na Babu imagine tulikuwa tunaanza saa3 Hadi saa8 ndo tunarudi na mizigo ya matunda tumechoka mbaya😹😹

Sisi video kipindi chetu huwezi kuikuta Kijiji kiza hata Kwa diwani huikuti wewe ulichoelezea ni miaka ya 2007 hapa tu Kuna CD/DVD!!

Ukweli na miss sana enzi hizo Kuna mto maji tulikuwa tuna yaziba Kisha tunakamata samaki na vidagaa mkimaliza ni kuchoma hapohapo pilipili tulizia huko kula acha kabisa

Kuna matunda mizizi Yale uking'oa linakuwa kama muhoga ila Lina maji tupu matunda Yale hata nyani wanayapenda sana..

Ni vingi vya kuelezea hii ni miaka ya 1995-2002 Hivi acha kabisa
View attachment 3286837
Vingi ulivyosimulia ni kama unasimulia uzoefu wangu 😀, kweli Tanzania ni nchi ya kijamaa hapa unazungumzia uzoefu wa usukumani lakini mi narelate hayo mambo kwa 85%+ na ya unyakyusani.

Teknolojia imetuharibia sana lifestyle siku hizi madogo likizo wanaishi kama mazombie, ni Ps na tablet asubuhi mpaka usiku 24/7
 
Yes mara nyingi tamaduni zetu zinafanana sana mkuu. Ukweli muda mwingine nikifika huko Kwa bibi na Kuta mapori yameshafyekwa nalilia moyoni. Madogo wa Sasa hawana jipya la kututishia
 
Yes mara nyingi tamaduni zetu zinafanana sana mkuu. Ukweli muda mwingine nikifika huko Kwa bibi na Kuta mapori yameshafyekwa nalilia moyoni. Madogo wa Sasa hawana jipya la kututishia
Hawa wakina junior bure kabisa, siku hizi hata kuogelea wanaenda fundishwa kwenye swimming pool na walimu wao.

Ingawa mi kwabibi bado kupo ila wenyewe ndio hawapo, mara moja moja familia uwa tunakutana lakini siku haiwi na hekaheka nyingi kama zamani, siku hizi tunaokula tungi tunakaa na wenzetu, wazee wa kanisa kivyao vyao. Tabia zimebadilika na mambo yamebadilika ila nashukuru angalau tunaonana.
 
Sisi kwetu likizo ilikua kama camp ya mateso ni mwendo kwenda shamba hapo kulima, kuchimba mashimo ya kupanda migomba, kutifua & kupalilia pia kusomba majani hapo mpaka likizo iishe ushakua mweusi mweusi hivi
Hahahaa ila hiyo nzuri
 
😂😂 Mkuu kwa bibi sio lazima kuwe bush haswa, babu na bibi walihamia kijiji kilichoendelea, barabara, maji , umeme havikua shida. Kwa bibi sio lazima kuwe na shida mkuu.

Hata mleta uzi kwa bibi yake kuna bonge ya geti, tv, movies kila mtu ana expirience yake nzuri anayokumbuka.

Na hata miaka hiyo ya 80 unayoisema wewe bado walikuwepo wenzio wanaenda kwa bibi na umeme sio bush.
Waw! Kumbe wapo watu humu jamvini hawaijui koroboi na taa za chemli. Heri zao.
 
Hawa wakina junior bure kabisa, siku hizi hata kuogelea wanaenda fundishwa kwenye swimming pool na walimu wao.

Ingawa mi kwabibi bado kupo ila wenyewe ndio hawapo, mara moja moja familia uwa tunakutana lakini siku haiwi na hekaheka nyingi kama zamani, siku hizi tunaokula tungi tunakaa na wenzetu, wazee wa kanisa kivyao vyao. Tabia zimebadilika na mambo yamebadilika ila nashukuru angalau tunaonana.
Hakika
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi michezo yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Na kuchunga mbuzi na cha kufurahisha enzi hizo hakuna matukio ya ajabu ajabu.
 
Mnacheza huko hadi mbuzi zinapotea😂😂
kuna siku yalinikuta, michezo imetukolea mbuzi zikarudi zenyewe nyumbani, sasa shida sio kurudi nyumbani shida ilianzia babu kashaziona nyumbani alafu kaja kutuchora tulitafuta wote mbuzi zaidi ya lisaa 😂
 
Hahahahahahah na mbuzi zikipotea giza likiingia zinarudi nyumbani zenyewe nyie mtatafuta hadi vijiji vya jirani. Kwa babu yako ni mkoa upi mkuu?
 
Back
Top Bottom