Nakumbuka kijijini kwetu huko Tarakea bhn, yaani ilikuwa nyumbani tupo familia yetu na watoto wa ndugu zake baba
Sasa bhn unajua watoto mkiwa wengi jioni tukiwa jikoni kila mtu anawahi sehemu yenye joto, hapo ni full kugombania sehemu yenye joto mpaka mama anatufukuza tukae nje ya jiko mpka chakula kiive,
Au kwenda kukata majani acha kabisa, tunaenda kukata nyasi au matete bhn, afu ukute ni msimu wa mvua au ndo mvua zimekata tuu ynavyokuwa mazito ukiyabeba kichwani, Ila kwakuwa tulikuwa wengi ilikuwa full burudani,
Njoo kwenye chakula kinapikwa kingi na ni marufuku chakula kumwagwa, matunda sasa asubuhii mnaamka kuwah maparachichi kama yamedondoka ni kuyakusanya tuu,
Kulala kulikuwa na vitanda vya 6*6 ni kugombania mm nalala ukutani ukiamini mwizi hatokuona š Ila kwa ujumLa nakumbuka kumbukizi nzuri niliyopata na ndugu zangu kaka, dada na mabinamu zangu!
Hakika siku zinasogea aseeh